JK akiwa na waziri mkuu wa denmark Mh. Anders Fogh Rasmussen (kati mbele), Naibu Katibu Mkuu wa UN Dk. Asha Rose Migiro, Mwenyekiti wa Tume ya Africa Jean Ping (shoto mbele) na makamishna wa tume ya maendeleo Africa katika mkutano wao wa pili uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia
Jk akisalimiana na balozi Manongi ambaye ni msaidizi maalumu wa Naibu Katibu Mkuu wa UN Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kuanza mkutano wa pili wa Tume ya Afrika inayodhaminiwa na Denmark. Shoto ni Waziri Mkuu wa Denmark Mh. Anders Fogh Rasmussen na mwingine ni Waziri wa Maendeleo wa Denmark Bi. Ulla Tornaes

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiwasili katika ukumbi wa mkutano wa Sheraton hotel jijini Addis Ababa kuhudhuria mkutano wa pili wa Tume ya Maendeleo Afrika

AJIRA KWA VIJANA MUHIMU BARANI AFRIKA- JK

Jakaya Mrisho Kikwete amesema Mahitaji ya ajira kwa vijana ni makubwa zaidi katika nchi za Afrika , hivyo suala la kutengeneza ajira kwa vijana hao ni changamoto kubwa ya maendeleo inayolikabili Bara hilo na dunia kwa ujumla hivi sasa.

Rais kikwete ameyasema hayo katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Afrika uliofanyika kwa siku moja tarehe 20 Novemba, 2008 Addis Ababa nchini Ethiopia ambao Mwenyekiti wake alikuwa Bwana Anders Fogh Rasmussen ambaye ni waziri Mkuu wa Denmark.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose-Migiro.

Akifungua rasmi Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Sheraton Addis, Bwana Rasmussen amesema ajira ndiyo injini muhimu kwa maendeleo ya Bara la afrika na kwamba ongezeko la idadi ya vijana linawakilisha fursa pekee kwa Bara hilo ambayo inatakiwa kutumiwa kikamilifu katika harakati za kuleta maendeleo.

Amesema hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa ili kutoa msukumo katika kutekeleza Maendeleo ya Milenia (MDGs).Aidha amesema ukuaji wa uchumi hauna budi kuwanufaisha raia wote na ndiyo maana jitihada za Tume zimelenga, pamoja na mambo mengine, katika masuala ya ajira.
Kwa upande wake, Rais Kikwete amesema kwa zaidi ya asilimia 89 ya vijana duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea na kwamba idadi ya vijana wanaoishi katika nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara ni asilimia 13 ya vijana wote duniani.


Amesema ajira kwa vijana zinahitaji ongezeko kubwa la uzalishaji na utengenezaji wa fursa zaidi za ajira kwa kuongeza kiwango cha uwekezaji wenye tija zaidi.

Ameainisha mambo muhimu katika kukabiliana na tatizo la ajira kuwa ni pamoja na utekelezaji wa dhana ya ushindani, ukuaji wa uchumi, ujasiriamali, maendeleo katika biashara pamoja na maendeleo ya elimu, mafunzo na ujuzi.

Mambo mengine ni uwezeshaji na kuwepo kwa fursa za kupata mikopo na kutumia vema fursa za sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Amesema ujasiriamali unatoa fursa kubwa zaidi za ajira kwa vijana na wanawake na hivyo kupunguza kiwango cha umaskini.

Hata hivyo amesema changamoto zilizopo ni namna ya kuwawezesha vijana kuwa wajasiriamali kati ya mamilioni ya vijana waliopo ambao kwa sasa hawana ajira, namna ya kuwasaidia wale ambao tayari wameanzisha biashara zao na namna ya kuwafanya wajasiriamali wadogo kukua hadi kufikia ngazi ya kati ya ujasiriamali.

Amevitaja vikwazo viwili vikubwa vya ujasiriamali kuwa ni kukosekana kwa ujuzi wa ujasiriamali na uhaba wa fursa za kupata mitaji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AJIRA SI KWA VIJANA TU BA;LI KWA WOTE, KWANI WAZEE HAWAHITAJI AJIRA ILI WAISHI, A GOOD POLICYISBTO CREATE JOBS FOR ALL THOSE WHO ARE ABLE TO WORK, NOT JUST FOR THE YOUTH, SHOULD BE FOR ALL.

    ReplyDelete
  2. Huu ndio umiss tunaoutaka zaidi, dada yetu kuikalia dunia kwa kichwa(akili)sio kwa kudengua tuu kama kwa wasichana wadogo wanavyotamani.

    Halafu huyu dada hata hana majivuni, ona hata urembo wake very nechurao. Huyu dada ni mfano wa kuigwa na watanzania woote wenye nyadhifa.

    ReplyDelete
  3. Mama unawaka! Nikikukumbuka pale UDSM na heka heka kwenye sheria mitaani, kweli Mungu ana yake. usikate tamaa hata siku moja ndugu zangu!

    ReplyDelete
  4. Kwanini hii mikutano yetu tunawaalika hawa watu wengine. Huyo mdenish na wengine wa nini?

    Wao wakifanya G20 yao na apec wala hawatualiki. Kwanini nasisi tusijaribu kutatua matatizo yetu
    bila kuwashirikisha hawa?

    Nadhani kwa vile tunajua shida zetu basi wenyewe ndio tutajua jinsi ya kuzitatua.

    Hawa watatutake for a ride tu uchumi ulivyoanguka mwishowe tutaambiwa siye tupunguze thamani ya hela zetu tu hapa

    ReplyDelete
  5. JK nae alikuwepooooooo,,,,
    teh teh teh
    migiro swaaaaaaafi sana uko juu,kip it up babe,,,wakilisha Tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...