Mtunzi bin Fulani, ahsante kwa majibu
Niloleta barazani, siswali setaka jibu
Niliwapa burudani, kwamambo yalonisibu
Ukweli sikula penzi, pweza ameniumbua
Utunzi ni kitu fani, kwakweli umejaribu
Wewe kwangu nimtani, au niseme swahibu
Ufafanuzi wa ndani,niko nao mahabubu
Ukweli sikula penzi, pweza ameniumbua
Moyo upo furahani, kwazako zote sababu
Shairi nilolibuni, kiutunzi limesibu
Mmefika malengoni, nakuhakiki karibu
Ukweli sikula penzi pweza ameniumbua.
Nimefika ukingoni, sitaki tunga kitabu
Malenga mbele songeni, tutimize taratibu
Ingieni ulingoni,tuache zetu hesabu
Ukweli sikula penzi,pweza ameniumbua.
PWEZA
ReplyDeleteMoyo kumkinai,iwache mbovu tabia
taaban bin hoi, humtaki watwambia
Hutaitwa bedui,pweza kumkimbia
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Muhibu rohoni, na magesti kuhamia
Bara na visiwani, kote kuvinjairia
Watokapo ndani,nawe uliwaipamia
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Msako masokoni, kwa fedha kumnunua
Bei poa jamani, au ghali maridhia
Hujihisi burudani, kila ukiparamia.
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Hima mavyumbani, pweza kumtumia
kwa mziki na asumini, uturi kunukia
Vifupi vigauni, na vidani kupambia
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Kila ulipotamani, kuwa beep huamua
Huwaficha ndani,Esta,Lily na Ua
Hutaka wawe laini,urojo hujilia
Huna kinga jamani, peku huingia
kwa sasa hutamani, pweza wamkataa
Miwasho mapajani, mabaka amekutoa
Tiba hospitalini,bado hawajaitoa
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Waganga wa darubini,waijua sababu
Mwili hauna amani,kwa dhiki na tabu
Kinga zote mwilini,kufifia taratibu
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Hongera kuamua, kwa msimamo thabiti
Sote tungejua, majuto ni laiti
Giza penye jua, huo ndio usimart
Pweza sote hatufai, wala kumkurubia
Profesa Mlimani, mtihani wataka jibu
ReplyDeleteAloleta barazani, swali lataka jawabu
Hakuleta burudani, kwa yalomsibu
Ukweli kala nini,hayo nimasaibu
Tungo yakale fani,muuliza hana jibu
Nashangaa jamani, ni mtihani wa hesabu
Sasa ni mwalim gani,test iso majibu
Eti kaleta utani, kijiwe cha ma swahibu?
Ukweli na undani,pweza kamuumbua
Moyo haupo furahani, kwa zake zote sababu
Shairi aliolobuni, kingano apata aibu
Eti kaleta utani, kijiwe cha ma swahibu?
Ushauri nasaha fani, msaada wa karibu
Au nyota ya kijani, AMREF si tabu
ANGAZA wako mtaani, usiwe bubu
Waeleze kwa makini, pweza alivyokusibu