nyumbani kwa bayern munchen
shopingi nzito
mtangazaji nyota wa EATV ben kinyaiya yupo vekesheni ujerumani na alipitia klabu aipendayo ya bayern munich. anatoa salamu nyingi sana kwa washbiki wake wooote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. BEN MBONA WAZUNGU WAKUNYANYAPAA?INAELEKEA AWAKUPENDA WAFOTOLEWE DUH!!!!!KAAZIII KWELIKWELI.

    ReplyDelete
  2. mbona hao jirani zake kama wamenuna afu wanataka watimke?

    ReplyDelete
  3. Mbona hao watasha wanaonekana kumtenga kidizaini fulani... wanaepa kimtindo

    ReplyDelete
  4. HAO WAZUNGU WANAONEKANA HAWAKUTAKA KABISA KUPIGA PICHA NA KINYAIYA, EBU ONA HAO WAWILI WALIOKAA KARIBU NAE UPANDE WA KULIA NA KUSHOTO KWAKE WALIVYOINAMA, WAJERUMANI WABAGUZI UKITEMBEA MTAANI UTASIMAMISHWA KUULIZWA PASSPORT, KITU AMBACHO NI KINYUME NA HUMAN RIGHT, MTU UNAMUULIZA PASSPORT PALE TU ANAPOINGIA NCHI KWAKO BAADA YA HAPO SI SAWASAWA, HATA MTU AKIFANYA TATIZO MJINI UNAMUULIZA ID SI PASSPORT SASA KAMA HUNA ID AINA INGINE THEN UNAWEZA KUTOWA PASSPORT.

    ReplyDelete
  5. Kaka! hao wazungu uliwalazimisha kupiga nao picha? Mbona wapozi kama vile walikuwa wanakwepa wasipigwe picha

    ReplyDelete
  6. Yaani unangojea hapo kwenye stopu la dalalala likuchukue kule chumba chako katika mabweni eneo wanakoishi wabeba maboksi? manaake hao vijizee mliokaa pamoja hawaonekani kama mashabiki wa Bayern Munich bali wanaonekana kama nao wanarudi makwao baada ya kucheza bingo!!!au siyo?

    ReplyDelete
  7. Mbona hao akina mama Wazungu wanaomzunguka hawakupenda apigie picha katikati yao? Mambo ya kkulazimisha nini?

    ReplyDelete
  8. hiyopichaya mwishoinazalilisha,kwa wale mlioughaibunia nadhani hiyo body language si ngeni .

    ReplyDelete
  9. WW beni, jimama linajua kweli umetuma picha yake kwa michuzi?

    Nitafutie na mimi mmoja. ua niunganishie maswala na ndugu yetu johnie mashaka kule kwa mjomba Obama

    Kila la kheri, ila usikae mbali na maiwaifu wako mkienda mpirani

    Mmwaga zege Dar.

    ReplyDelete
  10. mshikaji. nadhani akili zinakuruka. kwa niniuache kazi yako unende kuuza kwenye duka la nguo?

    ReplyDelete
  11. Jamani hao wazungu vipi mbona kama walikuwa hawataki kupiga picha na Ben Kinyaia!! au ndio manjonjo ya picha hayo?

    ReplyDelete
  12. Du vibibi vya kijerumani vinakukwepa? Kaz kwel kwel!!

    ReplyDelete
  13. Picha ya chini kabisa yaonekana aliwavamia hao vizee na kulazimisha picha bila ya kuwaomba, maana wanaonekana kumkwepa ila yeye anachekelea tu URODA kibongo bongo.
    Angalia kijana style hizo za kizaramo ukiwaletea watu hapa USA, wanakulima SHABA tuu... kwani utaonekana kama kibaka au gaidi.

    TEXAS.

    ReplyDelete
  14. Looking at the last picture, it looks as if the white grannys are diverting a scud missiles, LOL.

    Body language says a lot!

    ReplyDelete
  15. Mbona wazungu wamempisha wameinama kabisa kuwa hawako naye inaonyesha aliomba kukaa apigwe picha Tozi huyu

    ReplyDelete
  16. Kinyainya,
    Mbona vibibi vya watu vinakukwepa vyote??Haina haja ya kutuonyesha wazungu ndo tuamini uko huko Ulaya.Wewe piga tu picha tutajua uko nje ya Dar

    ReplyDelete
  17. Hallow Kinyaia, Mbona hao wazungu wawili walio karibu nao waonekana kukukwepa? Au ndo ubaguzi wenyewe? check out??!

    ReplyDelete
  18. Hallow Kinyaia, Mbona hao wazungu wawili walio karibu nao waonekana kukukwepa? Au ndo ubaguzi wenyewe? check out??!

    ReplyDelete
  19. Eh! hivi kuvaa vinguo vidogo namna hiyo ndo fesheni Bongo ama kubana matumizi mnashea nguo na wadogo zenu? Afu inaelekea bw. Ben Kinyaa (I mean Kinyanya) Deodorant hajaweka, manaake vibibi vinachapwa na kikwapa mpaka vinaepa. Mnaotupiga madongo kubeba maboksi watu wa majuu, poa...lakini nyie kufuka makwapa kwanini jamani, inamaana Deodorant ni ghali kiasi hicho? Ukipanda daladala huo mtemo wanaofuka masistaduu na matozi balaa...kichefuchefu!.

    ReplyDelete
  20. JAMANI AKILI NI NYWELE.....NCHI ZA WATU JAMANI....MTOTO WA KIENYEJI HUNA WASIWASI UNAFYATULIWA PICHA SIJUI NA MSWAHILI MWENZIO.....ONA RESPONCE YA HAO ULIO JIRANI NAO....UNAFIKIRI WAMEFURAHIA KITENDO CHA KUPIGWA PICHA BILA RIDHAA YAO!......JAMANI MKIENDAGA HUKO NJE MUWE NA NIDHAMU NA MJARIBU KUELEWA CULTURE ZA WATU!

    ReplyDelete
  21. UJANJA UKIZIDI SANA MWISHOE UNAKUWA MSHAMBA...nadhani mmenisoma.

    ReplyDelete
  22. KAKA BEN HAO MABIBI WA KIJERUMANI NI WABAGUZI TU WA RANGI.AFU NA WEWE BEN INAELEKEA HUKUWAOMBA HAO SIJUI WAJURUMANI UPIGE NAO ILA WAWEKE WAZI KUA MTU SASA YUKO IKULU USA NA HAO WAJERUMANI WAKAE CHONJO.

    ReplyDelete
  23. siamini hakuna hata mdau mmoja ambaye ameweza kugundua kuwa picha ya mwisho ni usanii (photo-shopping) tu.

    kwanza, arena hakuna viti vya mbao (juu ya chuma) kwenye dug-out!halafu check the background..ameikatakata tu na kuipindisha ionekane kama jukwaa (la taifa ya zamani). arena ni mzunguko kama yai, huwezi kuona view kama ile..inakera; tunaaibishana hivi.

    ReplyDelete
  24. Tatizo la huyu mtoto ni bishoo sana, na mshipa wa aibu ulishakatika siku nyingi.Ben Ushaelezwa kupiga picha na wazungu ndio tukujue uko Ulaya?? Halafu unakurupuka tu unapiga picha wazungu bila ridhaa yao!!!!watch out my friend, watakurudisha bongo hao!!hawana urafiki, we mwenyewe fikiria anakuja mluga luga mmoja toka shamba halafu anakupiga picha bila ridhaa yako utafanyaje???
    Dogo huo ni ushamba mtu wangu, mambo hayo!!! ole wako uwafanyie wa-marekani ndio utajua kama wao wanatawala dunia au kinondoni.

    ReplyDelete
  25. Tatizo si ubaguzi, ila mtu yeyote yule ukikaa nae jirani akaona unapiga picha hatataka atokee ktk picha yako kwa sababu haimuhusu. Iwe ulaya au Africa, wote hawatopenda hilo. Hata wewe uliyechangia hapo juu, sidhani kama utapenda kutokea ktk picha za strangers

    ReplyDelete
  26. YAELEKEA WEWE MAMTONI NDIO KWANZA UNAKANYAGA HALAFU YALIKUAJE MBAKA UKAWAJAMBIA HAO WAZEE WAWATU SIO KAMA HAWATAKI KUPIGWA PICHA ILA HARUFU YA MAHARAGWE NI NZITO MJOMBA

    ReplyDelete
  27. ukitaka kupiga picha na wazungu ili kulazimisha watu wakujuwe upo ulaya inabidi uombe kaka japo kijerumani noti richabo omba kiingereza matokeo yake ndio inakuwa kama hivyo wanakukwepa kama upepo wenye vumbi.

    ReplyDelete
  28. JAMANI WAOSHA VINYWAA!!KUMBUKENI KUWA KATIKA NCHII ZA ULAYA,UJERUMANI NI NCHI YENYE UBAGUZI WA HALI YA JUUU KTK ULAYA NZIMAAAA!!NA PIA KUNA VITONGOJII BADO MWEUSI AKIONEKANA WANAMUUA,FATILIENI MUWAJUE WAJERUMANI JAMANI,ALIVYOFANYIWA BEN NI KITU CHA KAWAIDA UJERUMANI,NI MA RACIST KINOMA!

    ReplyDelete
  29. WAJERUMANI ULAYA WANAITWA WA-NAZI,NI WABAGUZI ILE MBAYA,HAWATAKI KUMUONA BLACK KABISAA,YANI HAPO WANATAMANI WAMFUKUZEE,MI NISHAKAA NAO HAOOO!

    ReplyDelete
  30. The postures proves that this guy is a gay, nowonder the old ladies dont want to get close to him. Say hi to your man in Germany.

    ReplyDelete
  31. mimi nipo germany hao watu si mchezo..mpaka sasa hayo mambo yapo ila wafanayaje na benn ameshalazimisha..

    ReplyDelete
  32. Huyu jamaa ni limbukeni sana. kwani lazima upige picha na wazungu ndo ujulikane uko ulaya? halafu kama alivosema mdau mmoja hii picha ni usanii tu (photo shoping). mi siamini kibaridi hiki kilichopo saivi mtu anaweza kuvaa mavazi hayo ya summer na kupozi namna hiyo. kaka hiyo picha labda ungepeleka kijijini kwenu ila siyo hapa kwa wanajamii wa ulimwengu. kila la kheri na vekesheni yako hewa.
    mdau, Aalborg Denmark

    ReplyDelete
  33. Beni ukiangalia hata wewe mwenyewe, wakina bibi wanakukimbia kila upande. Ina maana walikuona kana kwamba una ukoma vile.hii ni Sababu, mavazi ya ajabu, shati inayobana, pini mdomoni nk.huku mavazi kama hayo wanajua moja kwa moja siyo kijana wa kawaida ila ni.. homosapiens ....wewe ukadhani ni ujiko, tena unapiga picha kitabasamu kubwa?

    Pili nani alikukuwa akikupiga hizo picha. Haya haya siyo maadalili ya kitanzania, kazi kwako bwana il msalimie rafikiyo. yaani rafiki, girffriend, boyfriend whatever....

    Asante sana kwa picha nzuri

    ReplyDelete
  34. inawezeakana hao kina bibi walikuwa wanakimbiza pochi zao tu!

    ReplyDelete
  35. Picha ya zamani hii.Ujerumani hivi sasa ni baridi na mtu hawezi vaa kama hivyo kwenye picha.Michuzi kwanini unatumika kuhadaa watu?

    ReplyDelete
  36. Comments zote toka juu mpaka hapa mwisho wa comment yangu inaonesha ni jinsi gani Tanzania haiwezi kuja kuendelea kabisa...

    Comments zote ni negative tu, ambapo hakuna hata moja ya kuweza kuungana mkono. Ingekuwa picha ya mzungu basi wabongo wangeweza kutoa comment na kuunga mkono, lakini Mtanzania mwenzao inakuwa ni noma, jee hii ni roho mbaya au?

    Maendeleo ya Mtanzania yana anzia pale jinsi akili na mawazo ya wananchi wake yanavyokuwa, Ukiwa na mawazo na akili nzuri basi ata maamuzi yenu kama wananchi yataweza kuwa mazuri na kufanya kuleta maendeleo ktk Taifa. Lakini sio akili kama zinazo oneshwa ktk hii post ambazo zinaleta Negative na chuki kwa huyu Kijana ambaye ni Mtanzania mwenzenu.

    Kitu ambacho Watanzania mnabidi muweze kujibadirisha ni kuonesha upendo kati yenu, angalieni nchi za wenzenu wao wakitoa criticism basi ni Constructive criticism or Constructive arguments ktk issues ambazo zinaleta maendeleo.

    NaWaKiLiShA.

    ReplyDelete
  37. We anony wa 12.31, hatuwezi kusapot kila ujinga unaofanywa kwa jina la mtanzania mwenzetu. Tukifanya hivyo tutawaunga mkono hata wahusika wa EPA. Huyu bwana kwanza sio mkweli (hiyo sio ndani ya Allianz Arena) halafu kulazimisha kupiga picha na vibibi vya kizungu ni ujinga na hutuungi mkono. Halafu nahisi anafikiri hata huko wanamjua, hao wazungu bwana hakuna kufagiliana ni kazi tu. Acha ushamba bwa mdogo, kuwa simple tu kama wenzako

    ReplyDelete
  38. Daima nitaendelea kusema kama ukifanyika utafiti au kukusanya takwimu za watu waliokuwa na mawazo hasi kabisa na wasiopendana nadhani WaTanzania watapata nafasi nzuri sana.Sijui ni sehemu ya utamaduni wa KiTanzania kuwa negative na roho mbaya.Nikisoma maono kwenye hii blog na blog zingine pia,ni kawaida sana za WaTanzania kushambuliana na kutoa maoni yasiojenga.Nasishangai nchi inakuwa nyuma kimaendeleo maana hivi ndio watu wanavyofikiria.Daima hamna maendeleo kama watu hawatabadikika,na wengine haisaidii hata kama wakiishi nhci zingine,ile sehemu mbaya ya UTanzania na desturi inabakia.
    Ndio maana watu wengine wanaishi nje na hawana muda sana ana kujuana na WaTanzania wenzao maana hawana maana,ingawa huwezi sema wote.Nchi zingine na tamaduni zingine wamevuka hapo,WaTanzania bado safari ndefu.Sasa huyo jamaa kakosea nini kubwa kutuma hizo picha,baadhi mnaanza kuchambua hili na lile,basi na nyie tumeni picha.Wengine wanasema huyo jamaa hayuko Ujerumani mara hii picha ya zamani na kwa nini tufike huko,na tufikiri hivyo?Mimi nadhani WaTanzania tunaweza kufikirii zaidi ya hapo na chambua mambo,tusiwe wavivu wa kutumia ubongo zetu.Kitu kimoja kuhusu hizi blogg unazidi kuwajua waTanzania wanavyofikiri na walivyokuwa negative(hasi) maana hapa hatujuani kwenye maisha ya kweli,watu wako huru zaidi kutoa maoni yao na kujua wanavyofikiri.Kule Tanzania ilikuwa ngumu kujua maana wengine walishindwa kusema bayana,ila walisema kwa kujificha na wanakuteta na kusema vibaya mtu akiwa hayupo hii ni kwa wanaume na wanawake umbea tuu.

    ReplyDelete
  39. Advice: Ungeweka picha ya kwanza na ya pili tu. Ya tatu unajibagua mwenyewe!

    mtoto

    ReplyDelete
  40. KWENI HUYU JAMAA SI NDIYO YULE ANAYEVAA HERENI KWENYE MDOMO? AU NI MWINGINE? BADO ANAVAA? TATIZO LA WATOTO WA USWAHILINI, KILA MMOJA ANATAKA AONEKANE BABKUBWA NA KWAMBA HASHINDWI NA WENGINE. MATOKEO YAKE NDIO HAYA KUPIGA PICHA ZA AJABU AJABU. PLEASE PLEASE PEOPLE OF AFRICAN DESCENT: DON'T IMITATE EVERYTHING WHITE PEOPLE DO. KUVAA HERENI MIDOMONI NI PURE SIGNS OF HOMOSEXUALITY(ORAL S#* STIMULATION). UNLESS OTHERWISE HE IS GUY, THEN MY COMMENTS USELESS. thanks.

    ReplyDelete
  41. Ben kama utaipata hii meseji basi wasiliana nami

    Kitubio Malisa
    Bulgaria

    ReplyDelete
  42. Kitubio Malisa
    Bulgaria
    kjmalisa@abv.bg

    ReplyDelete
  43. Nionavyo, picha ya tatu ina ujumbe maalum uliokusudiwa na Ben na/au Michuzi, ama ambao mtu anapaswa ang'amue mwenyewe. Safi Ben!

    ReplyDelete
  44. we kinyaaaaaa! umemfuata hawara yako ujerumani mmhhh kazi kweli kweli mtoto wa kijaluo kakuchengua angali bro ......

    ReplyDelete
  45. Haya ndo mambo sisi wanaume wa kiafrika tunayokumbana nayo ulaya na hata Uingereza pia.

    Kijana wa kiafrika unanyanyapaliwa hata na dada zetu wakiafrika hapa Uningereza.

    Mfano utaona ukiwa ndani ya usafiri wa treni jijini London kina dada wa kiafrika wanaona bora wasafiri wakiwa wima ikiwa siti iliyotupu ni jirani na mwafrika mwanaumme.

    La kushangaza utaona wasichana na wamama wa mataifa mengine wawe waingereza, wajapani, wacolombia n.k hawaono noma kukaa jirani na vijana/wanaumme wa asili ya kiafrika ktk usafiri wa umma.

    sasa kichechesho ni ikitokea siti tupu imepatikana jirani na mtu asite kijana/mwanaumme wa kiafrika yuleyule dada/mama wa kiafrika atatoka bomba kukimbilia akae ktk hiyo siti.

    Nilijaribu kuwauliza washkaji wangu wa kike vipi mnakuwa hivyo, wanadai wanataka wanaumme wa rangi nyingine wazae machotara n.k n.k?!

    ReplyDelete
  46. Oyaa wazalendo! mbona inakuwa hivyo mmesahau kuwa namna mnavyopambana nae ndio mnazidi kumpa umaarufu huyo bwege anawafanya wote matindiga na mtabaka kununua migazeti ya udaku na kusahau mambo ya maendeleo ktk nchi. Yeye kama kaona akipiga picha na kutoa hapo sawa hata kama ana sababu zake who care`s! Nafikili kuandika mineno kama watu wengine wanaharisha haitasaidia, yeye kama kachemsha kivyake na hata kama anataka kuonyesha kuwa mambo yake poa aje apige changa la macho bongo poa tu wangapi wanaiba na waosha vinywa mpo na mnapigwa changa la macho kama mnavyozidi kumpa umaarufu huyu jamaa kwa maneno yenu mnamuona tindiga. Mimi naona labda mshikaji alikuwa na ndoto ya kufika hapo na kafika tatizo lipo wapi! anaweza akaonekana mshamba kwa namna moja ama nyingine katoa katika web ya michuzi kwa sababu zipi za msingi. Kwani kuna wengine wamefika na kuhifadhi picha zao majumbani mwao na kwa faida zao binafsi, sasa lengo la kutoa picha zake hapo analo yeye na michuzi? Picha zifuatazo sasa, Ben Piga uchi mwanangu tukuone, au ukienda kuangalia mpira hapo uwanjani mimi ni shabiki yako mkubwa mtu wangu, nipigie/tuwasiliane kupitia mail hii mwanangu- Atakua112@gmail.com. Nataka ukifika pale ukamkumbatie golikipa mimi nikuone ktk T.V tuwafunike waosha vinywa mzee ben!

    ReplyDelete
  47. Waswahili bwana, Sijui mnafikiri Ben yupo na hao Wazungu au anataka kupiga picha ili uwanja uonekane? Na pale dukani mnajujae kama Ben anauza duka au ameenda kununua ile t-shirt? Wewe uliyetoa maoni yako wa mwisho unasema wadada wa Kiafrica hawataki kukaa na wakaka weusi labda ni hisia zako tu. Mimi ni mweusi na nafanya kazi London na natumia tube kwenda kazini kila siku na sina ubaguzi wa kusema nikae na nani karibu yangu wala nini. Na kwa taarifa yako mume wangu ni mzungu na tunachukia sana mambo ya ubaguzi wa watu weusi wanavyobaguliwa. Kusema ukweli weusi wenyewe ndo wabaguzi, Ben kakaa pale kutaka kupiga picha hakuna hata mtu mmoja aliyesema amependeza au vipi ni kuangalia hao wazungu tu. Mmefika London mkaona watalii wanavyopiga picha? ni sawa na Wazungu kupiga picha Dar.UBAGUZI, USWAHILI WENU UTAISHA LINI? Badala tuwe ngangali ili tuweze kufurahia maisha yetu na hata Ben kuwa kapata bahati ya kwenda Ujerumani kuona nchi nyingine tofauti mnakaa majungu tu! Achaeni hivyo....

    ReplyDelete
  48. Jamani, kinachomponza Beni ni tabia na vituko vyake hakuna hata mmoja anayemchukia.

    Swali, mlitaka tumuite Beni mfano wa kuigwa?

    Tukimuita mfano wa kuigwa Dr. Shayo tutamuitaje? Jonie Mashaka tutamuita nini?

    Lazima mpime mambo, ingawa hawa ni wataalamu tunaweza kuwaiga kutokana utaalamu wao.

    Hatuwezi kumuiga Beni kutokana na kuvaa nguo zinazobana sawa na za kike, au kuvaa pini mdomoni.

    Vihoja mahakamani !!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  49. Kwa kweli hii blog ya michuzi ni kama kioo amabacho kinaanika mawazo ya watanzania wengi walioko nje.

    Ukiangalia comment nyingi za humu ndani zimejaa chuki na wivu usiokuwa na maana.Ingawa Beni kajiletea, lakini haya yote ni wivu

    mfano mzuri ukitaka kujua chuki hasa za binafsi, mtu awekwe ile mashine kubwa Joni Mashaka, rafiki yangu yako wewe beni itakuwa cha mtoto.Blog zote siku hiyo zitajadili alichovaa siyo aliyoyafanya

    Utajikojolea kwenye nguo kusoma comments anazowekewa.Anawatia waosha vinywa na wabeba boxi kiwewe wakimuona na maendeleo yake, hata afanye la maana watamsema tu, sijui kavaa kofia mara miwani, mara hilfiger, mambo kibao lakini kaka wa watu hajali


    Watu hawapendi kuona mwenzao kapiga hatua ya kimaisha na kufanya kitu positive.

    Kuweni na wivu wa maendeleo mtafanikiwa sana na kuleta positive impact kwenye society.

    Lakini kama mkiwa na wivu mbaya na chuki itakua affect wewe mwenyewe.

    Ukiangalia watu wengi ambao wametoa comment utakuta toka wamefika ulaya hawajafanya kitu cha maana.

    Wengi wako huko miaka 15 na waliondoka huku tanzania kuja kupata elimu huko nje. Badala yake wakaingilia starehe na ubishoo kama alivyo Beni Kinyaha

    Lakini wamesahau ni kitu gani kiliwaleta huko na kujiingiza katika masuala ya kipumbabvu na mashindano yasiyokuwa na msingi wowote.

    Benina wewe, kama unataka ujiko na ulimbukeni wako, mtafute mtaalamu wa Interneti Joni Mashaka a.k.a Obama akufundishe gia za kuingilia interneti, ukiingia kichwa kichwa utaparamiwa na kutoka kimgongomgongo

    Mwenzio kafanya makubwa tena mazuri ya kuvutia lakini waosha vinywa na wabeba boxi wakiona jina lake wanajikojolea kwenye nguo zao kutokana na wivu, lakini yeye hajali, anaendelea na shuguli zake.

    Kazeni buti, na kurudi shule na acheni majungu yasiyokuwa na maana.

    Kidagaa

    ReplyDelete
  50. Mie naona watu karibu wooote mliotoa comments mna wivu unawasumbua kwa uyo kijana, acheni upumbavu watanzania, kwanini hampendani nyie...

    ReplyDelete
  51. Si bure .... Nahisi jamaa alijamba.... sa si unajua mambo ya maharage na mayai ya kuchemsha ...?

    ReplyDelete
  52. hahahahahahaaaaaa kwi kwi kwiiiii uwiiiiiiii,,,kweli wabeba box
    sina mbavu u make my day wow!!ktk hili

    ReplyDelete
  53. Mtu yoyote mwenye akili timamu anaona kuwa wazungu wanajaribu kumpisha Ben apige picha sio kuwa ni wabaguzi.

    Inaonekana kabisa kuwa Ben kaja kibarazani baada ya watu kukaa na akataka kupiga snap yake. Ni tabia ya kawaida kabisa ya binadamu kujikinga namna hii, kama mtu anajaribu kupiga picha bila ya wao kutaka kupigwa picha naye kama hamjui. Labda Tanzania tunapend a kupigwa picha na watalii lakini sio kila mtu anataka snap ulaya.

    ReplyDelete
  54. Mjomba hii ndo mara ya kwanza kutoka bongo nini??? kwi kwi kwi

    ReplyDelete
  55. jamani hebu muacheni kijana wa watu.Picha ya mwanzo hamepiga pale pale kuna studio hapo ambayo inatoa picha hizo mimi nilikuwa huko hivyo naelewa.Kingine hebu amkeni mwanamume kuvaa heleni,vipini nk ni kitu cha kawaida haina dalili ya u-gay.Jamani amkeni!msitoe kasha zisizo na msingi.Kuna ma-gay kibao ambao ambao huwezi amini lakini mjue kuwa hayo ni maamuzi ya mtu binafsi mradi hakuuingilieni maisha yako/yenu.Amkeni jamani huu ni ulimwengu mwingine.Kila mtu anafanya anavyoona ni right kwake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...