magari kibao bandarini, yakisubiri kuvamia barabara zetu njiwa
kama utitiri
na yanazidi kushuka tu...mgogoro kuyagomboa - wadau mnasemaje juu ya hili



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. 1.) PANUA JIJI/MIJI/VIJIJI NA BARABARA.

    2).KILA KAMPUNIINAYO INGIZA MAGARI (YALIYOTUMIKA) YAWE NA (WARRANTI YA MIAKA/MAILI ZAKUTOSHA)

    3.) NA BADO !!!! WENZETU WANAINGIA KWENYE DUNIA YA "HAI BRIDI" KWENYE KILA KITU "HYBRID" KAZI KWETU

    ReplyDelete
  2. HIVI UNAJUA TANZANIA NZIMA KUNA MAGARI 600,000 TU. NA HIYO IDADI NI YANAYOTEMBEA NA YASIOTEMBEA! NA POPULATION YA TANZANIA INAKARIBIA MILIONI 40.

    TATIZO SIO MAGARI MENGI TATIZO NI INFRASTRUCTURE TULIYOKUWA NAYO NI YATOKA MKOLONI HAKUNA KIPYA. NAOMBA NITAJIWE KAMA KUNA BARABARA AMBAYO SI YA MKOLONI TANZANIA.

    BADO MAGARI YANAHITAJIKA SANA TANZANIA. CHA KUFANYA NI KUJENGA BARABARA ZA KISASA.

    ReplyDelete
  3. Hii ndio Solution kwa sisi ambao tunapata tabu na Public Transport, hivyo inatubidi tuagize tu magari. Sasa tutafanyaje wakati Daladala hazijatulia kabisa kabisa

    ReplyDelete
  4. Kama nimeelewa vizuri tatizo ni kugomboa, maana yake uwezo wa watu kifedha kuweza kuyalipia kodi au urasimu wa bandarini katika kuyakomboa. Kama tatizo ni uwezo wa watu kifedha basi nashauri TRA kuweka utaratibu ambapo watu wataweza kulipia kodi kwa installements yakiwa yameshatoka. Bank pia zinaweza kushirikiana na bandari na TRA kuwawezesha watu kupata mikopo ya kulipia hizo kodi kwa watakaoshindwa kulipia magari full payment. Utaratibu huu naamini uatboresha ufanisi.

    ReplyDelete
  5. "KIINI MACHO" MAGARI MACHACHE KUPITA KIASI HAPO BONGO. KWENYE KILA FAMILIA KUNA ANGALAU GARI MOJA ?

    ReplyDelete
  6. Bongo hakuna magari kabisa tatizo ni barabara kama walivoeleza wengine kwani hayo magari hapo bandarini ni sawa na parking ya shoping mall moja na kama hapa zipo zaidi ya miatano kwahio tatizo ni sirikali yetu wamekaa tu hawaongezi japo barabara ziwe freeway kama pale fire ilitakiwa barabara hazikutani nyengine juu na nyengine chini na mapipa sehemu nyingi tu zakufanya hivo sidhani kama hatuna fweza ktk serikali yetu kujenga hivo vidaraja uchurwa

    ReplyDelete
  7. Watu badala ya kukazana na uhamasishaji wa usafiri wa jumuia tunakazana kuiga hata yale yasiyofaa kwa nchi kama yetu.Tunahitaji mji upanuliwe kwa mpango,barabara tulivu,bahari itumiwe kwa usafiri wa wakazi wa Kawe,Bahari Beach nk.Hata treni pia zishughulike toka stesheni hadi nje ya mji.Sio mambo ya kuwa na gari ishirini kwa familia moja!!

    ReplyDelete
  8. Tatizo wabongo wanajua kumiriki gari ni umaridadi kumbe huku ulaya ni kitendea kazi tu cha kuokolea muda....kwa hiyo naona bora kuwa na magari mengi ya jumuiya ili tukaokoa muda kuliko kuwa na magari mengi ya binafsi wakt barabara zipo chache ni kucreate folleni tu kila siku...tena huko tunakoelekea ndio balaa zaidi kwani hadi akina Mwakitwange wanamiliki magari sasa sijui kwa barabara zipi? Sijui kwa kweli mstakabali wa taifa la watanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...