Kwenye mgongano kati ya watu wenye madaraka na wale wenye pesa mara nyingi (kama siyo zote) wale wenye madaraka hushinda, kwa kadiri ya kwamba bado wana madaraka yale. Wakati huo huo hakuna watu ambao hawawaamini watawala kama watu wenye pesa.
Hata hivyo ni wenye pesa kutokana na kutowaamini wenye madaraka hujikuta wakijiweka karibu na wenye madaraka ili angalau kuwa katika mazingira ya "kujua" nini wenye madaraka wanapanga dhidi ya wenye pesa.
Hata hivyo wenye madaraka mara zote wana hofu na wenye fedha kwa sababu wanajua kabisa kama wenye fedha wakitaka madaraka wanaweza zaidi kuliko wao (watawala) kutaka kuwa wenye fedha. Kutokana na mkinzano huo basi wenye madaraka mara zote wanawaangalia wenye fedha kwa shuku na wale wenye fedha wanawaangalia wenye madaraka kwa shuku.
Mgongano unatokea siku watawala wanapoamua kufanya kitu kinachowatishia wenye fedha au wenye fedha kufanya kitu kinachowatishia watawala; pande hizo mbili zinajiandaa kugongana na mgongano huo hauepukiki; ni mgongano wa lazima. Mgongano huu ni wa lazima ili kuweza hatimaye kuamua ni nani kati ya pande hizi mbili ndiyo mwenye nguvu zaidi (the most powerful).
Katika kuamua hili aidha mwenye madaraka anajitahidi ili na yeye awe na fedha nyingi au yule mwenye fedha nyingi naye apate madaraka. Ukimkuta mtu mwenye fedha pia ndiye mwenye madaraka basi utaiona nchi ambayo hakuna kinachofanyika zaidi ya kurushiana vijembe, migongano, chuki n.k lakini pia utaiona nchi ambayo watawala wake wanatawala kiimla zaidi na jamii inakuwa kama kiunga chao cha mpunga ambapo wanaweza kuamua kuvuna wapendapo au kuacha ndege wajilie.
Katika sakata tunalolishuhudia Masha ataweza kushinda tu endapo ataendelea kuwa na madaraka na Mengi ataendelea kuwa tishio kwa kadiri ya kwamba yeye ni tajiri. So one of them has to give in; mmoja asiwe na madaraka au mwingine asiwe tajiri! Kwa vile vyote viwili vina mvuto tofauti, ni rahisi kwa tajiri kuwa maskini (kwani anaweza kuanza upya kutengeneza biashara yake) kuliko kwa mwenye madaraka kuachia (kwani ni vigumu kuyapata tena).
Kwa vile mwenye madaraka anauwezo mkubwa wa kushiinda katika sakata hili, lakini kwenye kushinda mioyo ya wananchi, ushindi utakuwa kwa Mengi (yawezekana ndicho alichochezea kamari?), kwani at the end, watu watalign up na mtu mwenye fedha kuliko mtu mwenye madaraka!
Don't ask me why!
Mdau Mwanakijiji
Hivi Mengi ni tajiri wa kutisha mpaka anatishia wenye madaraka? Mbona ninamuona ni tajiri wa kawaida tu wala si tajiri mkubwa sana wa hivyo! Dar kuna matajiri bwana wala usisikie wako kimyaaaa! Hata kina Bakhresa hawaoni ndani, kuna mtu aliwasaidia watoto yatima milioni 40 kwa mkupuo bila hata kutikisika sijui kuwalipia deni la nyumba iliyokuwa poni hata kwenye radio hatukumsikia akitajwa na mpaka leo watu hawajui. Wengine mchango tu ya elimu wanatoa milioni 100 bila kupepesa macho! Zaidi ya lunch ya walemavu ambayo inarekodiwa kwenye matv na kutangazwa gazetini sioni hizo pesa za Mengi!
ReplyDelete1. Mdau wa 1:46 unayosema ni kweli kuwa pengine katika kumi, tano au tatu bora Tanzania, Mengi anaweza kuwa hayumo. Lakini bado hiyo haiondowi ukweli na sifa ya Mengi kuwa ni mmoja wapo kati ya matajiri wa TZ maana si wengi wenye fedha au umiliki wa mali kama zake. Wengine hata kumiliki tu printer ya kuchapa 'Ki-Cheche'cha Mwanakijiji tunashindwa sembuse tuwe hata na hisa moja ndani ya dude la IPP?
ReplyDelete2.Mwanakijiji mada yako ni nzuri isipokuwa umeiwakilisha katika tungo za kifilosofia zaidi kuliko elekezi au zenye ushawishi fulani katika kuchochea maendeleo ya Mtanzania.
Yaani hapa tunaweza kujikita hypothetically katika kuprove kuwa nani ni matawi ya juu kati ya mwenye Mamlaka na Tajiri wakati watu wanatakiwa kuchangia juu ya hali halisi iliyotokea ya ama kumrekebisha au kumpongeza Mengi au Masha au wote wawili katika mwendelezo wa malumbano yao halisi yaliyopo sasa.
Hivyo mimi napasua jipu kuwa:
Masha: Ukiona kama mtu kakashifu serikali na tena kasema kuwa taarifa kazitoa polisi basi wewe nyanyua simu mwagize OCD ashughulike na hilo na akupe feedback mezani kwako badala ya wewe nawe kwenda kwenye media na kutoa altimatamu zako kama vile nawe umekuwa polisi au mahakama.
Baadaye mtu akifikishwa mahakamani na akahukumiwa adhabu kwa kutoa kashifa pasipo uthibitisho hapo mbona utakuwa matawi ya juu kuliko kubwabwaja sasa ambako hakika kisheria pengine wewe utahitajika sasa kukaa kando ya kiti chako ili mahakama ikupe nafasi kama mtuhumiwa au mlalamikaji kazi ambazo zina wenyewe akina polisi na hata Mkurugenzi wa makosa ya jinai.
Waziri ukisha anza kutoa maagizo sasa OCD afanye nini jamani????
Watoto yatima milioni 40 wa Afrika nzima au? Maana Tz hata ukichanganya na watu wazima hatujafika pale.
ReplyDeletePengine ulitaka kuandika idadi tofauti ukateleza kidogo
what si going on????wadau
ReplyDeletepliz explain kidogo mana sijaelewa kuna vagi gani btn "tajiri" na wanasiasa (nigeandika apa jina linalowafaa wengi)ila michu ataiminya meseji
wanagombania nini tena???
yan adi tufike mambo mengi yatafichuka tuuu waaaaaaaaa