Babu unajua leo ni siku ya choo, loo,msalani uwani toilet duniani?unajua mwandamu wa kawaida hu spendi miaka mitatu ya maisha yake akiwa juu ya choo.?? tuletee mambo kwa blog je watu hutumiaje hiyo miaka mitatu? wataalamu wana dai ni sehemu ambayo ni ya amani nyumba nzima je ni kweli?na wavuta sigara wanadai sigara huwa tamu zaidi. wengine wanadai ndo muda wa kusoma magazeti ya udaku.. sina picha ningekutumia picha ya choo changu but sijakisafisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. BWANA MICHUZI ASALAAM ALEYKUM.

    MADA YA KUJILIPUA. Hivi mtu aliyejilipua, akapewa nyumba ya kuishi bure, na akaweza kusomeshwa bure? Na mtu mwingine asiyejilipua akaishi kwa kufanya kazi na kujisomesha mwenyewe (we know hoe difficult that is); Au na mwingine anayeishi kwa kutumiwa pesa kutoka bongo. Katika hawa watatu nani mjanja?
    NAKUOMBA BWANA MICHUZI UITUNDIKE MADA HII IJADILIWE.

    WAKATABAHU

    ReplyDelete
  2. How long a minute is, depends on what side of the toilet door you're on.

    ReplyDelete
  3. How long a minute is, depends on what side of the toilet door you're on.

    ReplyDelete
  4. Suala la Vyoo linaweza kuonekana kama utani lakini ni Zito kwelikweli na halina budi kuhusishwa na Suala la MajiTaka "Sewage Disposal".Kwa jiji la D'Salaam ili tatizo la kuzagaa kwa majitaka liweze kupungua na hatimaye limalizike kabisa natoa pendekezo kwamba upo umuhimu wa kuzitenganisha hizi idara mbili za MajiSafi na MajiTaka ili ziwe mbili tofauti kabisa na kila moja ijitegemee.Kazi ya kusafisha vyoo au mashimo ya majitaka ni kazi ya suluba sana na inayo hitaji mishahara na malipo makubwa zaidi pamoja na Bima ya Afya kwa wafanyakazi.Idara ikijitegemea yenyewe,mishahara ikawa mizuri na ya kuvutia,wafanyakazi wakapewa bima ya afya,na pensheni zao zikawa za kuvutia basi yatatokea mabadiliko makubwa zaidi.Tufanye mambo haya kwa vitendo tuache maneno matupu.MajiTaka sambamba na Ujenzi wa Vyoo Vya Kisasa katika kila nyumba.Kwa sababu jiografia ya D'Salaam ni tambarare kwa sehemu kubwa basi jiji ligawanywe katika zoni nne au zaidi na katika kila zoni njia za maji machafu au majitaka zielekezwe katika Dampo hilo la zoni na utaratibu utafanyika wa kuyafyonza majitaka ya kila zoni kwenda kuyatupa mahali patakapo chaguliwa kwa kazi hiyo.Katika Miji yetu mingine,kwa mfano Mwanza,zaidi ya robotatu ya wakazi wa jiji hawajaunganishwa katika gridi ya jiji ya majitaka!Nyumba nyingi hususan za milimani hazina mifumo mizuri ya vyoo na majitaka.Tuondokane na ile dhana ya kiswahili kwamba Mswahili akijenga nyumba kwake ubora wa choo hauna umuhimu!Atajenga nyumba yote imalizike lakini atasahau kujenga choo.Mwishoni kabisa ndipo atakapokumbuka umuhimu wa choo,na chumba chenyewe kitakachojengwa kwa ajili ya choo Mungu nihurumie!Katika ramani ya nyumba,jamani,sehemu ya Jiko na sehemu ya Choo na Bafu lazima zipewe umuhimu mkubwa unaostahili!Tubadilike.Tatizo la vyoo katika shule za msingi ndiyo kubwa zaidi!wanafunzi elfu moja wanalazimika kutumia tundu moja la choo katika shule nyingi za msingi.Hii ni hatari.Shule nyingi za msingi hazina bomba za maji salama.Nyingi bomba zake zilikatwa na Mamlaka za Majisafi na Majitaka katika miji husika kwa kushindwa kulipa bili za majikwa muda mrefu.Suala hili liangaliwe upya na wizara ya elimu kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika.Huwezi kuzungumzia Vyoo salama bila kuzungumzia upatikanaji wa maji safi na salama kama vile ambavyo huwezi kuacha kuzungumzia utupaji wa majitaka katika hali ya kiafya!Ni masuala madogo sana (bread and butter issues)lakini yanatushinda watanzania pamoja na madhahabu yote haya yaliyopo wajameni!

    ReplyDelete
  5. Choo ni sehemu ambayo isipoangaliwa vizuri na kutunzwa basi ni chimbuko la magonjwa na matatizo mengi ya kiafya. Inasikitisha kuwa suala hili katika jamii zetu halitiliwi maanani na vyoo havitunzwi na kuwekwa katika hali ya usafi. Matokeo yake magonjwa mengi ambayo yanaweza kuepukika kirahisi yanatatiza jamii. Shime tuimarishe usafi wa vyoo na kutunza afya zetu.

    ReplyDelete
  6. Michu

    Wadau wa blogu hii naungana na wanadunia woe kuadhimisha siku ya vyoo(ningeomba waongeze na bafu pia).

    Hizi ni sehemu maalum katika maisha y mwanadamu. Ni sehemu ambazo zinakamilisha moja ya matukio 7 ya mwanadamu ambayo ni kupumua, kula, kuzaliana,kutoa uchafu, n.k.

    Kwa maana hiyo basi choo nacho kinatakiwa kipewe umuhimu kama ilivyo kwa sehemu za msosi, uzazi, kulala,etc. Vile vile inatakiwa tukumbuke kuwa chooni ndio sehemu pekee ambayo huwa tunaweza kuwa tuko peke yetu kabisa hivyo ukipafanya pawe pazuri na pa kuvutia hutaona tabu kuingia na kufanya shughuli yako.

    Wadau tupende vyoo vyetu kwa uwezo wetu.

    ReplyDelete
  7. chooni ni mshauri wanguvu kwani nikigombana na mama watoto huwa naenda chooni kutafakari nikirudi nampa kisi halafu namwambia tuna bahati saana juu twapendana.

    ReplyDelete
  8. Issue ya choo jamani sio ya mchezo. Kwa mlio huko majuu mnajua wenyewe... uzoefu wa huko sina ila kwetu hapa Bongo ni magonjwa mengi ambayo asili yake ni kutokuwa na vyoo au kuwa na vyoo vibovu/vichafu au kwa wengine visivyo na mfumo mzuri wa kusukuma uchafu. Hivyo kwa kusaidia kupunguza tatizo hilo nadhani ni wakti mwafaka sasa kuwa kila mwenye nyumba ahakikishe amejenga choo kizuri; kwani huko ndiko mahala pekee mtu hukamilisha alichokikusudia kukifanya tena bila ya ucheleweshwaji wowote, sasa ili kuboresha zoezi hilo basi vyoo viwe safi na salama jamani kwa mtumiaji. Sasa ndugu yangu Michuzi nina kaswali ka uzushi kidogo kuhusiana na zoezi la kujisaidia naomba wadau wanieleze... kujisaidia(hasa haja kubwa) iwe kwenye choo cha kisasa, kibovu au hata iwe porini na wengine kule pwani kweupee!! Ni vipi mtu akitaka kujisaidia akifika sehemu aliyoamua kutimiza haja zake ni lazima ageukie kule alikotoka ndipo aendelee na zoezi???

    ReplyDelete
  9. nini iki,,,
    MWANZA NUSU MILLION YA WATU HAWANA CHOO,,,CAN YU IMAGINE TENA MJI UMEJENGWA VILIMANI??teh teh teh
    ILA JAMAA WA UKU WASHASHI,GETE-GETE NK NI VICHEKESHO WACHAFU KINOMA (ila sio wote)
    BT NUSU MILLION NI WENGI ATI!!!
    hii ni true newz siku ya choo duniani takwimu izi zilitolewa napo nafikiri ni kiduchu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...