NDUGU ISSA MICHUZI,
HAKIKA CHANNEL TEN TV TUNAIPATA HADI HAPA OMAN NA DUBAI PIA NAIMANI SEHEMU NYINGI KAMA SIKESEI MAANA IMO KWENYE SETALLITE.
TATIZO KITU CHA KUSIKITISHA 99% INAONYESHA MAMBO YA TV ZA EUROPE NA CNN BADAL A YA KUONYESHA VITU VYA KUVUTIA KAMA VILE MIJI, MBUGA ZA WANYAMA, MAZIWA, MICHEZO YA KUIGIZA NA KADHALIKA HII ITAISAIDIA SANA TANZANIA KUJULIKANA DUNIANI.
MAANA KWA SASA UKWELI HATA KUANGALIA UNAONA TATIZO. SUDAN SOUTH WAMEANZISHA CHANNEL MPYA AMBAYO INAONYESHA MAMBO NILIYOONYESHA HAKIKA HADI RAHA UNAPOANGALIA.
SHUKRANI
MOHAMMED

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. MOhd...tatizo la stesheni zetu kuonyesha vipindi vingi vya nje cyo chanel 10 cyo tu hata stesheni yetu ya taifa ndo ivyoivyo.

    ReplyDelete
  2. watu wapo kibiashara zaidi sio kurusha tu matangazo unayotaka sababu mwangaliaji sio wewe peke yako hawa wanalenga soko la dunia nzima,Pia mambo ya kuonesha maigizo NANI kwa lugha ya kiswahili huko dubai watelewa kiswahili.Matangazo ya Mbuga serikali yako ishatoa Bil 3.1 kwa CNN kutangaza,Channel 10 haiwezi kutangaza bure wakitoa pesa utayaona,La msingi zaidi Channel 10,CTN,DTV,Magic FM zote zinamilikiwa na mtu mmoja na Si Mtanzania kwa hiyo usitegemee vitu kama hivyo,najua unatamani sana progam za kiswahili lakini ndiyo haiwezekani.

    ReplyDelete
  3. labda tuanzishe channel inayoonyesha,ufisadi,maradhi,ujinga,ujambazi,rushwa,barabara mbovu,kukosekana kwa umeme,kukosekana kwa maji safi,polusheni ya magari mabovu,mauaji ya waalbino,utajiri wa wachache n.k.
    Na jina la channel labda iwe...Tanzania my beloved hell!!!

    ReplyDelete
  4. Mwenyekiti tunaomba matokeo ya Tusker.

    ReplyDelete
  5. UJUMBE HUO NI MUHIMU SANA,KWANI HATA PICHA NYINGI ZILIZOCHUKULIWA KTK MBUGA ZA TZ HAZINA ALAMA YOYOTE YA KYTANGAZA TZ,UTZSIKIA TU SERENGETI,NGORONGORO,LAKINI SIO JINA TZ.
    MDAU PIA TUAMBIANE ,MNAPATAJE CHANEL TEN KTK INTERNET?

    ReplyDelete
  6. Naunga mkono na mguu.

    ReplyDelete
  7. we Mud channel ten ni TV binafsi so wao ni biashara tu, hayo mambo ta kutangaza nchi ni kazi ya TVT inayotumia pesa za walipa kodi hawa jamaa wanafanya hivyo kwa sababu kuandaa vipindi ni gharama ndo maana wanaonyesha hizo CNN na zingenezo kwa kuwa ni bure, hiyo inawafanya kuwa hewani all time for cheap na wakaweka matongazo yao ya biashara kiana.

    ReplyDelete
  8. sikubalilani na mdau wa pili hapo juu. dunia nzima kuna televisheni kibao zinazoonyesha mambo hayo hayo mfano cnn au bbc. siamini kama wana watazamaji nje zaidi ya ndani ambao cnn au bbc ndo option kwani haipo available. nje wanazo cnn na bbc eljazeera n.k

    tatizo nadhani ni ubumifu mdogo.

    ReplyDelete
  9. siyo lazima yawe mambo ya mbuga za wanyama lakini originality. sijui kama hao walengwa wana haja sana na cnn kwani huko nje zipo kwa wingi. kama walengwa ni ndani ambao hawana uwezo wa kuziona cnn isipokuwa kwa channel 10 hakuna haja ya kubroadcast kupitia mitandao n.k

    mdau tujuze jinsi ya kuiona basi hiyo c.10

    ReplyDelete
  10. hii ndiyo sababu iliyinifanya niache kuangalia star tv, nilikuwa nalipa dollar zangu alafu kuangalia utumbo, nikajifutilia mbali. kila siku walikuwa wakitangaza next week igizo fulani linaanza hiyo next week haikufikaga. siyo vizuri mbasdilike

    ReplyDelete
  11. naendelea kidogo we ndugu unayetaka kupata chanel ten kwenye intanet ingia www.jumptv.com hapo utapata kila aina ya tv. huko ndo nilkokuwa nimeipata star tv na ndiyo chanel ya kwanza ya kibongo kurushwa nao. lakini waliitoa naona wateja walikosa, nilikuwa nalipia miezi mitatu nasubili hayo maigizo weeeeeee lakini wapi, tabu tupu.

    sicenga

    ReplyDelete
  12. wadau jamani imekuwa Ugomvi,si mueleweshane mdogomdogo??
    wabongo bwana,badala ya kujenga sie tunabomoa!!!
    haisaidiii!!!

    ReplyDelete
  13. ulieoomba ushauri usijiumize kichwa bure nchi yetu tayari inajulikana duniani kote imejipatia umaarufu wa gafla kabisa kwa mauaji ya albino, hayo mengine hayana umuhim tena nchi yetu tayari ni celebrettttiiiiiii wa dunia au sio wadau

    ReplyDelete
  14. Ni kweli channel Ten msipuuze maoni ya mtazamaji wa Omani.

    Jiulizeni Al-Jaazeera wangekubali kuwa hawana ubavu wa kushindana na BBCworld service au CNN int'l leo wangekuwa wapi? Au hata nyumbani TZ,iliiwezekana vipi Radio One na ITV kufikia kuwa vyombo vya 'TAIFA' kabla ya TBC na Televisheni ya Taifa.

    Suala hapa ni kuwa na mawazo ya kiubunifu, na serikali au makampuni binafsi au ya kitaifa yataweka matangazo ktk Channel Ten kuhusu sekta za madini, utalii, kilimo n.k ili wawekezaji wenye mitaji Arabuni wawekeze na kuitembelea Tanzania.

    Kwa somo fupi tembelea www.youtube.com na muangalie Nyerere speech 3 na speech 4 ili uongozi wa Channel Ten au Air Tanzania n.k kupata somo fupi la mawazo endelevu.
    Mdau
    Rocky
    London.

    ReplyDelete
  15. ZIDUMU FIKRA ZA MWALIMU NYERERE??? ZIDUMU NDO MAANA HAKUTAKAGA TUWE NA TV JUU WATZ TUNGEJAZWA UTUMBO PROPAGANDA ZA WESTERN KAMA TUNAYO YAONA SASA.

    ReplyDelete
  16. Nyie wa wapi jamani,sio TVT ni TBC

    ReplyDelete
  17. Wakati mwingine sio kuwa wanapenda kurusha vipindi vya nje bali wanalipa kodi. Kwa mfano TBC1 sio kwamba wanapenda kurusha mambo ya uchina bali ni moja ya makubaliano baada ya kutembeza bakuli.

    Hata hivyo kuna haja kwa vituo vyetu na vyombo vya habari kutangaza TANZANIA kwa mitindo tofauti. Kwa mdau aliyeongea juu ya mbuga n.k kuwa hazitangazi TANZANIA, naungana nae, na nadhani tatizo liko kwenye idara ya masoko. Many adverts are too myopic!

    ReplyDelete
  18. Mohamed ametoa pendekezo lenye akili, lakini wabongo kwa uvivu wa kufikiri wanakurukupuka kupinga tuu. Hivi nani anadhani Channel 10, au TBC wanapata mapato yoyote kwa kurusha vipindi vya nje nani? Na mtu gani wa nje atakwenda kutazama CNN, BBC au matangazo mengine kupitia Channel 10? Kwa nini wasiangalie moja-kwa moja tena in HD?

    Vituo vya ndani na hata watanzania wote, tunatakiwa tuwe wabunifu,maoni ya Mohd kwa mfano yatafanya wapate watu wa nje kweli, maana watakuwa nawaonesha kitu unique!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...