
Habari yako mdau Michuzi,Mimi ni mdau niliyoko hapa kwa mama kishule. Katika research zangu za mambo ya FASHION, nilishanazwa kukutana na dada ESTELLE kavaa gauni lilio tengenezwa na kanga inayo toka Tanzania.
Angalia picha nilizo attach. Zi wape insperation madesigner wa Bongo, kwamba kanga inaweza kuvaliwa katika RED CARPET
MDAU NEEMA ULOMI(Mrs Mwanyika)
Textile & River Island Fashion Clothing Designer
Reading
UK


Dada nadhani ulikuwa unamaanisha INSPIRATION na sio "INSPERATION" au sio?Ungetumia tu neno CHANGAMOTO au HAMASA tungekuelewa.Otherwise,asante kwa picha nzuri inayoonyesha kutambulika kwa utamaduni wetu.
ReplyDeletehiyo kanga nimeipenda sana
ReplyDeletePicha nzuri
ReplyDeleteInsperation gani tena Mbona Ally Remetullah sijui kama nimepatia anafanya mitindo hiyo ya kanga na pengine ndio kapatia huko nenda katizame facebook ya jamaa huyo ndio anafanya mitindo hiyo ila ahsante pia kwa kuwafunguwa watanzania wenzako japo tayari ipo hiyo. na pengine na pengine John Legend kamnunulia Estelle alivyokuja bongo akampa Estelle kama zawadi huwezi juwa. sababu hao ni marafiki.
ReplyDeletehuyu dada ni mbongo kabisa wadau so nowonder amejikhangalicious!hata ukimcheki kwenye video ya wimbo wake na kanye west anatabia za dada zangu kina mwajuma wa kule manzese kwa mfuga mbwa(nawamiss sana)
ReplyDeleteNiliingia duka moja wakati wa summer macho yakanitoka nilipoikuta nguo/gauni la kanga yametundikwa, nakwambia moja linauzwa £45. Halafu hayo magauni yametengenezwa Kenya lakini kanga ni made in Tanzania, zile kanga nzito za urafiki kama sikosei. Niliona raha kukuta kanga ya TZ dukani lakini karaha kwa kuwa ilishonwa Kenya na faida yote imeenda huko mpaka na sifa pia.
ReplyDeleteKwa mbali nimeona "Textile & River Island Fashion Clothing Designer" Kama ndio hivyo kwanini wewe usifanye hayo unayo yasema!???
ReplyDeleteTetehet teheh! Inachekesha kidogo sio sana!!!
Hili toto ni zuri acha mchezo!Katika wimbo wake wa hivi karibuni wa "American Boy" kanisuuza ile mbaya!vile anavyocheza kulingana na beat ya mziki,typical afroamerican!typical african!I think she gonna make a very great musical artist in the near future.Simple and Elegand,simply put,"black and beautifull"!
ReplyDelete