BRO MICHUZI,
HABARI?
NAMI NIUNGANE NA WENZANGU KATIKA KUWASILISHA MADA KATIKA BLOG YETU YA JAMII.
MIE BWANA NAULIZA, JE KAULI HII AMBAYO HUSIKIKA SANA KATIKA MASHEREHE YA HARUSI NI SAWA NA JE HUWA INA MAANA GANI?

UTASIKIA MC ANABWATA "MAHARUSI WAMECHOKA WAKALALE WENGINE TUTAENDELEA NA MUZIKI"
HII IMEKAAJE?
AKSANTENI KWA MAONI YENU WADAU.
MDAU KUBEJA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Mpaka harusi kukamilika ujue kuna kazi kubwa imefanyika. Katika western culture utakuta maharusi wanajigharamia wenyewe kwa mambo mengi. Mavazi, pete, ukumbi, keki, vyakula, vinywaji mpaka honeymoon. Hata mahali kama bongo pamoja na michango pia maharusi bado wako responsible na mahitaji yao kwani hutalipiwa kila kitu. Ukiondoa maandalizi pia kuna ule mchecheto wa kuhakikisha kila kitu kiko sawa. Sijui watoto wako sawa, nywele saloons, magari, etc. Kumbuka mara nyingi mambo huwa hayaendi kama unavyopangilia. Hivyo by the time harusi inafika watakuwa wamechoka

    ReplyDelete
  2. Kwenye swala hili naomba kuchangia.

    Moja inawezekana kabisa maharusi wamechoka kweli kutokana na misuko suko ya siku yenyewe mara saluni mara kanisani mara picha huku mmebanwa na foleni sehemu na vile vile kule kusimama muda mrefu etc vyote vikachangia uchovu wa mwili na akili katika siku yenu tukufu kabisa.

    Lakini vile vile kuna fikra nyingine kwamba hawa wanandoa wapya "wanatakiwa wakabariki" ndoa yao ikiwa imehalalishwa na MUngu mbele ya macho ya uma.Ni siku ya kwanza kabisa ambayo wanandoa hawa watakuwa hawafanyi zinaa au uasherati bali watakuwa wanafanya tendo la ngono pasipo hatia kimaadili na kidini pia. Nafikiri wengi wa wanandoa hujerea malengo yao ya maisha katika usiku huu na mambo kama hayo.

    Naomba kuwasilisha hoja..

    ReplyDelete
  3. Na wewe mdau ulioliza sali inaonyesha hujaoa ama kuolewa hujui ile ni geresha toto kwa sababu kwa mila zetu hatuwezi kutangaza tendo kamili linalowakimbiza kutoka holini ina maana maharusi wawahi kwenda kuonjana a.k.a kupeana penzi kama mume na mke, kwa luga ya Kidhungu wansema "Consummate the marriage".Mmmh Usiku huu unakuwaga mtamu sana with soo high expectation.Hata kama watu mlikuwa mnaperform kabla ya ndoa usiku huu una raha yake kujua kuwa unafungua dimba kuanzia hapo mali ni zako waziwazi na bila hiyana ......

    ReplyDelete
  4. chechee! D.c

    We dogo kua uone!najiuliza kuwa we ni mtoto au mwanaume! kaka michuzi ningependelea kama kungekuwa na age limit kupata access ya hii blog! ndio hawa wanatukana wahenga baadae! anyway appart from that kama wewe ni mtoto ushindwe na ulegee take you ass home and study! afu kama ni mtu mzima ushauri wangu tafuta mwanamke wa kizigua um date na ukue uache ujinga wewe shwaini Al-Magharibi Mahlaaah bukh..

    Mdau
    D.C

    ReplyDelete
  5. Hii ni kweli kabisa, and I am speaking from experience. Kumbuka kuwa maharusi huwa wameanza maandalizi ya harusi yao siku nyingi sana. Sherehe ya harusi ni siku yao na hata kama wanandugu na kamati wanasaidia, ni jukumu lao kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Ukiondoa hio physical fatigue, pia kuna emotional fatigue. Kwa maharusi wao wamefunga ndoa, (a lifetime commitment) tofauti na harusi, ambayo ni siku moja ya kusherekea na kuserebuka. Kwa hivyo maharusi wana haki ya kuchoka wakati wageni wakiendelea kujirusha kwenye harusi.

    ReplyDelete
  6. mimi namshukuru Mungu, nimeoa hivi majuzi tu. Kwa kweli ndugu zanguni, arusi ni njema. Wale ambao wanataka wafanye kinyemela, nawashauri wafanye arusi kwa sababu hata hivyo hufanyi wewe bali watu wanakufanyia. Pale unapokuwa na marafiki matapeli ndio mambo yanakuwa magumu. Lakini baada ya arusi na ule usiku wa manane, ni kweli, unachoka saana. Mimi nilikuwa simjui mke wangu mpaka baada ya ndoa, lakini usiku ule nililala fofofo, sikuweza hata kuomba vitu. Na hata ningeomba vitu, nikapewa ningecheza chini ya kiwango, na huenda mke wangu pia angecheza chini ya kiwango chake. ni kweli washereheshaji hawakosei, maarusi wanachoka.
    nawasilisha

    ReplyDelete
  7. Kaka misoup!
    Naomba kwa kutumia Blog yako tukufu kuwaomban ndugu zangu wa Bongo aka waafrika kote barani tuijadili na kuwaelimisha kiundani vijana wa taifa la leo nini maana halisi ya ujamaa na kujitegemea wa mwalimu (jk nyerere) against ubepari(capitalism)na wapi nchi yetu tukufu ielekeze dira yake kwa kutumia mafunzo halisi ya sera hizo mbili kwa kuingalia nchi za Marekani na
    Urusi kwa sasa.
    naomba maoni pevu kutoka kwenu wana blog.

    ReplyDelete
  8. Wee nadhani umechoka. Nenda kalale huko.

    ReplyDelete
  9. hauna points za kuongea? Unaweza ukasoma tu za wenzako

    ReplyDelete
  10. hili ni suali gani? wewe unataka ikaaje? tafuta la maana ufanye, usipoteze muda wako na wetu

    ReplyDelete
  11. hahaha kiswahili ni mafumbi hiyo inama bwana na bi harusi wanaenda ku.....

    ReplyDelete
  12. ofcourse wanachoka, maandalizi yote ya harusi mwezi mzima na siku nzima.na kusimama kusalimia watu na kupewa mkono wa hongera. so lazima wachoke, siku yao ndefu.

    ReplyDelete
  13. Wee anon wa D.C NOVEMBER 19,2008 6:44 P.M.....Yani kidogo nipaliwe na kitumbua.....hao wanawake wa kizigua ni aje dear....ina mana umeoa mzigua na siku yenu ya harusi alikuwa haishi kukupa signals kwamba AMEWAKA MATAMANIO JUU YAKO!!!.....na hizo hela za watu mlizotapeli mnafikiri mlitaka iweje.......HAKUNA BIASHARA YA KUCHOKA.....WAWE WANAENDELEA KUKOMAA HOLINI MPAKA WALIOWACHANGIA WACHOKE MZIKI NA KUONDOKA......KAMA KUNA KUCHOKA BASI WAJIGARAMIE WENYEWE....KHA!

    ReplyDelete
  14. Kaka Michu, mimi naomba kutoa ushauri kwa wadau wenzangu wa blog yako tukufu. Iwapo mtu hana ushauri au anaona swali la mdau mwingine ni lakitoto asito maneno machafu kama alivyofanya madau D.C...Kuuliza si ujinga ila mjinga ni yule anayekaa na ujinga akidhani ni mwerevu...HEKIMA inahitajika sana katika kuelimishana.
    Mdau
    AAM.

    ReplyDelete
  15. Naungana na na ANON wa November 19,2008 7:02 PM. Mimi nilioa muda sio mrefu. Yaani nilichoka ile mbaya. Tulipoenda kulala sikukumbuka kuuliza mchezo. Tehe eheeee, oohoo na hata Mke wangu naye alichoka sanaaana.

    ReplyDelete
  16. dah ,nafuu wadau hata nyie pia mmeona sasa hili nalo ni swali gani?kwanini mtu usikae kimya tu?pumba pumba tupu arrrrrrrrrrrgh,utakuta mdau kama huyu labda alizamia kwenye mnuso wa watu dakika za majeruhi akakuta watu wanaaga sasa kaibeba ndio topic hapa.mdau funga bakuli kama huna la kuongea plzz

    ReplyDelete
  17. Nahakika hujaoa/kuolewa. Subiri siku ukifunga ndoa utatueleza vizuri. Pundamila we. Uliza vitu au lete motion za maana sio upuuzi kama huu. Kenge wa madoa doa. Balozi naomba uwe unatuwekea mambo ya maana sio ya watoto kuuliza mbona mama analiaga usiku kwenye gidha!!!!Muuliza swali, guruguja wa kienyeji wewe. ~~~'''@''Xcsichwiiii!!

    ReplyDelete
  18. Mheshimiwa balozi pole kwa kazi hapo uhabesh, nimeguswa na comment za Anony Nov,202008 2:44PM yaani wewe tu kwa huo mdomo wako waonekana ni mtoto wa uswazi kinoma ninanukuu baadhi ya maneno kama guruguja,,,damn shit funga mdomo wako kwani lazima uongee!!!

    CHANGARAWE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...