Mhe. Balozi wa ZAIN,
Pongezi nyingi kwa kuchaguliwa kwako kuwa balozi wa kampuni yetu mkubwa na inayofanya mambo ya maendeleo kwa jamii kwa ujumla. Nafurahi kusema kuwa ZAIN hawakukosea kukuteua wewe kuwa balozi wao kwani blog yako maarufu inasomwa na watu wengi kila pembe ya dunia hii. Hongera Bw. Michuzi.
Lengo kuu la kuandika maneno haya machache kwako ni kutoa kero yangu kwako wewe balozi wa ZAIN kuhusu tangazo linaendelea kwenye vyombo vya habari linalohusu "promotion ya jiachie" sitaweza kuandika maneno yote ila sauti ya kike inasema "James mbona leo umenipa moja au ..... ukweli ni kuwa tangazo hilo halina ujumbe wowote wa kufurahisha zaidi ya kukera.... halifurahishi kusikika masikioni kabisa au tuseme halina mvuto kabisa.
Naomba kutoa ushauri kwenu ZAIN mliondoe kabisa na kutafuta maneno mengine ambayo yataleta maana na kufurahisha jamii. Kero hii iwekwe kwenye blog ya jamii ili kupata maoni ya wale ambao wanasikia tangazo hilo.
Asante ni mimi
Mdau Blog Jamii


We mdau, acha fix zako! Lile ni bonge la Tangazo wewe! Lile bonge la Tangazo kwa kweli. Labda wewe una matatizo yako ya kijinsia na kisakologia. Mimi siyo mteja wa Zain, ila nikisia ile add, moyo wangu unatulia kabisa!
ReplyDeleteMh. Michu, wewe ukiwa kama Balozi wa Zain, nafikiri ujumbe huu ungeufikisha kunakohusika - idara ya masoko na mauzo- baadala ya kuanika hadharani hapa
ReplyDeleteMimi sijaona kero bali naona kuwa Michuzi ana changamoto katika mgongano wa mapendeleo kati ya upande mmoja wa KUENDELEA KUIFANYA HII BLOGU KUWA YA JAMII NA HIVYO KUWAPA COVERAGE SAWA WANAJAMII, ASASI NA BIASHARA ZOTE SAWIA NA upande mwingine, KUTETEA NAFASI YAKE YA UBALOZI WA ZAIN KUWANYANYUA KIBIASHARA DHIDI YA WASHINDANI WAO KWA KUTUMIA MTANDAO HUU.
ReplyDeleteUSHAURI WA BURE:
Kaka Michuzi katika hili unaweza kujifunza kwa mfano wa Oprah alipokataa kuwaita wagombea katika SHOW YAKE YA JAMII ingawa alikuwa kati ya washabiki wakubwa wa awali wa Obama.
Nakubaliana na mtoa hoja, unless umalizie maneno ya hiyo komasho ili tuanalyze zaidi, but the way ulivoiandika, it sounds kind of creepy! nisingependa kuwa nimekaa na wazazi wangu au siblings wangu na komasho yenye hayo maneno ikawa hewani, sound kinda dirty!
ReplyDeleteMh. Deval Patrick.
Binti anamwambia jamaa ktk sauti ya mapenzi "james mbona leo umenipa mojaaaaa!!!!" msichana analalamika akionyesha njaa kali ya mahaba, kana kwamba mrembo huyo hatosheki, au hajafikishwa. Tangazo linapoanza kama upo na watoto its ok, cause they dont interpret much. lakini kwa sisi watu wazima ni aibu hasa unapokuwa na watu wa heshima. Litakuwa jambo la busara ZAIN wakiliondoa. kama wame-target soko la vijana wahuni wahuni wasio na aibu, basi wajue kuna watu wengi wanaowasikiliza. Waangalie biashara na ustawi wa jamii pia.
ReplyDeleteMdau
Binafsi naona Tangazo hilo halina maadili. Na sio hilo la zain tu, yako mengi sasa hivi. Kuna lile la redio linalosema 'mbona umechomoa, chomeka mpenzi', Lingine linasema, mbona umenipa moja tu mpenzi au unampa mwingine? Serikali imechapa usingizi?
ReplyDeleteKiukweli kwangu mimi Tangazo lile naliita Tangazo TATA! Ni vyema likaondoshwa. Inabidi ZAIN na makampuni mengine yawe makini saana katika kuandaa matangazo yao ili yasilete utata, na wajaribu pia kusoma na kuyafanyia kazi maoni ya wateja wao katika kuboresha huduma zao. Zain kazi nzuri.
ReplyDeletewadau lazima tukubaliane lile tangazo la zain wanangu ukikaa na fadher kimfano au madher unajuwa inakuwa ngumu kulisikiliza lile tangazo silo kabisaaaaaaaaa.kwa maadili ya kibongo mdau ngatunga from TMK.
ReplyDeleteHilo tangazo halina tatizo kabisa, wewe mwenyewe ndo una matatizo.
ReplyDeleteBig Sam
Kiukweli kwangu mimi Tangazo lile naliita Tangazo TATA! Ni vyema likaondoshwa. Inabidi ZAIN na makampuni mengine yawe makini saana katika kuandaa matangazo yao ili yasilete utata, na wajaribu pia kusoma na kuyafanyia kazi maoni ya wateja wao katika kuboresha huduma zao. Zain kazi nzuri.
ReplyDeleteTusidanganyane, tangazo la Zain kuhusu Jiachie halifurajhishi na lina matukanyo, tusitoe maoni kwa jazba. Tangazo halifai kabisa. Ashakum si matusi binti analamika kupewa kimoja na anadai eti Hunipi tena kingine? haiona uhusiano na lengo la kutuma SMS. Nashauri tangazo libadilishwe kama kweli tunajali maadili ya asili ya kitanzania.
ReplyDeleteni mimi Andrew Chakupewa-mzee wa manzese
lile tangazo sio lenyewe kabisa mazee, fanyeni mpango wa kuliondoa, kulilea ni sawa na kulea ugonjwa. its true kwamba linavuta hisia za watu wengi, maana mtu akilisikiliza atakuwa na hamu ya kuona linaishia wapi ila kama mstaarabu mwisho wake doesnt sound gud kabisa
ReplyDeletemimi ni mpya kunako blogu kwa upande wa kuandika meseji bt 4 ril lile tangazo sio i hed it mara ya kwanza i was like what z this nkajijibu mwenyewe labda ndo maendeleo kiukwel dats nat gud kibiashara na kijamiii, km baloz plizzzz do wat u kan
ReplyDeleteToeni hilo tangazo haraka sana na siku nyingine muwe mna editor wa matangazo yenu kabla ya kuyaweka hewana otherwise mtakuja kuharibu biashara yenu .ni Mtazamo wa wangu na watanzania walio wengi.
ReplyDeleteTangazo ka Zain linatia kichefuchefu, linapoanza linakera linapoisha ndio linasema kichaa kapewa lungu, sasa inamaana wateja wa Zain ni vichaaa? ati balozi naomba msaada?
ReplyDeleteTangao ukilianalyze, halina neno baya. Ila lina viashirio vinavyolenga kwenye mahaba. HALISOUND VIZURI.
ReplyDeleteMheshimiwa balozi, tufikishie hilo, kwa Zain.
Pia tunaomba utufikishie ujumbe kuwa hata na lile la jiuisi lisitangazwe. Lile la akina Joti lenye maneno "wachomoa kisha wachomeka" haliashiriii kitu kizuri na ukichukulia tangazo lenyewe linapendwa na watoto.
Brother Michuzi,tangazo la ZAIN nila kusikitisha , and that is to say the least.Kulinganisha maongezi ya simu na NGONO si suala la heshima au lenye maadili yanayoeleweka kwa mtanzania aliye na akili timamu.Nilikuwa na mpago wa kujiunga na ZAIN lakini nimeghairi, nisingependa kujihusisha na likampuni la NGONO.
ReplyDeleteMichuzi fanya hima kama balozi wa zain uwafikishie ujumbe, tangazo linatia aibu hasa mkiwa watu wa rika tofauti. Naelewa kuwa watu wengi wapenda kutumia vitu au maneno ya mahusiano ili kuvuta watu , lakini kwa kampuni kubwa kama zain ni kujishushia hadhi na kupoteza muelekeo. Ushauri wa bure kwa zain na makampuni mengine, hayo makampuni ya masoko mnayo ya subcontract wawatengenezee matangazo yenu, inabidi mpitie kazi na kuhakiki, kwani mnaajiri wataalam wa nini? si kila kitu mnacholetewa mkipitishe.
ReplyDeleteNaomba kunukuu maneno ya mchekeshaji mmoja kuwa ' ni uhuni mtupu' mliondoe mnatusababishia embarassment zisiko na msing.
Mdau, Mikocheni- DSM
mimi pia siliungiki mkono hilo na hata yanayofanana na hayo yananitia kichefuchefu nimefikiria hata kuhama zain. Lazima kutunza maadili na heshima katika swala la matangazo, mkijua kuwa matangazo yanasikiwa na watu wa rika zote.
ReplyDeleteHii inasemeka kabsaaa!!!..No wonder ile kampuni yenye rangi ya Blue na Nyeupe inazidi kuwa namba wani mwaka hadi mwaka, sasa na vijitangazo vyenu vya kuudhi watu, mnadhani mnafanya marketing ya maana,. alafu huyu lazima ni yule jamaa aliyetoka kampuni flani maana yeye ndio alipeleka Idea ya kutengeneza tangazo lao linasema "KATA WEWE, AAH BWANA KATA WEWE" kama sio u***** ni nini wafikiri? Hebu igeni makampuni ya wapinzani wetu wa jadi, kwa mfano MTN, SAFARICOM, ZAIN KEN, ZAIN UG,UTL, WARID UG...Wako JUU!
ReplyDeleteSina mengi ila KIMAADILI lile tangazo halijakaa sawa. Michu tunaomba uwe mjumbe wetu, WALIBORESHE liweze kuleta maana halisi inayokusudiwa. Jinsi lilivyo naona kama linapoteza jamii tu!! Ahsante kwa mdau uloleta hii mada. Nagira!!
ReplyDeleteHALIFAI NASHAURI LIONDOLEWE KWA KUWA MSG YAKE NI YA KIHUNI NA SAUTI YA YULE DADA KAMA YUPO KITANDANI ANAHITAJI (NEED SOME MORE) INAKERA KWA KWELI HASA TUWAPO KATIKA DALADALA ASUBUHI TWAENDA KAZINI UMEKAA NA MTU MZIMA RIKA LA BABA YAKO AU MAMA YAKO THEN LINASIKIKA TANGAZO HILO DUUH! NATAMANI NITOKEE DIRISHANI. TUFIKIRIENI WADAU PLIZ.
ReplyDeleteKila nisikiapo hilo tangazo huwa nafeel kuwa embarrased!!!!!!!! Nanyori.
ReplyDeleteKwa hizi comments hapo ndo utajua unafiki wa Wabongo, hadharani wanajifanya ni watu wa maadili kwelikweli wanajifanya ''wanapiga vita uasherati kwa nguvu zote'' sasa subiri wakishakuwa faragha, hayo maneno wanayotamka, hayo matendo wanayofanya, mmh! matokeo yake ukimwi unaongezeka! mimba kibao, etc. Mi nawashauri wabongo wenzangu tuwe watu wa maadili kuanzia rohoni na sio juu juu tu!
ReplyDeletejamani tangazo la kina joti la juice..eti unachomoa...unachomeka alafu unavyonzaaa! uchafu mtupu!
ReplyDeletenaungana na mdau hapo juu ukitaka kujua wabongo hatuna adabu nenda kwenye ile blogu ya matusi matusi sijui utamu sijui upuuzi gani! yani matusi ya humo..alafu unakuta ni mibaba na mimama yenye akili zao badala ya kufanya kazi(wa hapa bongo) au kubeba maboxi(wabongo wa nje) wanashinda wakitukanana!wabongo hamjiheshimu mfano mzuri ni huyo utamu mwenyewe..kaka michu inabidi siku moja umuwekee topic huyo mpuuzi wa maadili!
ReplyDeleteunayesema wabongowanafiki inaelekea hujaelewa mada hapa, hapa linazungumziwa tangazo linalotolewa hadharani wkati wowote kusikilizwa na mtu yeyote... we unazungumzia mambo ya faragha? au website za matusi sasa ukienda huko si umependa mwenyewe? lakini hapa tunazungumziwa tangazo linalotolewa kwenye vyombo vya habari vinavyosikiwa na jamii nzima ndio. Jitahidi kuwa mwelewa wa kinachozungimziwa. asante
ReplyDeleteNa kweli inaelekea hajaelewa mada kabisa. Faragha ni faragha, na ndiyo mana ikaitwa faragha vinginevyo watu wangefanyia kwenye public like kwenye daladala, barabarani etc. Na hizo blogs za matusi like utamu ni wewe binafsi unaamua kuingia humo kwa hiyo ni private yako, huwezi linganisha na hilo tangazo la ZAIN linalosikika na watu wote kwenye public bilq kujali jinsia wala umri. RESPECT!!
ReplyDeleteNakubaliana na wenzangu apo juu, ni tangazo bovu kuliko matangazo mengine yote niliyo pata kuyasikia kwenye masikio yangu.
ReplyDeleteKama idara ya matangazo ya zain ilijua apo ndipo itakapo konga nyoyo za wasikilizaji naomba niwaambie kwamba mmechemsha vibaya mno.
Tunaomba lisitishwe haraka iwezekanavyo.
Mdau
TANGAZO NI KERO KUBWA SANA
ReplyDeleteKatika siku niliyofurahi ni leo nilipokuta hii msg sijafungua site yako siku nyingi kaka. Kwanza napenda kumpongeza mdau aliyetuma hiyo kero. Nilikua sijui nianzie wapi. ASANTE BALOZI
Jamani hata mimi hilo tangazo limenikwaza sana nilikuwa tu sijui nisemee wapi nilishawaza hata kuandika barua kwa wahariri mbalimbali wa magazeti. Yaani halifai kabisa ina maana huko zain huwa hawajadiliani kwanza na kupitia matangazo kabla hayajarushwa. MBONA WANAFANYA MAMBO KIHUNI JAMANI?
ReplyDeletemimi binafsi sijawahi kuona tangazo la zain ambalo lina mvuto, mbali la hili ambalo ndio linatia aibu. hata tigo ambayo haifanyi vizuri wana matangazo mazuri kupita hao zain, naomba waamke, matangazo ni muhimu sana katika bishara.
ReplyDeleteKaka Michuzi naomba kusema asante kwa hili kero. Inanikeraga sana loh!
ReplyDeleteWEngine tumelelewa kimaadili. hivyo basi unapokuwa na mzazi wako sting room mkijadiliana kuhusu maisha au masomo, halafu tangazo kama lile linasikika, kwa kweli (its not fair)Ni bora likaondolewa kabisaaaaaaaaa litafutwe lingine lenye kutoa maana nzuri kwa jamii inayozunguka. BALOZI WA ZAIN, FIKISHA UJUMBE HUU TAFATHALI
ReplyDelete