Mkurugenzi wa Fedha wa Zain Tanzania Heiko Schlittke akipokea cheti kutokakwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Marcelline Chijoriga (R) ikiwa ni tuzo ya Zain kutambuliwa kuwa mchangiaji mkubwa wa kodi wa pili kitaifa wakati wakilele cha siku ya Mlipa Kodi. Halfla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hello DC,
    Kwenye maelezo hapo juu baada ya jina la /kiti wa bodi ya TRA umeweka R kwenye mabano. Hiyo R ina maana gani?
    Just curious!

    ReplyDelete
  2. kaka ni ZAINA au ZAIN?tafadhali waombe radhi wadhamini wako

    ReplyDelete
  3. Mh. Balozi,

    Zain wamelipa kiasi gani na kwa kipindi gani? Mlipa kodi mkubwa zaidi ni yupi?

    Pili, Mh. Balozi, serikali yetu ina hisa Zain kama ilivyokuwa kwa celtel? Na imefaidika vipi na 'uuzwaji' wa celtel kuwa zain?

    Kuna ka mchezo ambako makampuni ya kigeni hucheza, kanaitwa 'badili uchume.' Sikafafanui sana ila sijui kama kuna athari hasi ambazo serikali imepata hasa kimapato kutokana na uuzwaji wa celtel > zain, tukizingatia misamaha ya uwekezaji hasa kwa makampuni ya kigeni.

    Tatu na mwisho Mh. Balozi, Bongo inasuasua sana katika suala la internet. Si 'next-to-zero' lakini spidi ziko chini sana, na bei ziko juu mno!!! Jamani hii ni changamoto na fursa kwa wajasiriamali na mabepari pia.

    Voda wanajaribu lakini gharama ziko juu mno. Zantel nafuu kiduchu lakini spidi iko chini na hawapatikani 'pahala popote' kama wanavyodai.

    ReplyDelete
  4. HIYO NI POLITICS, MLIPA KODI MZURI MAANA YAKE NINI? NI WAJIBU WAKE KULIPA KODI KWA MUJIBU WA SHERIA ZA TANZANIA, HIVYO HAMNA HAPO CHA MLIPA KODI MZURI, NA WAFANYAKAZI WANAOKWATWA DIRECT KUTOKA KWENYE MISHAHARA YAO WAO SI WALIPA KODI WAZURI? PENGINE NINGEELEWA KAWA UNGESEMA MLIPA KODI MKUBWA KWA KIWANGO KIKUBWA CHA PESA, LAKINI SI MLIPA KODI MZURI, NA HAMNA SABABU YA KUPOTEZA PESA YA UMMA KUTENGENEZA CHETI KUMPA MTU ETI MLIPA KODI MZURI WAKATI NI WAJIBU WAKE KISHERIA, EBU ACHENI HIZO ZA SIASA NDANI YA MASLAHI YA UMMA, NI OBLIGATION YAKE KULIPA KODI.

    ReplyDelete
  5. I wonder kuna walipa kodi wazuri na wabaya. Nilizania kulipa kodi ni wajibu wao na wa kila mtu.

    Ahaaa Tanzania yetu imekosa kazi kutengeneza vyeti vya walipa kodi bora na wasiolipa wanafanywaje....wanapewa fine au wananyimwa tu vyeti

    ReplyDelete
  6. Sevedo, welcome to the real world, Celtel haikuuzwa kwa Zain, imebadili jina but uongozi ni ule ule uliokuwa unamiliki Celtel, mbona hamuelewi ilhali hata bungeni ilielezwa? kha

    ReplyDelete
  7. MIMI TANGU NIAJIRIWE ZAIDI YA MIAKA ISHIRINI NA TANO SIJAWAHI KUKWEPA KODI HATA SIKU MOJA, HATA MEAL ALLOWANCE YAANI CHAKULA NINACHOKULA NINAKILIPIA KODI LICHA YA KUWA NIMEKINUNUA LAKINI TRA INANIONA SI MLIPAKODI MZURI! KISA, NI MWEUSI WA USWAZI. HAWA WANAOSAMEHEWA KODI NDIYO TUNAOAMBIWA WALIPAKODI WAZURI ILI TUSIHOJI MISAMAHA WANAYOPEWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...