Rais wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,(mwenye kibandiko kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Carl Bro ya nchini Denmark Ole Alenker,alipotembelea ujenzi wa Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar jana,katikati ni Mkurugenzi wa shirika la Bandari Mustafa Aboud Jumbe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kisheria Hawa watu wote walitakiwa wawe wamevaa safety clothes (PPE) Kwa vile ni sehemu ya ujenzi (Construction site)naona huyo Mzungu tu ndio amevaa hard-hat, ikiwa hata Raisi ama washauri wake hawalijui hili basi safari ni ndefu sana!!!! si ajabu wanafunga mikataba mbofumbofu, iwapo simple things kama uvaaji hawaelewi, wataelewa wapi kufunga mikataba yenye term&conditions zinazohitaji macho makali na vichwa vilotulia?

    ReplyDelete
  2. Na wewe Anoy unayesema raiai hajavaa kofia la chuma usitubabaishe.

    Hiyo inayojengwa ni barabara ambayo iko chini siyo jengo la ghorofa kiasi kuwa kuna vitu toka juu vitaporomoka viponde kichwa cha Raisi.Hiyo kofia inavaliwa kujilinda na vitu vya kutoka juu.

    Usiniulize kwa nini huyo mzungu kwa nini kavaa kofia la chuma wakati inayojengwa ni barabara.Jibu ni rahisi ni kuwa ushamba wake ndio unamsumbua.Anafikiri kila mahali hata kama unapiga lipu chini lazima uvae kofia.Mzungu huyo naye mshamba tu.Kwani hamna wazungu washamba?

    Mwacheni Karume wetu na baraghashia yake ya mtumba aendelee kukagua barabara.

    ReplyDelete
  3. Mtoa maoni acha ushamba, we lazma utakuwa wa Mtakuja weye! hata barabara inahitaji kofia kumbuka risk haitokani na kuporomoka kwa vitu tu hata vijiko vinapogeuka vinaweza kukugonga kwa hiyo mtoa maoni wa kwanza yuko right hata kuteleza pia unaweza kuangukia rough surface ukaumia kichwa. Acha pararira inabidi Karume na wasaidizi wake waende shule !

    ReplyDelete
  4. mtowa maoni wa pili "wajinga ndo waliwao" hufikiri jee kama katika kutembea yao hapo mtu anaweza akalikwaa tofali, chuma au zana yeyote ilokuwa karibu na akaanguka na kugonga kichwa kwenye machine yeyote ilio karibu? tena PPE sio tu kofia hata na viatu ona walivyovaa, hapo wakilikwaa tofali na kuvunjika vidole au mguu watamlalamikia nani?

    ReplyDelete
  5. rais wa wapi?

    ReplyDelete
  6. mi kanifurahisha mzungu alivyovaa tu, mana yake simple kishenzi, watu wameniga Kaunda suit zao, yaani anajua kabisa rais wa zenj anakuja na wakubwa wengine, aah hataki tabu, katinga kaptura,,tena kawaheshimu kweli na hilo shati, angeamua angewatilia ki singland kabisa, duuu mzungu jamani tumuacheni awahi ameshatupita kwa mengi, waafrica tuna akili sana na ujanja mwingi lakini sijui TATIZO HASWA ni nini....

    ReplyDelete
  7. SIS WA-AFRIKA TUNAMATATIZO GANI? HATUJIAMINI, KILA ANACHOFANYA MZUNGU TUNAKIONA KIZURI, TUNAVYOFANYA SISI WENYEWE HATAUFANYEJE KINAONEKANA KIBAYA, TUACHE ULEMBUKENI

    ReplyDelete
  8. kaka michu (balozi)naomba ufikishe salamu zetu kwa rais wa zanzibar kwamba hatuna haja sana na bandari kwanza atujengee uwanja wa ndege wa kimataifa wadau tuliokuwa majuu tunapata taabu saana tukitaka kuja home town

    ReplyDelete
  9. Engineer mzungu kavaa kaptula. Vaa wewe Mtanzania kaptula kama hujaona kesho wanakutoa u-engineer. Wanataka mkanda nje ma-engineer wa kibongo na mikono mfukoni. Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...