napiga mchi kijijini ng'wanswenhele katika kata ya iseni wilaya ya kwimba. hapo usipotwanga na na kupepeta unaweza kuula wa chuya.... mwanakijiji upo???
kliniki ya watoto kijijini hapo. hapo mtoto anadandia mzani na kubembea huku kazi ya kusoma vipimo ikiendelea. kwimba oye!


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Jamani huyo mtoto si ataanguka? Kweli tembea uone. Kwimba oyeeeee

    ReplyDelete
  2. Ee bwana hapo umenikumbusha mbali kijijini kwetu huko nassa, wilayani magu. Haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania, kweli safari bado ndefu.

    ReplyDelete
  3. Tabu yote hii ni kwa sababu ya ufisadi, yaani mtu anakosa hata pesa ya kwenda kukoboa mpunga mashineni!!

    ReplyDelete
  4. Matokeo ya ufisadi hayo. Kazi kwelikweli!!

    ReplyDelete
  5. Mheshimiwa, kutwanga huko ni kwa wema gani?

    ReplyDelete
  6. Mkuu nakuona tuu, ila angalia viganja hujazoea hayo mambo tuachie sisi tuliyo yazoea, usije ukashindwa kuandika bure! Ha ha haaaa....!!!!! Napiga mchi? Mhhh....kwa vijana hapo sijui utaelewekaje.

    ReplyDelete
  7. Huku ndugu yangu Chuuuuzi lazima uozwe Mke!Kama Bunduki haina Risasi itakuwa Sorry Mze,utabaki unaichungulia tu!

    ReplyDelete
  8. Hii inaonyesha jinsi gani maisha ya Mtz yalivyo mabaya. Sasa hawa Mafisadi na mawaziri wanapokuwa wanakula mali ya umma huwa hawaangalii hali hiyo ya mkulima wa jembe la mkono wanapo muibia? Hebu sheria iendelee kuwaweka huko rumande mpanka hayo matumbo yao yale maharage na kupata vidonda vya tumbo au TB liwakute huko kama wafungwa wengine watokao huko wakiwa tayari taabani! Mungu wafungue macho mapema watanzania ili wapate kuondokana na hayo maovu kama vile pepo wabaya waondokapo wakati wa mapambazuko. Mungu bariki Tanzania.

    ReplyDelete
  9. Oyeeeeeeeeeeh!
    Kwimba Oyeeeh!
    Mafisadi Ziii!

    ReplyDelete
  10. HEEEEE WEE MICHU,UJATULIA KBS
    SAA NDO NINI UKIWA NA MOKAS,JEANS,ZE NEW FULANAZZZ???NDO WENZIO WATWANGAGA IVO???
    SOOO INNOCENT LIFE JAMANA I MISS IT

    ReplyDelete
  11. mhh mkuu wa wilaya piga mchi kwa kishindo vinginevo hupati lunch manake naona kuku pembeni wana hasira yakumuona mgeni wanajua zao zimefika. maisha ya vijiji vetu magumu sana sasa huo mzani wa magunia ndo wanapimia watoto itabidi wabongo tuanzishe harambee za kuwachangia sehemu kama hizi. picha zinanikumbusha mbali na zinasikitisha kiasi ndo sababu mkuu wa wilaya blog ilikuwa kimya sehemu hii sidhani hata 3g yako inafanya kazi kweli> hapo ni km ngapi mpka mwanza mjini??

    ReplyDelete
  12. Picha kama hii inanifanya nijisikie uchungu na ni kumbukumbu ya tulikotoka. Je tunawezaje kuwasiadia kununua mizani? Kuna namna yoyote ya kuweza kuwatumia either mizani au hela wakanunue wenyewe?

    ReplyDelete
  13. NJIA PEKEE YA KUSAIDIA KUPATIKANA PESA ZA KUNUNULIA HIZO MEZANI KWA HAO NA WENGINEO NCHINI KOTE NI KUHAKIKISHA KUWA WALE AMBAO WANAIIBIA NA WALIYOIIBIA NCHI KWA MABILIONI WANAKAMATWA WOTE, WANATUPWA JELA NA MALI ZAO ZA NDANI NA NJE YA NCHI KUFILISIWA

    ReplyDelete
  14. You see the greatness of the country, by looking how it treats its vulnerable.

    We all feel your pain.

    HATA MIZANI BASI????

    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  15. inapendeza sana bwana michuzi.

    ReplyDelete
  16. MWANAWANE SALAMU KWA BIBI NG'WANANG'WALWE WA NGUDULUGULU
    SHANGAZI NG'WABESH AKIWA NYAMBITHI GINERY
    TATU KWA MJOMBA MASHIMBA AKIWA MWABUKI NA SHANGAZI MBISE AKIWA MASWA. UJUMBE TUDUMISHE KILIMO CHA PAMBA.
    MATHIAS YAYABUYAGA

    ReplyDelete
  17. Mh. Balozi, huo usimamaji, mmm mmhu mhu, unatia shaka. Afu nasikia huko ka waenda oa ni lazima wakupe gunia zima utwange!!!! Saasa, balozi!! naona upo hoi mkuu wangu. Ah, ndo maisha.

    Mpiga Box nimechoka na Box, lakini hii picha nimecheka sana, wajua huku ughaibuni waweza kaa mwezi hujacheka, sasa unapopata kama hizi siku moja moja inakuwa faraja kweli kweli. Duu, nimefurahi sana.

    Sasa ndugu zangu, hasa wale tulio ughaibuni, Mh. katuletea picha ya hali halisi ya vijijini kwetu ambapo kwayo wengi wetu tumekulia. Najua adha ya box wakuu wangu, ila inafika pahala (Mahala kama sijakosea) inabidi tufikirie ndugu na jamaa zetu tulowaacha huko vijijni.

    Binafsi (Mimi Mpiga Box) nadhani sasa wakti umefika, kupitia jumuiya zetu ughaibuni, na matawi ya chama cha nahii tujikusanye, walau hata kwa dola moja moja, pound moja moja na kama sio Euro moja moja mathalani tuchange na hata Mh balozi anaweza kuwa balozi wetu japo tuwajengee ndg zetu walau Cliniki kwa ajili ya kina mama na kama sio kutoa misaada ya mizani na vitu vidogo vidogo vitakavyo wasaidia. Suala la kupiga kelele sijui mafisadi, watu gani halitawasaidia sana. Shime ndugu zangu. hayo ni mawazo tu hasa kwa viongozi wetu wa jumuiya zetu na mashina yetu yaliyoshamiri pote ughaibuni.

    Kabla sijamaliza, napenda kurudia tena, hayo ni mawazo yangu Mpiga Box binafsi. Lakini pia kwa wenzangu na miye waosha vinywa halika dhalika yaweza kuwa burudani kwao na sehemu ya kutuondolea uchovu.

    Wakatabahu.

    MBxc

    ReplyDelete
  18. Jamani tooooo Sad. Kama tunachanga kwa mengine basi hata tujichangishe wapate mzani wa kukanyaga.

    Kutoa ni moyo jana nimeona kwenye CNN hero ...nanny kutoka malawi anashule yake na kila mwezi anapeleka 1000....well ni nanny wa ricky lake but still ni wangapi can afford to do that but never think about it?

    Michuzi ukirudi huko andika note ya mambo amabayo siye wananchi tunaweza kujichangisha kuwasaidia. Tukisubiri serikali yetu mpaka ije ikumbuke watu wa vijijini sio leo wala kesho

    ReplyDelete
  19. Sheikh Michuzi inaonekana weye umeamua kupiga hiyo picha kuzuga watu. wewe umeshika gongo na si mchi kama mchi unaavyofahamika. Kama huyo mama anadai huo ndio mchi wake basi lazima awe ni mjane au mme wake ni mlevi mbwa. Sheikh mchi ni kama bati mbili (200) hivyo ukitoa kama mia tano annunue michi safi bila shaka huyo mama atakukumbuka milele

    ReplyDelete
  20. Haiambatani na picha. Lakini stori hii ni ngumu:

    Museveni guards ransack EAC conference facility (in Arusha)
    The Monitor Fri, 28 Nov 2008 11:23 AM PST

    ReplyDelete
  21. Wewe unayesoma hapa sasa hivi ni mmoja kati ya watanzania wachache waliopata bahati kuaccess mtandao na ndiyo unaona kuwa wanavyoishi si sawasawa.

    Maisha bora yanatokana na kuzalisha bidhaa kwa wingi,
    Je umelitambua hilo?
    Je, umekwisha wasaidia hao ndugu zako kwa kiasi gani kuondokana na hali hiyo duni?
    Au ndiyo kawaida yetu kuwa hata yale matatizo yaliyo ndani ya uwezo ni lazima tutafute kisingizio?
    Kwa vile serikali si mtu basi lazima tulalamike tu? hatuna alternatives?

    ReplyDelete
  22. MICHUZI UNAKALIA KUTWANGA MPUNGA HATA KAZI HUFANYI, UMETUBOA LEO KWANI SISI WADAU TUMESHINDWA KUPATA MATOKEO YA TAIFA STARS NA SUDAN KATIKA MUDA MUAFAKA KUPITIA BLOGU YETU HII, MWANA KAMA KAZI ZINAKUSHINDA BINAFSISHA BLOGU, HATA TOA DEIWAKA PALE UNAPOPATA NAFASI UNASHIKA USUKANI.NI HAYO TU

    ReplyDelete
  23. Hiyo kutwanga inanikumbusha mbali sana. Enzi hizo bush wakati wa mavuno ya mpunga, unakoboa kwa kutwanga. Principle mojawapo ya kutwanga ni kwamba, Lazima mchi utue pale pale kwenye tundu ulipotua mchi wa kwanza, Ukikosea mchele wote unaruka pembeni na kutua nje ya kinu yaani chini. Sasa hapo ndipo utakapopata mabao na kuambiwa kama ulikuwa hutaki si ungeacha?.

    Zamani babu yangu alikuwa anasema mchele wa kukobolewa mashineni unanuka chuma anataka wa kutwanga. Ukimaliza hapo mikono yote ina malengelenge (yaani kama umeungua moto ikajaa maji ndani ya ngozi).

    ReplyDelete
  24. Mzee wa kutwanga na kupepeta mbona huleti matokeo ya starz? au no mtandaoooz huko Maswa mzee wa vijisenti kashejichukulia chake

    ReplyDelete
  25. Picha kama hizi ndiyo zinanifanya nipende kuangalia blog yako. No offense, hii ndiyo hali waliyo nayo ndugu zetu wengi mno hapo Tanzania. Zile picha zako za Dar tambarare yale ni maisha ya asilimia ndogo mno ya watanzania na most of them wameweza kuishi hivyo kwa gharama ya watanzania wengi wanaoishi far beyond poverty line. WE NEED CHANGE TO BRING HOPE IN OUR BELOVED COUNTRY FOR OUR BELOVED PEOPLE.

    ReplyDelete
  26. Nashangaa wachangiaji wengi humu ndani wamejaa ubinafsi...utasikia uchangiaji wao katika Picha ya hapo juu kuwa "huko ndiko tulikotoka", acheni unafiki na ubinafsi...mlikotoka ndiyo maana yake nini? bado mko huko huko..kama baba yako na mama yako au hata shangazi yako na binamu zenu bado wako huko...nadhani kwa kuihisi shida iliyoko huko ungesema angalia maisha yetu tunavyohangaika...na siyo angalia wao wanavyo hangaika....huu ubinafsi wa kujifanya kama vile mlitoroka shida ni ubinafsi usio na maana kwani hata wengine huko muliko tofauti mliyonayo nasisi ambao tunaishi huku au ndugu zetu bado wako huku nadhani ni ndogo sana kama kweli mnafikra za kizalendo.
    Huko mliko wengine mnafukuzwa na hata nauli za kuwaleta huku kwetu au kwa shangazi zenu hamna...mnachogombania ni kulipia bills hizo na kuishi kama maisha ya hand to mounth.....Watanzania mtakapo acha huo ulimbukeni wa kuwaita wao...wao na sisi..sisi, nawahakikishia hata huko mliko mtaishi kama watumwa tu.
    Tufike mahali hizi picha tuziite kuwa ni kwetu na tusianze kuwa na akili ya kitoto ya kuongea hata kwa kubana pua kuwa "huko ndiko tuliko toka"...bado tuko huko kwani ndiyo kwetu na hata kama hatuko huko tutarudu tu "dead or alive".

    Poleni sana watanzania kwa kupenda kujifanya kuwa kwenu kuitwe kwao...na kwa mtu makini atakuona kuwa huna mwelekeo maana inaonyesha huna kwenu...
    Jalibuni kukomaa kifikra na nawaambia hayo ni maendeleo wakati wengine tunazaliwa hata hiyo mizani haikuwepo hivyo hata uzito wetu kama walikuwa wanauandika ulikuwa wa kukisia.

    Michuzi nakushukuru kwa kuweza kutuletea hizo picha ilituwezekuona tuko mbali kiasi gani tukilinganishwa na wenzetu wa huku tulipokuja kwa muda ilitunaporudi kwetu Tanzania tuangalie ni mchango gani tunaweza kuwa nao hata wa mawazo ambao utatuwezesha kujikwamua na kwenda mbele.
    Dawa ya kutatua tatizo siyo kulikimbia na kukaa na kulitatua...maendeleo ya Tanzania yataletwa na watanzania wenyewe kwa hiyo hizi hoja za kwenu kuitwe kwao...binafsi naona ni kufilisika kimawazo.
    NAWASILISHA HOJA

    ReplyDelete
  27. mkuu hapo unanikumbusha kijiji changu cha lumuma wao i love that life it is so healthy to live like that.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...