Mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania Italy ndugu Abdulrahaman A.Alli (tai nyekundu) akimtangaza rasmi mwenyekiti mpya wa tawi la jumuiya ya watanzania Italy mjini Modena.Ndugu Nyalus Pascal Jonas aliechaguliwa kwa asilimia 90% ya kura zote.Tawi la Modena litajumuisha mikoa yote ya karibu ambayo ina watanzania wachache. Tayari mwenyekiti mpya amesha itisha mkutano wa viongozi wa tawi ambao utafanyika siku ya jumamosi,katika mkutano huo mwenyekiti anategemewa kumteuwa kaimu wake na wajumbe wawili wa tawi la jumuiya Modena. Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania kupitia blog anapenda kurudia tena kuwashukuru wale wote waliopata fursa ya kuhudhuria na kufanikisha uchaguzi kwa jumla,na kwa wale wote waliokosa nafasi ya kufika na hata wale ambao taarifa hazikuwafikia kwa haraka waungane kwa pamoja na kuyakubali maamuzi ya wengi.
Mweka hazina Bi Halima akitoa shukrani kwa kuchaguliwa na machache juu ya utendaji wake wa kazi za jumuiya,alisema ingawa itamuwia vigumu kimuda lakini aliahidi kwa jumuiya kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa katiba.
Katibu wa tawi jipya la Modena aliyechaguliwa kwa kura nyingi sana ndugu Mwinyimwaka Khatibu,akiongea machache mara baada ya kutangazwa rasmi na mweneykiti wa jumuiya ya watanzania Italy.Ndugu Khatibu amekuwa akijishughulisha sana na masuala ya jumuiya hata kabla ya kuundwa kwa tawi mjini Modena. kulia ni mweka hazina ndugu Kombo Kajembe na kushoto ni mjumbe maalum kutoka Padova ndugu Zacharia ambae alikuwa msimamizi wa kura. Ndugu Zacharia aliongozana na mkewe na mtoto.
Huu ulikuwa wakati wa maswali
Bi Halima Mwevi (Mrs H.kasongo) alichaguliwa yeye pamoja na ndugu Kombo Kajembe(wa mwisho kulia) kuwa ni waweka hazina wa tawi jipya la jumuiya ya Watanzania mjini Modena.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Hivi Chibiriti pamoja na heka heka lundo hivi kumbe hana kitu huko Italy?!! Sisi tulitegemea angalu angepata ukatibu mwenezi wa huko!

    ReplyDelete
  2. Chibiriti vipi! Au jamaa wa Roma na Napoli wameji-organise wakakusahahu? Maana tungekuona hata kwenye picha star wetu. Tunasikitika sana na huu uchaguzi na hatuutambui kabisa! Ni wa kifisadi kabisa

    ReplyDelete
  3. Bendera yetu ni alama ya nchi yetu; itundikwe vizuri!

    ReplyDelete
  4. italy imedoda sikuizi ITALY enzi zetu bwana enzi za kubamiza mzigo kwa makiro,
    watu mmechokaaaa ile mbaya.
    vipi ile caffee ya napoli ya kibongo bado ipo? HIDAYA ajambo? na pale kwa wa ethiopia Roma train station vipi? pale ndo palikuwa penyewe kwa mitikasi.

    enzi zetu tulikuwa hatuna time ya mikutano watu ni kuvaaaaaa mavalentino na kuspend pesa mkutano? unga tungebamiza saa ngapi?
    mmekosa mitikasi poleni.

    ReplyDelete
  5. dada halima ,mambo ya jangwani girls na akina chiku, zuhura na wengineo.nawakumbuka sana . mdau wa azania , enzi hizo 1983-85

    ReplyDelete
  6. Lakini mlivyotundika bendera ya nchi yetu sio right

    next time jaribuni kuiweka inavyotakiwa

    ReplyDelete
  7. Bi Halima Mwevi (Mrs H. Kasongo) inachanganya?

    ReplyDelete
  8. MICHUZI NA WADAU WOTE

    ANGALIA PICHA YA 2,3,4 NA 5 UTAONA JINSI GANI BENDERAYA TAIFA INAVYOFANYIWA UFISADI. INWEKWA JUU CHINI CHINI JUU.

    HIYO BENDERA KILA RANGI INA MAANA YAKE NA IMEWEKWA HAPO KWA SABABU ZAKE. KIJANI JUU, UTEPE WA NJANO NA MWEUSI KATI NA BLUU CHINI. SIO MUWEKE MNAVYOTAKA NYINYI.

    MAENEO MENGI HUONA BENDERA IKIFANYIWA VITUKO VYA KUGEUZWA GEUZWA. NADHANI KUNA HAJA YA WADAU KUREKEBISHA HILI. KAMA HAMNA UTAALAMU SI VIBAYA KUULIZIA KWA WATU WA SHEREHE NA MAPAMBO. KUMBUKA KUWA BENDERA NI IDENTITY YA TAIFA.

    PILI NASHANGAA KWA NINI MDAU MWENYE MAKEKE, BARAKA WA CHIBIRITI ASIPEWE JAPO MWEKA HAZINA. NADHANI ANASTAHIKI KUFIKIRIWA JAPO POST NDOGO ILI ACHANGIE KATIKA UMOJA HUO.

    ReplyDelete
  9. MICHUZI NA WADAU WOTE

    ANGALIA PICHA YA 2,3,4 NA 5 UTAONA JINSI GANI BENDERAYA TAIFA INAVYOFANYIWA UFISADI. INWEKWA JUU CHINI CHINI JUU.

    HIYO BENDERA KILA RANGI INA MAANA YAKE NA IMEWEKWA HAPO KWA SABABU ZAKE. KIJANI JUU, UTEPE WA NJANO NA MWEUSI KATI NA BLUU CHINI. SIO MUWEKE MNAVYOTAKA NYINYI.

    MAENEO MENGI HUONA BENDERA IKIFANYIWA VITUKO VYA KUGEUZWA GEUZWA. NADHANI KUNA HAJA YA WADAU KUREKEBISHA HILI. KAMA HAMNA UTAALAMU SI VIBAYA KUULIZIA KWA WATU WA SHEREHE NA MAPAMBO. KUMBUKA KUWA BENDERA NI IDENTITY YA TAIFA.

    PILI NASHANGAA KWA NINI MDAU MWENYE MAKEKE, BARAKA WA CHIBIRITI ASIPEWE JAPO MWEKA HAZINA. NADHANI ANASTAHIKI KUFIKIRIWA JAPO POST NDOGO ILI ACHANGIE KATIKA UMOJA HUO.

    ReplyDelete
  10. Hongera Mrs. Kassongo - Zk

    ReplyDelete
  11. KWeli yak ifisadi hata chibiriti hayupo hivyo ndio vikao vya njaa kutafuta fedha tu zakuwachukulia watu. sasa tutasikia mpaka Iraq pia viongozi wetu ila bora hawak uliko wale wauza unga.

    ReplyDelete
  12. Duuuuuuu wazee wa Italy hao (ya joka italio) mbona hawafanani na watu wa mtoni utazania picha Ya watu wa Tunduma au Makambako ..wachovu na wamepauka kiasi hicho kweli Sie wabongo tunatia aibu jamani ...
    Yaani mtu unakaa Italy(European fashion heart ) hata nguo za seli na viatu huwezi kununua au ndiyo mambo yetu ya kutumia hela vizuri ili ukajenge kibanda chako Bongo poleni sana salamu zake B.Lusikoine naona kaamua kumshikia bango Obama....
    Mdau wa Muleba

    ReplyDelete
  13. Naona wameiweka bendera vizuri lakini aliyeishona ndio hakufuata vipimo vizuri ndio maana ikaonekana kama iko squire na iko wrong...lakini ukiangalia rangi za majani zipo juu na bahari

    ReplyDelete
  14. Heri wenye moyo kama wa Abdulrahaman maana wataitwa wana wa kujenga umoja wa Watz- Italia.

    Ole wao akina Maina na timu yake wanaotafuta kuunda matawi ya CCM maana hizo nguvu zao zinatakiwa huku Tz badala ya ughaibuni Uingereza.

    ReplyDelete
  15. WADAU NAPENDA MJUE KUWA HUYU MTU KIBIRITI SI CHOCHOTE HUKU NA HAKUNA MTU ANAEMJUA.WALA HANA CONTACT NA UMOJA WA KITANZANIA. SASA WADAU MNAOMJUA HUYO KIBIRITI MWAMBIENI AWASILIANE NASI KWA SABABU KWELI TUNAPENDA WATU KAMA HAO WANAOWEZA KUCHANGIA MAWAZO.

    ReplyDelete
  16. kuhusu bendera kweli wadau hayo yatafanyiwa kazi .ahasanteni sana kwa hilo.siku ya uchaguzi kulikuwa na tensheni sana ndo maana hata wakuu hawakushtukia lakini tutawafahamisha.halafu huyo mdau kuwa watu wamechoka unashangaza sana wewe inaonekana hujui kuchoka.pole sana kumbe wewe bado unaushamba wa kuvaa,huku watu wamekinai na wanavaa kutokana na shughuli sio kuvaa tu.

    ReplyDelete
  17. mdau wa nov 20 5.37 acha kusema wauza unga walisaidia TZ nchi ilijaa vimini bass wao ndo walikuwa wakwanza kusaidia TZ kwenye mambo ya usafiri na magari makubwa ya mizigo.
    ilikuwa wakirudi fresh ilikuwa ni kula raha tuu ukizingatia enzi zile maisha yalikuwa magumu

    mpaka nguo za thamani ilikuwa hamna bongo mpaka uwe na ndugu ulaya ndo uta hambulia vya thamani.

    ReplyDelete
  18. wewe 11/21 12:34 pm unasema chiribiti si chichite huko and at the same time unataka awasiliane na nyie. AAAAAGGGRRRRRR sasa kama si chochote wewe una muhitaji wa nini.......??????? msione mtu anajulikana na kupewa sifa zake lazima mtafute mahali pa kumkata mguu.....

    Chibiriti simfahamu in personal but it seems to be a very nice and a funny guy to be around ndio maana watu wa hapa kwenye michuzi blog tunampenda. Sasa kama huko kwenu si chochote huku kwenye michuzi blog ni mtu tunayempenda.


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...