Kaka Michuzi na wadau wote wa blog hii, nilikuwa nasikia tu toka kwa watu kuhusiana na chupa za maji ya kunywa kuokotwa na baadhi ya wananchi wenye nia mbaya na kujazwa maji kiholela mitaani na kuuza mitaani tena.
Hali ipo hivi; chupa za maji ya kunywa huokotwa na kujazwa maji yasiyo salama na kuuzwa mitaani, mfano hai ni huu; usiku wa jana 19/11/2008 nilikuwa wilaya Masasi mkoani Mtwara wakati napata dinner akanijia mtoto wa miaka takribani 10-12 akiniomba chupa yangu iliyo na maji nimpatie pindi nitapoyamaliza.
Nikamuambia asubiri nikayanywa yale maji na baada ya hapo nikaifinyanga ile chupa ili isijetumika tena na kumpatia yule mtoto…
Cha kustaajabisha yule mototo aliikataa ile chupa na kuitupa chini papo hapo. Jibu nikalipata kichwani kwa nini huku nikiwa na wadau wengine waliolishuhudia tukio lile.
Hapo zikazuka stori nyingine ambazo zasemekana kuwa mkoa jirani wa Lindi ndio vijana wengi wamekubuhu kwa tabia ya kuuza maji si salama kwa afya ya binadamu kwa lengo la kujipatia kipato (hususani kwa wasafiri kwenye mabasi ndio huuziwa sana). Sijajua kwa jiji kama la Dar hali ikoje na kwingineko.
Ombi kwa wadau woote wanaosoma habari hii, pindi umalizapo kunywa maji tujitahidi kuzifinyanga finyanga chupa za maji ili kuepusha hii hali kutokea kwako au mwingine.
Nawatakia siku njema.
Wenu Mdau.
J.M
Wenu Mdau.
J.M
Kufinyanga itasaidia labda huko vijijini. Kwa jiji kama Dar, sidhani kama maji feki yanategeme sana chupa zilizotumika. Si mnakumbuka vile viroba vya Power no 1 kutoka malawi? Miaka kumi baada ya kufungwa kiwanda, bado bidhaa hiyo ilikuwa tele Bongo.
ReplyDeleteJ.M asante kujibu wingi wa maswali yangu yaliyokuwa yanakosa jibu kichwani,nini hiyo chupo moja ya mtoto?, mimi nilikuwa darwiki iliyopita nikafikia mtaa wa msasani mtaa wa magunia nyumba iko nyuma inaangaliana na ubalozi wa marekani, wa ima pale ni dampo la hayo machupa matutupu ya kila size, niligundua hilo asubuhi niliamshwa na kelele za wachuuzi na wanunuzi na magari wanapiga kelele wakinadiana hizo bei. Ukweli ile sehemu imerundikana uchafu hup wa hizo chupa hadi panatia kinyaa, nilipouliza ni kiwanja cha nani au ni dampo? nikaambiwa ni kiwanja cha mama mmoja amewakodisha hao jamaa, kwa minajibu ya kufanyia biashara yao, sasa ni biashara yenyewe ni hiyo ya kadhia kwa majirani na uchafuuuu utafkiri uko wapi jamani kumbe msasani sijui watu wa jiji hawajaliona hilo plastic bags kibai kwa ajili ya kutunzia hizo wanazoziita mali wakishatoa mali mifuko inazagaa hovyooo yaani acha tu, sasa uliposema kuhusu hayo maji ya kubumba ndo nikapata jibu ya marundo yale yanafanyiwa nini.
ReplyDeletePili mwenye kiwanja hicho kama hayuko tayari kukijenga basi atuuzie watu wanatafuta sehemu za kujenga mjini pale yeye miaka nenda rudi anaruhusu uchafu uwekwe pale kiwanjani na mjumbe wa mtaa nae anakaa kimya na kuona mtaa wake ulivyomchafu kama uko gulioni.sisemi uongo jamani wanaofahamu sehemu hiyo watapata picha na kujua ni sehemu gani.
Mimi pia nimeuziwa maji feki bus stand Moshi wiki moja iliyopita wakti nasafiri nikitokea Dar,
ReplyDeleteAhsante kwa baathi ya kampuni za maji ambazo zimeanza kuweka 'seal' japo najua inaweza kufojiwa pia.
tuwe makini