Msanii kutoka Mombasa-Kenya Nyota ndogo akiwa na densa wake zawadi wakilipagawisha dume la kizenj pichani mbele ya wana wa kizenj
Baadhi ya wakazi wa zenj waliojitokeza jana usiku kwenye tamasha la fiesta jirambe 2008

Kikundi cha muziki wa asili cha Kindumbaki mjini Zanzibar kinachoongozwa na mzee Makame Fak kikiwa jukwaani kikiwatumbuiza wenyeji na wageni kutoka sehemu mbalimbali waliofika uwanjani hapo


Tamasha la fiesta jirambe 2008 jana usiku ilikuwa ndio kilele chake rasmi kwa wakazi wa Zenj,ambapo umati wa watu ulijitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mao Tse-Tung uliopo Michenzani kuwashuhudia wasanii mbalimbali wakitumbuiza katika tamasha hilo jana usiku.Pichani ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Bushoke akiwakumbusha washabiki wake baaadhi nyimbo zake ukiwemo ule wa barua.Kwa picha zaidi ya tamasha hilo ingia michuzijr.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kweli yakhe! Kule kwetu umefika sana. Twashukuru kwa kutuletea Fiesta. Karibu tena yakhe

    ReplyDelete
  2. Cheki wenyewe walivyotulia kama wanaangalia sinema vile.Usiniambie ilikuwa poa kivile coz hapo sioni uhai.

    People of DSM na Mwanza ndo wanajua kuparty!

    ReplyDelete
  3. marekebisho madogo tu uwanja wa Mao Tse-Tung haupo michenzani upo kikwajuni au kwa jina jengine ni kiski

    ReplyDelete
  4. Michuzi,

    Hawa waliohudhuria hapa almost ni watu kutoka Tanganyika au wazanzibara ambao wamevinjari kuona milka na silka za watu wa Zanzibar zinapotea kabisa ili shetani atawale Zanzibar. Wanataka kuizima Nuru ya Allah kwa vinywa vyao na matendo yao. Lakini inshallah na sisi tutahakikisha hilo litashindikana kwa uwezo wa Allah.

    Ndio ukaona sherehe zote za ubilisi na ushetani zinaletwa Zanzibar.

    ReplyDelete
  5. We anon November 16, 2008 6:50 PM
    acha ubaguzi. Unaleta ubaguzi hata kwenye matamsasha!!Umeona dili sana huko zanzibar? hamna lolote nyinyi kila kitu mnategemea kutoka bara, kuanzia nyanya,mboga nk.
    Unaletea mambo ya udini hapa??
    Ushindwe na tena ulegeee

    ReplyDelete
  6. mabo ya usheitwani na uilisi waletwa zenji??? wee annon una maluhani nini???
    ivi mashoga na wasagaji wako wapi??afu watu wengine kujiona wako peponi aya hama basi uende paradiso
    hahahahhaaaaaa
    eti zenji "watakatifu"duh kazi ipo na hii tanganyika/zanzibar(pemba na unguja)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...