leo nilikuwa katika msafara wa ushenga ulioongozwa na kaka ahmed kipozi (shoto, nyuma) pamoja na mdau misanya bingi (kati) pamoja na aboubakary liongo kwa mzee mvungi sehemu za mbezi samaki. misanya bingi, ambaye umahiri wake katika utangazaji pale itv unakumbukwa hadi leo, hivi sasa ni mhadhiri msaidizi idara ya sosholojia (sio biashara, samahani kidole hakina breki) wa chuo kikuu udsm na kipozi pia anafundisha chuo kikuu cha kiisalamu mji kasoro bahari. abou ni mtangazaji idhaa ya kiswahili sauti ya ujerumani na yupo vekesheni bongo kwa sasa. mtarajiwa ni mdau adolf wembo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya burundi ambaye anaishi essen, ujerumani. taarifa zaidi zitakuja baadaye majibu yakitoka...
leo nilikuwa katika msafara wa ushenga ulioongozwa na kaka ahmed kipozi (shoto, nyuma) pamoja na mdau misanya bingi (kati) pamoja na aboubakary liongo kwa mzee mvungi sehemu za mbezi samaki. misanya bingi, ambaye umahiri wake katika utangazaji pale itv unakumbukwa hadi leo, hivi sasa ni mhadhiri msaidizi idara ya sosholojia (sio biashara, samahani kidole hakina breki) wa chuo kikuu udsm na kipozi pia anafundisha chuo kikuu cha kiisalamu mji kasoro bahari. abou ni mtangazaji idhaa ya kiswahili sauti ya ujerumani na yupo vekesheni bongo kwa sasa. mtarajiwa ni mdau adolf wembo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya burundi ambaye anaishi essen, ujerumani. taarifa zaidi zitakuja baadaye majibu yakitoka...

Ehh bwana kumbe Misanya Bingi sasa hivi Lecturer!! Aisee hongera sana, mi nilijua tu maana hiko kichwa kilikua si mchezo. Kule ITV ulikua una underutilise brain yako mzee!! Bila shaka karibuni tutasikia umekua daktari.
ReplyDeleteBig up sana in academics, ingawa tunakumiss sana kny utangazaji. Labda unaweza kua unasaidi hapo mlimani redio kwa kujitolea tu; hata kama ni mara moja kwa mwezi, tutafurahi sana kusikia sauti yako tena!
KWA HIYO WATANGAZAJI WA ITV NI WALE WALIOKUWA WANASHIKA MKIA EEH. THATS EXPLAINS
ReplyDeleteDu yaani Misanya ni Mhadhiri Chuo Kikuu. Mimi nilikuwa na undermine uwezo wake alipokuwa ITV, ila sina uhakika sana na hicho kichwa. Labda wanafunzi wake watatueleza. Hata hivyo hongera sana kaka...
ReplyDeleteNyie watu wa hapo juu. Kwani kuwa mhadhiri siku hizi deal? Mi nawajua watu wengi tu waliokataa hiyo kazi na kwenda kwenye mashirika. Mshahara kidogo. Huwezi kulinganisha Injinia mwalimu na Injinia wa say Vodacom.
ReplyDeleteHivi kwani uhadhiri ni nini hasa. master degree unakua mhadhiri bongo...I don't yhink it is a big deal kwa vile mjomba wangu ni mhadhiri pia hapo na kila siku anatafuta pa kukimbilia
ReplyDeleteNashe anaolewa?
ReplyDeletekazi ni mtu aipendayo sio mshahara tu.acha maneno ya kimaskini wa juu hapo
ReplyDeleteMisanya Bingi yuko faculty of arts and social sciences not biashara, although wewe mdau mwenye mawazo mafupi ya engineer wa vodacom na engineer mwalimu, mawazo yako mafupi sana wewe, tena sana !!! engineer mwalimu ni discussant kwenye kila engineering whatever ya nchi hii, engineer mwalimu ni consultant wa mambo kibao ya engineering ya nchi hii the difference is..............engineer wa vodacom ni engineer wa vodacom tu ! kalagha baho !!!
ReplyDeletejamani fanyeni kazi mnayopenda sio mshahara tu kweli na kubaliana na jamaa aliyesema hivyo. kengine watanzania tufanyeni kazi tulizosomea sio umesomea udaktari ukifika tz unagombania ubunge na kuwa waziri wa fedha fanya kazi yako usaidie wananchi wako kama daktari mungu ndio kakupa uwezo huo usikimbilie tamaa ya pesa ndomana nchi yetu inaumia.
ReplyDeletewaache..waosha vinywa waendelee..kazi ni kazi bwana!!!Shwari ndugu yangu Bingi...nakukumbuka sana ulivyokuwa headboy wetu pale Dom Sec 1989,mie nikiwa form one..keep up man!!!
ReplyDeleteBig up Misanya, lol. Nakumbuka enzi za Dom Sec tulikuwa tunacheza mechi Form One na Form Two wewe ulikuwa form two. Mshikaji wangu Majaliwa alikupiga kichwa ukazimia, lol. Keep on keeping on.
ReplyDeleteOk, kumbe bado kuna watu wanafanya kazi kwa ujiko tu. Sawa. Lakini wengi tunapenda pesa na maisha mazuri (bila ya kuiba). Kwa hiyo tunapenda kazi zenye kulipa vizuri. Ndiyo maana vyuo vyetu vina upungufu wa walimu. Naamini wote tungekuwa tunafanya kazi kwa ujiko tu, basi vyuo vikuu visingekuwa na upungufu wa walimu kwa vile ni kazi yenye ujiko mkubwa. Kwa wale waliomaliza university within the last one decade watakubaliana nami kwamba kufundisha chuo si kazi inayowavutia watu wa siku.
ReplyDeleteMmh! kuna watu wana mawazo negative sijapata kuona, yote hiyo ni wivu tu. Misanya karidhika kazi yake ya uhadhiri pamoja mshahara na anaishi maisha yake mazuri sana na mkewe na familia yake tena kajitosheleza. We utabakia kubwabwaja tu mpaka uchoke. Mtu anaishi anavyopenda na anavyotaka yeye na si unavyopenda na unavyotaka wewe. UNDERSTAND!!!!???
ReplyDeleteNashukuru sana kwa marekebisho yako kuhusiana na kazi ya Bw. Bingi.
ReplyDeleteNakumbuka sana hiyo FCM ilivyokuwa na urasmu na watu hao kujisikia kuwa bora kuliko fani zingine. Kumbe wasiwasi wangu ulikuwa sahihi.
Ok. Hongera sana Bw. Bingi, nilikuwa najiuliza huyu bwana kapotelea wapi? Endeleza fani bwana!! Tunataka mabadiliko huko kwenye sosoloji, japo nasikia huko hakuna "Disco"!!! kwa hiyo kula kuku kwa mrija.
Wewe hapo juu nani alikuambia FCM wanajisikia bora kuliko fani nyingine? sema wewe ndio unajiona duni kwa fani uliyonayo! What i know is that hakuna fani iliyo bora zaidi ya nyingine,zote ziko sawa ndugu yangu,kama wote tungekuwa FCM wanasheria na sociologist wangetoka wapi? U should be proud of yourself na fani uliyonayo!!!
ReplyDeleteMa-engineer wa bongo ndio hao wanaweka matuta kwenye Motorway na kujenga barabara zisizo na sehemu za kutembea waenda kwa miguu na baiskeli au hao wanaoweka minara kwenye magazi ya watu na kuuwa watu na mionzi??? ebu nifahamisheni au ndio wanadesign majengo yanaegemeana kariakoo???!!!
ReplyDeletedah misanya bingi???sosholojia pale udms nakukumbuka asa zile semina rooms,,hahahahahaaaaaa
ReplyDeletenow lecturer mie now ni meneja ktk shirika la nguvu (mihela)
TIZAMA TULIVYOKUWA NA MAWAZO MAFUPI HIYO PICHA HAPO JUU NA HABARI ZAKE ZINAHUSU MAMBO MENGINE NA SI KAZI YA HUYO MNAYEMZINGUA. OYAA KAMA HAMNA [POINT ACHENI KUANNDIKA UJINGA , MARA HIKI MARA KILE HAVINA MSINGI NAFIKILI LA MUHIM HAPO NI KUMPONGEZA ANAYEOA NA PIA NI MTU MWENYE BAHATI KWANI WASHIKAJI NA MIJINA YAO NDIO WASHENGA. KAMA HUNA BAHATI HII MPELEKA NDUMILAKUWILI TUACHE TABIA YA KUFUATILIA MAMBO YA WATU MSHIKAJI AU WASHIKAJI HAWAGOMBEI UBUNGE KUWA SCRUTINIZED.
ReplyDelete