Rais Armando Guebuza wa Msumbiji akimkaribisha JK katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Msumbiji.
JK na mwenyeji wake Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya Rais na Mkewe kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo leo tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.

JK na mwenyeji wake Rais Armando Guebuza wakifurahia na watoto waliojitokeza kumpokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo leo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hapo kweli Rais wetu sikuwezi!

    ReplyDelete
  2. Hao askari kwenye gwaride mbona kila mtu anaangalia kivyake, mwinge kulia mwingine kushoto..ni sahihi au show gem??
    mdau namba 6

    ReplyDelete
  3. hawa ndo ndugu zetu wa kweli, jirani zetu wa kusini. Tumefanana nao sana kwa mengi. Hawa ndo wangefaa kufanya nao muungano. Good people Mozambique, Aluta continua!!!

    ReplyDelete
  4. Ukiangalia picha ya kwanza ya huyo Rais wa Msumbiji, ukitizama macho yake, pua na mdomo vinanikumbusha picha za "TASWIRA" za Braza Michu

    ReplyDelete
  5. aluta continua

    ReplyDelete
  6. Hao ndo wa kufanya nao FEDERATION si watani-wa-jadi, wanajifanya wajanja kuliko sisi. GO KIKWETE GO. muungano na NCHUMBIJI, MALAWI ZAMBIA, DRC safi tu.

    ReplyDelete
  7. JK kwa kusuuzwa roho na watoto huwa unanifurahisha sana. Yaani ukiona watoto unakunwa kabisaaa hadi sura inaonyesha. Kweli upendo wako kwa watoto ni wa kutoka ndani sio usoni

    ReplyDelete
  8. Jamani brother Michuzi, mbona pua, midomo, meno na uso wa Rais Gwebuza haviendani? Kamera ilikosea au ndiyo alivyo? Naomba jibu maana picha hii inatisha na kama ni kamera basi tujue.
    Mdauzzzzzzzz

    ReplyDelete
  9. Najibu swali la mdau 6 siyo kila gwaride lazima lifanane na la kwetu kwani haya magwaride yanategemea na huko siku za nyuma nani alikuwa mtawala wako.Kwa maana hiyo inawezekana saluti ya hawa wenzetu ni kumpokea Rais kwa kichwa/macho na kuendelea kumsindikiza anapokupita.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...