Hizi taa za solar , zinatumia betri yenye kutumia mionzi ya jua , zinatengenzwa na WODSTA , (Women Development for Science and Technology Association ) huko Arusha. Hakuna haja ya giza kijijini jamani .
Hizo bulbu ndogo zinawekwa kwenye mfuniko wa chupa ya plastiki iliokuwa inahifadhi maji .( Recycled water bottles bulb covers ) System nzima ni betri ndogo inayodumu miaka mitatu na taa tatu .
Inagharimu kama $100 za kimarekani . Kwa kweli huwezi kulinganisha na gharama ya kuvuta umeme na bili za kila mwezi . Waliotaka kuwajengea mama zao au ndugu zao yale “majiko ya mama”
tuma email
kwa taarifa zaidi.
Muda umefika jamani wa kuunga mkono bidhaa zetu za kiTanzania zenye kustahili.
Mdau Msafiri SS
JAMANI TUACHE USANII, HIVI HAWA AKINAMAMA WANATENGENEZA HIZI TAA AU WANAAGIZA ZIKIWA TAYARI ZIMETENGANEZWA TOKA NJE? NIJUAVYO TANZANIA HATUNA KIWANDA KINACHOTENGENEZA VIFAA VYA SOLAR IKIWA PANEL, BULB NA BETRI YAKE.
ReplyDeletemimi nina kibanda changu/boys kota shambani kwangu mlingotini bagamoyo nimevutiwa sana na umeme hu,nitawapataje hao wamama ili wakanifungie kwenye hicho kibanda changu.Transport cost itakuwa juu yangu au? Grama za fundi ni inclusive ua ? Maelezo zaidi pleaseeee!!!!
ReplyDelete