usiku wa kuamkia leo hasheem thabeet ameisaidia timu yake ya U-Conn kuishinda Buffalo 68-64 katika ligi ya vyuo inayoendelea huko. kwa taarifa kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kumbe 68-68 siku hizi ni USHINDI eeh?! Haya, twende kazi!

    ReplyDelete
  2. WATANZANIA WANAKUNA VICHA HETI


    MIDUNDO YA VIKAPU === HASHEEM THABIT


    UMAHIRI WA KIMATAIFA ==== JONIE MASHAKA


    UONGOZI BORA BARANI ===== JK KIKWETE


    UDIPLOMASIA WA HALI YA JUU === ROSE MIGIRO

    HAWA WOTE NI WAZAWA WA TANZANIA NA SIYO WAKENYA

    ReplyDelete
  3. Hapo sijaelewa vizuri kidogo, yaani ameiwezesha kuishinda Bufallo 68-68 au ameiwezesha kutoa DROO?? Lakini yote kwa yote Hasheem kiukweli anatisha katika libeneke la kikapu, na natumaini atatutoa wabongo kimasomaso kwenye michuano ya Kikapu inayotarajiwa kuanza huko Nairobaa. Wasiwasi wangu ni kuwa wapinzani wa jadi haswa Wakenya wanaweza kugoma kwa kudai kuwa mshkaji ni mrefu kupindukia.

    ReplyDelete
  4. samahani kama nimekosea mie sio mtu wa kikapu ila kusaidia ushindi wa 68-68 ? ni ushindi au Draw na navyosikia kikapu mpaka apatikane mshindi au ni 168 kwa 68? turekebishie hapo tuelewe huyu jamaa kweli 20yrs Old? si kwamba majungu nauliza tu swali nipate jibu.

    ReplyDelete
  5. hiyo ni typo. Ukifuata link utaona ni 168 164

    ReplyDelete
  6. HIYO 68 - 68 MMEIPATA WAPI MIMI NAONA 68 - 64 AU MIMI KIPOFU. HATA KWENYE WEB KUNAONYESHA 68 - 64 HATA UKICHEKI VIDEO UKIHESABU 68 - 64 NA HATA BOARD INAONYESHA HIVYO, ANYWAY BPENGINE MIMI NI KPOFU

    ReplyDelete
  7. Nyie mnaosema 68-68 mna matege ya macho nyie. Angalieni vizuri sio mnadandia kihiace kwa mbele.
    Ni 68-64

    ReplyDelete
  8. Hao walioandika 68-68. Wote ni watanio wa jadi makengaza kiba teeeeeeeh.

    ReplyDelete
  9. Sasa hayo sijui ni makengeza, au matege ya macho, au trakoma ndio imevamia bongo ama sijui niaje! kote hata hapo juu alipoandika Michu panasema 68-64!! Msiwe mnajaribu kuomba lift kwenye ndege au kudandia treni kwa mbele ...!!

    ReplyDelete
  10. NAni aliwaambia basketball ina draw nyie!! Na hao bila shaka ni wabongo tuu!! Basketball haina draw sio soka hii...!! Acheni kudandia hiace kwa mbele...

    ReplyDelete
  11. mwanzo michuzi alikosea sio kama matege hamshangai asilimiak ubwa wa mwanzo wameona 68-68 sababu mwanzo ilikuwa hivyo michuzi angeomba msamaha kwa kukosea sasa ndio karekebisha kwahiyo si makengeza na bila hao asingebadilisha sababu wamelalamika huo ushindi au draw na kikapu hakuna kitu draw ikiwa hivyo inaenda Over Time zaidi ya muda sijui noti richabo kutafsiri hahaha.

    ReplyDelete
  12. unayosema kudandia Hiace kwa mbele wewe ndio ndugu yangu unashika mpini wa kibao cha nazi kabla kuuliza ungeuliza ilikuwaje ndio ungejuwa mwanzo alikosea kuandika aliweka 68-68 ila ni binadamu kukosea inatokea matokeo ni 68-64 sasa ndio kapatia kuandika. ukiniambia kuchemsha kachemsha aliyesema 168-164 huyo ndio kachemsha peke yake.

    ReplyDelete
  13. OOh huyu Thabeet ni Mkalenjin, hamuoni hivo yuko mrefu? Sasa! Mwabisha nini ni Mkenya huyo ndio maana yuko na success, angekuwa Mtz angekuwa lazy lazy asingekuwa hapo alipo! {(hapo inabidi uongee kwa lafudhi ya Kiswahili cha Narobi (Nairobi inatamkwa hivyo na wenyewe)}

    Huyo ni dada wa Kikenya huyo anadai kuwa Thabeet ni Mkenya, ukienda kwenye you tube, wanamuziki wazuri wanaoimba vizuri woote utasikia huyo si Mtz ni Mkenya huyo, wakibanwa aah si atoka East Africa! yote ni mojja hiyo!!

    ReplyDelete
  14. Hapana, hawajakosea..

    mwanzo ilikuwa 68-68

    sasa hivi imerekebishwa.

    ReplyDelete
  15. Kuna watu hapa sasa inabidi wapewe special threads na ziwe kama picha ndefu za kihindi au kilatino zilizopachikwa kimfululizo (series): sasa tuko hapa

    Hasheem Thabit series XXII.

    JOhn Mashaka series XXI

    Vekesheni Mkuu wa nanii series XX

    Rhemtullah series IX

    CCM shina la reading series VIII

    Zain series VII

    Flavian Matata series Coming back soon

    Richard BBA- series- OS


    Baadaye series za matukio zitafuata zikiongozwa na EPA-UFISADI

    ReplyDelete
  16. Stony Brook next.. Muombeeni MTZ ashinde. inamuongezea nafasi huko NBA..

    ReplyDelete
  17. Thabeet is the new Lebron.
    New York Knicks inakusubiri kwa hamu.

    ReplyDelete
  18. ASANTE HASHEEM,BIDII NDIO MSINGI WA MAFANIKIO KTK MICHEZO.
    BIDII MPAKA SIKU UNASTAAFU GAME .

    ReplyDelete
  19. hasheem is no where near lebrom but he still got a chance to improve his game though

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...