Mh. Balozi wa Zain
Napenda kutumia fursa hii kufungua mjadalawenye kichwa cha habariMAPISHI NDANI YA NDOA.
Kwa wale walio ndani ya ndoa na unampenda mkeo sana, ikiwa mapishi ya chakula anayopika mkeo hujaridhishwa nayo, nina maanisha ladha ya chakula. Jinsi gani utaweza mshauri na ili pawe na amani ndani ya nyumba? kwani wanawake wengi wa kiswahili ukimwambiakuwa hawezi kupika au ajirekebishe au umfundishe, unazua mzozo.
"Utasikia wewe mwanamume una gubu sanaunasema chakula sio kitamu, Haya...Nenda kale huko wa
napo kupikia chakula kitamu,au atakuambia huko wanakokupikia hawajakuwekea leo chakula?"Lengo lako lilikuwa ni zuri tu, kuwa ungependa ajirekebishe au aboreshe mapishi yawe matamu.Wana blog ya jamii naomba mnisaidie mie mwenzenu
MdauMpenda Misosi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. mara nyingi sana huwezi ukaamka asubuhi ukaanza kukipenda chakula . lazima ni chakula unakipenda siku nyingi na kimezoea mwili wako . Ni muhimu saaaaaaaaana kuoa mwanamke aliyeelimika au ambae ametoka kwenye familia yenye usomi wa mlo otherwise ukioa mswahili ndio utaishia machapato na michuzi asubuhi baada ya kupata oatmeal unaanzishwa na vitumbua na supu sasa hapo arteries zako zitajaa mafuta .
    Wamnawake wengi sana wanambiwa mwanaume kula hiyo ilikuwa zamani . kama umeoa watu wapwani huyo maisha yake yote kajifunza nazi, nyanya kopo, na spices zisizokuwa na mbele.
    SHULE pia walizosoma kama mke wako alisoma KIFUNGILO huyo mlo anaujua kuanzia oatmeal to wheat bread ,rain bran breakfast , MCHANA maharage , dengu , samaki , ndizi(za kuchemsha) na majani ya kujaa bakuli, usiku makande, lamb , chicken .VIBURUDISHO ilikuwa lapton tea , green tea, chai ya kichina .
    MATUNDA ya kumwaga mpaka yalikuwa yanabakia ya nguruwe.
    UNAHAKIKISHA UNA 20 GRAMS OF FIBRES PER DAY .
    UKISHAFIKA MIAKA YA 30 VITUMBUA NA MAANDAZI NI KULETA MAGONJWA MAANA DIGESTIVE SYSTEM HAIFAI KITU

    ReplyDelete
  2. NDIO MAANA WATOTO WAKIFUNGILO MASHAPU NA WAKO UP TO DATE SANA . WAKIRUDI LIKIZO WALIKUWA WANANGAA LAKINI WANAJIDAI HAO KUPITA KIASI . WATOTO WA 1990S ENZI ZA SISTER FIDESTA WAKATI HUO WATOTO WAVIGOGO TU .
    SASA HIVI WANAKWENDA ULAYA WATU WAKAWAIDA NDIO TUMEACHIWA INSHALLAH

    ReplyDelete
  3. imeandikwa wapi kama katika ndo mke ndio apike?

    ReplyDelete
  4. KWANINI UNANGOJA MKE AKUPIKIE????
    KAMA SI KITAMU BABU INGIA JIKONI MWENYEWE.

    ReplyDelete
  5. Unajua ni nini wanawake wanakasirika kwa sababu wanaume zao hawatumii kauli nzuri katika kuwarekebisha we kama chakula hakikuvutii kaa chini na mkeo mueleweshe vizuri hata kama ni kumsaidia hata kumpeleka akajifunze nutrition kidogo sio mbaya tatizo la wanaume kauli mbaya kama mtu ni muelewa ataelewa tu.

    ReplyDelete
  6. IKIWA SIKU MKEO KAKUPIKIA VIBAYA UJUE KACHOKA KUINGIA JIKONI KWAHIYO WEWE MUME UWACHE UBAHILI WAKO LAZMA UMUWEKEE SIKU NYENGINE KWENDA KULA OUT( NJE) MAHOTELINI SIO KILA SIKU KUMTIA JIKONI MWENZIO
    NA UKIRUDI SHUKURANI HUNA UNAANZA KUSEMA CHAKULA KIBAYA KUMBE UMESHASHIBA MIKUKU YA KUKAANGA NJE NA HAWARA YEYE UMEMNUNULIA SEMBE KILA SIKU NA SUKUMA WIKI UKIBADILISHA NI VYAMA VINGI AU KALIKITI...

    ReplyDelete
  7. KWASABABU HUMPELEKI AUT NDIO MAANA
    AKAKUPIKIA VIBAYA SOME TIME....
    WANAUME WACHENI KUWAFANYA WAKE ZENU WAFANYAKAZI WA NYUMBA ZENU IKIWA SIKU CHAKULA HUJAKIPENDA BASI MWAMBIE MKE WANGU LEO TWENDA TUKAJICHANE MIKUKU KULE KONGO BAR....

    ReplyDelete
  8. Wewe anon wa kwanza umesoma kweli hilo swali au? Maana badala ya kujibu swali unaanza kujisifia mlivyokuwa mnakula makande na burga (kizungu ndio mnaita oatmeal) huko Kifungilo, nje kabisa ya mada. Nahisi nyie ndio wale wale anaowasema huyo jamaa kuwa hamjui kupika, sababu ukitoka boarding unarudi kwenu unamkuta housegirl ndio mpishi mapishi ya kijijini, saa ngapi utajua kupika mahanjumati mwaya! Nyie ndio watoto wa uswahilini wanawabebea waume zenu kiulaini kwa kukazania madayati yenu kumbe kupika ZERO. Unaweza kupika chakula kizuri tena chenye virutubisho vyote na kina ladha bila kuathiri afya ya mumeo, alokwambia kupika vizuri ni kuondoa virutubisho au ndio uswahili nani? Basi uwe unatazamaga hata vipindi vya Nigel au nunua vitabu vya mapishi dada!

    Hiyo moja ni kukutia adabu kwa kututukana watoto wa uswahili.

    Pili kwa kaka uliyeuliza swali, na kwa wakaka wengine pia, kwanza unataka kuoa mke ili awe mpishi wako (cook), washing mashine, na trekta lako ndani au mke wa kukupa raha za dunia?

    Kwa kukusaidia tu kama lengo ni kupata mwenza wa kuishi naye na kwa siku anazokuwa nyumbani au kama ni mama wa nyumbani na anapika basi mapishi yanateleza au ndio umeoa mtoto wa geti kali au alisoma kifungilo, pika naye chakula unachotaka! Sijui kama umenipata, maana yangu ingia jikoni wewe na mkeo halafu mpike wote hicho unachotaka upikiwe chenye ladha ili na yeye huyo bibie afahamu test zako, yaani ni nini unapenda kwenye chakula. Kwa sababu mpaka ufikie uone kuwa hiki chakula kimepikwa vibaya utakuwa unajua tu mapishi mazuri, na kama hujui nunua vitabu vya mapishi na vitu siku hizi vimejaa tele madukani vya kunogesha chakula, ingieni jikoni mkalangize bibi na bwana. Sasa wewe ukipika chakula kizuri na kitamu lazima tu huyo mkeo ataona aibu na kama ni smati atajirekebisha au ataiga kutoka kwako, lakini na kama ndio dizaini ya kubinua mdomo basi kama ni hivyo kula hivyo hivyo utakavyopikiwa kuepusha shari. Lau kama muislam kaoe mke wa pili mtoto wa uswahilini akupikie mahanjumati!!!! Hehheheee!

    ReplyDelete
  9. Mke wangu wangu hajui kupika kunizidi mimi hilo analitambua na mimi pia natambua hilo. Kinachoendelea hapa kwetu nikufundishana kwa upole na maisha hayana dosari. Mbinu moja ni kwamba usimtukane mkeo au kukejeli kama kweli hajui kupika. Muonyashe chakula kinavyopikwa na akiri kwamba wewe unajua kupika zaida yake. Usichoke kumuelekeza kila anapohitaji msaada hayo ndio maisha. Hao wanawake wa kifungilo hamna kitu hizo ni hadithi tuu. Dada zangu wawili wamesoma kifungilo lakini kila siku nawashangaza. Mnoja wao alisha shangaa jidini nyumbani kwangu akidhani kua ni sabuni hii siungo. hIVY MSITU DANGANYE UPISHI VILEVILE NI KIPAJI

    ReplyDelete
  10. Hii issue ya msosi ni balaa kwa wanawake wa kiswahili maana hawapendi kuambiwa walau chumvi imezidi kidogo. Tabia za unafiki unaosababishwa na malezi yanayosisitiza kutokuwa wazi na kusema ukweli vinatugharimu sana waswahili. Mama anadhani ukimweleza kuwa msosi wa leo umepinda ni kwamba kuna sehemu unapikiwa na hivyo unalinganisha na wake!!! Hajui unaweza ukanyamaza ingawa hujaridhika ili kuondoa shwari tu.
    Sio lazima mama akupikie, lakini malezi ya Kiafrika yanawafanya wanaumme wengi wasijue kupika kwa sababu walinyimwa nafasi hiyo utotoni na mama zao.
    Nadhani wanaume wengi hula misosi wasiyopenda kwa gharama ya amani ya familia vile mama hapendi kuambiwa huu leo sio wenyewe

    ReplyDelete
  11. ushauri wangu na maswali kwako ni hivi je hicho chakula unachotaka kiwe kizuri unaleta vikaangizo vyote? Isijekuwa unapeleka kila kitu kwa bibi mdogo lakini unategemea kuwa nyama na mchele tu basi kwa mkeo atamake miracles chakula kiwe kitamu. Think about that.

    Pili kwanini usipike mwenyewe kama unapeleka hivyo vikaangizo na bado chakula hakinogi basi ingia jikoni.

    At first kila ninachopika mume wangu alikua anasema mama yangu alikua napika hivi , mara alikua anaweka vile...Siku moja nikamkalisha kikao nikamwambia first I am not your mama, second kama unamiss chakula cha mama yako mlete huku aje akupikie kila siku, third, the kitchen is open you have the right to cook however you like. Mpaka sasa hivi ninavyoongea mimi napika mara chache sana...tumeshift majukumu mimi ni cleaner yeye ni chef...

    Sasa ushauri wangu ni kuwa kama unaona huenjoy chakula ingia jikoni. kam mmepanga kwa mama mwenye nyumba chumba kimoja na jiko liko nje wew wala usitie aibu ....mambo ya zamani ati mwanaume haiingii jikoni. Lwani mkeo akiumwa nani anapika???? Au inakua takeout kila siku?

    ReplyDelete
  12. nimekunwa sana na mada ya leo. Mke wangu sijui nianzie wapi, hajui kitu kabisa. Lakini yeye anajiona bonge la mpishi.sijui nimwambieje?

    ReplyDelete
  13. Mdau mpendamsosi pengine na wewe hujui kupika chumbani!! Ushauri wangu kabla hujalalamika kuhusu chakula jihakikishe na wewe mapishi yako ya chumbani yako kisawasawa.

    ReplyDelete
  14. Western culture iko tofauti ambapo mke hatarajiwi kuwa mpishi. Usipokuwa makini mnaweza kukaa hata mwezi hakijapikwa kitu. Ni mwendo wa kufix sandwiches etc au ku-order. Hata kama ukiwa na mtoto wa kiafrika inabidi saa nyingine uhimize kwa angalau kusaidia kukatakata nyanya na vitunguu. Sasa ukiwa katikati ya mechi kama hiyo ndipo unapoweza fungua domo lako na kusema mapishi siyo matamu na tena kwa vitendo upike mlo wa mfano.

    ReplyDelete
  15. asilimia 80 ya waliotoa comment katika hii mada ni gender discriminators...
    mna assume kuwa mwanamke ni jiko hizo ni mila za kizamani ndiyo maana chakula hakipandi!
    kupika siyo kipaji ni mazoezi!
    mimi mke wangu alikuwa mtoto wa geti kali aliyekulia southern africa nimemfundisha kupika na anapika kunizidi mimi.
    tumenunua vitabu tumeangalia vipindi katika tv tukiwa na muda na matokeo yake tunayaona.
    acheni hizo za kizamani eti mke lazima apike.
    halafu kuna mshamba mwingine eti anasema mpenda misosi labda hajui kupika kitandani.
    there is no connection between the two but there is an advantage in a relationship if the bed games are good.
    halafu kama mnaandika kiswahili andikeni kiswahili fasaha siyo kusema hivy badala ya hivi
    pia kama mnaandika kiingereza andikeni kiingereza vizuri
    siyo kusema test badala ya taste.
    mnaboa sana wabeba mabox ndiyo maana shule haipandi!

    ReplyDelete
  16. HAHAHA, KAKA NANI KAKWAMBIA KAZI YA KUPIKA NI YA MWANAMKE PEKE YAKE? MIMI NI MWANAUME NA NINAPIKA SAFI SANA TU KWA HIYO KAMA WEWE UNAJUA MAPISHI MAZURI NA MABAYA MFUNDISHE MWENZA WAKO, USHAURI WA BURE

    ReplyDelete
  17. Mtu aliyetoa mada hii nampa pole kwanza kwa kuachwa na wakati. Katika enzi hizi useme kazi ya kupika ni ya mwanamke sio sawa maana kila mtu anawajibu huo ukubali ukatae kila mzazi anajitahiji kumpeleka shule mtoto wa kike na kiume apate elimu ili aweze kuishi vema. Wanawake nao wanafanya kazi nyingine acha zile za nyumbani ikiwa ni pamoja na kupika.Kilicho muhimu ni kujadili jinsi ya kufanya vizuri kwa yale familia isiyo pendeza nayo kama chakula hakina radha basi kuzungumza jinsi ya kufanya au toa mfano kwa familia jinsi unavyopenda radha ili kila mmoja arurahie sio mwanaume tu wote pamoja baba mama na watoto. Lakini kusema mwanamke hajui kupika nimrekebishe vipi? Huo ni umaskini wa mawazo kwa nyakati hizi

    ReplyDelete
  18. Kuna baadhi wamechangia mada hii kwa hasira,oh mara imeandikwa wapi kuwa mwanamke ampikie mwanaume? Nashindwa kuelewa mtu kama huyu anauelewa utamaduni wa mwafrika au la na isitoshe sio kila kitu ni mpaka kiandikwe ndio kieleweke. Kina dada wa siku hizi ndio wanakuwa na mawazo ya namna hii mnajiona mko juu na bila shaka ni sababu mojawapo inayochangia ndoa za siku hizi zisidumu. Kina dada mmekuwa ni "headache,BP,everything". Kwa kifupi mnaboa japokuwa inabidi tuwe na ninyi coz bila ninyi probably hatuwezi,may be yes,may be no.

    ReplyDelete
  19. Mheshimiwa Mkuu wa wilaya na balozi Michuzi..

    Kuna kitu watu hawaelewi hapa. Moja Mungu alipowaumba Adam na Hawa alimaanisha wajaziliziane kwenye mapungufu(complementing each other).Kuna vitu mwanamke atavifanya vyema kuliko mwanaume na vile vile kuna vitu mwanaume atafanya vyema kuliko mwanamke.

    Kwa mantiki hiyo basi mwanamke amejaliwa karama na uwezo mkubwa katika kuendesha mambo ya nyumbani kusimamia usafi, kulea watoto, upishi na mambo kama hayo ili hali kina baba wamejaliwa zaidi kwenye kazi za nguvu na hizo za nje ya uwanja wa nyumba. Nawashangaa wanaotaka kupishana na uasili wa kitu kwa kusema kuwa kazi ya mwanamke si kupika ili hali ni moja ya umaridadi wa mwanamke(competence of a woman). Ukiona kina baba wanafanya hivyo ujue ni hobby.

    Sasa ishu inakuja utamwelezaje mkeo kuwa hujaridhia mapishi? Jibu ni usimwambie kwa ukali ila mweleze kwa utaratibu na pia kama unawazo wapi paboreshwe hiyo nayo itasaidia sana. Kwamfano anapika chakula hakina vitu kama iliki,tangawizi, limao, pilipili kwa mbali ili hali wewe unapenda vitu hivyo, unamweleza kwa kumshauri mfano, "mpenzi kwa nini tusiwe tunatumia pilipili kidogo kwenye misosi yetu?" atakupa mawazo yake mtajadiliana na mtafikia muafaka na mambo kama hayo. Ile ya kumwambia huu msosi hamna kitu kabisa chakula kibaya bila kutoa mbadala haisaidii.

    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  20. Mimi mke wangu ukianza kutoa ushauri wa mapishi anakuwa mkali ***yaani ni kama huyu dada anon November 18, 2008 12:53 AM(bold text).
    Sasa jamani ukali wa nini??wewe dada kwei kiboko hiyo 1,2,3 uliyompa jamaa nadhani alikuwa mdogo kama sisimizi Du!!!!tehe heeee ehehe
    ***Mdau anon wa November 17, 2008 11:54 PM jamaa amenikunaa saana. Namnukuu
    "Tabia za unafiki unaosababishwa na malezi yanayosisitiza kutokuwa wazi na kusema ukweli vinatugharimu sana waswahili" mwisho wa kunukuu.Yaani brother hapo umesema LIVE mtu wangu. tamaduni zetu eti nikisema atajisikia vibaya au ataniona namdharau, yaani wewe hata kama mke wako ananuka kikwapa usiseme jamani?????khaaaa!!!!!!!
    Namnukuu tena,
    anon ***Mdau anon wa November 17, 2008 11:54 PM anasema
    "Nadhani wanaume wengi hula misosi wasiyopenda kwa gharama ya amani ya familia vile mama hapendi kuambiwa huu leo sio wenyewe"
    mwisho wa kunukuu.
    Jamani sipendi kuwa mnafiki siwezi kuficha jambo moyoni, nawashukuru wadau waliotupa busara jinsi ya kuwambia mai-waifu wako. Busara inahitajika sana. Lakini wake zetu muache ukali wapenzi, tunawapenda saana.
    Naomba mwana jamii yoyote kama anayo maarifa/masomo RECIPE mbalimbali hapa bongo anifahamishe.
    Alumni wwa kifungulo mmepanda CHAT

    ReplyDelete
  21. Mchangiaji wa kwanza yaelekea unabeef na watu wa pwani na ungejua ukisema watu wa pwani unamaanisha nini usingerudia kuiga lugha za watu bila kufikiri, na kwa kuonyesha huyajui mambo ni pale uliposagia wanawake wa pwani mapishi ni nazi tuu, hebu uliza uambiwe, wapishi wa mapishi ni kina nani? khabari zote ziko huko basi kwa mapochopocho na mahanjumati, kuanzia puding faluda na tamtam zote mpaka aina zote za sharbati zaidi ya hapo kusanifu unga na mayai mchele usiseme kila aina ya wali achilia mbali wali mchafu almaaruf biriani au pilau kuna wali wa asumini na wali wa mseto na nafaka, wali wa chenga kwa maana ya bokoboko/bulga ambalo wewe waliita oats, ulishawahi kuvisikia? na kuku wake mpaka samaki, fruits, mboga za majani kwa mitindo ya kachumbari/saladi n.k kwa mitindo mbalimbali alimuradi aweze kumfurahisha mlaji, wewe nafkiri unaongelea baadhi ya wanawake waliolelewa kizembe au kutokana na uzembe wao wenyewe wasiopenda kujiongeza, au sababu za fedha katika familia za maisha hali ya chini sana, ndo ukaambiwa wanawake wa pwani wana gharama sana gharama hiyo pamoja na chakula chake anachopenda kuandaa kwa ajili yake na mmumewe, sisogei kwenye mavazi hilo tutaongelea siku nyengine.

    Kwa mpenda bin kula/mpenda msosi. kwanza ningependa ukumbuke hukuoa mpishi umeoa mke ili ufurahi nae na msaidiane katika raha na shida, hivyo ni kumshauri kwa upendo mkeo unapenda nini na kama wewe unaufahamu juu ya mapishi umfundishe, au kama yuko mtu karibu anaeelewana vizuri na mkeo anaweza kupata shule na vitabu pia. Sikufichi kuwa kupika ni mazoezi kwani hata kama ulikuwa mpishi mzuri sana zamani ukakaa kwa mida mrefu bila kupika lazima utasahau vitu vingi tu hivyo kwa kuendelea kumfundisha kupika mfululuzo anaongeza uzoefu na makosa yataisha na kuwa hodari

    ReplyDelete
  22. Mapishi mapishi! mapishi hayo yapi? Maana mi najua mapishi mazuri ni ya kitandani mengine yapi tena mnazungumzia, mume ukishampa mlo mzuri kwa bed mengine ni story tu, mjitahidi kuvisha pamoja kwa bed hata mezani itakuwa shwari tu.

    ReplyDelete
  23. nimerudi tena mtoto wa uswahilini ili kuwapa faida wanaotaka recipes.

    Kwanza yule mwalimu wa lugha anayekosoa wengine eti wameandika hivi badala ya vile afahamu kuwa hakuna spell checks wala nini humu watu wanaoandika ni binadamu na makosa hutokea hakuna aliyeperfect ndio maana kunakuwaga na drafts kisha final docs upo hapo?

    Halafu dadaangu Bi Majivu umenikosha kwa majibu yako, nafikiri ujumbe umefika.

    Turudi kwa aliyetaka recipes, ziko za kumwaga ngoja nianze kulist websites zenye recipes

    1.zanzinet
    2. zanzibarwebsite
    3. alhidaaya mapishi
    4. mirecipe.com
    Huko mtakuta mpaka vitumbua vya kuku!

    Ya kizungu
    1. martha stewart
    2. jamie oliver
    3. deliaonline
    4. nigella Lawson

    Hizi unaweza kuazima dvd zake library, niliwahi kuazima dvd za Nigella hapo British Council library mwaka 2007.

    Mtoto wa uswahilini

    ReplyDelete
  24. Mtoto wa uswahili nakupa big up.
    Maelezo yake yamenyoooka.
    Jamani wabongo kwa NGONOO??????????akhg!!!!hadi inakera. watu wanazungumza misosi nyie mmekazania ooh..kitandani. Kitandani KUNANI?????
    Bila afya njema huo mpira utachezwaa????nauliza swali.

    leo hii kama ngekewa vile nimepata COOKBOOK ya Betty Crocker Imeandikwa "Everything You Need to Know to Cook Today" kitabu bomba sana, hasa kama unapenda misosi ya kizungu.
    Kaka wa Uswazi

    ReplyDelete
  25. oyaa mbona mnalaumu wa kiswahili tuu. ni wanawake wote duniani wanaamini jikoni ni dept yao. awe mzungu mchina au mchaga wote moja. inabidi uwe na diplomasia ya nguvu. au jifanye penzi limezidi uingie jikoni mwenyewe tofauti na hapo wee andaa talaka tu.. how rude!! sijui kupika??? weweee ndoa imeisha.

    ReplyDelete
  26. website nzuri sana hii imesave sana

    allrecipe.com

    Kupiga ni mazoezi na jinsi unavyopika sana ndio jinsi unaweza kupiga mlo.

    Mimi ni wa mwisho nyumbani kwetu na nimekua na dada wawili, mama mpenda kupika , house girls all my life. Nilikua sijui kupika chochote mpaka nipo form six nilikua sijawahi kupika kabisa. Lakini sasa hivi kila mtu anatamani chakula changu.

    ReplyDelete
  27. heeeeee aya mapishi yatatoa watu roho,,,watu wanaendekeza mlo kuliko mke basi,,,ni roho za kwanini tu
    ahahahahaaaaa, dada uliempa ukweli mmeo swaaaaaaaaaaaaaaafi sana kuna majanadume hawana kauli zuri eti mtu aowa kisa kachoka kujipikia na kufua (YAN HII NDO KUBWA ASWA)
    annon unaewaponda kinadada wa siku izi BP nk nyooooooooooooooooooooo ovyooooo ujioe na mwanaume mwezio nyamafu
    na habari ndo iyo

    ReplyDelete
  28. Yaani mnabishashana kuhusu mwanamke kumpikia mwanaume? hiyo ni basic obligation yake, because a man is a master of a woman. hata maandiko yanasema hivyo. hayo mambo yenu ya usawa wa kijinsia ndio yanaharibu shauri yenu mnaenda against God's orders.

    ReplyDelete
  29. kupika ni hobi na mudi, kwani kuna siku mtu anakuwa hajisikii kupika hivyo akiingia jikoni lazima ataharibu, pia uswahilini au uzunguni hakuwezi kumfanya mtu ajue kupika chakula au asijue, ni tabia na mwenendo na malezi aliyekulia. Nani anapenda nini ndio swala la msingi la kujifunza.
    Hivyo kama mkeo hajui kupika mfundishe ajue la mpeleke shule za kujifunza kupika.Lakini kupika sio kazi ya mwanamke kila mtu anaweze akapika ndani ya nyumba kutokana na makubaliano ambyo wawili hao wameyafiki.
    mama ushauri

    ReplyDelete
  30. Mapishi yana-matter. demu akiwa dhaifu ktk misosi ni rahisi jemba kunogewa na vya nje. akija home kashibaa!!! Anakula kuzuga tu.
    tehe hee he heeee

    ReplyDelete
  31. kwa kuongezea tembelea www.foodnetwork.com, kama ni mpenzi wa mapishi ya kizungu, kiitaliano lakini kwa mapishi ya kiswahili alhidaaya.com ni safi sana.

    kwa mpenda kula, wanaume wengi ni mabahili panapokuja suala la pochi la sokoni hawamwamini mwanamke kwa kufikiri kuwa atabania vijisenti na wengi hudiriki kwenda wenyewe sokoni, dukani, gengeni na hata supermarket na kujitahid kubania na kuja na vinyanya vyake viwili akitegemea mke atafanya maajabu na kuja na rosti la kufa mtu na asipoliona hilo hulalama ooh mke wangu hajui kupika!
    wengine weshalishwa unga wa ndere huko na ugali wa hamira kwa amama nipe, kwa hiyo hata upike nini ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, hawaridhiki tu! mpaka wakipate kile kile.
    BADILIKENI!

    ReplyDelete
  32. Uzuri wa hii blog ya jamii, tunatoa maduku-duku yetu bila mtu kukujua. Hivyo tuko huru zaidi.
    na vitu ambavyo imekuwa vigumu mwanaume kumwambia mwanamke mdomo juu, ni kama mada hii.
    Sasa wanaume waendelee kukaa kimya???au wakale nje????

    ReplyDelete
  33. Sikutaka kurudi tena humu jamvini nilichelea kwenda nje ya mada ila swahib we wa Nov. 19, 3:35 umenirudisha hapa.Kila siku kwenye makitchen part kuna sentensi aghlab hurudiwa rudiwa kwa kusema mwanamme ni kichwa cha nyumba, au kiongozi wa nyumba, sasa mchanganyo unakuja pale inapogeuka unaambiwa tena palepale kuwa mwanamme ni kama mtoto, kwa maana ya kuwa anabadilika kutokana na mazingira alipo,sasa naomba ukichwa uudhihirishe ili na sehemu ya kulelewa kama mtoto na mama ionekane. Mawasiliano ya upendo na heshima ya kustahiyana yawepo palepale, wakati wa kuwasilisha hoja ya udhaifu wa mkeo juu ya mapishi yake, sio unaongea kama bwanyenye na bepari au nyapara, wakati unaeleza shida yako ya kutoridhishwa na upishi wa mkeo.

    Hapa nakujibu wewe swahib juu ya maswali yako hayo mawili,Kukaa kimya sio suluhu ya tatizo kwani unabaki hufurahii maisha ya kula nyumbani na kukimbia tatizo pia si suluhisho kwani huko nje utajikuta umejiingiza sehemu ambayo hukutaka kwenda. Na kwa mwanamke ni kujiongeza tu kama vile ubunifu na manjonjo ya kwa bed chambile cha dogo wa Nov, 18, 11:13, kuwa mambo yote story ni kwa bed, nataka nikuhabarishe kuwa hiyo gijigiji ya kwa bed bila nyamnyam dadako utakiona kihangahanga utalala mlango wazi kwani hukuufunga na mwizi akija atauchota mpunga, matokeo yake mara tutaona unapiga mbinja humu jamvini Kuwa jamaaniieee msaada kwenye tutaaaa, wapiii... ummeyatupa mausia yetu kwani kuna usemi unasema mdharau biru hubiruka yeye.

    ReplyDelete
  34. kama hujapenda mapishi ya mkeo kwanini wewe usiingie jikoni nae aonje mapishi yako then hapo ndo mnaweza ku compare notes zenu za nani mpishi zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...