hivi wadau hii bendera yetu rangi ya bluu inakaaga juu ama chini?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Du!!!, huu mchemsho, inamaana Kikwete hajaona Hii? Si upo naye Michu?

    ReplyDelete
  2. rangi ya kijani ambayo ni kiwakilishi cha ardhiinakaa chini na kati kati ni rangi za njano,kiwakilishi cha rasilimali na nyeusi kama kiwakilishi cha watu na buluu kama kiwakilishi cha maji inatakiwa kukaa juu( kimtazamo ni kuwa unakuta ardhi(kijani)unachimba (madini)katikati ya maji au matope ambapo watu wanahangaika katikati kutafuta maisha na juu ni maji. hiyo ndio tafsiri yangu kwa mtazamo wangu.

    ReplyDelete
  3. Muulize raisi wetu. Mimi nilifundishwa ina rangi nne lakini sikuambiwa ipi iwe juu

    ReplyDelete
  4. comrade Michuzi hapa ulitakiwa upigane kama kweli wewe mzalendo..ulitakiwa uakti kama kaseba,ulete varangati pale mpaka washangae..."inakuwaje mkosee bendera ya nchi yangu???#***?/#Arggg..r"

    ReplyDelete
  5. THE GREEN ALWAYS STAY ON TOP, BLUE INAKAA CHINI...TULIVYOFUNDISHWA, YA KWANZA KIJANI (MIMEA), YA PILI MANJANO (MADINI), YA TATU NYEUSI (SISI WENYEWE), YA NNE BLUE (BAHARI ZETU). FOR THAT CASE TOENI HIYO MBADILISHE!

    ReplyDelete
  6. Hapo mchemsho!..nakumbuka tulijifunza kuwa nchi yetu inakua kwenda juu na kwenye bendera yetu, hiyo diagonal huwa inaelekea juu kutoka mlingotini...naama ukijua hivyo basi hutasau kamwe!

    ReplyDelete
  7. Hapo mchemsho!..nakumbuka tulijifunza kuwa nchi yetu inakua kwenda juu na kwenye bendera yetu, hiyo diagonal huwa inaelekea juu kutoka mlingotini...naama ukijua hivyo basi hutasau kamwe!

    ReplyDelete
  8. Hiyo bendera haijatulia Kaka Michuzi, bluu hubeba zote za juu. Pole na safari na ahsante sana kwa kazi nzuri!
    Maggid

    ReplyDelete
  9. Mimi niliambiwa kuwa rangi ya bluu huwa inakaa chini.

    ReplyDelete
  10. Hivi tujuulize rangi ya binadamu ni Black au Brown? hizi rangi naona zipitiwe upya sasa..tujuwe ipi ni sahihi na ipi iwe juu na chini. we need format..

    ReplyDelete
  11. kijani juu, blue chini

    ReplyDelete
  12. Sie tuliokuwa chipukizi wa Chama tulifundishwa wimbo ufuatao:

    Beeenderaeee, bendera yetu ya taifa ina rangi nne, ya kwanza KIJANI...

    Nadhani jibu mmelipata

    ReplyDelete
  13. Hahaha huu mchemsho, rangi ya blue inakaa chini na ya kijani juu. Du Michu mchukunuku yaani mpaka imeliona hilo!!. Hapo watu walishakula 10% yao wakafunika kombe! Si unajua sisi ni wajasiriamali wa kufoji!

    ReplyDelete
  14. Blue iko CHINI siku zote. Waliyoipandisha hiyo bendera kwenye picha wamchemsha hasa!

    Green stands for the forests and agriculture. Gold symbolizes the country's mineral wealth. Blue represents the sea. Effective date: 30 June 1964.

    Kuna haja yakusema nyeusi ni kwa ajili gani kweli?

    ReplyDelete
  15. Nadhani ni vyovyote tu mradi rangi nne zipo. We huoni wana jumuiya ya Italy walivyoiweka yao?

    Kama serikali yetu tu anything goes

    ReplyDelete
  16. hii yote ni kwakuwa bendera yenyewe haitambuliki kichwa wapi miguu wapi huwezi kubiruwa bendera ya iraq, saudi arabia , wala ya marekani maana inautambilisho wapi kunatakatikiwa kuwa wapi na kwa kuongezea hata ya zanzibara ukiiibiruwa tu watu tutajuwa hatukuwa makini na mark

    ReplyDelete
  17. Hii inanikumbusha wakati fulani nilipoenda kutembelea museum fulani kwenye moja ya nchi za scandinavia. Kulikuwa na tufe (globe) kubwaaa, mara nikasikia kitoto cha miaka kama sita kikipiga kelele na kumkimbilia mwangalizi(curator) wa hiyo museum. Nilipouliza kulikoni, nikaambiwa kwamba kwenye hilo tufe hakukuwa na nchi ya New Zealand(walisahau kuichora. kale katoto na wazazi wake kumbe walikuwa watalii wa new zealand kwa kweli kale katoto kalionyesha uzalendo wa hali ya juu sana, ikabidi hatua zichukuliwe mara moja kuichora new zealand kwenye lile tufe. KAKA MICHUZI ULICHUKUA HATUA GANI ZA HARAKA ULIPOONA BENDERA YETU IKO UPSIDE DOWN?? Je hao watu wa itifaki wanafanya kazi gani

    ReplyDelete
  18. rangi ya blue siku zote inakaa chini,ikiwa juu inamaanisha nchi yetu imefunikwa na bahari.

    ReplyDelete
  19. Niliambiwa na mzazi wangu wakati ule wa awamu ya kwanza kuwa kila mkuu wa nchi akisafiri kikazi huwa kuna watu toka ofisi mbalimbali wanaotangulia kufanya maandalizi. Sasa hapo inaonekana waliokwenda kule walikuwa vekesheni tu maana hiyo ilikuwa juu kabla mheshimiwa Rais hajatia timu, je hawakuiona? Huko ni kuvunjiana heshima jameni, watu wawajibike!!!!

    ReplyDelete
  20. kuna wimbo tulikua twaimba darasa la 3 ivi,,,bendera ya Tz
    bendera ya Tz,ndio ya kujivunia
    ilianza kupepea,mwaka 61
    hapo inashuhudia,tunavojitegemea
    hapa kwetu Tz,uhuru umechanua
    Muumba wetu rabuka,ijaze yako fanaka.
    ------------
    ------------
    Rangi ya jani kibichi,yaonyesha mbuga zetu.
    manjano ndio madini,yaliyo nchini mwetu
    nyeusi ni yetu sisi,waafrika asilia
    bluu huonyesha maji,yaliyo nchini mwetu
    Muumba wetu rabuka,ijaze yako fanana

    SO KIJANI IKO JUU,heeeeee afu na wewe michu ukakaa na kupiga picha afu basi,,,jaman
    siku tulienda kwa awa watani wetu ktk kikao official,yan bendera za nchi zooote zilikuwepo except ya Tz,weeeee watasahau yan tuliwanyea aswaa na mkwara mzito,waliitafuta adi nairobi na usiku tu ikatundikwa.mana walianza longolongo oooooh tuko nje ya mji sana basi tuache tuu,tulisema NOOO adi muitundike
    nyamafu

    ReplyDelete
  21. Jamani tuwe waangalifu, haya mambo yana maana zake. Kwa Unce Sam (US) bendera ikipandishwa upside down ina maana yake, yani hapo ni kwamba kuna state crisis. Je sisi upside down maana yake nini? Huo mchemsho jamaa wamezingua, kama alivyosema mdau kaka michu ungezua varangati la maana hapo liruke hewani watu wastuke........

    ReplyDelete
  22. NDUGU ZANGU NAFIKIRI HAO WAMECHEMSHA KWENYE KAMBA WAKATI WA KUIPANDISHA WAMEPANDISHA NCHA ,NATHANI WANAOFAHAMU HILO WATANIELEWA.

    ReplyDelete
  23. Blue inakaa chini (kulia) kama bahari ya hindi inavyoonekana kwenye ramani.

    ReplyDelete
  24. Please visit http://www.tanzania.go.tz/ ,utaona bendera ya tz na jinsi inavyotakiwa kuonekana.

    ReplyDelete
  25. Yawezekana pia hiyo bendera imewekwa Kiarabu, kwamba unasoma rangi zake kuanzia kushoto!

    ReplyDelete
  26. Kwa kweli hii inasikitisha sana kuona hata bendera inawekwa ndivyo sivyo.Nadhani wahusika wanajijua hivyo naomba wawe makini hili lisirudiwe tena tafadhali maana linatisha

    ReplyDelete
  27. HIVI KWANI BENDERA YETU INA RANGI? MBONA MIMI SIKUWAHI KUSOMA KAMA BENDERA YA TANZANIA INA RANGI YOYOTE? EH, BASI NAOMBENI MUNIAMBIE HIZO RANGI NA MIMI NIZIJUE NINAISHI DUNIA YA NGAPI SIJUI!

    ReplyDelete
  28. ni sawa,hii inaonesha kuwa sasa hivi nchi inaenda kinyumenyume

    ReplyDelete
  29. Bluu inakuwa chini na juu ya zote ni kijani, hapo ni mchemsho tu kwa kwenda mbele.... Michuzi kwa kuwa huwa hivyo vijivakesheni havikupigi chenga hebu fanya na utafiti mwingine inawezekana hata wimbo wetu wa taifa jamaa wanauimba kwa kuanzia na ubeti wa pili !!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...