RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE DK AMANI ABEID KARUME,AKIMKABIDHI KIKOMBE NAHODHA WA TIMU YA STONE TOWN HAMZA MBWANA JOZI YA JEZI MARA BAADA YA KUIBUKA WASHINDI WA KOMBE LA KARUME KWA KUWASHINDA POLISI VIKAPU 60-47 MASHINDANO YA KARUME CUP YALIYODHAMINIWA NA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TIGO
MCHEZAJI WA TIMU YA POLISI UZIA AKIRUKA JUU KUWANIA MPIRA WAKATI FAINALI YA KOMBE LA KARUME CUP MPIRA WA MIKONO WANAUME ULIOCHEZWA KATIKA KIWANJA CHA GYMKANA JUZI NA STONE TOWN KUTOKA KIFUA MBELE KWA VIKAPU 60-47


Rais wa Zanzibar Bwana Amani Abeid Karume amesema wakati umefika kwa viongozi wa vilabu kuhakikisha wanapata makocha wa kigeni ambao wataiwezesha Zanzibar kuwa na wachezaji way kulipwa katika siku za baadae.

Rais Karume ametoa kauli hiyo mara baada ya kumaliika kwa mchezo way fainali way mpira way kikapu way kuwania kombe la Karume kati ya timu ya Polisi dhidi ya Stone Town uliofanyika kwenye uwanja way gymkhana mjini Zanzibar.

Katika mchezo huo, timu ya Stone town iliibuka kidedea kwa kunyakua kikombe hicho baada ya kuwachapa mahasimu wao wakubwa maafande way polisi ponti 60 dhidi ya 47.

Akihutubia wanamichezo baada ya mashindano hayo, Rais Karume alisema timu ya Stone Town imepata mafanikio makubwa kutokana na kumtumia vizuri kocha way kigeni Raymond Dwight kutoka nchini Marekani.

"Nataka nitoe wito kwa vilabu vingine vya mchezo huu, huyu kocha way kigeni asiishie Stone Town, nataka vilabu vingine viige mfano wa Stone Town kwa kuleta makocha way kigeni wenye uwezo mkubwa ambaye atawasaidia vijana wetu kutamba Afrika Mashariki na hata huko Marekani, ndio uwezo huo tunao tumewaona vijana wetu walivyoonesha umahiri mkubwa katika mchezo huu" alisema Rais Karume.

Aidha Rais Karume alizipongeza timu zote mbili kwa kuonesha kiwango kizuri hasa mabingwa way mchezo huo Stone Town ambao waliweza kuibana vyema polisi na kuweza kushinda mchezo huo.

Aidha alisema wachezaji way timu zote mbili walionesha uwezo mkubwa way kujituma uwanjani na kumuhakikishia kuwa Zanzibar ina hazina kubwa ya vijana ambao wanatakiwa kuendelezwa kwa kupatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi.

Rais Karume aliwapongeza wadhamini way mashindano hayo kampuni ya tigo kwa msaada wao wanaoutoa katika sekta ya michezo Zanzibar ambapo katika fainali hizo mshindi way kwanza alipata zawadi ya shilingi laki tano na mshindi way pili shilingi laki nne na mshindi way tatu shilingi laki tatu.

Kwa upande wa wanawake, timu ya JKU iliibuka malkia wa mashindano hayo baada ya kuilaza nyuki pointi 29-28 ambapo Pili Peter way JKU alijinyakulia shilingi 50,000 baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora, wakati Mohamed Kassim way Polisi aliondoka na kiwango kama hicho.

Fainali hiyo ilihudhuriwa na mlezi way kombe hilo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume na Mwenyekiti way BTMZ Sharifda Khamis 'Shery' ambaye amepongeza mchango way kampuni ya simu ya tigo kutokana na kuchangia kwa kiasi kikubwa kudhamini michezo mbalimbali Zanzibar.

Baada ya kukosa ubingwa wa mashindano ya soka ya kombe la majimbo, timu ya Stone Town kutoka jimbo la Mji Mkongwe jana ilimalizia hasira zake katika mashindano ya mpira way kikapu ya Karume Cup kwa kuibuka mabingwa way mchezo huo Zanzibar.

Timu hiyo ilifanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuwapigisha kwato timu ya maafande way Polisi pointi 60-47 katika mchezo way fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar.

Mchezo huo uliohudhuriwa na mamia ya mashabiki kutoka ndani na nje ya mji wa Zanzibar ulihudhuriwa na Rais Aman Abeid Karume aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali ya mashindano hayo ambayo yana lengo la kumuenzi Rais way kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume.

Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua, hasa kutokana na utani wa jadi uliojengeka kati ya maafande wa polisi na vijana wa mji mkongwe ambao unatokana na mazingira ya siasa za Zanzibar.

Katika pambano hilo timu zote ziliunza mchezo kwa kasi kubwa ya kutaka ushindi mapema lakini kasi ya mchezo ilikuwa kali sana na kumfanya mgeni rasmi kila mara kupiga makofi katika meza kutokana na kufurahishwa na mchezo huo.

Stone Town ikiwatumia wachezaji wake wakongwe akiwemo Masha Humud aliyepachika magoli 10, Ali upepo, Said Marine, Fuadi Kassim Nabil Ali, ambao waliweza kuwamudu vyema wakali way Polis waliokuwa wakiongozwa na Abass himid Saidi Bilu, Baraka Uzia na Ramadhan Zimbwe.

Kwa upande wa wanawake timu ya JKU iliibuka na ushindi way pointi 29-28 na hivyo kuwa Malikia way mchezo huo kwa mwaka 2008/09.

Mshindi way kwanza alipata zawadi ya shilingi laki tano, mshindi way pili 400,000 mshindi way tatu 300,000 kwa timu zote za wanawake na wanaume, wakati mchezaji bora kwa wanaume alikuwa Mohamed Kassim wa Polisi na Pili Peter wa JKU ambao walipata shilingi 50,000 kila mmoja.

Wakati huo huo kampuni ya simu ya tigo ilikabidhi zawadi ya seti 20 za jezi na mipira 20 kwa ajili ya timu zote zilizoshiriki mashindano hayo zote zikiwa na thamani ya shilingi milioni sita.
Naye Katibu Mkuu way Chama cha mpira way kikapu Zanzibar(BAZA) Abdulrahman Mohamed aliipongeza kampuni ya tigo kwa kudhamini mashindano hayo mwaka huu.

Mashindano ya kombe la Karume hukutanisha timu za kisiwa cha Unguja ambapo bingwa wake atapambana na bingwa way mashindano ya kombe la Thabit Kombo ambayo hufanyika kwa timu za kisiwa cha Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...