neshno kwa ajili ya kikwangua anga kipya imeshaandaliwa na sasa bado zege na nondo tu. hapo ni mtaa wa ohio katikati ta ppf tower na posta house. kule shoto ni kikwangua anga kingine ambacho redio mbao zinasema ni cha benki moja hivi....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. du, si mchezo ila hao hapo wapo wapake tu rangi jengo lao, mpaka tujute,utafikiri jengo limetelekezwa, yaani hata hilo tangazo halikuvutia kwa jinsi jengo limechakaa.

    ReplyDelete
  2. Ila ni uppuuzi kuvunja majengo ya zamani na kujenga mapya, kwani mji hautasogea na kuongezeka, pia kupoteza historia ya majengo ya zamani.
    Hapa Cadiz(Spain) kuna Cadiz Old city ambayo kimandhari inafanana kabisa na Stone town hapo Zanzibar.. Then wakajenga Cadiz New town ambayo viberiti vimepangana kiumahiri. Yafaa sasa kuachana na ubomoaji wa maeneo ya Posta na ujenzi wa kisasa uelekeze maeneo ya K/Nyama, Magomeni, Kinondoni na maeneo mengine jirani ambayo bado ni karibu na City centre.

    ReplyDelete
  3. Exim tower hiyo ..inafunguliwa soon..http://www.spasmindia.com/images/exim.swf

    ReplyDelete
  4. Mabenki ya marekani yanasemekana yaliporomoka kutokana na kukopesha sekta ya nyumba ambazo zinashindwa kulipia deni.Sijui hilo jumba ni mopo wa benki au la.

    Lakini wachumi koko waliosoma fani zingine nje ya uchumi kwenye vyuo vinavyoongoza kwa migomo wanasema wachumi wa marekani waongo wakubwa wasio kuwa na haya.Mabenki Marekani yamefilisika wakati za kipindi cha uchaguzi wa Marekani kwa sababu wagombea walichukua mipesa mingi kwenye mi-akaunti ya Benki kwenda kuhonga vyombo vya habari na wapiga debe wao nje ya kaunta za benki.Rushwa imefilisi mabenki Marekani yakajikuta hayana hela kwenye kaunta zao zimeyeyukia mitaani.

    Hivi ni kweli kipindi cha uchaguzi mabenki huwa yanakuwa hayana pesa za kutosha? Wataalamu tupeni jibu tafadhali.

    ReplyDelete
  5. wasomi wetu waache kutoa sababu za kitanzania katika matatizo ya dunia ya kwanza.

    huo ni mfano wa kutosha; eti mabenki ya america yamefilisika kwa sababu ya uchaguzi.

    hicho ni kichekesho cha mwaka;uchaguzi wa marekani haufadhiliwi na mabenki. mathalan obama amekuwa akikusanya michango toka kwa wananchi ,tena watu wamekuwa wakichangia dola 5, 10 .15 mpaka akiwa na kibunda cha dola milioni mia sita,
    uchaguzi wa tanzania ndiyo hufadhiliwa na vyombo visivyo julikana, matokeo yake ndo hayo mara hili mara lile linaibuka .
    hivyo basi suala la credit crunch na uchaguzi ni mambo mawili tofauti.
    zaidi ni kuwa hata kwetu tanzania inabidi wale wote wenye kutoa michango kwenye vyama wajulikane, na ni wajibu wa kila chama kubainisha nani kachangia nini has mchango unapokuwa mkubwa.
    nashukuru ndugu zangu;

    ReplyDelete
  6. Annoy wa Tarehe November 17, 2008 11:04 AM

    Maoni yako yamekwenda shule.

    Huu ujenzi wa kulazimisha katikati ya jiji una kila sababu ya kupingwa vita. 1. Unaondoa mandhari ya historia yetu kati kati ya jiji (mfano hai ni pale Salamander, samora ave). 2. Unazidisha msongamano wa watu na magari kati kati ya jiji. 3. Unapunguza nguvu ya maendeleo maeneo mengine jijini. 4. Hauji na miundo mbinu ya kutosha kulingana na idadi ya watumiaji.

    Serikali ingesitisha utoaji vibali vya majengo mapya kati kati ya jiji, na badala yake kuweka msukumo wa wenyewe kuyatunza majengo yao hivyo hivyo yalivyo (mfano mzuri ni jengo la British Council, kona ya Ohio na Samora Ave).

    Hawa wanaojenga majengo mapya ni dhahiri wana mitaji ya kutosha kujenga majengo haya maeneo mengine ya jiji kama Kinondoni, Keko, Magomeni, Ilala n.k. Tena maeneo hayo arthi ni gharama nafuu kuliko mitaa wa Ohio, Samora, Shabban Robert etc (mfano wa kuingwa ni Ubalozi wa USA pale Drive Inn, na HQ za Stanbic, Kinondoni).

    ReplyDelete
  7. Anoy 3:30 Huyo mwenzio hajasema benki ndizo zilizofadhili.Kasema watu walitoa pesa taslimu kwa wingi kwenda kuchangia kampeni mitaani kiasi cha kufanya pesa zilizoko kwenye mabenki ziwe za kukopesha n.k zipungue na kuzifanya benki ziyumbe.

    Hiyo michango ya dola 5,10,15 na kadhalika waliyompa Obama taslimu unayosema hizo pesa walizotoa wapi kama siyo kutumia debit au credit card zao kutoa kwenye account zao benki na kuzifanya akaunti zao ndogo zenye dola chache zipunguwe kwenye mabenki kwenda kuzagaa mitaani kuhonga?

    Marekani nao wamejaa wala rushwa na waongo tu.Wizi mtupu.

    ReplyDelete
  8. yah nakuunga mkono anonymous wa2 hata hapa ıstanbull kuna mjengo mengi ya zamani wenzetu wanatunza kumbukumbu hayo majengo ni kivutio kikubwa cha watalii wajao uturuki lkn viongozi wetu hawajali vitu muhimu kama hivi.

    ReplyDelete
  9. nyinyi na serikali yenu huwa mnanishangaza hiviiiiiiiiiiiii TANZANIA ni hapo tuu DAR mbona miji mingine huwa mnainyanyapaa mmekazania DAR tu nendeni huko sumbwanga,singida,shy,tabora.mtwara,lindi hamuoni wenzenu ulaya.

    ReplyDelete
  10. ni kweli kabisa mikoani ukiondoa mwanza,na arusha huko kwingine hamna kitu utafikiri hata sio miji ni vijiji halafu naambiwa eti baada ya miaka kumi miji yote itakuwa na city status puuuuuuuu,hata kragerø japo ni ka wilaya hapa majuu kangekuwa bongo kangekuwa sijui nini tuseme metropolitan duu.tuna safari ndefu..

    ReplyDelete
  11. za ufisadi watu wanywee bia kisha makaburu wakombe zote wapeleke kwao sie tusibaki na muundobinu hata mumoja? asa tukitaka ku-trace hizo pesa tutazipataje kama zilinywewbaadhi ya matumizi ya fedha za ufisadi ndio sasa yanaanza kuonekana kwa kujenga mavichuguu yanayokwangua anga kwa kwenda mbele utafikirini kuna mashindano.

    na wale mnaotetea kwamba waende wakajenge kwenye outskirts na sie kina kajamba nani tutajenga wapi? au hamjui kwamba wakija kule uswahilini wakachukue maekali na maekali kisha wazungushie miseng'enge na kutumalizia ardhi sie walalahoi? waache walundikane hapohapo katikati ya jiji. kama ni tatizo la usafiri sisi tulishazoea! mimi sioni tatizo liko wapi waache wajenge tu. hamwoni majiji ya wenzetu wanapotupangia vibiriti? huko china hasa katika jiji la tokyo huwezi kukuta jengo lenye tugorofa tuwili, tutatu. thubutu! unafikiri wao waliweza wana nini halafu huku kwetu tushindwe tuna nini hasa ukizingatia kwamba serikali inajidai kwamba haina hela, hela zote wamekomba mafisadi? mnataka hizo helaa bia? si afadhali wajengee miundombinu ndio itakuwa rahisi kufilisi?

    ReplyDelete
  12. Anonymous wa saa 5:44 MUNGU Akubariki ...umesummarize kila kitu . Ni jambo la kushangaza kila kitu kinawekwa katika mji mmoja ! No wonder they can't solve machinga problems.

    ReplyDelete
  13. pesa aliyo kusanya obama ni dola milioni mia sita tu, congress imeombwa iidhinishe dola bilioni mia saba ili uchumi upate nguvu,sasa hizo zilizokopwa na watu wa obama mbona ni ndogo sana,lazini watanzania bado tunatoa sababu ileile,ukweli ni kwamba haikuwa hivyo.

    ReplyDelete
  14. Siku zote hizi sikujua kwamba Tokyo iko China.Ahsante anony. mmoja kwa hilo.
    Suala la michango ya kampeni za Obama,data zinaonyesha kuwa alikusanya jumla ya $640m kufikia Oct 15.Sasa unaposema kwamba benki zimeishiwa pesa kutokana na watu kutumia debit na credit card ajili ya michango,haipandi kabisa!
    Ninaamini kwamba benki zina pesa zaidi ya hizo na isitoshe sio watu wote waliochanga wana account kwenye benki moja!

    ReplyDelete
  15. WATANZANIA MKIAMBIWA ELIMU NI NZURI NA ELIMU YA BONGO FEKI MNABISHA, OBAMA AMETUMIA KATI YA £600M NA £700M NA NI MICHANGO TOKA KWA WATU WA KAWAIDA NA BAADHI YA MAKAMPUNI MAKUBWA, KUNA WATU WALIKUWA WANATOA HATA $2 KUPITIA WEBSITE YAKE NA McCann ametumia kati ya $300m na $400m total of $1billion both of them sasa hizi zitawezaje kufanya uchumi wa dunia au nchi kama amerika kuyumba, acheni ukihiyo, nendeni shule za matawi ya juu, AZIM BANKI IS AN AMERICAN BANK AS WELL AS CITI BANK AMBAYO INAPUNGUZA WAFANYAKAZI 75,000 DUNIANI KOTE, INAWEZA PIA KUWAKUMBA WATANZANIA, NA KUNAWATU WALIKUWA WAKIBISHA UKATA HUU HAUWEZI KUTUKUTA WATANZANIA NA KUMBISHIA SANA JOHHN MASHAKA NAONA SASA WATAONA UKWELI WAMBO HASA PALE HATA CHAKULA KINAANZA KUPANDA BEI HAPO KARIOKOO

    ReplyDelete
  16. Mi naona watanzania wengi wanaoishi ulaya na kwingineko wanadharau sana walikotoka. Ni kweli tupo nyuma kimaendeleo, lakini sion kama kudharau tulikotoka kutatusaidia. Mathalan, mtu anasema "..waliosoma kwenye vyuo vinavyoongoza kwa migomo", kwangu mimi kama mtu anagoma ina maana ana fikra mbadala.Huwezi kuwa na wasomi wanaofanya mambo kama kasuku.Niwakumbushe tu kwamba migomo ya wanafunzi ilisaidia sana kuhitimisha ubaguzi wa rangi afrika kusini.Wanafunzi wengi walipoteza maisha, lakini hawakuacha.

    Unaweza kusoma chuo kizuri (kama Havard, MIT) lakini usiwe mwanafunzi/mhitimu mzuri ktk fani uliyosomea. Kuna wanafunzi wengi ambao wamesoma UDSM (vinara wa migomo) ambao ni "world class products"-fuatilia utakubaliana nami, sitaki kutaja majina.Obama ametuonyesha mfano mzuri sana,ameonyesha kwamba kama mtu una malengo unaweza ukafanikiwa bial kujali historia,rangi, mahali unapoishi,mali nk.

    Anaeabudu mji wa "kragerø" ajue kwamba mji huo ulijengwa na wenyewe. Aje tujenge TZ!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...