Habari za leo balozi. Aisee kuna mdau amepost hii kule Jamiiforums.com. Nikaona ngoja niilete hapa kwenye blogu la jamii ili wadau wa hapa nao watoe maoni yao.
Mdau Robert
______________________________________________________________________________________________________________________Huwa ninapenda kuangalia movie za kibongo.
Ingawaje tunajitahidi kwenda na wakati, lakini naona kuna makosa kibao ya wazi tunayafanya ambayo yangeweza kuepukika.

Editing:Kosa kubwa la kwanza ambalo tunafanya ni kukosa Editors ambao wako serious na kazi zao. Unategemea Editor ndio ambaye angefanya kazi mzuri ya kureview movie , yet bado kuna makosa madogo madogo kibao ambayo yananakera sana kuyaona.

Mfano – Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)
1)Sauti - sauti ya hii movie inatoka kama sauti ya mwangwi (echo). Ni kama vile walikuwa wana record kwenye chumba cha mwangwi, halafu baada ya kuchukua sauti za waigizaji wenyewe, wakachukua sauti za ule mwangwi wenyewe. Yaani sauti inatoka kama ya mtu unayeongea naye kwenye simu ambaye amejifungia chooni.

2)English subtitles - Hapa ndio kuna vituko kweli. Yaani unasoma hizo tafsiri ya English kwenye hii movie mpaka unabaki kushangaa. Ndio najua wengi tunachemsha kwenye English, lakini kama film industry ya Bongo inataka kuwa serious (kujiingiza kwenye soko la nje), basi haitakiwi kuruhusu makosa kama yale. Kuna part moja ndio iliniacha hoi kabisa. Steve na Irene walikuwa restaurant, Zanzibar. Basi Steve akawa anamwambia Irene “tafuna…tafuna…tafuna,” akimsisitizia kuwa atafune chakula anamchomlisha. Sasa kwenye subtitles tafsiri yake ikawa “cat…cat….cat.”……I was like ‘enhe!’ Mwanzo sikujua walikuwa wanajaribu kuandika nini, lakini nikaja kugundua kuwa dhamira yao ilikuwa kuandika “cut…cut…cut,” neno ambalo bado sio tafsiri sahihi ya tafuna.

Sasa makosa mawili kama haya yalitakiwa yashughulikiwe na editor. Hapa ndipo editor anapo onyesha umahili wake katika fani hii. Udhaifu wa makosa kama haya unaonyesha jinsi gani editors wa kibongo wasivyo serious na kazi zao.

Wardrobes: Ukweli ni kwamba waigizaji wana overdress mno. Sasa sijui wanajaribu kuonyesha kuwa wanajua kuvaa sana au vipi? Lakini mara nyingi wanavaa ‘loud clothes’ mno kulingana na scenes/story za movies.

Mfano - Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)
Vincent - anavaa very loud suits just kwenda kazini tu. Tena ana match na fancy shoes na hat kabisa. Unakuta kakupigia all white, kuanzia viatu, suruali, koti, kofi, na kakupigia shati moja kali jeusi…. Halafu anaishia kwenda kazini mchana kweupe. I mean, watu upiga hayo mavazi wakiwa wanakwenda kwenye mtoko jioni.

Steve – huyu yeye anakuvalia jacket moja zito la nguvu kwenye 100 degrees condition. Pia anakupigia miwani moja kubwa sana…Anavaa hivyo vyote only kwenda chuo.

Miss Uwoya - Huyu ndio alikuwa anafunga kazi kabisa. Well, lazima nikubali kwanza, kuvaa tu anajua. Maana baadhi ya mavazi yake yalikuwa yananifanya niweweseke ile mbaya…lol. Anyway, bibie huyu alikuwa anavaa pamba kali kama zile tulizozizoea kuwaona dada zetu wanugu wakivaa clubs (huku waki drop-it-like-its-hot). Yaani anakupigia capri ya nguvu, huku akimachisha na sleeveless top na fancy cowgirl hat (or whatever it’s called) mchana kweupe…..halafu huyo anaelekea sokoni kwenda kununua nyanya.
ScenesHawazingatii umuhimu wa mazingira wanayofanyia baadhi ya settings.
Mfano - Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)
Vincent supposedly ana ofisi pale kwenye jengo la Millenuim Tower. Sasa unakuta kila anapoenda kupaki pale juu, hakuna hata gari jingine kwenye ile parking. Well, inavyoonekana ile sehemu ya scene walitengeneza either jumamosi or jumapili. Lakini katika hali ya kuongeza ufanisi wa utengenezaji wa fialmu, ningetegemea pengine wangetengeneza scene ya ile sehemu angalu kwa siku mbili tofauti.
Yaani, kwa sababu wameazima ofisi ya mtu kutengeneza filamu, basi wangefanya shooting ndani ya hiyo ofisi siku ambayo hakuna wenyeji (jumamosi au jumapili). Halafu wakafanya shooting ya kwenye parking siku ya weekday ambayo kuna magari yamepaki. Hiyo ingeipa movie ufanisi wa reality. I mean, hutegemei parking ya jengo kama lile kuwa empty siku ya kazi.
All in all, kwa mtazamo wangu, hili hawa wasanii wetu wa filamu waweze kuendelea na kutengeneza filamu zenye angalau standard quality, basi inabidi kuwe na panel ya critics.
Ukosoajia utakaotoka kwa panel hii utawasaidia sana wasanii hawa kuzingatia kanuni za uigizaji. Ningependekeza baraza la wasanii Tanzania (kama lipo) liunde hii panel. Njia nyingine ni wadau kuunda a private panel of critics.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Thanks mdau kwa kuweka wazi haya makosa ya wasanii wetu wa filamu. Mimi sijavutiwa na hizi muvi zao kutokana na kutukua makini na makosa mengi kwenye filamu moja. Wanavyoakti na kuongea ni tofauti kabisa na mazingira yanavyohitaji. Na hata lugha iwe kiswahili au yai wao ni tatizo. Badala ya la wanasema ra thamini wanasema samini basi kazi kweli. Msibobadilika mtabaki na soko la "waswahili" tu kama hamtakuwa serious. Editors na directors nendeni shule please.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  2. ni kweli ndugu yangu hujakosea.hawa wasanii wetu hawavai kutokana na mazingira.nguo kama za club mtu anaenda nazo kazini.ukija kwenye swala la ngeli kama msanii anaona ngeli yake imepinda kwa kweli tumia kiswahili kuliko kuchekesha watu.ila kwa upande mwingine wanajitahidi ni vitu vidogo tu wanatakiwa warekebishe

    ReplyDelete
  3. ni kweli ndugu yangu hujakosea.hawa wasanii wetu hawavai kutokana na mazingira.nguo kama za club mtu anaenda nazo kazini.ukija kwenye swala la ngeli kama msanii anaona ngeli yake imepinda kwa kweli tumia kiswahili kuliko kuchekesha watu.ila kwa upande mwingine wanajitahidi ni vitu vidogo tu wanatakiwa warekebishe

    ReplyDelete
  4. ni kweli ndugu yangu hujakosea.hawa wasanii wetu hawavai kutokana na mazingira.nguo kama za club mtu anaenda nazo kazini.ukija kwenye swala la ngeli kama msanii anaona ngeli yake imepinda kwa kweli tumia kiswahili kuliko kuchekesha watu.ila kwa upande mwingine wanajitahidi ni vitu vidogo tu wanatakiwa warekebishe

    ReplyDelete
  5. Nimekukubali wewe unaipenda nchi yako.

    ReplyDelete
  6. Robbert hongera sana kwa mawazo yako si tu yaliyoenda shule bali zaidi ni ya busara.

    Naunga mkono 100% uliyosema na hii si tu katika 'Film Industry', yaani unapokodelea macho na kunyanyua masikio huku umetuliza ubongo wako kwenye 'Music Industry' yetu mbona hawa jamaa wa Sinema wana unafuu, maana kwenye Muziki hali ndio mbaya kabisa.

    Yaani tuna vijana na wazee wa masauti wa nguvu sana na maproduza waliobobea kuchanganya ala na hata kupindisha ulaka wa mtu n.k lakini kazi nyingi za wanamuziki wetu hazifanyiwi UHAKIKI WA KITAALAMU.

    Kwamba je ujumbe unaotolewa umekaa sawa na katika video cassetes /VCDs /DVDs je muonekano wa waimbaji na kile kinachoimbwa kinalandana(hakuna ukinzani)?

    Unajua unaweza kuimba wimbo yaani zile beats zake zikawa zinachengua watu au hata sauti yako ikawa inamtoa nyoka pangoni lakini ukachafua hali ya hewa kwa mstari mmoja tu ambao ama unadharisha au kulinyanyepaa kundi la watumishi fulani, wenye ulemavu (sio walemavu) fulani au jinsia fulani pasipo kujijua.

    Matokeo ya makosa haya ni kuwafukuza wateja wa makundi hayo uliyowakosea na zaidi ya yote unakuwa umemkosea Mungu pia.

    Kwenye Kwaya za dini unaweza kukuta kasehemu ka picha ya 'Jesus of Nazareth' kamechomekwa bila hata kupata kibali toka kwa produza na au mmiliki wa album hiyo. Huu ni wizi na siku mambo haya yakifumuka mbona kuna Kwaya au Makanisa au Maproduza watakubwa na wimbi la vyesi sawa na za ufisadi?

    ReplyDelete
  7. Very constructive critisism, namna ya ukosoaji kama huu ni wa kuigwa kwani wengi tukifanya hivyo kazi za wale wakosolewaji itakuwa nzuri na tutakuwa tumewatendea haki. Nadhani hata wahahusika huenda wamefurahia posting yako.

    Ni vema pia tukakumbushana hasa kwa wale wanaopenda kukosoa kwa kuwadharau wengine na hata kuwatukana huo si ustarabu kabisa. Fuateni nyayo za Mdau huyu.

    ReplyDelete
  8. Bwaba Robert maoni yako nayaunga mkono. Hata mimi hujiuliza maswali mengi juu ya mambo uliyo yaongelea, ususani kwenye sehemu ya kuigiza. Mwigizaji mwenye taaluma ya kazi hiyo, anapaswa kujiweka katika hali ama mazingira ya jambo analo liigiza kiasi kwamba mtazamaji akimuangalia, aweze kupata taswila au jumbe zilizolengwa na mwigizaji bila hata mtazamaji kusikia maneno. Kwenye sinema zetu hilo ni gumu sana, yaani mtu anacheza sinema akiwa na nia ya kuonyesha uchungu, lakini atazamwapo usoni, ile sura uchungu haipo kabisa.
    Jambo jingine linikwazalo mimi ni ( suspense). Hili neno silifahamu kwa kiswahili. Ila maana yake ni hari inayo muacha mtazamaji asijue mwisho wa sinema utakuwaje. Sinema nyingi za kimatumbi utazijua mwisho wake unapoanza kuicheza tu.

    ReplyDelete
  9. Nakuunga mkono ndugu.Mbali ya hayo uliyokosoa pia ningependa pia waigizaji wetu wangekuwa pia wanajaribu kuongea natural ninamaanisha kuwa ukiangalia sinema ,michezo mingine wanakuwa kama wanasoma.Pia uigizaji umezidi sana ku-copy filamu za kinigeria.Pia kwenye maagizo wanaohusika wangepata kozi fupi ya First aid.Ilikama kuna sehemu mtu anaanguka kwenye part ya uigizaji(Mchezo ulivyopangwa) wawe wanajua jinsi gani ya kumuinua mtu -Ninamaana tuende kitaalam.Kujifunza tekniki za ubebaji ni muhimu.Tunajitahidi lakini inabidi kutumia utaalamu na wataalamu tunao wazuri tu ni kuwatumia vizuri.

    ReplyDelete
  10. hii ni kweli kabisa bongo movie zinatia aibu hasa ukiwa ubatazama na mtu ambae sio wa bongo ndio maana watani wa jadi wanapata point unakuta movie haimaliziwi ili wapate kuuza sehemu ya pili yaani kila movie ya kibongo ina pt2 wacheza filam ndio kabisa hawajui kitu wanachojali kuonekana ktk luninga.. kitukinachonifanya hata baadhi ya movie's nyingine huwa sizimalizi nikizitazama na hata nikiimaliza ndio huwa siirudii tena kuitazama sababu ya kukosa utamu kabisa

    ReplyDelete
  11. Yani nimeguswa kweli na hizi critics. Mimi mpaka nimekuwa sipendi tena kuangalia movie zetu kwasababu muda mwingi najikuta nakosoa tu. Our artists are not natural kabisa, yani you can feel it kabisa!

    ReplyDelete
  12. KWA KWELI HONGERA SAANA

    KWA HILO ULILOSEMA YAANI MOVIES ZAO HASA SUBTITLES DUH TAABU KWELI KWELI

    TUNAOMBA WAHUSIKA MBADILIKE NA KULEKEBISHA MAKOSA

    ReplyDelete
  13. Robert!
    umeangalia dar to lagos?
    Kanumba anasema zis food iz too much pilipili.
    Anyway makosa haya yansababishwa na wadau wa film coz sasa ivi filamu za kibongo zinalipa ndo maana unaona kwa mwaka mtu ka ray au kanumba anatengeneza zaidi ya movie 10...umeona wapi wewe? scene ya mwezi mzima wao wanaact kwa masaa 5, wakijitahidi sana wanatumia only one day...ndo yaliyotokea kwenye oprah hasa kwenye location ya kiofisi.

    ReplyDelete
  14. Ndugu yangu Robert uliyosema yote ni ya kweli, ila unasahau kuelewa kitu kimoja muhimu kwa sisi Watanzania, ukweli ni kuwa sio kwenye movie tu hatupo "serious" kwa kila kitu. Yaani tu wababaishaji flani hivi, na hili lita "tucost" sana wabongo kwa sasa na siku za baadae.

    ReplyDelete
  15. Yaani mdau hapo umegusa wengi, loh yaani hizi movie za bongo wakati mwingine zinatia kichefuchefu! Kwanza waache kuiga themes za wanigeria! halafu kwenye suala zima la subtitles, ebo hivi wanaona tabu gani kumuajiri mtu aliyesomea fani ya lugha akafanya hiyo kazi ya kutafsiri?! Yaani huwa ni utmbo mtupu, maana wanapoteza mwelekeo mzima wa filamu, basi kama hawawezi si waache kuweka hizo subtitles!? Ah! Tuna utamaduni mbaya wa kufanya vitu nusu nusu na kurukia rukia mambo! Na ubahili pia, pale Chuo Mlimani kuna wataalam kwa nini wasishirikishwe kama washauri?

    ReplyDelete
  16. 101% support kwa ulichobainisha, kama wadau wengi walivyosema ni makosa madogomadogo, mimi nashauri wakati wa kuweka subtitles wawashirikishe baraza la kiswahili au walimu wa lugha chuo kikuu, kazi zao zitakuwa bomba sana. Kuna kitu kimoja ambacho ningeongezea katika kushauri, wabongo tunaiga sana hadi tamaduni ambazo sio zetu, mfano movie nyingi zinakuwa na scene za "romance' kali mno kiais cha kukimbia sebure kama mnaangalia na watoto, sasa kuwaengua watoto wasiangalie hizi movie za wabongo wenzetu hatutawatendea haki, kuwe na kiasi ujumbe utafika tu kwa watazamaji, matokeo yake madada wetu mnaotoa denda mtaachika sana kwa sababu mimi mchumba wako au mme wako siwezi kukuona unatoa tongue kiss (french kiss) halafu kesho nipite na wewe barabarani, na sisi watoto wetu wataenda ku fanya mazoezi na matokeo yake mimba zisizotarajiwa etc.

    ReplyDelete
  17. Safi sana ndugu yangu.Tatizo la matatizo haya ni kwamba M'bongo akikosolewa hufikiri CHUKI BINAFSI(Japo wakati mwingine kweli) lakini "CRITICISM IS THE ENGINE OF DEVELOPMENT" Watu ambao walikuwa very bright wamekosolewa"Them considered Genius but people still drew shortcomings from their findings" Aristotle,Plato,Newton,Michael Faraday,Various Arch Bishops, Pope,Apostles, Prophets and Kings (k.m Daudi na Ubakaji) etc wamekosolewa. Lakini mpaka mwisho wa dunia watu wana-salute achievements zao and they are considered most accurate,smart and bright human beings.Sembuse wasanii wa Kibongo ambao wengi wao ni Armatures and not Professionals. Ni vema tujifunze kuelewa na kukubali"understand and accept=msaada tosha kuliko hata shule" huku tukiutetea ukweli kwani kweli itatuweka huru kweli kweli."Watu wangu wanateseka kwa kukosa maarifa"
    CRITICISM IS THE ENGINE OF DEVELOPMENT.

    ReplyDelete
  18. Nashukuru kwa kukosoa filamu zetu. Nimetokea kuchukia kuangalia AMag+ (DSTV)kwa sababu filamu nyingi za kitanzania hurushwa hapo but zina kingereza kibovu kinachotumika kwenye subtitles, tuwe serious ni aibu jamani kwani twaonekana nchi nyingi za afrika,hii ilikuwa ni Opportunity kwetu kutangaza filamu zetu, lakini tunachofanya hakieleweki, tumeshindwa hata kuajiri watu wa kuweka kingereza kizuri pale? TUWE SERIOUS JAMANI HATUWEZI TUENDE TUKAJIFUNZE KWANZA.

    ReplyDelete
  19. duh hii mpya na kali sana "cat cat cat" ikimaanisha tafuna tafuna kiasi wakenya watucheke

    ReplyDelete
  20. igizeni zenu na sisi tuzikosoe....yaani na maana
    wakosoaji wengine hawana sifa za kukosoa bora wawe kimya!

    ReplyDelete
  21. True that these movies need critics and the critics can be some of us viewers of African movies specifically Tanzanian movies.

    The same stories in Africa are making the rounds that's why there seems to be similarities between these movies in Bongowood and Nollywood. Foreign films too suffer the same - remember "Beverly Hills Cop"? Well, there is an Bollywood movie called "Jalwa" with the exact same theme. Remember "Bad Boys II" the scene where will takes a Hummer through the hillside slum
    in supposedly Cuba? That scene Jacki Chan did it way before in a movie called "Police Story" If I am not mistaking the name.

    Bongowood has come a long way. One thing I think they should start doing is act and speak naturally eg in a movie called "Point of No Return" (actually its playing right now on African Magic Plus while I am writing this, though I have seen it before)the lead actress former Ms TZ Wema Sepetu speaks in a way that is not everyday Swahili - I guess you have to see the movie to understand as she keeps thanking the actor "Macheni" where there is no need to thank etc

    I am not a film director or in that industry but I think the camera stays too long on one scene. I think the standard is 2 minutes but some Bongowood scenes stay forever! Well, figuratevly.....

    The English subtitles are worse! When someone is leaving going out somewhere the subtitles show "living" instead. I also think it suffers from direct translation and they want to translate each and every Swahili word into English. Petty conversations in Swahili suffer the most - try translating into English this sentence on a Swahili movie "Dunia tambara bovu, baba, we acha tu" Keep in mind that "baba" was a word a lady used while conversating with her"son"

    I don't see a problem in making many movies, heck, Chackie Chan and them Honk Kong movie industry make one films in 1 week or less! Bollywood too used to be the same.

    All in all, there are some gems there in the Bongowood movies. Ever watched a movie called "Masaa 24"?. How about the double role nicely done in "The Twins"? "Mtoto Haki ya nani?"? and many more.

    ReplyDelete
  22. My fellow Tanzanians, It’s good to disagree without being disagreeable. Let’s not be a firewall towards regional trade. Global and regional trade is the norm of the 21 century. The fact of the matter is the whole world is moving toward global and regional trade liberalization.

    Mashaka made his opinion in the debate. None of us rule with our opinion in a debate. Mashaka himself knows well that US gave him that opportunity to advance and realize the American dream. This wouldn't be possible if US had its doors shut to foreigners. Mashaka opinion absurd and its like building a firewall towards international free market which put him in Wall Street at the first place. Misleading people by rationalizing the US recession and unemployment problems is a result of bad treaty such as NAFTA is a day break lie. Greed, mismanagement of corporate America and Wall Street in particular is to be blamed, and Mashaka you are a part of it. Brother, be honest with your facts while gaining your little fame back at home for your future endeavors. You and I, we both know what went wrong in the US. Let us be real about it.

    After taking a moment in scrutinizing the whole debate of East African federation, I can understand Warigi's point of view even though he had a negative delivery tone. His harsh words are a result of frustrations caused by Tanzania being a firewall in EA federation progression. Warigi even mentioned if we are not ready we can pull out and let other member countries proceed with the federation. I agree with him since Tanzania is putting other member countries in stagnation.

    On the other hand, I understand my fellow Tanzanians concerns and I strongly agree with them in issues related to land privatization to foreigners, employment, national security, mining industry, and tourism industry. I feel we should pull out of the federation and let other countries proceed while we take care of our own problems at home. By doing so, Tanzania will have a clear picture as we pay close attention of the federation’s progress before committing itself.

    The urgency of solving our own problems in the country overrides the significance of joining the confederation at this moment. Our priority right now should be: building our democracy; building our infrastructure; combating graft and corruption; fighting poverty and diseases; raising our economy with its people’s living standards; and educating our people.

    ReplyDelete
  23. MIMI NINA MENGI SANA YA KUONGELEA KUHUSU TOPIC HII, LAKINI KWA LEO NATAKA TU KUJUA KITU KIMOJA, HIVI NI LAZIMA KILA FILM INDUSTRY INAYOANZISHWA SIKU HIZI MPAKA IISHIE NA "WOOD"?, HONESTLY MIMI INANIKERA SANA PALE AMBAPO WATANZANIA TUNAPOSHINDWA KUWA CREATIVE NA VITU VYETU WENYEWE.
    JUST BECAUSE MAREKANI YAO NI HOLLYWOOD, INDIA-BOLLYWOOD, WANAGERIA NAO ETI NOLLYWOOD BASI NA SISI BONGO ETI BONGOWOOD, HONESTLY ARE YOU GUYS SERIOUS? VITU VIDOGO VIDOGO KAMA HIVI NDIO VINATUNYIMA HATA OPORTUNITIES ZA KUENDELEA MBELE!!!

    ReplyDelete
  24. nashukuru sana mdau
    you are right

    ReplyDelete
  25. Mnapo andika vitu kama vivyo lazima muwe "fair" angalau elezea kidogo uzuri uliomo kwenye filamu hizi na baadaye toa hizo "critics" zaidi ya hapo ni kama mnawaambia watu wasizinunue kitu ambacho siyo "fair" kwa wachezaji wa filamu hizo.

    ReplyDelete
  26. Siyo siri jibaba umeongea Ukweli mtupu sema kuna kitu kimoja ambacho mimi naona hujakisisitizia:DAYALOG. MUVI INAWEZA KUWA NZURI SANA lakini utakuta imepewa dayalog mbaya hadi inakuchefua,
    HOWEVER ningependa kuwashukuru waigizaji wetu kwa kujitahidi kwao kutungeneza hizi muvi na vilevile nawashukuru wabongo wazalendo kwa kununua na kuwafanya vijana wetu wenye vipaji kuendelea kupata ajira.thanx

    ReplyDelete
  27. tatizo ni hao waigizaji wa hiyo muvi,wamekutana wote wakuja na hapo wameekti pamoja basi kila mmoja kataka kuuza sura,nani anajua kuvaa zaidi ya mwenzie,nani anapendeza zaidi akipiga mkorogo,nani anajua kurembua macho zaidi,na ingewezekana wangetuonyesha mpaka nani anavaa shanga nyingi na kukata mauno vizuri maana hawa akili zao wanazijua wenyewe

    ReplyDelete
  28. hahahahaaa yan u guys made my day
    dah cat,,,cat,,,cat???paka au???
    yan kiinglish hiki
    annon apo ndani alosema "wakenya" watacheka umenikuna saaana
    ebu waacheni ao wakenya jaman
    ila izi movi ni kweli utaaramu waitajika saana tu,,me sielewi au no ushirikiano???kuna wasomi wanamalizaga pale UDSM kozi ivi FP sijui ya maswala aya apa wana kazi gani???au na pale bagamoyo na baraza la filamu sijui utamaduni what on erth ur paid for???
    au kuna zengwe gani apa

    ReplyDelete
  29. Nimefurahi sana kwamba kila mtu amemuunga mkono mtoa hoja. Nami ijapo nisingelipenda kusema namuunga pia mguu, sorry mkono, lakini nimekunwa sana na hoja hii kwani imekuwa ni kilio changu siku nyingi.

    Pamoja na yote yaliyo tajwa ya lugha, mavazi na mengi mengineyo, shida kubwa yangu ni ubovu wa uongozaji (directing) ubovu wa wa uhariri (editing), uigaji wa mambo yasiyofaa (mambo msiige...) mfano filamu za kimataifa zinakitu kinaitwa PG, R, etc etc ikiwa na maana kwamba kila filamu ina walengwa. Filamu za watoto hazina mambo ya kipuuzi puuzi na zinakuwa rated PG, za wakubwa zinaandikwa kabisa R na kadhalika. Sasa filamu za bongo kwanza kabisa hazihakikiwi na kuwa rated. Sijui kama kuna chombo cha kufanya hivyo hapo Bongo. Sirikali ipo wapi kwa hili sijui. Nilipata filamu moja ya bongo nikaitizama mbele ya watoto nikijua kwamba utamaduni wetu sio ule wa kuonyeshana mwanamume na mwanamke wamelala uchi kitandani. Lakini niliboreka na kupata aibu mbele ya watoto wakati filamu hii ilivyoonyesha vitu hivyo bila mpangilio. Sasa imekuwa kila nikipata filamu ya bongo ni lazima niicheki kwanza mwenyewe kabla sijashirikisha watoto. Aibu gani hii?

    Asikudanganye mtu, Mila na desturi za kila jamii zinabakia zilezile na zikizingatiwa zinaleta mvuto sio tu kwa wanao husika bali hata na wageni wa jamii ile. Angalia baadhi ya movies za wahindi zinavyo zidi kupendwa na zinalenga zaidi zaidi desturi zao. Hata kama kuna vya kuiga lazima viigizwe kwa mantiki ya desturi zao. Sasa siye wabongo ni kuiga hata visivyoigikwa. Ndio movies zetu hizo.

    Ukweli kwa upande mwingine ninawapa hongera wana filamu wa bongo kwa kujitahidi hata wakafanya kidogo walichoweza kufikia. Lakini sio lazima kubakia pale pale. Kuna haja ya kusogea zaidi mbele kwenye ufanisi zaidi ya kufyatua mimovie kibao ambayo haina ladha.

    Kuna vitu kadhaa wanahitaji kujifunza zaidi ukijumuisha na yale yoote yaliyonenwa hapa na wachangia hoja pamoja na mtoa hoja mwenyewe.
    1. Upigaji - nadhani wanapaswa kujifunza upigaji mzuri wa filamu. Bahati nzuri fani hii ninaijua na ninapo angalia wanachokifanya kinanichefua (samahani).
    2. Kila mtu ana kipaji chake. Hivyo wanafilamu wetu wanahitaji kutafuta watu wenye vipaji kweli kweli kwenye kila jambo ukianzia na mavazi, hadi after effects etc etc. Ninavyodhani, hizi movies huwa mtu huyohuyo anakuwa ndiye Director, ndiye mpigaji, ndiye editor na producer kila kitu yani. You cant be the jack of all trade brother. Hata movies za wadau wa majuu utaona wanakuwa na wataalamu kibao kwenye movie moja kwani kila mtu akiingiza ka utaalamu kake basi mambo yanakuwa mazuri. Pengine ni kuwa Bongoni kwetu kila mtu anataka kuwa kila kitu badala ya ku specialize.

    Anyways ni mengi lakini ukweli ninaweza kusaidia sana kama nikiwa consulted. anwani ni bunyenye@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...