Baadhi ya wahitimu waliokula nondozzz mbalimbali katika chuo Kikuu cha Kenyatta kilichopo mjini Nairobi Kenya wakimpungia Rais Jakaya Kikwete(pichani hayupo) wakati alipokuwa akiondoka katika viwanja vya mahafali vya chuo hicho baada ya kunukiwa Shahada ya heshima Doctor of humane Letters(Honoris Causa) ya Chuo hicho kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha mazungumzo ya amani nchini kenya na sehemu mbalimbali za Afrika.Makamu wa Rais wa Kenya Stephen Kalonzo Musyoka naye pia alitunukiwa shahada hiyo ya heshima katika mahafali hiyo.
Mwenyekiti waUmoja wa Afrika Rais Dk. JK akiagana na Rais Mwai Kibaki wa Kenya baada ya kufanya mazungumzo katika ofisi ya Rais kibaki mjini Nairobi, Kenya Jana jioni.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta University nchini Kenya, Dr.Harris Mule, akimtunuku nondozzz ya Phd ya Heshima ya chuo hicho Rais Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya 25 ya hicho mjini Nairobi. Phd hiyo inatokana na jitihada zake za utatuzi wa nmigogoro kwa nchi za Afrika hasa mgogoro wa Kenya.
JK akipongezwa na Mkewe Salma Kikwete baada ya kutunukiwa Nondozzzz Phd ya Heshima ya chuo hicho katika mahafali ya 25 ya hicho mjini Nairobi jana. Phd hiyo inatokana na jitihada zake za utatuzi wa migogoro kwa nchi za Afrika hasa mgogoro wa Kenya.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Dr. Jakaya,

    Hongera mkuu. Sasa mkuu inabidi wahusika wa-update profile yako na kuanza kukuita dr.

    njapuka

    ReplyDelete
  2. Baba JK na Mama Salma JK hongereni kwa nondozzzz ya uzamivu. Naona sasa familia nzima imekula nondozz katika different levels za university. Ridhiwani (LLB), Salama (Dentstry), JK (BA Economics, PhD, PhD) na wengine wako katika levels mbalimbali za kishule. Hongera sana JK. Pia Mama Salma uko bomba. Kweli JK hakukosea kuchagua. Hongera sana mama! You are beatiful na ndiyo maana hata watoto unaozaa pia wanafanana na wewe. Salama is exactly like you.
    Hongereni sana.
    Mdauzzzzz

    ReplyDelete
  3. Hongera sana JK, Mchango wako watani wameutambua!!!!
    Sio utani mama kapendeza na kung'aa. Nawatakia amani tu katika kuongoza jahazi la Tanzania

    Mdau Oslo Norway

    ReplyDelete
  4. Hawa Wakenya wanajipendekeza kumpa JK nondo za mezani ili akubali kuuvaa mkenge wa EAC, tumeshtuka hata mumuhonge nini- HATITAKI ASEE!!

    ReplyDelete
  5. Kofia za ki-akademia nyingine..., kama ya huyo "Chief Chef" Dr. Harris Mule!

    ReplyDelete
  6. Mama yetu salma inabidi aelezwe sio lazima kwenye kila safari ya Rais na wewe uende mara moja moja baki nyumbani na kuangalia watoto.

    ReplyDelete
  7. JK NI HANDSOME NA ANA MVUTO.

    MY WAIFE WAKE NAYE NI MZURI NATURALLY NA MREMBO PIA

    ReplyDelete
  8. Wow..!!!! Mmependeza ila mama siku nyingine akipiga picha hasiangalie mpigaji,muhandishi wa habari,awe busy na kumuangalia mzee, kwani amuoni mwenzio Machelle Obama anavyofanya jamani..........!!!!!!

    ReplyDelete
  9. watu wengine kwa uongo mmezidi we annon 4.18 acha kuongea usiyoyajua
    Kwa taarifa yako Salma is not Kikwetes first wife,na hao Ridhiwani, Salama sio watoto wake,ni watoto wa marehemu mke wa kwanza wa kikwete...Salma anao watoto wadogo wavulana wawili
    Ati Salma kafanana na Salama..jamani jamani

    ReplyDelete
  10. You guys! so obsessed with JK you give him too much misifas for nothing!!

    ReplyDelete
  11. Land, no no no

    ReplyDelete
  12. Mabilioni ya EPA sasa yamchanganya Wasira

    2008-12-20 14:33:54
    Na Mashaka Mgeta


    Wakati baadhi ya watu wakiendelea kuhoji kuhusu fedha zilizorejeshwa na baadhi ya watu walioziiba kutoka kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira amejichanganya wakati wa kuzitolea ufafanuzi.

    Akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma Agosti 21, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alisema ameagiza fedha hizo zirejeshwe na kuelekezwa Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika katika mfuko wa pembejeo kupitia Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB).

    Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Wasira alisema sehemu ya fedha hizo, zimeanza kutumika katika mpango wa ruzuku ya mbolea inayotolewa kwa kutumia vocha kwa wakulima wa baadhi ya mikoa hapa nchini.

    Wasira, alisema fedha zilizotokana na marejesho ya EPA, zilichangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha utekelezaji wa mpango huo.

    Hata hivyo, Wasira hakutaja kiasi cha fedha zilizoelekezwa kwa mpango huo kutoka katika fungu la marejesho ya EPA, kwa madai kuwa mfumo wa utoaji wake kwa wizara hiyo, ulifuata utaratibu wa kawaida wa Hazina.

    Nipashe ilipowasiliana na Mkulo kwa njia ya simu jana kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu mchakato mzima wa wizara yake kupeleka fedha hizo katika mfuko wa pembejeo, alionekana kukasirika na kusema hajui lolote kuhusu hatua ya wizara yake kuekekeza fedha za EPA kwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

    ``Mimi sina habari na hizo fedha, labda yeye mwenyewe (Wasira) akwambie ni kiasi gani, sina comment (maoni) kwa hilo. Kama anasema alizipata hizo fedha, yeye mwenyewe awatajie kiasi gani, mimi sijui kabisa,`` alisema Mkulo.

    Aliongeza: ``Mpigie simu Wasira ama Katibu Mkuu wake, waambie Waziri wa Fedha kasema yeye halijui hilo suala...huyo bwana (Wasira) akutajie mwenyewe ni kiasi gani.``

    Kauli hizo, zilidhihirisha kuwepo utata kuhusu uwepo na matumizi ya fedha hizo, hofu iliyowahi kutolewa pia na baadhi ya wananchi, wakiwemo wanaharakati na viongozi wa vyama vya upinzani.

    Wamekuwa wakisema kuwa mchakato wa urejeshaji wa fedha hizo haukuwa na uwazi kwa kuwa serikali haijawahi kueleza ni akaunti gani fedha za EPA ziliingizwa.

    Wasira aliwaambia wandishi wa habari kuwa fedha zilizoibwa kutoka EPA na kurejeshwa serikalini zimeanza kutumika katika mpango wa utoaji ruzuku ya mbolea kwa mtindo wa vocha, ambapo jumla ya wakulima 700,000 watanufaika.

    ``Kwa kweli pamoja na fedha zilizotengwa kwa kipindi cha mwaka wa bajeti, fedha zilizotoka EPA zilituongezea nguvu kubwa sana katika kufanikisha mpango huu,`` alisema Wasira.

    Hata hivyo, Ofisa mmoja wa TIB aliwahi kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni, akisema kuwa benki hiyo bado haijapokea fedha zilizochotwa kutoka EPA.

    Aidha, Wasira alisema mfumo wa kutumia vocha ulibuniwa na serikali, kama njia ya kuepusha ukiritimba na ufujaji wa fedha zilizotolewa kupitia fidia ya mbolea.

    Kwa mujibu wa Wasira, wakulima waliopo katika mpango huo, wanapata mifuko minne ya mbolea aina ya minjingu na kilo 10 za mbegu bora za mahindi na mpunga.

    Alisema gharama ya jumla ya pembejeo hizo, inakadiriwa kuwa zaidi ya Sh 100,000.

    Wasira, alisema mpango wa ruzuku ya vocha, utaendeshwa katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Ruvuma, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na wilaya za Tarime mkoani Mara na Sikonge mkoani Tabora.

    Alisema, awali ilibainika kuwa fidia iliyolipwa na serikali kwa kampuni za usambazaji mbolea ya ruzuku, haikuwanufaisha wakulima, badala yake iliishia mikononi mwa wafanyabiashara hao.

    Kutokana na hali hiyo, Wasira, alisema serikali ililazimika kujifunza mbinu ya kutumia vocha, iliyosaidia kuinua kilimo cha mazao ya chakula katika nchi jirani ya Malawi.

    Alisema mpango huo wa vocha utawawezesha wakulima katika maeneo ya vijijini, kununua mbolea kutoka kwa wafanyabiashara wadogo, watakainunua kwa waagizaji wa jumla.

    Aliwaonya wahusika katika mpango kujiepusha na vitendo vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wake.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  13. mama naona anaonekana amependeza na nywele zake 'natural' sie zile za bandia kwenye picha za zamani..Hogera JK

    ReplyDelete
  14. Kuuliza si ujinga huyo mwanajeshi ambae kila sehemu yupo nyuma ya Rais kazi yake ni nini?

    ReplyDelete
  15. "Tarehe December 21, 2008 6:42 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Kuuliza si ujinga huyo mwanajeshi ambae kila sehemu yupo nyuma ya Rais kazi yake ni nini?"
    Huyu anitwa "Mpambe wa Raisi" kazi yake ni kubeba makabrashi yote ya Raisi, hotuba, zawadi nakadhalika . Ndio maana neno 'mpambe' linatumika mitaani wakiona mtu upo kila kona na mtu flani.

    ReplyDelete
  16. anony uliye mkosoa huyo mwenye viherehere vya kujifanya anaijua familia ya jamaa big up. watu wengine bwana hivi hamuoni haya? ? ? mwe.
    na wewe unaye sema salma abaki nyumbani huna akili kabisa. aliisha baki sana nyumbani sasa zamu yake kutesa kwanza hanyoyeshi huyo.unataka we ndo uende na jk nyoooooo koma eh zamu yake sasa mlichonga sana .


    kingine ni kuwa hoo wakeyna hatuwataki hata mngemuongezea phd nyingine ITS big No juzi mmemtukana leo mnamuita mpatanishi kisa kiland chetu mshindwe wapumbavu nyie

    ReplyDelete
  17. khaaaaaaa,,,hhahahahaaaaa
    iyo ni janja ya nyani kunraghai JK EAC eti tuingie tuuze ardhi,uraia nk nk
    afu mama JK kumbatia mumeo huyoooo!nini aibu izo au mzee aligomaz,yan apo ilibidi wamwagia zinga la busu la kufa mtu!!yan ata ilo kumbato mboni kama sio-----

    ReplyDelete
  18. na mabulet proof inawezekana kweli we vip ? hawa wanakumbatiana kwa sana tu na si desturi zetu watanzania kufanya vihyo hadharani ushindwe na ulegee.

    au we unatamani kumkumbatia ?

    hafu jamaa mmoja kanichekesha sasa kusema WAKENYA WANA MLONGA KIZUNGU ILI ATOE GO AHED SINA MBAVU LAKINI wakumbuke huyo ni mkwere

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...