kocha marcio maximo akionesha furaha yakemamia ya wakazi wa dar walijitokeza kuipokea stars iliyokuwa katika msafara toka uwanja wa ndege hadi mjini
uzalendo hautushindi tena
baadhi ya wachezaji wa stars wakiwa matumbo wazi baada ya mashabiki kuchukua fulanazzz zao kwa furaha

mkereketwa na mmoja wa viongozi wa kamati ya saidia stars ishinde dk. ramadhani dau naye alikuwepo toka sudan na katika msafara ambapo alidanda juu ya gari toka eapoti hadi mjini
mitaa kibao ilizibwa kwa muda

Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) tunaipongeza timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufanikiwa kupata tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast.

Ushindi wa Taifa Stars ambao iliupata Jumamosi kwenye Uwanja wa Al Hilal jijini Khartoum, Sudan dhidi ya wenyeji Nile Crocodiles umefungua ukurasa mpya wa mpira wa miguu Tanzania kwani ni changamoto kwa michezo mingine kuwa pale ambapo wahusika wanapotimiza majukumu yao ipasavyo hakuna kisichowezekana.

Kwa hatua hiyo mbali ya wadau wengine tunatoa pongezi za pekee kwa wachezaji na benchi lote la ufundi likiongozwa na Marcio Maximo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadhamini wa timu hiyo Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na benki ya NMB.

Ni wazi kuwa mafanikio hayo si changamoto kwa wachezaji wa Taifa Stars watakaokwenda Ivory Coast katika fainali hizo zitakazoshirikisha timu nane, bali itakuwa vilevile kwa wachezaji chipukizi na wale wanaoinukia lakini hawafanikiwa kupata nafasi ya kuitwa kwenye timu hiyo.

Pia tunaupongeza uongozi mpya wa TFF uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili chini ya Rais Leodegar Tenga na makamu wake wawili Athuman Nyamlani na Ramadhan Nassib.

Uongozi huo una changamoto kubwa ya kulinda mafanikio yaliyopatikana na kutekeleza mengine ambayo hayakufanyika katika awamu iliyopita. Changamoto hiyo ni kubwa kwa vile wadau wana matumaini makubwa kutoka kwa safu hiyo mpya.

Lakini shukrani za pekee ni kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kuchagua safu ambayo TASWA tuna imani kuwa ina nia, uwezo na sababu ya kukabidhiwa majukumu hayo hasa wakati huu ambapo hamasa katika mpira wa miguu hasa kwa timu ya Taifa imeanza kurudi.
Boniface Wambura
MWENYEKITI




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. hongera sana taifa stars, kwa kweli wamefanya,.. kazi kubwa na yenye kuletea taifa sifa,.japo ndoto za watanzania zilikua ahead of time and far from reality,wapo walio laumu na kuvunjika moyo hata kutoa maneno ya kejeli kwa kocha, pale timu ilipo shindwa kupata nafasi kushiriki fainali za mataifa ya afrika, pamoja na kombe la dunia, walisahau kwamba ili mtoto atembee anaitaji kutambaa kwanza, sasa tumeanza kutambaa, tusubiri kutembea.
    pia naomba kutumia fursa kumuomba kocha mziray kumuomba msamaha kocha maximo na uma mzima wa watanzania kwa comments zake i mean negative ones, kuhusu ufundishaji mzima wa kocha na staili nzima ya kocha maximo ya kubadili wachezaji kila mara, leo hii bila aibu anadiriki kukaa mbele ta tv taifa na kumsifu maximo pamoja na timu nzima,.sikatai yeye kuiunga mkono timu, ila naona ingekua vyema angeomba msamaha kwanza, kwani mimi ni mmoja ya walio kerwa article zake.
    mdau Anu...naomba kuwakilisha.

    ReplyDelete
  2. Katika watu ambao kwa kipindi chote cha Maximo walikuwa ni kikwazo na kukatisha Tamaa ni Silversaid Mziray. Mpaka leo hatujui ni kwanini alikuwa na ngebe na Kocha huyu siku chache tu baada ya kuwasili. Nadhani amejifunza sasa kuwa mtoto hawezi kukua in two years.

    Hongera Maximo.

    ReplyDelete
  3. Mbona sasa wachezaji wenyewe wamenuna baada ya kupokonywa T-shirts zao?! Ahhh, jamani!

    ReplyDelete
  4. Anony 5.15 PM Kumbuka kuna swala la kuzilipia hizo Tshirts!

    ReplyDelete
  5. Kilichobaki sasa ni kuwaongezea lishe wachezaji, maana walikuwa wakilalamika kina Rigobert Song na Jeremi wa Taifa Cameroun walikuwa wanatumia chakula kuwabana kimchezo.

    Nashauri Maximo aombe usaidizi wa dietician(baba lishe) na kuwapeleka gym wajenge mwili.

    Tukiongeza hilo huko Kampala na Ivory Coast tutatisha na wawili watatu ktk Stars watapata timu Ulaya.

    Mwisho pongezi kwa sana Stars.

    ReplyDelete
  6. duuuuuuuuuu, jamani Maximo ana dole gumba refu kweli! angalia picha ya kwanza, utadhania soseji!!!

    ReplyDelete
  7. hongera staz kwa ushindi, pamoja na hongera nina hoja zifuatazo
    1. Je ni haki kuandama na kufunga barabara (ingekuwa Chadema wanamshanglia mbunge wao ni virungu kwenda mbele)
    2. Hivi Taifa letu linawezaje kunghalimia Maximo millions za hela, wakati walimu wa michezo mashuleni wamechoka? hapa ikumbukwe kuwa hata kama tunashinda, stars ni sehemu ndogo sana ya watanzania, na haichangii chochot kwenye pato la taifa kwa sasa na wala kwa miaka kadhaa ijayo.
    Maoni
    1. Polosi wanapaswa kufanya kazi kwa usawa na kufuata sheria, Maana sidhani kama hawa stars walipewa kibali cha kuandama?
    2. Serikali inapaswa kuweka msingi toka chini na sio kutumia pesa zetu za kodi kutafuta umaarufu usiotusaidia kwa sasa au miaka kadhaa ijayo wakati kuna mambo ya kibao yanalala kama vile shule hazina madawati, mahama zetu za mwanzo ni mbovu nk.

    hapa hakika hatutaelewana na fans wa mpira,lakini think of Tanzanians? kwa sasa tunahitaji mambo ya msingi si pride ya kushinda vikombe? ingawa ushindi ni jambo la kheri.

    Naipenda sana Lipuli ya Iringa? though kuna gazetu liliniudhi sana kwakuandika Lipuli yalipuliwa baada ya kuchapwa bao kadhaoo miaka hiyo ikiwa daraja la kwanza (super league haikuwepo enzi hizo)

    ReplyDelete
  8. Kazi saa ngapi?

    ReplyDelete
  9. wewe madawati nani akujengee ?wewe umeifanyinyi serikali ? watu wa waporini alinaimbia babu yangu nimesoma shule za kata nguvu ya wananchi pale migombani watu wadiriki kulima hata shamba za walimu ...na sasa niko kwa msovieti nikiendeleza libeneke... ulaya wanasema kujitolea ipo sana na inachangia sana maendeleo , go star inatia moyo kwa cha muhimu ni kuandaa mfumo mzuri wa michezo yote ili kwetu ushindi uwe ni kawaida pambana kwa maarifa na mchango wako unahitajika kwa hali na mali kwa maendeleo ya tanzania,na serikali ni watu kama mimi na wewe,aluta kontinua

    ReplyDelete
  10. Pumba nyingine mpaka mtu unashindwa kujibu. Haya mdau wa Lipuli mshindi wewe.

    ReplyDelete
  11. Jamani hii imetokea baada ya miaka 28 kama kazi mmeshindwa kufanya miaka yote hiyo siku moja itabadilisha nini? Achezi roho za korosho acheni watu wale raha.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Taifa Stars na Maximo hongera kwa uvumilivu wako!! Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  13. Sudan fired coach Mohammed Abdallah Mazda following what was their first home defeat since 2005.

    ReplyDelete
  14. TFF KAMA HAMTAWALIPISHA WACHEZAJI WALIOGAWA JEZI ZAO KWA WATU, BASI HAMTAMTENDEA HAKI MCHEZAJI MLIYEMLIPISHA JEZI KWA KOSA HILOHILO. LAZIMA WAZILIPE HIZO JEZI ILI HAKI IWE SAWA MBELE YA TFF.

    ReplyDelete
  15. CHAKULA MUHIMU HAPA KWA WANAMICHEZO HUU NI UTAPIA MLO . TWENDE MBELE TAFUTA MAMA BABA LISHE ILI VIJANA WAJENGE MWILI. EVIDENCE BASED RAMOS NA TOTENHAM HOTSPARS. LISHE NA ZOEZI NI IMPORTANT KWA ATHLETIC YEYOTE YULE. MAMBO YA AKINA KHAMISI GAGA NI YA ZAMANI HAYAKO TENA KWA ULIMWENGU WA SOKA=IMEAN GONGO NA ZOEZI. HONGERENI STARS

    ReplyDelete
  16. Wewe Michuzi acha uongo, jina la utani la timu ya Tiafa ya Sudan sio "NILE CROCODILES"...Hapo blaza misupu umejikwaa, Timu ya taifa ya Sudan inaitwa "Desert Hawks" kwa jina la utani...ooooi oi oi...usikonde misupu!!....Pamoja Daima.

    ReplyDelete
  17. Wewe uliyemwambia Michuzi muongo naona unachanganya mambo. Timu ya Sundan inaitwa "Desert Hawks" na jina la utani ni "NILE CROCODILES". Taifa Stars siyo jina na utani, ni jina linalojulikana Fifa na vyama vyote vya kandanda. Kuna watu wanaiita JK 11, wengine Maximo 11, na wengine vijana wa Maximo sasa hayo yote ni majina ya utani. Ingekuwa vizuri kama ungemuomba Michuzi msamaha na pia homework yako ya leo tafuta kwa nini timu ya Sudan inaitwa "NILE CROCODILES" ukija tena hapa uje na homework yako ili tujue kweli umeshaelimika.

    ReplyDelete
  18. Uzuri wa kocha ni timu kushinda,fikiria kama Taifa ingefanya kinyume chake weee
    m3

    ReplyDelete
  19. kombe la mbuzi ilo jamani acheni kelele!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...