

Picha na Habari na Ali Meja
Mheshimiwa Batilda S. Burian (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) alitembelea Indonesia kuona jinsi kilimo cha mmea ujulikanao kama Sugar Palm kinavyoendeshwa na kushuhudia faida nyingi za mmea huo katika kuhifadhi mazingira, kuondoa umaskini na kupata nishati mbadala.
Kilimo cha mmea huo kimefanyiwa utafiti kwa muda wa miaka 20 na Dr. Willie Smits ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali kilichoko huko Indonesia. Shirika hilo limefanikiwa kuwashawishi wakulima wadogo kupanda mmea huo kwenye mashamba yao na wameshaanza kufaidi matunda yake.
Kwenye ziara yake hiyo Mshimiwa Batilda alielezwa kuwa sugar palm ni mti unaostawi kwenye hali ya hewa mbalimbali. Hustahimili ukame wa kiasi mvua za mm 700 kwa mwaka.
Kila sehemu ya mmea huo ina matumizi yenye faida. Kwa mfano utomvu wake hutumika kuzalisha sukari na “etanol” ambayo hutumika kama nishati mbadala; majani yake ni mbolea na hutumika kuezekea; shina lake ni mbao nzuri sana; mizizi yake ambayo ni imara sana hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu kwenye magari na matunda yake ni chakula cha mifugo.
Kwa upande wa hifadhi ya mazingira, mmea huu huzuia mmomonyoko wa ardhi kwani mizizi yake huingia ardhini meta saba hivyo hustawi hata kwenye miinuko mikali. Unafaa kuhifadhi vinazo vya maji. Unafaa kuongoa maeneo ya mazingira yaliyoharibika. Huzalisha nishati mbadala mara 4 zaidi ukilinganisha na jamii ya mimiea nyingine katika nyanja hiyo.
Mmea huu huongeza ajira. Hustahimili magojwa ya mimea na haushiki moto kirahisi. Hustawi sana kwenye kilimo mseto. Hivyo basi huongeza pato la mkulima na kuboresha maisha yake.
Matumizi hayo yote huanza lupatikana mmea utakapokuwa na umri wa miaka mitano na huendelea hadi miaka kumi.
Baada ya ziara yake hiyo Waziri alieleza kuwa ni vyema mmea huo ukafanyiwa majaribio nchini kwetu kutokana na hizo faida zake. Alieleza kuwa suala nishati ya mimea ni muhimu hasa ukizingatia wawekezaji mbalimbali wanaojitokeza katika eneo hilo.
Alisema ili kilimo hicho kisiwe na athari kwenye mazingira na chakula serikali ipo katika hatua za kukamilisha kanuni na mwongozo wa kilimo cha mimea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...