Mheshimiwa mkuu wa wilaya!
kwanza nakupongeza kwa kazi nzuri inayofanywa na blog ya jamii ktk kuwapa habari na kuwaelimisha wanajamii ikiwa ni pamoja na kusaidia kutoa ushauri kuhusu utatuzi na uboreshati wa mambo mbalimbali ya kijamii.
Mkuu naomba msaada wa ushauri kupitia tuvuti yako kuhusu afya ya kijana wangu. Ni kwamba kijana wangu wa kiume ana miaka 13, tatizo ni kuwa kila wakati mara baada ya kutoka kuoga huwa analalamika kuwa anawashwa sana mithili ya mtu aliyemwagiwa upupu.
Tumejaribu kubadilisha kila aina ya sabuni lakini hali haibadiliki na inakuwa mbaya zaidi wakati wa joto maana hata akitoka jasho huwa anawashwa.
Najua tovuti hii husomwa na watu mbalimbali hivyo naweza kupata ushauri makini kama kuna mtu amewahi kupata taitizo hili au anajua sehemu ambayo ninaweza nikapata msaada hapa Dar au kwingineko.
Ni hayo tu mkuu naomba kuwakilisha.
Mdau wa Tegeta Kibaoni!


ni maoni tu, anaweza kuwa na allergy na maji(liquid) kuna program moja niliona (usa)kuhusu binti aliyekuwa ma matatizo similar na huyo wako, fanya uchunguzi zaidi
ReplyDeleteI hope this will help to understand what i was suggesting on my first commen, visit this article
ReplyDeletewww.dailymail.co.uk/news/article-520329/The-teenage-girl-allergic-WATER.html
Mpe pole nyingi kijana wako. Kama alivyosema "anonymous" hapo juu, kwa maoni yangu inawezekana kuwa ni allergy. Katika maji ya bomba huwekwa baadhi ya kemikali kupunguza uwezekano wa vijidudu kuwepo na "kuyasafisha".
ReplyDeleteUshauri wangu ni katika sehemu tatu. Mosi, jaribu kumpa maji ya chupa ambayo ni purified by distillation aogee na sabuni ya kawaida. Angalia kama atawashwa, kama haijasaidia basi chance kubwa ni kuwa allergy imo kwenye sabuni.
Most likely ni ingridienti ambayo inawekwa katika asilimia kubwa ya sabuni inaitwa "sodium lauryl sulfate". Hii ndiyo husababisha kuwepo kwa povu katika shampuu, dawa za meno, nk. Hii ingredient hutumika katika maabara kuharibu uwezo wa ngozi kuzuia vitu kupenya mwilini. Wanasayansi wakitaka kujua nini kitatokea endapo kemikali fulani itaingia mwilini, hutumia SLS. Kwa kifupi SLS huharibu ngozi, lakini hutumiwa tu kwa sababu wateja hupenda povu kwa wingi, na hupatikana raisi zaidi ya vitu vingine ambavyo pia huweza kuzalisha povu. Kijana wako yuko tofauti na wewe, au na wengi. Ngozi yake ipo sensitive zaidi ya za wengine, kwahiyo huathirika zaidi na hiyo SLS. Ufumbuzi? tafuta sabuni isiyo na hiyo ingredient "Sodium Lauryl Sulphate" Unapoenda kununua shower gel, au sabuni...soma ingedients.
Kitu kingine inawezekana, (mungu saidia isiwe hiki) ni genetical condition inayoitwa "Aquagenic Pruritis". Narudi kukubaliana na uwezekano alioutoa mwenzangu hapo juu. Hii ni condition kwa ufupi tunaweza kusema ni kuwa na allergy na maji. Kama njia zote mbili hapo juu hazikusaidia, basi upo uwezekano huu. Hakuna tiba, (ya uhakika) ila wengi wenye tatizo hili wamesema husaidia kujifuta na kuvaa nguo nzito mara tu baada ya kuoga. Na kupata jua (tanning kwa wazungu wa ulaya). Bila shaka kijana anapata jua la kutosha kwa siku. Ipo dawa ambayo asilimia kubwa ya wenye tatizo hili wamesema huwasaidia. Inaitwa Zyrtec.
Tafadhali, jaribu njia mbili za mwanzo kwanza, zisipofanya kazi, omba ushauri juu ya kutumia Zyrtec kwa Daktari. Usitumie dawa bila ushauri wa mmwanafamasia au daktari, kwani mara nyingine kuweza kusababisha matatizo endapo hiyo dawa ina ingredient ambazo mgonjwa yupo allergic nayo, au inaweza ku-react na dawa nyingine anazotumia. Habari njema ni kuwa wengi huondokwa na tatizo hili wanapokua, kama liliwaanza udogoni.
Kila la heri, tupe maendeleo ya kijana.
Kuna binti mmoja alikuwa na tatizo kama hilo, alikuwa haogi kabisa zaidi ya kunawa tu. Anaoga mara chache mno, na akishaoga basi inakuwa kazi. Huyo ana allergy na maji, kupunguza hilo tatizo ni kuyaweka maji detol ama maliao, ama ndimu, ama chumvi na yawe vuguvugu. Nina maana unayachemsha maji, then ukyaweka katika ndoo ya kuogea unaweka dettol, am limao, ama ndimu, ama chumvi ndio aoge, akimaliza tu ajifute na taulo safi. Ikishindikana fanya yafuatayo:-
ReplyDelete1. Mpeleke akafanyiwe allergy test, then watajua ni ushauri gani wampe.
2. Nenda kwa wamasai, waeleze hilo tatizo,watakupa dawa, hawa jamaa kuna nyakati wanasaidia sana.
Yule dada alienda hospitali na kwa wamasai, yeye alikuwa Mwanza. Baada ya kuondokewa na hilo tatizo hajui alipneshwa na dawa za hospitali ama za wamasai, manake alizitumia pamoja.
Lakini meleke kwanza hospitali, ndio muhimu. Namtakia NAFUU ya haraka na Mola amsaidie.
Mpe pole sana Mwanao!
ReplyDeleteMimi mwenyewe nilikuwa na matatizo kama hayo, wakati mwingine ngozi inakuwa kama ina mapunye madogo madogo lakini sio mapunye wala sio allergy. Nilitumia dawa na creme nyingi lakini wapi, nikizimaliza kuwashwa kupo pale pale.
Mafuta ya samona na sabuni yake yanasaidia sana. Hayo ni mafuta kutoka Uganda, Jaribu kuyatumia. Mi yamenisaidia sana.
Baada ya kuondoka Tanzania nilidhani hilo tatizo litaisha, lakini ngozi ilinibadilikia mpaka nikawa sina raha kabisa. Nilionana na dermatologist na aliniambia. kuoga sana kwa kutumia sabuni pia kunasababisha ngozi kuwasha. Ngozi hususani ya mwafrika huwa inatoa mafuta yake ya asili kwa ajili ya kutunza ngozi, hivyo unavyotumia sabuni, yale mafuta unayaondoa na ngozi unakosa ulinzi. Alishauri kuoga mara moja kila siku kwa kutumia sabuni, kama ukioga mara nyingine katika siku hiyo tumia sabuni kwapani, sehemu za siri na miguuni, sehemu nyingine tumia maji matupu. Nimejaribu ushauri wake kuwashwa kumepungua nadhahani nikiendelea na ushauri wake ngozi itarudisha kinga yake. Huyo ni mtoto na mazingira ya uchezaji ya Tz ni vumbi tupu sijui hapo itakuwaje, siwezi kucomment.
Kuna lotion zinaitwa Eucerine au aquaphor ni nzuri zinamoisturize na kutuliza ngozi. Kama zinapatikana Tz nunua na ujaribu.
Creme za Amol-G, cotrizone zinasaidia sana kutuliza ngozi kuwasha, unaweza kuanzia hizo huku ukitafuta ufumbuzi wa kudumu.
Hali ikizidi kuwa mbaya nenda kwa wataalamu wa ngozi, wanaweza wakafanya culture ya ngozi na kugundua tatizo ni nini.
Umemcheck kisukari? Je uzito wake ni wa normal au ni mnene? Kuna watu wanye kisukari kabla ya hawajagundulika na kuanza kutumia dawa huwa wanawashwa sana wakitokwa na jasho au wakitoka kuoga pia.
ReplyDeleteMimi sio Dr wala nurse lakini baba yangu alikua anawashwa hivyo hivyo. Akitoka bafuni, akisweat kidogo...yaani alishachoka kwenda hospital kwa ajili ya kuwashwa. na kama unavyojua bongo yetu ukienda na hili hawacheck jingine bali lile lile ulilosema. Miaka ilipita mingi lakini alivyoanza dalili za kisukari kujitokeza ndio akaenda kupimwa na alivyoanza kufuata masharti ya kisukari na kutumia dawa na kuwashwa kwake kuliondoka na wala hata sielewi kwanini.
Anaweza akawa hana bali ni allergies nyingine but there is nothing to loose. Akiwa hana basi.
Ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama ukurutu pia huanza kama hivi yaani dalili zake, lakini ni bora akawaone wataalamu (specialist) wa ngozi kwa ushauri zaidi
ReplyDeletepole sana kwa matatizo.
ReplyDeletejee umewaona madaktari? nadhani mabingwa wa magonjwa ya ngozi au masuala ya allergies wanaweza kukusaidia.
pia umezungumzia wakati akioga tu je akiwa ananawa tatizo hilo lipo? je maji ya bahari nayo yanamsumbua?
Nenda kwa daktari wa ngozi anaweza akakushauri dawa nzuri ya kutumia ila hilo tatizo mara nyingi huwa ni eczema au labda anaweza kuwa na skin asthma. Ila nenda kwa daktari atakushauri vizuri zaidi
ReplyDeletePole sana...Hii ni hali hujitokeza na mimi ni mmojawapo ambaye nilishawahi kupata sana hili tatizo na huwa linanitokea kwa nyakati fulani tu katika mwaka na huwa nasikia kama pini zinanichiomachoma nyingi sana ghafla na kupotea. Inaudhi sana kwani inasumbua sana. Niliashauriwa na Daktari wa kichina hapa Canada kuogea sabuni ya 'Dove' isio na perfumes au ikiwezekana maji kabisa bila sabuni kabisa na pia lazima uogee maji yalio na joto dogo sana karibia baridi kabisa. Kwa kweli ilinisaidia. Kila lakheri.
ReplyDeletepole sana usibaatishe madawa kwani unaweza ukatumia na yakakuletea matatizo mengine. Nenda pale Luther house (Azania Front) kuna Dr Mmboneko wa ngozi mimi alishawahi kunisaidia.
ReplyDeleteUpanga kama unaenda muhimbili ile njia inayopita mabasi yanayoingia muhimbili hosp. kuna clinik ya ngozi ya Dr. Masawe (muone masawe mwenyewe)
Nawashukuru sana wadau wote kwa ushauri pamoja na mkuu wa Wilaya kwa kuniweka hewani. Mungu awabariki sana .Ntawapa maendeleo ya kijana siku za baadae.
ReplyDeleteMdau wa Tegeta Kibaoni
Mpeleke kwa Professa Massawe lazima atampatia dawa. Huyu ni daktari bingwa wa ngozi na ana Clinic Binafsi ya Ngozi inaitwa Meise Skin Clinic. Wengi waliomuona na mwenye matatizo ya ngozi (ikiwa ni pamoja na mimi) wamepata tiba. Clinic yake iko njia ya kuelekea muhimbili hospital (Kutokea kituo cha Superstar - UN road). Nategema atapona.
ReplyDeletePOLE SANA KIJANA, MIMI NILIKUWA NA TATIZO KAMA HILO TANGU NILIPOHITIMU MIAKA TAKRIBANI 17 NILIANZA KUWASHWA VIBAYA SANA PINDI NIMALIZAPO KUOGA MUASHO WENYEWE NI KA UMEMWAGIWA UPUPU AU VILE VIDONGE VYA QUALOROQUIN VILIVYOKUWA VIKIWASHA ENZI HIZO BWANA SIMULIWA YAANI UNATAMANI UICHUNE NGOZI MANAKE HUWO MUWASHO NI WA MAUDHI SANA NI KAMA VITU VINACHOMAMA NA KUCHEMKE NI NOMA,KWA KWELI NILIENDELEA KUWASHWA KWA MIAKA MINGI SANA NA HATA HASA NIOGAPO MAJI YA BARIDI NA HILI TATIZO WALIKUWA NALO BAADHI YA KAKA ZANGU NA MAMA VILIVILE LAKINI MIMI NDO ILIKUWA ZAIDI.BAADA YA KUJA US NA KUANZA KUOGA MAJI YA MOTO FROM SHAWER KWA KWELI KWA KWELI NI KAMA MATATIZO HAYO YAMEISHA BUT NIKIOGA TU MAJI YA BARIDI NINALO. KWA HIYO NAMSHAURI DOGO AOGE MAJI YA MOTO HIYO NI ALLERGY
ReplyDeleteUSHAURI: NI JUZI NILIKUWA KWENYE PEKUA PEKUA YANGU NIKAKUTANA NA HABARI MOJA INAFANANA KABISA NA HUYU KIJANA MWENZETU.
ReplyDelete1;KUTOKANA NA MAELEZO ULIYOELEZA HAPO HUYU KIJANA MWENZETU ANA ALLERGY NA MAJI MAGUMU(HARDY WATER),AKISHAYAOGA ANAWASHWA KUTOKANA NA KEMIKALI ZILIZOMO KWENYE MAJI HAYO NA KAMA SIKOSEI AKISHAKAUKA ULE MUWASHO UNAPUNGUA KUTOKANA NA ZILE KEMIKALI ZINAKAUKIA MWILINI ILA AKITOA JASHO ULE UNYEVU WA JASHO UNAZIFANYA ZIWE ACTIVE NA NDIYO MAANA ANAANZA KUWASHWA TENA SASA BASI HILO ENEO MNALOISHI LINA HARDY WATER TAFADHALI JARIBU KUYACHEMSHA ILI APATE MAJI LAINI HALAFU MUANGALIE KAMA ITASAIDIA.
2;KUMA UTAWEZA KUNA DAWA ZINAUZWA ZA KUYAFANYA MAJI MAGUMU KUWA LAINI NA TAFADHALI ACHANGANYE NA DETTOL ILI IWEZE KUSAIDIA ZAIDI.
3;KIJANA ANAWEZA KUWA NA SENSITIVE SKIN KWA HILO TAFUTA USHAURI WA KITAALAMU ZAIDI IKIWEZEKANA MTAALUMU WA MASUALA NA NGOZI.
USHAURI TU TUTAFURAHI KAMA UTATUPA MAENDELEO YA KIJANA MWENZETU.
Jamani hili tatizo mimi lilishanitesa sana. Nilikuwa natamani kulia nikisha maliza kuoga. Nilikuwa nawashwa sana ngozi kwangu mimi ilikuwa kwenye mapaja. nawashwaaaaaaa, kila nikikuna ndio vinazidi kuwasha, nikiacha vinawasha pia!!!da!! Basi niliteseka sana sikujua dawa, nilikuwa nalalamika sana kwa rafiki na ndug zangu, hakuna aliye jua chanzo wala dawa. Mungu saidia vilikuja ondoka venywewe tu. wakati mwingine nilihisi labda taulo chafu, nilibadilisha nguo za kujifutia maji baada ya kuoga lakini tatizo liliendelea.Leo hii nashukuru tumepata jukwaa la kuliongelea hili jambo. Nimeweza kupata ushauri toka kwa wadau waliochangia hapo juu. mimi Nilipona siku nyingi, bila dawa, lakini cha moto nilikiona. Naomba huyu mdogo wetu kijana anayeumwa aweze kufuata ushauri haraka uliotolewa hapo juu, asifanye kama mimi, mimi sikujua dawa. Mungu tu aliniponya. Niliteseka muda mrefu.
ReplyDeleteafadhali umeuliza mzee maana kuna kipindi nlianza kukonda kwa kudhani labda ni 'ngoma'!!ubishi wote ukaisha mwenyewe nikaenda pima wakanambia niko fiti tu ila nikitaka kuoga yani hadi niweke kikao kujiuliza.naanza kuamini huenda tunaowashwa tuko allergic na kemikali flani kwenye maji(hususani ya baridi).nikioga ya moto hata siwashwi sana ila ya baridi kwakweli sigusi.mzee nasubiria kudesa tiba ya mwanao!
ReplyDeleteMAMBO VIPI.kuna hali ya baathi ya wanaume wenye kifua chenye muonekano wa kike,ambayo hali hiyo mimi pia ninayo,nimekuwa nikiuliza uliza watu na kuniambia eti ni homons za kike ziko mwilini,naomba mnisaidie kunifahamisha kama kuna dawa au njia ya kuweza kuondoa tatiza hili mwilini mwangu kwani lina nikera sana
ReplyDelete