Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zain Tanzania, Khalid Muhtadi akibonyeza kitufe kuchagua shule mojawapo kati ya 26 za mikoa yote Tanzania zilizoshinda nafasi ya kupewa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni 1 kila moja na Zain, katika hafla iliyofanyika mjini Arusha mwishoni mwa wiki. Zain inatoa vitabu kwa awamu nne kila mwaka kwa shule 26 za mikoa yote Tanzania kwa lengo la kutekeleza programu ya Zain ya Build Our Nation (BON). Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima, Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe na kushoto ni Mhandisi wa Mtandao wa Zain Tanzania, Idan Msuya
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima (kulia) akikabidhi vitabu kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day, Nafikaheli Mmasa vilivyotolewa na kampuni ya simu ya Zain mjini Arusha mwishoni mwa wiki kwa lengo la kutekeleza programu ya Zain ya Build Our Nation (BON). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zain Tanzania, Khalid Muhtadi na wa tatu kulia ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakicheza ngonjera wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa shule 26 na kutangaza nyingine 26 zitakazonufaika katika mradi wa Build Our Nation (BON) wa Zain Tanzania wa kutoa vitabu kwa shule 26 za mikoa yote Tanzania.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Arusha Day ilianzishwa mwaka 1993,nawakumbuka sana waalimu waanzilisi wakati huo mimi nikiwa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza.Alikuwepo Mwalimu Shayo,Marehemu Mwalimu Shayo,Nyamasagara,Mmasa,Mwalimu James Shemdoe,Mwalimu George Marwa.
    Leo hii Mwalimu Nafikaheli Mmasa ni mkuu wa Shule,Mwalimu Mmasa ana sifa zifuatazo amabazo zinafanana na za Mwalimu Nyamasagara.Kujipendekeza,majungu,husuda,wivu na kuwachongea waalimu kwa Mkuu wa kituo,tabasamu la uongo.Ila kila mtu na utaalamu wake Nyamasagara alipata ukuu kabla ya Mmasa kwa kujipendekeza kwa Andrew shayo,miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwa Arusha Day Mmasa naye amepata faida ya kazi yake ambayo ameifanya kwa nguvu zote ya kuharibu maisha ya wafanyakazi wenzake na kujiweka karibu na wakuu wa kituo.Angalia hapo anapiga magoti kuficha maovu yake,ila kila kitu kina mwisho wake kwani hata mimi alinifanyia ubaya sana na kunifukuzisha shule kwa kujenga hoja ya uongo dhidi yangu.
    Malipo ni hapa hapa Duniani,Nawakumbuka Mr Lungu,Miss Kessy,Mr Siza,Miss Mgonja.

    ReplyDelete
  2. mdau asante sana kwa maelezo. Nimejiuliza sana shule yangu arusha sec siku hizi inaitwa arusha day????Kumbe hii ni nyingine na ilianzishwa 1993 ndio maana sikuijua kabisa.

    Iko sehemu gani pale arusha?

    ReplyDelete
  3. Kukuza vvipaji hivi ingekua muhimu sana. Watu wanaopenda ngonjera wanakuaga malawyer wazuri sana.

    ReplyDelete
  4. Hongereni sana Zain.
    Hilo goti sijalipenda, goti la kishkaji ili kuonyesha heshima halikatazwi, ila hilo, laonekana ni la kinafiki au la kumuabudu mtu. Tusikubali kuwa watumwa mbele za viongozi

    ReplyDelete
  5. Pamoja na kuipongeza Zain kwa mchango wake mkubwa wa Vitabu vya masomo kwa Shule mbalimbali,ningependa kutumia fursa hii kuiuliza serikali yetu kimefikia wapi kuhusu ahadi za kuiomba Sullivan Books For Schools Foundation iweze kutoa msaada wa vitabu mbalimbali kwa ajili ya shule zetu za msingi,sekondari,vyuo ya walimu na vyuo vikuu pamoja na maktaba za taifa?Sullivan wana kitengo maalum kwa ajili ya Msaada wa Vitabu kwa Shule na Vyuo katika nchi masikini katika Bara la Afrika.After the Historic Sullivan Summit in Arusha I had thought that one of the prime needy areas where our country could quite easily benefit from the Sullivan Initiative was on BOOKS & BOOKS & BOOKS!Surprisingly,all is gone with the wind!Tumebweteka bwelele eti tunasubiri wao Sullivan huko Marekani ndio wafanye jitihada ya kutukumbuka na kuanza kutusaidia misaada kama hiyo ya vitabu kwa ajili ya shule zetu mbalimbali!Ridiculous isn't it?Kama kuna shule hata moja ambayo imeshapokea misaada ya vitabu na pengine hata used computers toka Sullivana Foundation toka umalizike ule mkutano w Arusha hebu yeyote atueleze kuhusu hilo tujue kipo kilicho fanyika!Sitashangaa iwapo baada ya mkutano muhimu kama ule wa Sullivan ambao waanzilishi na watendaji wake wakuu walitoa ahadi nzito na kuguswa sana na hali duni waliyoiona katika shule zetu HAKUNA KAMATI MAALUM ZA KIUTENDAJI ZILIZOUNDWA KUFUATILIA UBAINISHAJI,UOMBAJI,UPOKEAJI,USAMBAZAJI NA UFUATILIAJI WA MISAADA MBALIMBALI KUTOKA SULLIVAN FOUNDATION!Misaada ianaweza ikatolewa kule Marekani.Lakini tuwe tayari kuisafirisha kwa gharama zetu wenyewe ikitokea kwamba usafirishaji ndiyo kikwazo.Tukisaidiwa Suruali,ni utovu wa adabu kutoshukuru kwa msaada ule tu wa suruali tutakapoanza kudai hata Shati pia tupewe kama vile ni lazima na ni haki yetu.Msukumo uanzie wapi,kwa Viongozi pale Juu au tumsubiri mwanakijiji ambaye hana hata taarifa iwapo hiyo Sullivan yenyewe ilifanya mkutano hapo Arusha kwa maslahi yao?Huku Kuzubaa kwa Watanzania kutaisha Lini,toba yarabi?Wakubwa hapo acheni Ugoigoi,eeboooo!

    ReplyDelete
  6. Wewe zumbukuku acha hizo... akili sasa zimekwisha lemaa kwa kufikiria misaada. eti sulivan watupe misaada ya vitabu. sasa kila kitu mtasema tuombe msaada. ni vile tu haujui nchi ya Tanzania ni tajiri kiasi, na ni vile hujui kuwa viongozi tulionao ndio hao maslahi yao kwanza. huwezi amini kama Tanzania ninchi ya tatu kwa kuzalisha dhahabu africa baada ya Afrika kusini na ghana. Hujui kama Tanzania tuna bandari kubwa tatu(Dar, Tanga na Mtwara) ambapo nchi kama Rwanda, Congo DRC zambia wanapitisha bidhaa hapo, ni mapato kiasi gani tunayopa nchi kama Rwanda hawana, lakini angalia maendeleo ya Rwanda. Hujui kama Tanzania tuna lakes kama Victoria, Tanganyika na nyasa.. wote huu ni utajiri.. chekishia mbuga za wanyama na wanyama wenyewe.. ni mapato kiasi gani Tanzania inapata kwenye utalii.
    hujui Tanzania ilivyojaliwa na ardhi kubwa yenye rutuba, kahawa, chai, pamba, alizeti, mahindi, mpunga mwake baabake!
    Hujui soko kubwa la Tanzania watu million 40 .
    Lakini kwa kuwa na serikali yenye viongozi mafisadi, wamewashindilia ujinga vichwani mwenu, sasa kila kitu tuombe wafadhili watoe misaada.. sasa kama hali hii itaendelea, ninauhakika mtaanza kuomba mbegu za wanaume wafadhili ili wasadie kutotoaa.. shenzi type...

    ReplyDelete
  7. goti limekuwa kubwa kwa sababu ya mila zao hawa watu wawili na mazingira walikulia kwa sasa kuona watu wa rika la vijana wakifanya mambo ya mama huyu ni vigumu kwa sisi tulilelewa migombani ni kawaida pia tuachane na kasumba ya misaada tujifunze kujitegemea maendeleo ya kweli hayaletwe na misaada hakuna msaada wa bure niliona kwenye tv ya china jinsi wanakijiji walivyoamua kujenga barabara wenyewe baadal ya kusubiri serikali kuu watu ata dawati kutengeneza mpaka msaada wakati miti..wa nini wanashindwa kujipanga mi nakumbuka wakati niko migombani babu bibi na watoto wote tulikuwa kila jmosi kwenye ujenzi wa sec kitambo hacha hizi za lowassaa kijijini shule za msingi zilikuwa tano sekondari tatu ambazo ndio nilizosoma sasa niko kwa msovieti nasomeshwa na serikali bila watu kujipanga pale mgombani si ajabu mi nisenguwa hapa kama kila kitu ni msaada kwa msoviet hapa kila mwalimu wa somo sio ana kitabu ametunga bali ni vitabu sasa wasomi wetu angalia wamesha funga vitabu baada ya degre wao na nyama choma bia sasa maisha ni misaada watu wanamsumbua matonya kumbe sisi wote ni matonya kwa kimantiki tunakazi ya kupambana na kasumba ya misaada siasa ya kujitegemea ndio msingi wa maendeleo msaada unakamilisha sio mwanzo mpaka mwish ni msaada tuuu

    ReplyDelete
  8. ZAIN WAJINGA WALISHENI SUKARIGURU WAKATI NYIE IKIIBEBA KEKI YOTE NA KWENDA NAYO MAJUU. KATIKA BILIONI MOJA YA KODI HURU UKITOA LAKI MOJA UMEPOTEZA NINI.

    ReplyDelete
  9. mdau hapo juu kabisa umenikumbusha mbali sana mimi ni mmojawapo wa wanafunzi wa kwanza wa Arusha Day nimefurahi saana kuona shule yangu ..daa Mmasa ndo kawa head wa school .. na Nyamasagara yuko wapi? daa niko USA kwa sasa nitajitahidi saana kwenda kuwatembelea nikirudi home..kama utapenda kuwasiliana nipe email yako tutawasiliana....mdau USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...