mjane wa herry makange, jane mponzi, akiwa hataki kuamini kwamba mwenzie ndio keshatangulia mbele ya haki kwenye hafla ya kuaga mwili wa marehemu ostabei mchana huu. baadaye mwili ulipelekwa kibaha tayari kwa mazishi kesho
ganzi na bumbuazi kwa mjane jane mponzi
wafanyakazi wenzie herry wakimsindikiza
shemeji wa marehemu anashindwa kujizuia
wadau wa habari toka kila kona na chombo walikuwepo
maprodyuza waandamizi wa channel 10 na dtv wakimuaga mwenzao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Poleni sana kwa msiba Jane na Grace. May he rest in Peace

    Blandina

    ReplyDelete
  2. MAY HE REST IN PEACE, AMEN.

    ReplyDelete
  3. This is so sad. Poleni sana familia ya marehemu. RIP

    ReplyDelete
  4. Pole sana Jane yani nimeshtuka kukuona hapo wewe ndio majane pole sana. ni ngumu sana m/mungu atakupa moyo wa subira.

    ReplyDelete
  5. Jamani Jenny pole sana tena sana Mdogo wangu , nakuombea Mwenyezi Mungu akupe subira na moyo wa imani wewe na familia yote ya marehemu,kwa kweli nimesikitika sana kuona kumbe wewe ndio mfiwa lakini hii yote ni mipango ya Mungu na Mwenyezi Mungu uwe na imani yeye anajua amekupangia nini maishani mwako, kumbuka tuu sisi wote ni waja wake na kwake tutarejea , ni huko kutangulia tuu kugumu kwa wanaobaki hapa duniani. Mimi nakukumbuka sana ulikuwa mcheshi sana na mpenda watu na mwenye tabia nzuri Jenny, ulisoma na mdogo wangu pale Kisutu Vio mimi ni yule dada yake wa Zanaki. Nakuombea Mwenyezi Mungu akupe subira na imani.Ameen

    ReplyDelete
  6. Rest in Peace Herry!
    Poleni na msiba Jane na familia yote.
    Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu. Amen

    ReplyDelete
  7. pole sana dada jane.. umenikumbusha ukiwa,, hata niwe na furaha vipi ukiwa haujanitoka..
    poleni sana

    mpendwa pumzika kwa amani. amin

    ReplyDelete
  8. Its sad to see the young men like Henry anatangulia mbele za haki mapema, Lakini ni somo kwetu pia kuwa anytime tunaweza kuitwa kwenda nyumbani ambapo ndio makao yetu makuu kwa kila binadamu, pole nyingi sana kwa wafiwa pole sana Mjane maana nimesoma kwenye magazeti kuwa ndoa yenu ilifungwa mwezi wa kumi na moja mwaka huu so mmekuwa na mwezi mmoja tu wa kufurahia ndoa yenu lakini Mungu akampenda sana Herry na kumuita mbele za haki, kuwa mvumilivu kuwa mjasiri inauma sana kumpoteza mwenzako lakini kumbuka pia kuwa wote sisi ni wapitaji na kila nafsi ni lazima ionje mauti ndipo ipate kuingia katika uzima wa milele.
    BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE. AMEN

    NB:- Michuzi tunaomba utuwekee angalau picha moja ambayo angalau inaonyesha alivyolay kwenye coffin.
    Mdau Udsm

    ReplyDelete
  9. MDAU WA HAPO JUU.

    KUTOKANA NA MAADILI YA TAALUMA, KUONESHA MWILI SIO JAMBO JEMA SANA. NASIMAMA KUKOSOLEWA.

    ReplyDelete
  10. Jane pole sana na msiba wa mume wako. Nina amini kwamba Mungu hakupi mzigo usioweza kuubeba. I will remember you in my prayers at this difficult times.

    Phatlorenzo, MN

    ReplyDelete
  11. Poleni sana wafiwa. Mungu awazidishie amani katika kipindi hiki kigumu.

    Ni kweli Michuzi ulivyofanya. Naungana na wewe kwa hilo. Sio vizuri kuweka picha kwa ndugu zake na jamaa wa karibu kuna wengine watapenda kumkumbuka jinsi alivyokua hai. Na ukizingatia amefariki kwa ajali. Sasa hizo picha ni heri ndugu zake wanaotaka kuziona basi watakuandikia lakini huku kwenye blog sio vizuri.

    ReplyDelete
  12. Pole sana Jane, Poleni sana Wazazi, Pole sana Grace, Poleni ndugu, jamaa na marafiki wote....Ni kipindi kigumu na kinahitaji uvumilivu na ujasiri wa hali ya juu.

    Sipati uelewa wa kujua majonzi yaliyowafika, ukizingatia muda mfupi uliokuwepo toka Jane afunge ndoa na marehemu!!!!!

    Inauma sana lakini tumuombee kwa Mola wetu na tujiombee nasi atupe moyo wa uvumilivu, kwani kazi yake haina makosa.

    Yote atendayo huwa ni mema!!!!


    Amina

    ReplyDelete
  13. michuzi kasome vizuri taaluma yako, sina uhakika sana kuonyesha mwili wa marehemu ni kinyume na ethics za uandishi wa habari!! mbona mwili wa NYERERE tulionyeshwa kwenye TV na magazeti? kachimbuwe tena nondo zako!! nahisi si vizuri kuonyesha mwili wa marehemu ukiwa katika sehemu ya ajali, huwezi kuonyesha picha ya mtu aliye uchi ambaye ni mzima bila ya idhini yake, huwezi kuonyesha picha ya mtoto mdogo aliyeshitakiwa mahakama, huwezi kuonyesha picha ya mwanamke mwenye story ya ku-rapiwa/kuingiliwa kimwili kinguvu bila idhini yake, unless yeye mwenyewe ame-lift anonimity, pia huwezi kuonyesha picha za watu waliouwawa kwa tukio lolote lile na miili yao imeharibika vibaya, baadhi ya matukio hapo juu ni ubinadamu tu si sheria ukiachilia mbali ya mtoto aliyeshitakiwa mahakamani na mtu aliyerapiwa ni sheria huwezi kuonyesha picha zao unless for those who of age wamelift anonimity wenyewe for a certain lesson to the society.

    ReplyDelete
  14. Poleni sana wafiwa. Mungu awape nguvu.

    ReplyDelete
  15. It is a sad moment when anyone dies but more so when it is a beloved one and one so young. I did not know Herry and do not know the family but I feel very much for their loss. May God give you all strength during this very difficult time. Remember God giveth and God takes. May your mourning make you reflect on all the good you had together. Rest in peace Herry Makange you will be missed by many. Amen

    ReplyDelete
  16. Ok bwana Michuzi naheshimu mawazo na maoni yako lakini nafikiri si sahihi kutuambia kuwa kutokana na maadili ya kazi si vyema kuonyesha mwili wa marehemu, sasa why peples wanachukua picha?? marehemu wangapi tunawaona kwenye matv humu? waheshimiwa wangapi waliotangulia tunaonyeshwa picha zao?? Inamaana ha wanakiuka maadili?? Nafikiri ningekuelewa kama ungeniambia kuwa kutokana na maadili ya DINI yako si vyema kuonyesha mwili wa marehemu maana kwa nyinyi waislamu mwili haurusiwi kuona na watu ambao si wanandugu kama sikosei, any way mkuu naomba kuwakilisha fikra zangu.
    Mdau Udsm

    ReplyDelete
  17. Wewe dau unayetaka kuuona mwili wa marehemu kwa karibu una mamtatizo gani...??!!! mchawi nini...???!!!.Kwanini husiheshimu maamuzi ya mtahalamu wetu hata kama sio michuzi mwenyewe,haiingii akilini mtu ku-demand jambo kama hili wakati tuko kwenye majonzi.Ungeomba uletewe picha na habari zaidi za tukio lenyewe hapo Bagamoyo road, Tegeta at least tungekuona una "kijiakili" kidogo...!!!!
    Mdau.
    MN,
    USA.

    ReplyDelete
  18. Pole sana Jane na wanafamilia. Yaani kwa kweli ni pigo kumpoteza mume tena baada ya kipindi kifupi cha ndoa, mwezi moja tu. Yaani bado mlikuwa kwenye Honeymoon.

    Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    HERRY REST IN PEACE.

    ReplyDelete
  19. Hivi we mdau Mn Usa kweli hujakurupuka kuandika hii post?? Nyie wabeba box mnamatatizo kweli dah, hebu soma hiyo post ya mdau udsm amesema amekubaliana na maoni ya Mithupu ila akaonyesha kushangazwa kwake na hiyo mipaka aliyoiweka Mithupu, even mi namuunga mkono kwa asilimia mia tatu, kwa hili Mithupu ametuongopea ni maadili gani yanayokataza kuonyesha mwili wa marehemu?? Pia kumbuka sio wote walioweza kupata chance ya kwenda kutoa heshima ya mwisho pale nyumbani kwa kina Herry so hii ingekuwa chance nzuri kwa wale wote ambao wanamfahamu Herry kwa namna moja au nyingine kwa kupay their last respect through this Blog, mambo mengine fikirieni kabla ya kukurupuka kuandika.
    Ni hayo tu.
    Malick

    ReplyDelete
  20. POLE SANA JENI, M'MUNGU ATAKUPA NGUVU NA IMANI INSHALLAH. Poleni wote as a family. I'm told u've only been married a month ago. dah inasikitisha lakini yote mipango ya mungu.

    ReplyDelete
  21. Pole sana ndugu yangu sisi wote kwake (mwenyezimungu) tutarejea, mwenyezi mungu akujaze nguvu ustahimili majonzi hayo

    Zainab C

    ReplyDelete
  22. Ahsante Mzazi mwenzangu Michuzi kwa taarifa.
    Hakika mungu ametoa na yeye ametwaa, mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amina!
    Nimeumia sana na msiba huu wa baba mkwe namkumbuka Herry mchapa kazi , mcheshi na enzi hizo nikiwa DSM alikuwa akiniita Mama Mkwe, yaani akitania kuwa atachumbia binti yangu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...