nimepita hapa face book na kukutana na sura hii ambayo imenikumbusha mbali sana, hususan kampuni yake ya faces international ambayo ilikuwa chachandu kubwa kwa fani ya umodo nchini ambapo masupa modo kibao waliibukia. Amina Mongi tunakukumbuka na ulale sehemu njema huko uliko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. He! Huyu kumbe alifariki.

    Namkumbuka jina lake lilikua limepamba sana nikiwa namaliza form four.

    Jamani maisha haya ni mafupi kweli

    ReplyDelete
  2. Ni kitambo tangu utangulie mbele ya haki, nakumbuka was '99 kama sikosei ulipata mzinga pale wami ukitokea moshi kula sikuu ya xmass...nilipata habari toka kwa keizer kahama aliyekuwa mtangazaji wa clouds fm ambae kwa sasa nae ni marehemu kupitia kipindi cha trafic jam.....kweli ni kitambo, upumzike kwa amani ehee dada amina na mungu akusamehe zambi zako.

    ReplyDelete
  3. Uwii Mtu mwenyewe mbona ana mapengo? walimbonda wenziwe akaamua kukimbia mambo ya modo moja kwa moja kuogopa kung`olewa yote nini?

    ReplyDelete
  4. dah amina! nani kama amina! yeye ndio kainua fani ya model na urembo nchini tanzania.alianza yeye,sasa hivi ndio tunaona kina maria sarungi,but these lady right here did a lot bwana! ukitaja urembo,huwezi acha taja amina! alimzindua miriam odemba. i miss u amina! Pumzika kwa amani na pale kwenye neema

    ReplyDelete
  5. Amina! dah,Michuzi asante sana kwa picha hii.Huyu dada angekuwa mbali sana sasa hivi kama bado angekuwa hai.Alikuwa ana roho ya upendo sana,na nina uhakika huko aliko alipokelewa vizuri sana na wenyeji wa huko

    ReplyDelete
  6. Nakumbuka Amina Mongi alivyohangaika na Mariam Odemba (wakati huo anaitwa Mariam Ikoi)...Mariam alikuwa msichana mtundu, lakini Amina aliweza kumsimamia mpaka siku zake zilipo fika na Mungu akamuita Mbinguni.

    Mara yangu ya mwisho kumuona Amina Mongi ilikuwa March 1999 pale La Dolce Vita, tulikuwa pamoja tunaangalia live maonyesha ya urembo “Face of Africa” yakifanyika Afrika Kusini. Mariam Odemba alimaliza mshindi wa 3, Amina Mongi aliruka kwa furaha mpaka machozi yalimtoka.

    Huyu ndiye Amina Mongi niliyemfahamu mimi, mwenye upendo na huruma kwa wengine. Maendeleo huletwa na wenye moyo, Amina Mongi kweli ni mfano wa kuingwa.

    Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  7. Anon wa 11:13
    hujakosea sana huyu dada alifariki wakati wa Y2K, alikuwa anarudi toka Moshi baada ya kuhudhuria mwaka mpya wa 2000 kwao kwa kuwa ilidhaniwa kuwa ndiyo mwisho wa dunia na hivyo kupata ajali ya gari iliyokatisha maisha yake papo hapo.

    ReplyDelete
  8. Soames, Miriam Ikoa na Miriam Odemba ni watu wawili tofauti.

    ReplyDelete
  9. mdau miriam ikoa alikuwa miss dar es salaam sasa yupo celten/zain.

    ReplyDelete
  10. Mungu akuondolee adhabu ya kaburi Amina.. You are always in our prayers.. Always Baba mdogo (dRU)

    ReplyDelete
  11. enzi zile miriam odemba alikuwa anaitwa miriam julius, miriam ikoa na odemba ni watu wawili tofauti

    ReplyDelete
  12. enzi zile miriam odemba alikuwa anaitwa miriam julius, miriam ikoa na odemba ni watu wawili tofauti

    ReplyDelete
  13. Samahani wadau. Mbona kafanana na Ms Rukia Mtingwa? Wana undugu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanafananaga sana hata mm nshawachanganyaga mno

      Delete
  14. rrrrrrrrrrrrrrr.iiiiiiiiii.ppppppppppppp
    huyu dada alikuwa na roho nzuri sana Mungu amrehemu.

    ReplyDelete
  15. NILIKUWA NAIPENDA SANA BOB STYLE YAKE ...
    HALAFU ALIKUWA SOCIAL SANA JAMANII

    CHINI KUMEEMEZA WATU WENGI SANA. ILIKUWA SIKU ZA MWANZONI MWA MWAKA 3RD JANUARY KAMA SIKOSEI ..DADA HUYU ALIVYOPOTEA KWA AJALI YA GARI..

    MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI


    PAM

    ReplyDelete
  16. Ahsante wadau kwa masahihisho..kumbukumbu yangu ya miaka 10 inaniangusha..!! Kumradhi kwa Miriam Ikoa kwa kumfananisha. Ahsante

    ReplyDelete
  17. she was the best. Amina aliinua fani ya urembo Tanzania.Alikuwa na moyo na alipenda alichofanya.I will never forget her. Rest in Peace .

    ReplyDelete
  18. I didn't know her as a person but masha allah she is beautiful and even in the photo you can almost see right through her, those days alikuwa na ITV akitangaza na yule kaka Othman Njaidi oh my, those were the days anyways life goes on the rest is history :-)

    ReplyDelete
  19. Anony wa November 17, 2008 3:00 PM, we do not speak ill of the dead. May God forgive you. Rest in peace Amina.

    ReplyDelete
  20. Ni kweli kabisa, kama Amina angekuwa hai angekuwa mbali sana tena sana. Alipenda sana mambo ya usanii.

    Alikuja Bagamoyo April 1994 tulipokuwa tunafanya shoot ya sinema Maangamizi the Ancient One. Alifanya interview safi sana na ilionyeshwa kwenye ITV. Hivi hiyo footage bado ipo kweli? Nilisikitika sana nilipoambiwa kuwa alifariki katika ajali ya gari.

    REST IN ETERNAL PEACE AMINA.

    ReplyDelete
  21. Anonymous wa 17,2008, 3.00 PM. wewe ni mpumbavu sana tena akili yako ni fupi. lait ungejua usingesema hayo yote. hujafa hujaumbika. May God forgive u, u dont know what ur saying. My IN LAW Amina rest in peace wherever your.

    ReplyDelete
  22. Mdau uliesema Miriam Odemba ndo Miriam Ikoa acha kudanganya hao ni watu wawili tofauti. Usiandike mambo mengi usiokuwa na uhakika nayo.
    Rest In Peace dada Amina bado tunakumbuka juhudi na kazi zako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...