Bwana Michuzi,
Hongera sana, sana, sana. Blog yako inaendelea kuwa ni kitovu cha watu kutoa na kupata ushauri. Sijaona mfano wa blog tamu kama hii, yaani ina kila kitu kwa kila mtu. halafu hiyo gia ya kukumbuka ya nyuma aliyoingiza mdau wa dodoma naona imelamba bingo. mie mwenyewe nimechangia mara kibao. raha tupu!
Sasas bwana, Mada yangu haiwahusu waliopo majuu au mikoani, bali Inawahusu TUU wakazi wa JIJI LA MARAHA, Dar es Salaam.
Je, baada ya mtu kupata uwezo fulani kipesa, je ajenge kwanza nyumba au anunue gari? Sasa tupeane mawazo. Ni kipi cha kufanya na kipi kianze na kwa nini? wadau kazi kwenu. Mie nimeanza na gari....
NAWAKILISHA.
JOHN LAIZER,
MWENGE DSM
MI NAFIKIRI KAKA ANGU ULIEANZA KWA KUNUNUA GARI UMEKOSEA TENA SANA LABDDA NIENDELEE KFIKIRI TENA KWENYE GARI UWEZI KULALA KAKA SAWA AU SI SAWA KAKA UKIJENGA NYUMBA UTALALA LAKINI GARI UTALITEMBEZA MCHANA KUTWA?
ReplyDeleteAhsante sana mr john kwa kutupapa kachemsha bongo kidogo
ReplyDeleteKwanza inategemea kila mtu na mipango yake ya kimaisha akisha pata kiuwezo kidogo mwingine anapenda aanze na nyumba
SABABU labda mahali anapoishi anapanga au anataka awe na makazi yake mwenyewe sio kutegemea wazazi au kuendelea kulipa kodi ya nyumba
KWA MI MDAU MWENZENU NIGEANZA NA NYUMBA
MI NAFIKIRI KAKA ANGU ULIE NUNUA GARI UMEKOSEA aNDANI SASA NI KUULIZE SWALI LA MSINGI ,HAPO UKIWA NA GARI YAKO UMEKAA KWENYE NYUMBA YA KUPANGA AU YA URITHI?ALAFU PIGA MAHESABU YA KULAZA GARI CCM KWA MWEZI IKIWA KWA SIKU NI 700 SASA JE IKIWA KWA MWEZI NYUMBANI KWAKO UMEPANGISHA WAPANGAJI MFANO WATATU KILA MMOJA ELFU KUMIKUMI NI BEI GANI?NAWASILISHA MADA MEZA KUU MDAU ABDALLAH NGATUNGA
ReplyDeletesasa ndugu yangu hujachoka kukaa kwny nyumba za kupanga tu?na manyanyaso yote yale?acha ujinga jenga kwanza,,,,,mjini nyumba ndio heshima mwanangu.sio gari sifa za kijinga.ooohhhhh
ReplyDeletehalafu mkuu wa wilaya ya naniiii naye eti jana kanibania comment yangu sijui nae vipi au hadi tutoe rushwa?????haya na hii bana sasa tuone km utanenepa!!
Mbona inajulikana sana, hamna hata haja ya kuuliza, nyumba ni mhimu kuliko yote, wewe vipi?
ReplyDeletendugu yangu, wewe mwenyewe umechemka, utanunuaje gari wakati unakaa nyumba ya kupanga? aibu, ni anasa na kufuata mkumbo, labda uwe unaishi kwa baba na mama lakini kama una malengo ya kuwa na familia baadae ni lazima ujenge kwanza ndipo ununue gari ukiwa kwako, raha ya gari kuwa na nyumba kwanza.
ReplyDeleteSwali gumu sana kwani nyumba, gari vyote muhimu. Lakininami naona gari ni priority ya kwanza kwani inaweza kukusaidia kuwa mobile na kukupa mipango zaidi ya pesa. Petroli isituogopeshe sana kwani tukitumia kwa akili inalipa
ReplyDeleteswali sio gumu wala nini.nyumba ndio muhimu kwa vile ni assetmambo ya gari hayo madaladala yote.
ReplyDeleteSasa ukianza na kujenga huko site utakua unaenda na teksi au?
ReplyDeleteKWANI GHARAMA YA NYUMBA NA GARI ZINALINGANA? KUNA NYUMBA YA MILIONI TATU? AU MNAZUNGUMZIA KIBANDA!
ReplyDeleteANYWAY MI NAONA INATEGEMEA NA HALI YAKO. YOU SHOULD KNOW HOW TO PRIORITISE YOUR NEEDS.
usimuite mwenzio mjinga, inawezeka ana fungu na bado hajafanya uamuzi anatafuta ushauri wenu waosha vinywa.
ReplyDeletemimi mwenye nilipoanza kazi nikapata vijisent flani ivi, nikanunua plot ya 1m ilikuwa mwanzoni mwa 2000 mpaka sasa ujenzi haujaisha na kama 15m zimeenda...lkn nikanunua gari kwa 4.5m, jambo la kuelewa gari la kawaida ni swala la maamuzi ya mara moja unapokuwa na fedha lkn nyumba ya maana huchukua muda jamani,labda uwe fisadi kama ndugu yangu maranda alijenga hekaru mbezi kwa miezi 2...wewe mdanganyika na kima cha chini na 10% za kizushi utaweza? wale waliojenga wajiulize walichukua muda gani kumaliza mijengo yao then ndo mlete kejeli.
Ni kweli inategemea ni kiasi mtu alichopata,mfano mtu kapata milioni kumi,hana kiwanja,sasa hapo jamani kiwanja tu kasheshe,then ndiyo uanze kufikiria kujenga,si utaishia kwenye msingi?Kama deal yenyewe ndiyo moja na ya nadra,basi utabaki kusema tu mitaani,nipo kwenye ujenzi,lakini pesa ndiyo imelala chini.Kwa mtu kama huyu akinunua gari,let's say pickup akapambana nayo mwenyewe kijiweni(huku akimuomba Mungu kitu kibaya kisitokee) kidogo kidogo anaweza kujikongoja akajenga nyumba ndogo na pia kuendelea kuishi mjini.lakini kama ni pesa ya kutosha,hapo nakubaliana na nyie,aanze na nyumba kinachobaki biashara.Mpo hapo?
ReplyDeleteHII NI SAWA SAWA NA ILE HADITHI YA MMAKONDE ANAYEULIZA.....NIANZE CHAI AU NIANZE NKATE?...NIKIANZA NKATE, CHAI ITAPOA...NIKIANZA CHAI, NKATE UTAKAUKA....
ReplyDeleteKAZI KWENU...NYUMBA AU GARI...
INATEGEMEA NA MIPANGO. GARI INAWEZA KUGHARIMU MILIONI 7, NYUMBA MILIONI 30, SASA HAPO MILIONI 7 UNANUNUA KIWANJA TU, TENA NJE YA MJI. INATEGEMEA LABDA HIYO GARI INAWEZA KUKUFANYA UZALISHE ZAIDI NA UKAJENGA AU KUNUNUA NYUMBA BAADAE.
ReplyDeleteKWA MAONI YANGU INATEGEMEA UNAFANYA SHUGHULI GANI NA HIYO GARI NA ULAZIMA WAKE KUWA NAYO. KAMA UNAKAA KARIBU KABISA NA KAZINI KWAKO NA SHUGHULI ZAKO HAZINA MIZUNGUKO, NAONA HAINA ULAZIMA. ILA KAMA UNAFANYIA MBALI NA UNA MIZUNGUKO GARI NI MUHIMU KUWA NAYO MAPEMA.
-MZOZAJI
nyumba first full stop,,,mambo ya kuhama uvunje vyombo,ufagie zamu,music kelele,umekula nini nk ya nini aya??au walipa 1.2,1.5 kupanga why usijenge??
ReplyDeletegari+diesel/petrol kwa mwaka,,,,,
tumieni akili ata km unaprioritise ur things
Nyumba ni muhimu lakini gari ni kitu cha kukusaidia kufuatilia ujenzi wa nyumba yako. milioni 5 unapata gari 3rd hand wakati nyumba hapo ni msingi tu bila gharama za kiwanja mi nimenunua mawili na la wife kisha nikajenga baadae
ReplyDeletegari takusaidia kufuatilia nyumba, shamba, kazini, shughuli za kijamii, twanga pepeta n.k
gari ni short term plans na nyumba ni long term plan
Anony wa hapo juu umenifurahisha. Watu wote mnapoteza muda kumshauri huyu bwana wakati hajatuambia gari lake ni sh. ngapi!! Kuna gari la 4m so its not fair ufananishe gari kama hilo na nyumba. Labda ufananishe hilo gari na kiwanja tena uende Goba au Kerege sio hapa mjini. Ni kuivunjia hadhi nyumba unapoifananisha na gari la less than 15 m. May be it was wise idea to buy the said car coz with the cash you could not construct a house!!
ReplyDeleteSamahani kama nitalonga sana! Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Sioni kama kuna haja ya kumlaumu Laizer wala sioni sababu ya kumpongeza. Swala la kuamua kati ya ama nyumba au gari, mara nyingi kwa wakazi wa Dar huletwa na mazingira yanayomkabili mtu husika. Ukiacha wale wanaonunua magari kwa ajili ya ubishow, natumaini wengi mtaafiki kuwa mazingira na status ya mtu yanaweza kukufanya ukaamua kuanza na gari kama Bw. Laizer.
ReplyDeleteTuanze kuangalia mazingira: Imagine uko pale Mwenge kwa Laizer, unafanya kazi pale NBC Posta. Umejaladia fresh na tai yako shingoni, shati jeupe, unaingia katika ile kikiri kakara ya kugombania daladala pale Mwenge. Ukibahatika tu kuingia ndani, ukicheck shati, tayari limeshakuwa na mabaka mabaka ya uchafu...hapo unaingia sehemu nyeti na smart kama benk. Unaporudi jioni, ukibahatika kupata daladala, unapata mahali pa kusimamia mguu mmoja, ukiweka wa pili chini, abiria wa pembeni anang'aka unamkanyaga. Fikiria umesimamia mguu mmoja toka Posta, ule kwanza pozi kama la dk. 40 kwenye foleni pale Morocco, ndo uje Mwenge. Hapo sijawagusa kabisa rafiki zangu wa Mbagala, Temeke na Gongolamboto. Hebu fikiria ukipata centi zako chache utaanza na kipi? Jipe jibu mwenyewe. Gari sio solution ya kufika haraka, lakini bora uko kwenye foleni, umekaa kwa raha zako, kwa mbali ukipulizwa na kipupwe cha kiyoyozi.
Haya, pia tupo watoto wa town ambao tunaishi kwa mishe mishe za business. Riziki zetu zinatokana na uwepo wetu katika eneo husika kwa muda muafaka. Ukiwa na senti zako chache unadhani utawahi Wazo kufuata cement au Showroom kujipatia japo ka-STALET? Jipe jibu mwenyewe. Ila kwa mwenye hekima, naamini usafiri utakupaisha kimaisha, kodi ya nyumba utalipa, kiwanja utanunua na kujenga utajenga....na tena basi unapotembelea site mambo yanakuwa bwax!
Well, wapo tena wenzangu na mimi wenye ajira mitaa flani, kama TCC, City Group, CCBRT, ambao usafiri unakufuata mpaka mlangoni. Gari ina seat za kulala, waliomo ndani ni wafanyakazi wenza, wote wastaarabu. Kwa kifupi kero yako ya usafiri ni foleni tu ambayo ni ya kawaida kwa wabongo wote wenye za halali na mafisadi. Sasa mwenzangu wa hivi ukipata hivyo visent vyako...automatically mazingira yatakutuma wapi? Kwenye kiwanja, au showroom? Jipe jibu mwenyewe.
Kwa kifupi mazingira yanachangia sana katika maamuzi ya changamoto aliyoitoa Laizer. Ndio maana nasisitiza hamna haja ya kumlaumu wala kumpongeza aliyeamua ama nyumba au gari, endapo ameamua kufuatana na mazingira yanayomkabili.
kiroho safi, kila mtu na mtazamo wake na kila mtu na maisha yake.
ReplyDeleteswali kama hili ni vigumu 'kugeneralize',fikiria tu kwamba jibu sahihi ni kuwa na gari kwanza na kila mtu akafanya hivyo ingekuwaje bararani au kila mtu ajenge nyumba kwanza wengine tutakosa viwanja!!??
jaribu kufikiri kwa busara,kila kitu kinawezekana ukiwa na imani, fanya kimoja na vumilia kingine kwani at the end of the day vyote vitaisha thamani.
kila la kheri
mdau
Kila kitu ni priority ya mtu. Mimi nimeanza na gari kwa sababu zifuatazo.
ReplyDelete1. Nimepangiwa nyumba nzima na shirika ila usafiri walinipa mkopo ninunue gari
2. Nilijaribu kubana ila adha ya daladala ilinifanya ninunue gari kwani nikichelewa sieleweki kazini
3.Ninatembea na vitu sensitive vya ofisi kutokana na nature ya kazi yangu( Kama laptop n.k) kupanda navyo daladala ni risk sana either ya kuibiwa au ya kuharibiwa kwa kukanyagana.
4. Wakati mwingine namaliza kazi saa nne na nusu usiku na tax mpaka ninapokaa ni Ths 30,000 kwa trip
5. Ofisini ninapewa mafuta lita 40 kwa wiki( Mafuta si hela) kama sina gari sipewi.
hizi ni sababu za kunifanya nikanunua gari kwanza. Ila kama wewe umepanga nyumba ambayo maza house ni mkorofi basi ni bora ujenge kwanza, Ila hakuna nyumba ya Million 6, labla chumba na sebule.
JAMANI MSITOE USHAURI KWA KUKURUPUKA TUU,INATEGEMEA NA MIPANGO NA SHUGHULI ZAKO ZA MAISHA,INAWEZEKANA KUWA GARI NDO LINAKUPA ACCES YA KUINGIZA PESA KIRAHISI,LABDA TAXI DRIVER!AU MIPANGO MINGINE TUU YA KUKUINGIZIA PESA ZA HARAKA ILI MAMBO YAWEZE KUWA KWENYE MSTARII!VYOTE VINA UMUHIMU ILA INATEGEME NA SITUATION ULIYOKUWA NAYO,NA SIO KILA MTU NI MSHAMBA WA GARII,YANI UKINUNUA UNASHOW OFF,WENGINE GARI NI KAMA JEMBE!YANI NDO LINAWEZA KUKUINGIZIA BINGOO NA MAISHA YAKAWA TAMBALALE!NA UKIWA NA PESA KUWA NA NYUMBA SIO ISSUE KUBWAA,WATU MNAOGOPAA TUU,MANAKE KILA MTUU NYUMBAA,MBONA NYUMBAA RAHISII TUU,UKIWA NA MIPANGOO KILA KITUU KINAWEZEKANAA TUU!MFANOO MZURIII MUANGALIENII KAKA YETUU OBAMA! IS ALL ABOUT YOUR STRATEGY IN LIFE!JOHN HUJACHEMSHA WALAA NINI,KAMA GARI LAKO NDO JEMBEE WE FANYA MAMBO YAKO TUU!NAKUAMINI KUWA UNAMALENGO.
ReplyDeleteJibu rahisi ni ... inategemea.
ReplyDeleteNyumba ni asset lakini gari sio. Lakini nyumba itakugharimu milioni zaidi ya ishirini kuweza kuhamia bila umeme wala kuimalizia. Gari unaweza kupata ya milioni tano pengine hata pungufu ya hapo.
Kama gari itakusaidia kukuongezea tija ya kufanya kazi na hivyo kukuongezea kipato, tafuta gari kwanza. Lakini haina maana kwamba gari ni muhimu kuliko nyumba.
Angalia vilevile uwezekano wa kutafuta usafiri mbadala kama vile Bajaj na pikipiki ndogo, hivyo bei yake ni nafuu kidogo.
Mie nadhani bora kuanza na gari kwani litakusaidia katika mihangaiko ya ujenzi sidhani kama utapenda kutumia pesa zako kwenye taxi kila siku nasidhani kama daladala zote zafika huko mabonde kuinama kubuka dar inakuwa yakhe!
ReplyDeletePorojo pembeni.
ReplyDeleteJe gharama za ujenzi ni sawa na gharama ya kununua gari?
Hilo gari ni kwa ajili ya nini?
Kwa sasa unaishije?
Kama gari ni daladala inaweza kukusaidia kujenga nyumba taratibu.
Kwa kifupi sidhani kama gharama ya nyumba na gari zinalingana. Kama gari litakusaidia katika kuendesha maisha yako ya sasa na baadae nunua gari la kama ni gari la kutesea basi wewe anza kuchimba msingi.
mimi nafikiria ,nunua gari kwanza,maana mambo ya nyumba ni kuzizika fedha maana kwa fedha ambazo zinahijika kujenga nyumba ni nyingi kuliko kununua gari,na kama utajenga nyumba,basi itakuwa mkusanyiko wa mabanda,sio nyumba inayostahili.
ReplyDeleteINATEGEMEA NYUMBA YA AINA GANI NA GHARAMA GANI, NA GARI YA AINA GANI NA GHARAMA GANI, NA UNAKAA WAPI HADI WAKATI ULIPOKUJIAWA WA KUTOA MAMUZI HAYA. GARI YA MILIANI 3 HADI KUMI HAIWEZI KUJENGA NYUMBA YA KISASA, LAKINI UNAWEZA KUANZA UJENZI NAYO. WENGINE WENYE KIPATO KINACHOENDLEA WANAWEZA KUNUNA GARI KWANZA ALAFU NYUMBA, WAKISEMA GARI ITAMSAIDIA KATIKA UJENZI UKIANZA KWA VILE ANA UHAHIKA WA KIPATO KUENDELEA KUWEPO, LAKINI KAMA HICHO KIPATO NI CHA MGANDO NINA MAANA NI CHA MARA MOJA TU NI BORA UJENGE NYUMBA HATA NI KAMA NDOGO KAMA CHOO JENGA NYUMBA KWANZA GARI WAKATI MWINGI UKIOKOTE TENA.
ReplyDeleteKikwapa cha kwenye daladala kaka haujakosea kwa kununua gari. Jaribu usafiri wa daladala kutoka ferry utaona ukweli wa mambo na harufu za samaki.
ReplyDeleteTotoz bongo kwanza gari masuala ya nyumba baadae kwani si kosa kutumia vema ujana wako kuliko kujaribu uzeeni.
Kumbuka kituo cha basi na minyanyaso yote, demu wa kwanza kupata lift njemba lazima ipige kwata.
Bila kuhusisha uhakika wa mwajiri kuwa na imani nawe rudi nyuma uone minyanyaso uliopa kutokana na kutokuwa na gari. hata taxi driver anajua siri zote pale unaponyatia totoz an kupewa kibarua cha kusubiri usiku kucha kabla ya demu kutoka nyumani kwao kwani hizo ndio stori za kijiweni kuwa lile fala nalipeleka kwa demu na linabaki kungojea demu masaa matatu na nachukua hesabu kiulaini
Vyote ni muhimu ispokuwa angalia kipaumbele mkuu. Kama gari litakurahisishia utendaji ili upate nyumba, anza na gari. Kama nyumba itakurahishia njia ya kupata gari, anza na nyumba.
ReplyDeleteNi muhimu kufanya mambo kutokana na wakati pamoja na mazingira yaliyopo.
MBONA HILI SWALI NI RAHISI SANA. WEWE KAMA UMEPETA UWEZO MDOGO TAFUTA KIWANJA UWEKE MSINGI KWANI KWA KAULI ULIYOITOA INAONYESHA UNAWEZA KUNUNUA GARI KISHA UANZE KUBIP MAFUTA VILEVILE UWEZO WA KUJENGA NYUMBA MPAKA KUMALIZA UTAKUA HUNA. KIWANJA KINAUZIKA GARI BOVU UTAUZA?
ReplyDeleteAh, Ah, aaaah yaani jamaa kanigusa kishenzi, maana nipo ughaibuni na next year narudi bongo, nilipanga nianze nyumba, ila jamaa wananishinikiza ninunue gari, John au umewasiliana na washikaji nini??
ReplyDeleteAhsante sana, wadau wamenifungua macho. Piga ua, naanza nyumba.
Mliro- NY
gari muhimu kwanza litakusaidia kwenda sehemu mbalimbali na kama ni kazini utafika mapema nautapata muda mwingi wa kuwa na familia yako zaidi.
ReplyDeleteKwani gari linalingana na hela ya nyumba? Nymba ni investment lakini gari ni what we need to simplify our lives
Halafu kama ni nyumba bora ujenge na uishi au uweze kuoangisha mambo ya kujenga mansion huko mndenyi na usiishi kabisa hayana mpango na naona yanapitwa na wakati and one always disappointed in a long run
tunazungumzia nyumba, tunazungumzia nyumba ya gharama gani.Nyumba yaweza kuwa ya 10,000/= ( ya maboksi) au milioni 2000/= ( mansion). Na tunapoongelea gari nalo bei zinatofautiana. Kuna gari la millioni moja, na vile vile kuna gari la milioni 500.Hivyo basi kipi kianze kati ya gari na nyumba inategemea sana na uamuzi wa mtu muhusika. Na uamuzi wangu mimi wa kuanza kununua gari hauwezi kuonekana wa kipumbavu. Mfano mimi nilianza kununua gari miaka minne iliyopita na ilinigharimu millioni nne. Nilikuwa nazo cash na niliona nilikuwa siwezi kujenga nyumba, kwani nyumba niliyoilewa mimi siyo kibanda ila ni nyumba ambayo ingenibidi niwe na milioni 40 mpaka 60. Sasa miaka minne baadaye nina bungalow yenye dhamani ya milioni 62. Siyo fisadi wadau ila swala ni kiwango, kila mtu ana kiwango chake.
ReplyDeleteNawakilisha.
For ma side l would like to have the house before car, coz nikiwa na nyumba naweza nikawa na uhakika wa parking ya hilo gari lenyewe. Maana trafic jam iliyopo dar ndo inakatisha tamaa, unakuwa hanatofauti na aliyepanda daladala kwenye suala la kuwahi job. so house first then ndo car bro.
ReplyDeleteNadhani umefika wakati wa-TZ wafahamu kuwa gari ni kifaa cha muhimu kama vile TV, Friji, Jiko, Tochi, Redio nk. Hata kama unakaa kwenye nyumba ya kupanga nadhani TV, Friji, Jiko, Tochi, Redio nk utaacha kununua eti kwa sababu unaishi nyumbaya kupanga.
ReplyDeleteGari kwa sasa ni nyenzo muhimu kama zilivyo nyenzo nyingine nilizozitaja hapo awali.
Hebu fikiria mfano huu,
Unakaa kwenye nyumba yako mwenyewe Mbezi au Bunju au Tegeta kwa mfano, mvua inanyesha kubwa tu na wakati huo huo mmoja ya watoto wako homa imepanda joto lipo zaid ya nyuzi 40, je utaiambia nyumba ikupeleke hospitali?
What if upo kwenye nyumba ya kuoanga lakini usafiri wako ni wa uhakika itakuwaje?
Kwa kifupi unaweza ukatafakari mengi:
Kwa wanaojali muda na kuuona ni sehemu ya mali, basi huamua kuhakikisha wana usafiri wa uhakika wakati wote.
hi ni question nzuri sana maan hata mi mwenyewe nisha fikiria kuhusu kujenga kwanza au kununua gari
ReplyDeleteGari halina deali kabisa, investment bora ni nyumba. kama umefanya kazi sana na una chaguo la kuweka hela zako kwenya nyumba au gari basi no bora uchague nyumba.
thamani ya gari ina pungua ile siku unakanyaga ndani au imetoka show room. wakati nyumba unaweza kuongezeka thamni wakati mdaa unapita.
a sound investment is a house, as it has the potential of increasing in value over time as house prices increase. its level of depreciation is much lower as compared to a car, which literally depreciates from the moment its out of the showroom and its value will never rise on its own.
i believe if ur wise enough a car is a luxury u can have after having a basic necessity like a house.
well...Wadau unajua watu wanaogopa kununua gari sababu watakuwa wansrisk fedha,ni kweli gari saaa yoyote inakurudisha kwenye ground state from maintanance,fuel to accidents,..it takes money every single day,lakini unjue kwamba No life without Risk,and sometimes life is worthy living unless u live dangarously,..so risk taking is best decision sometimes!!Gari ni simplification of life,..na siyo anasa kama vichwa vywa watu wengi wanavyoamini na hii inatokana jamii nyingi ya wabongo gari hawazijui,,watu wachache sana wamezaliwa kwenye magari sasa MTu anajenga hisia kwamba gari ni ANASA n haifai kuipigia mahesabu....well LIFE IS A PROCESS of Change,if you are willing to change u can change if you are rigid then it will take you time to understand n u might die without having a CAR,...GARI siku hizi kama mobile unamiliki kulingana na uwuzo wako,siwezi mimi engineer mzima kupanda daladala harafu nimejenga MSINGI....unakuwa unanipa unnecessary stresses jinsi gani nimalize nyumba.....GET CAR ENJOY N KEEP praying for a better HOUSE
ReplyDeleteMpango wangu ni kuanza na GARI..ukiwa na imani za mwaka arobaini utakufa unapanda madaladala....MDAU,india
MAWAZO MGANDO (ashakum!)...ni ukweli usiofichika kuwa vyote viwili vina umuhimu wake sawia na busara za 'muhitaji'..lakini ndugu zangu wote mmeng'ang'ania katika 'kujibu mtihani kwa kuitarajia marking scheme' ya mwalimu. Mwenzetu ameleta changamoto,na kwa maoni yangu jibu lake lahitajia ‘thinking out of the box’. KInyume chake, wadau mmeshadidia ubishi wa Yanga na Simba, mwasontana vidole! Kambi moja yasema ‘kwanza banda’ na nyingine ‘kwanza mkoko’.. ukipiga urari tatizo liko palepale!..tatizo ni uwezo ama chanzo cha ukwasi (liquidity – ‘ulwa’) miongoni mwetu ili kukidhi kihalali ndoto yetu ya kuwa kiotani mwetu siku
ReplyDeleteNi huzuni na msiba mkubwa kwa uchumi wa jamii yetu, kusikia watu wakijitutumua humu kuhusu kujenga nyumba; Wengine kwa muda mfupi (miaka 4, bungalow la milioni 62 na gari! with all due respect, sikujui lakini hii yaweza kuwa na harufu kali ya ufisadi!) na wale ‘si mafisadi’ kutumia lifetime yao yote. Ni msiba pia kuona kiasi gani cha mtaji ‘ufu’ (idle capital) kimelala katika mahekalu yaliyoko vitongoji vyoote vya Dar es salaam (mbali na majiji na miji yetu mingine) ambayo tumeshupalia kulipia kutoka mifukoni mwetu.
Jamani, fedha/mtaji huo saa hizi ungepaswa uwe unazunguka ndani ya mfumo wetu wa fedha kuwapa wenzetu zaidi na zaidi uwezo wakumiliki nyumba na gari kwa kadiri ya kipato chao cha uhakika kila mwezi. Huo ndio ‘uchawi’ wa mortgage (pamoja na matatizo ya hivi karibuni ya sekta huko marekani ambayo naamini yamechangiwa na tamaa isiyodhibitiwa ya ubepari mkongwe sambamba na utanuzi wa sarafu ya kimarekani bila msingi thabiti wa thamaniye – huu ni mjadala mwingine, siku ingine…). Ndio kusema, kupitia mortgage, haya mazonge tete ya ‘nianze tsai au nianze nkatee’, hayana sababu ya kuwepo. Kwa kiasi kikubwa, pale ‘mheshimiwa’ unapopata ajira ya kueleweka na kutimiza masharti muhimu ya mwanzo ya vyombo vya fedha, basi unaelekea kwa ‘wakala magari’ na ‘wakala nyumba’ unafanya uchaguzi na mambo ni mbele kwa mbele!..kwa kiasi kikubwa, fedha yako ya kodi ya nyumba kwa mfano ingetosha kukupa uwezo wa kuwa na nyumba yako mwenyewe, na uchaguzi wa kipindi cha miaka cha kuilipia..nimerahisisha mambo mengi katika jibu langu (mfano uwepo na uwezo wa wajenzi pamoja na wawekezaji (developers) lakini uchumi wa kisasa wa ngazi yetu hauna budi kufikia hapa (Uganda na Kenya wamefikia hatua hii imeshakuwa zamani kidogo).
Kwa nyongeza/ maoni yangu, licha ya kuhuisha vilivyo ukwasi kwenye mfumo wetu wa fedha (naomba radhi, sina jinsi nyingine ya kusema hili!) hii njia ingepunguza sana ufisadi ikiwa pamoja na rushwa na wizi. Kwa kweli watanzania, kama walivyo waafrika wengi, wako tayari kufanya chochote ili kumiliki makazi yao wenyewe. Hili lachochea sana rushwa. Pia, vijana wengi siku hizi wameweka umiliki wa gari kama absolute necessity na wako radhi kujitumbukiza katika vitendo vya wizi (maofisi) kukidhi haja hii. Endapo wangepewa jawabu la namna hii, ingekuwa rahisi kwao kukabiliana na tamaa hizi. Nnasikia, karibuni sana vyombo vya kutunga sheria vitapitisha miswada juu ya mambo kama ‘mortgage’ ili iwe sheria na nchi yetu iingie katika mfumo, hadi hapo tutakuwa tumeweza kuepuka, naweza kusema, maswali ya kinyonge kama hili…..naomba kuwasilisha: Uzengere
Haitegemei!hili swala liko wazi.watu wote wasio na shule hukimbilia kujenga.kama una shule yako wala usiwe na haraka.Nunua usafiri kwanza ili ikurahisishie kufika kazini na kwenye mambo mengine.Pata kiwanja sehemu yenye good neighbourhood.Jenga kitu cha maana polepole.Wale ambao hukimbilia nyumba hata hawajawa financially stable hujenga nyumba za ajabu sehemu za ajabu,halafu baadae tena huingia gharama mara mbili kujenga sehemu nyingine.Ni suala la kutulia tu!
ReplyDeleteipe roho kitu inayopenda. Whatever makes you happy go for it. Life is just too short to worry
ReplyDeletekujenga nyumba ni mfumo wa kale wa maisha, nchi ziliondelea nyumba zinajengwa na serikali ama makampuni wananchi wananunua kwa kulipa kidogo kidogo morgage,
ReplyDeletehapa bongo mtu anajenga nyumba toka kijana anamaliza akiwa mzee, anakuwa hajaenjoy maisha hajenda Holiday wala nini?
sasa hiyo ni akili na ukifa watu wanagombea kama hawana akili, mkeo anaitaka,watoto nao wanaitaka waiuze hehehe sasa ujinga gani
nunua gari kula maisha ,hujazaliwa uje ujenge nyumba manawane!
Inategemea kama wewe ni mfanyakazi au ni mfanyabiashara
ReplyDeleteKama ni mfanyakazi nenda Benki kakope kama 1.5 milioni kanunue kiwanja nje ya jiji la Dar es Salaam kama vile Goba, Buyuni au Kiluvya(jiji linapanuka) kiwanja kina gharimu kama sh 1 milioni halafu laki tano simamisha chumba kimoja na choo .... halafu hamia ... kaa hapo kama miezi sita huku ukitengeneza matofali kidogo kidogo na baadaye ongezea chumba kingine....nenda kwa mwendo huu huku ukiendelea kukopa kila unapomaliza mkopo mpaka nyumba itakapokwisha(hakitakuwa kibanda kama baada ya miaka miwili hivi)... ukimaliza kabisa ...tulia pumzika kama mwaka halafu jipange kwa ajili ya kununua gari. Hivi ndivyo mtazamo wangu kama wewe ni mtu usiyependa makuu
a house has never been an asset, kwa waliojenga wanalifahamu..a house is liability same as gari kama ni la kutemebelea...uwezo kama upo nyumba muhimu zaidi
ReplyDeletejamani, kwa kuangalia mfumo wa ukuaji wa uchumi wa dunia, utandawazi na ushirikiano wa kimataifa kwa ujumla,nadhani imefika wakati inabidi fanye maamuzi kama wasomi. gari na nyumba vyote ni muhimu lakini kwa kuangalie mwenendo, katika nyakati za sasa ni sharti gari lianze. pamoja na kwamba tunakabiliwa na changamoto za miundombinu, Tanzania haina muda mrefu kabla haijakumbwa na uchawi wa mortgage. pamoja na matatizo madogo yaliyo jitokeza kwa wenzetu kutokana na upuuzi wao wenyewe, mortgage imeonyesha mafanikio makubwa kwa wale walio ifanya biashara hiyo. hivyo basi, kama mtu kweli unaangalia mbele na unasoma alama za nyakati si sahihi kujisumbua kujenga nyumba kwa sasa... lakini gari ni muhimu, safari zako zitarahisishwa, mahusiano yako yataboreshwa na utendaji wako utaboreshwa pia.
ReplyDelete