katika kuepusha usumbufu pamoja na ajali kwa wataotumia majengo ya machinga complex yaliyopo ilala, kidaraja kimetengenezwa kuunganisha majengo mawili kati ya matatu ambayo wmachinga takriban 10,000 wamejengewa kufanyia shughuli zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. MMh, haya, hako kadaraja!!! tusubiri kukabwa na vibaka hapo. Sijui!!!

    ReplyDelete
  2. Mzee wa Zain,asante kwa kutupa habari za jiji letu kongwe,kweli bongo tambarare,wasiwasi wangu ni "parking",miundombinu ya maji taka/maji safi (mvua ikinyesha kidogo tu hapo ni bahari) je vimezingatiwa? Na upanuzi wa barabara za kuingilia hapo? Maana hapo mahala pana foleni mbaya kutokea pande zote (iwe Chang'ombe,Ilala kwa Kandoro,Ilala au Shaurimoyo)! Mkuu wa wilaya ya nanihi wakumbushea wakuu wenzako wa jiji hayo yazingatiwe?

    ReplyDelete
  3. We annon Nov 16: 11:56 issues za parking si kubwa kuliko zingine. Kwanza wewe una gari gani la kushindwa ku-park wenzako wanapo-park?! Acha uzushi wako. rudi bongo achana na box hizo.
    Kinyesi hata ukienda India kuna mito na mabwawa ya sewage. Bado wanaendelea. Ndiyo maana bidhaa ya India au China ni cheap kuliko ya EU. Eu lazima i-comply na standards zote ikiwemo ISO zote mbili.

    Miundo mbinu, wewe umekaa uko ulaya juu ya box unasubiri zamu ya kulisuma ndani, unadhani nani atakutengenezea hiyo?

    ReplyDelete
  4. Wadau naomba mnifahamishe hapo ni Ilala sehemu gani? maana kila nikiskuti sipati jibu kwani nimeondoka Ilala kitambo kidogo

    ReplyDelete
  5. Hapo ni Ilala karibu na uwanja wa Karume.
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  6. Mwenzetu huwa hurudi nyumbani likizo? Au mambo hayajakaa sawa, pole.Wenzio huwa tunarudi kila tukipata likizo.

    ReplyDelete
  7. Hapo Balozi umetupiga fix.Ha!! kwani leo tarehe ngapi? isije ikawa tarehe 1/4. Hiyo barabara imekatiza wapi, Uwanja wa Karume au kwa Makofia?

    ReplyDelete
  8. wewe unayesema unarudi nyumbani kila likizo acha porojo unaishi kigali? Taja jina tukulumbue hata mbwembwe mtu kauliza mpe jibu hujui funga domo

    ReplyDelete
  9. JENGO HILI LIKO MTAA WA LINDI NA KAWAWA ILALA. HTA HIVYO HAINGII MTU HUMO NDANI ZIPO SABABU TELE ZILIZOANDALIWA IKIWA KUBWA ZAIDI NI ILE WATEJA WENGI WAKO CHINI HIVYO UWEPO UTARATIBU WA KUHAKIKISHA KUWA WAPITA NJIA WANAPANDA GHOROFANI, SI UNAJUA TUNAVYOJUA KUDEKA NA UCHAGUZI SI HUO UNAKUJA.

    ReplyDelete
  10. Michu,hivi majuzi nilisoma mahala flani kwamba baadhi ya wahandisi wa ujenzi walieleza wasiwasi wao kuhusu usalama wa jengo hilo,hususan wembamba wa korido zake na ngazi.Je ina maana ushauri huo wa kitaala umepuuzwa au ndio tunamtega Mwenyezi Mungu?

    ReplyDelete
  11. Hiyo barabara imekatiza yalipokuwa makaburi ya Wajapani (imejengwa double-road kuunganisha barabara za Uhuru na Nyerere). Licha ya kwamba barabara hiyo imejengwa juzijuzi na hapo kwenye picha imeonekana vizuri, lakini barabara hiyo imejaa mchanga mwingi, ni chafuutadhani ina miaka 10. Wasi wasi wangu ni kwamba muda si mrefu tutaanza kushuhudia mashimo japokuwa sina hakika kama hayapo.

    ReplyDelete
  12. Iwe machinga complex kweli, sio tukute maduka makubwa makubwa ambayo tayari yana majina mjini

    ReplyDelete
  13. naona annony wa 10.52 ndiye uliyeuliza swali maana ume panic ile mbaya na bila shaka umejilipua kurudi kwenu huwezi ,huo ndio ukweli. Mbwembwe siachi na jina sitaji.

    ReplyDelete
  14. Rudini nyumbani nyinyi mnaona deal sana kupiga BOX huko kwa watu mtafikiri mabeki tatu......Bongo tambarare sana tu.

    ReplyDelete
  15. Lobaaaaa ni wakati wa loba za mbao kunako darajani hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...