GLOBU YA JAMII INA FURAHA NA FAHARI KUTANGAZA KWAMBA HATIMAYE MDAU WA MILIONI 5 AMEPATIKANA MUDA SI MREFU ULIEPITA NA MDAU HUYO ALIYEBAHATIKA SAFARI HII KUJINYAKULIA DOLA 500 NI MDAU SABRA NASSOR ANAYEISHI DUBLIN, IRELAND.

JOPO LA MAJAJI NA WATAALAMU LIMERITHIKA NA KIZIBITI HICHO HAPO JUU ALICHOTUMA NA KUMTANGAZA MSHINDI.
GLOBU YA JAMII INAMPA HONGERA MDAU SABRA KWA USHINDI HUO. INATOA PIA HONGERA KWA WADAU WOTE WALIOJITAHIDI KUWA WASHINDI, LAKINI BAHATI HAIKUWA YAO.
MDAU SABRA KWA VILE HAUPO DAR WASILIANA NASI KUPITIA
ILI UTUPE JINA NA NAMBA LA MWAKILISHI AMBAYE TUTAPANGA NAYE AJE LINI KUCHUKUA KITITA CHAKO CHA DOLA 500 PALE DUKA LA ARISE. AJE AKIWA KAULAMBA MAANA KUTAKUWA NA SNEPU ILI KUTHIBITISHA MAKABIDHIANO HAYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. dola 500 au 5000??mbona wajichanganya?

    ReplyDelete
  2. Hapo Balozi mimi inabidi niwe Mshindi wa tatu. Maana kazi kubwa imefanyika kuwa mdau wa 5,000,002.sio mchezo.Haaahaaa!

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  3. kaka michuzi nimesikitishwa sana nimeonewa sana na nimedhalilishwa sana katika hili.
    hauwezi kutangaza mshindi pasipo kuweka sababu za uliyemtangaza kuwa mshindi kuwa ndiye aliye shinda
    Nasikitika sana kwa kuwa ulichoonesha hapo juu kwamba ndisho mlicho kithibiti nimetuma mimi Paul na ndio ukweli. sijui kama unasababu za msingi za kunithibitishia kwamba ushahidi huo hapo juu ni uongo na wakughushi kwa hili nimesikitika sana na nimeonewa.
    nakumbuka nilikuwa katika pipikapilika ilipofika majira ya saa 4.52 nilifungua blog hii na na mara nikakuta hicho ulichoonesha kuwa si halali.nilichofanya ni kuipungza size ya hiyo page kwani ilikuwa kama 3.78 MB ILI IWERAHISI KU ATTACH ikawa kama 78.8 kb kutokana na sehemu niliyofika ku brows internet was slow nikaituma kwako lakini nashangaa ww umeona kama ndo kanyaboya nafikiri hata huyo uliyemtangaza kama mshindi endapo ataona ujumbe huu atakuthibitishia kwamba si yy aliyeshinda.nafikiri mdau huyu mshindi atakuwa fair.
    na original ya hiyo niliyo resize ninayo kabla sijaichange kwenda jpg kutoka bmp ilikupata urahisi wa ku attach


    thank

    ReplyDelete
  4. Hongera kufiskisha wadau m5. Pia ujuwe kuwa wanaojifanya rafiki zako wana nia ya kuiuwa blog hii...

    hina mambo “serious” na hayana mvuto wa fikra na eti haina mambo muhimu na yenye kuhitaji kugonganisha vichwa (brain storming) ambayo yanawahusu wataalamu, wasomi na wanasiasa kama wao.

    Eti pia bulogu yetu ya jamii ni kwa ajili ya kurelieve stress za maisha ya kila siku! kwa kujadili mambo ya hovyo hovyo tu.Tuko kama panya aliyebanwa na mtego hasa yanapokuja mambo ya kitaifa na ya msingi, Eti Watanzania tuko kama tumerogwa hivi! Hatushikiani ngumi, panga wala bunduki kama Somalia.

    Badala yake tunajadiliana kukerwa na lebo na jinsi gani mtu amevaa suti ! Kinguoni mmoja anasema eti Hata leo akiibuka “Obama” wetu (Mh.Jepesi)na kuja na maneno kuwa “Change is coming” na kuwa “Yes we Can” ataangaliwa kwa kejeli na kuulizwa kama suti yake ya Ujiji ina lebo!

    Muelekeze apeleke hoja zake kwenye blog zilizo serious zaidi - zipo nyingi. Sisi tupunguzane stress humu na tawsirazzz zetu tukiendelea na libeneke kama kawa'.

    ReplyDelete
  5. Unanichanganya kidogo au mi ndo nakosea, ni dola 500 au 5000. Ninachojua mimi dola 500 hazifiki million tano za kitanzania

    ReplyDelete
  6. Sheikh Issa dola 500 ni sawa na milioni 5 au laki 5? Au ndiyo tuseme mfupa hauna ulimi na mikono haina macho?
    Hongera mshindi

    ReplyDelete
  7. kaka hapo mahesabu kidogo utata dola 500 sio sawa na million 5 ninaomba (tunaomba) urekebishezzzzzz merry X mas and Happy new yearzzzzzzzz kwa wadau wote

    ReplyDelete
  8. Tatizo lako wewe Michuzi hiikitu imeghubikwa na ufisadi sana. Nawasiliana na Hosea kujua kama kulikuwa na fair play hapa.

    ReplyDelete
  9. Michuzi nawasiwasi majibu umeyapika. Mdau 5,000,000 kutoka Dublin Ireland sio Sabra ni mimi.

    Nimemind lakini ndo ivo umeshatengeneza ZENGWE, eti uwamuzi wa mwisho ni wa jopo la majaji na hakuna kukata rufaa.

    Inabidi niwe mpole na siwezi kuacha kuperuzi blog yako maana ndo pakuondolea stress na kupata habari haraka za nyumbani.

    Zengwe: Uzushi/Uongo usioweza kuthibitishwa.

    ReplyDelete
  10. Ni mshindi wamiloni 5 sio wa shilingi milioni tano.Na wala Mwenyekiti na mkuu wa wilaya na balozi hakuandika kwamba dola 500 ndio sawa na milioni tano bali conclusion za waandishi wanaopenda kulaumu na kukosoa bila sababu za msingi.Mshindi amepatikana kelele hazisaidii.
    Mwenyekiti endeleza libeneke.Nyama ikishatoka buchani hairudi kuwa ng`ombe.

    ReplyDelete
  11. hana ndugu bongo. tumia western union umletee paund zake acha ubishani. je kama angeshinda mrundi ingekuwaje?? unajiletea moto na haya mambo michu. shria iwe ni western union au kuchukuwa pekee au through bank. globu ya jamii hii sisi tuko chile na tunaliendeleza tu. hatuna mtu aliye baki bongo tumjuaye labda wewe michu. xmas njema.

    ReplyDelete
  12. Hawa wanaoandika comments humu wametokea wapi?? Shule was not rechabo au? tukiandika ki english hamuelewi, kiswahili hamuelewi, sasa?? HAPA MICHU KASEMA WAZI MDAU WA MILIONI 5....WAPI PAMESEMA MDAU WA SHILINGI MILIONI 5?????

    Mwe!

    ReplyDelete
  13. Hongera Sabra! Hongera sana Kaka Michuzi kwa kazi nzuri!
    /Maggid

    ReplyDelete
  14. Mimi kaka yangu naona ni heri uache tu uchezesha hii kitu. Naona watu wanahasira kama nini. Wengine hawaeleweki wanalalamika nini sana sana. Wengine huko Europe hawakulala. Wengine wanaota kuhusu million 5.

    It is too much I think for you to handle this. I know unafanya hivi kwa madhumuni mazuri lakini hayo matusi wanayokuletea sijui unajifikiria vipi.POLE SANA
    Mdau
    USA

    ReplyDelete
  15. Michu,
    unachofanya sio fair, ukizingatia wote wanaoandika comments ni wadau wa blog yako, comments zao zinalenga kuboresha blog yako na hazina tusi hata moja ndani yake lakini nimegundua unachagua ipi ya kuiweka, usifikiri watu wote wana furaha kuona kile unachopost na kubania vingine vyenye point ambayo wamecomment na wewe ukavibania.

    Binafsi nimetuma comment jana asubuhi lakini cha ajabu naona unapost za wengine waliokuja nyuma na kui ignore ya kwangu ambayo haina ubaya wowote ndani yake. Kwani ukiweka zinafanya blog yako ife?? no.

    It doesn't matter mdau yupi au wangapi wametembelea blog yako, kumbuka hawa wote even wale ulioamua kutopost comments zao wamechangia kufikisha ile namba ya 5,000,000.

    Najua hata hii comment utaichimbia na kutoipost, but that's ok, ila ukweli ndio huo

    ReplyDelete
  16. Europe inaelekea njaa sana. Rudini bongo. Watu hamkulala na mmeshindwa kupata bahati lakini bado tu mnalalamika.Kama internet speed yako ni ndogo nani wakulaumiwa? michuzi ???!!!!!! Agrrrrrr

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...