Fally Ipupa, kizazi kipya cha muziki wa dansi nchini Kongo akiimba mbele ya umati mkubwa wa watu uliofika kwenye pati hiyo yan guvu usiku wa kuamkia jan nje ya uwanja wa New World Cinema-Mwenge jijini Dar

Fally Ipupa akitbuiza mbele ya mashabiki wake ambao kila mara walionekana kuvutiwa nae hasa akina dada/mama


Washabiki walipagawa mara walimuona Fally Ipupa jukwaani



Skwadi zima la mwanamuziki nyota katika kizazi kipya cha muziki wa dansi kutoka Kongo,Fally Ipupa likiwa jukwaani


Kuonesha kuwa bado yuko fiti,aliamua kudhihirisha wazi mbele ya washabiki na wapenzi wake kama hivi pichani kuwa bado wamo ile mbaya




Wageni waalikwa waliofika kwenye pati hiyo ya funga mwaka iliondaliwa na kampuni ya sigara ya TCC kwa ajili ya wateja wake wakilifuatilia kwa makini onesho la Mbilia Bel


Mbilia Bel akiimba taratiibu



Mwanamuziki mahiri katika miondoko ya rhumba Mbilia Bel usiku wa kumkia leo aliwakumbusha wengi hasa wakati ule alipokuwa anawika na vibao kadhaa ambavyo pia aliviimba usiku wa jana kwenye pati ya funga mwaka iliondaliwa na kampuni ya sigara ya TCC iliofanyika nje ya uwanja wa New World Cinema na watu kufurika kwa ajili ya kuwashuhudia wanamuziki hao kutoka kongo.Pichani kulia ni Mbilia Bel akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mpaka chini na nyuma ni densa wake akimpa tafu.Kwa picha zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Cheki midume ilivyo jaa mbele kwenye show ya Felly , baada ya kuachia mademu wakae mbele yenyewe imejaa na kushangilia hata aibu haioni.
    Kuna kisa kimoja kilitokea India, kuna group la BoyZone ,lilienda kufanya show, sasa Europe na USA kwa kawaida wananaume wana po ku a jukwaani ,screeming fans wanakua mademu mbele kibao, ila ajabu mbele kulikuwa kumejaa wavulana kibao waki scream at the top of their lungs , jamaa walibaki midomo wazi kwa mshangao.

    ReplyDelete
  2. Oooo nakumiss Maghambo le Presidaa mwana wa Fally!!!

    ReplyDelete
  3. Oyaa wewe anon hapo juu acha hizo, hao waimbaji na wachezaji wenyewe ni kama mademu, of course vitu kama mikorogo na blonde hair etc kama kawa sasa unataka jamaa wafanyeje?

    Jamaaa [wapiganaji] labda nao wanatafuta mdemu? au labda mademu kwa mademu wanatafutana?

    Michuzi tafadhari fikisha huu ujumbe acha ubaguzi!

    ReplyDelete
  4. mbili ya beli wamo sanaaa tu.. ndio bibi kidude wa congo huyo.. wanavuma na wamo... lol .. amenivunja mbavu sana na hiyo poziyake kama anataka kuruka.. hahaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...