Hii ni safu iliyoka Majira Jumapili iliyopitaNovemba 30, 2008.
Desemba 14 itatoka nyingine.
Tathmini Kutoka Washington,
Na Mobhare Matinyi
Ardhi ya Tanzania ni ya Watanzania tu!

HIVI karibuni jirani zetu hasa Wakenya, wamekuwa wakipiga kelele kulalamikia serikali yetu tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hasa hii ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba inazorotesha juhudi za kurahisisha nyendo za watu, ukazi wa kudumu na umilikaji ardhi Afrika Mashariki.

Kelele za majirani zimeongezeka katika siku za karibuni baada ya mjadala wa soko la pamoja kushika kasi. Kikao cha juzi juzi kisiwani Zanzibar kimeendeleza zogo hili. Hiki kilikuwa kimoja ya vikao vingi vya mchakatao huu ambao unafafa na ujambazi wa mchana kweupe.

Kama ilivyo kawaida kwa wenzetu Wakenya, kuropoka maneno makali hadharani kwao ni jadi, hata pale wasipokuwa na hoja.

Waziri wa Kenya aliyehudhuduria kikao cha Zanzibar, Jeffah Kingi, aliporejea kwao Nairobi alitoa tamko la kulalamikia hicho wanachokiita “ukwamishaji” wa Tanzania katika kufikia soko la pamoja na baadaye taifa moja.

Mara zote walalamishi hawa huwa hawaelezi kwa nini Tanzania inakwamisha, wao huwa ni kulalamika tu. Hivi nani aliwaambia kuwa ni lazima ardhi yetu igawanywe kwao? Wao ya kwao iko wapi? Watatupa nini cha mbadala? Kama haiwatoshi wasitupe shida, wajibane hivyi hivyo.
Waziri huyu wa Kenya hakuwa wa kwanza na wala si Kenya pekee, hivi sasa Rwanda na Burundi zimejiunga katika ulalamishi huo. Aidha, katika kikao kingine cha hivi karibuni kilichofanyika nje ya Tanzania, ilifikia mahali eti Rwanda na Burundi zinajadili misamiati ya kutumia kwenye kuhalalisha umilikaji ardhi.

Labda niulize swali: Kati ya Rwanda na Burundi, kuna anayetegemea kuwa watu wake watakwenda kwenye nchi nyingine kumiliki ardhi? Hivi Ututsi na Uhutu utakuwa umekwisha lini? Kujazana kwa watu Burundi na Rwanda kutaruhusu vipi umilikaji ardhi kwa watu wasiokuwa wazawa?

Jibu ni rahisi sana: Wanachotaka ni kuhamishia mamilioni ya watu kwenye ardhi ya Tanzania. Basi! Haiwezekani Mnyarwanda akahamia Burundi au Mrundi akahamia Rwanda, tusidanganyane mchana kweupe!

Uganda ingawa haijaanza kulalamika sana, lakini Rais wake, Yoweri Museveni alishawahi kusema maneno fulani na kisha kuyakimbia mwenyewe. Bahati nzuri kwa Uganda, ni nchi ya wanyonge wanaokimbizwa na Museveni mwenye ajenda za kisiasa na kiutawala huku vita vikimuandama.

Hata hivyo, Waganda nao wameanza kushituka na kujiuliza hivi wanataka nini kwenye hii Jumuiya ambayo Wakenya wako mstari wa mbele kuitaka iwe Shirikisho ghafla. Mwezi uliopita wakati akizungumza kwenye semina ya Taasisi ya Wahasibu Uganda (ICPAU), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wauzaji Bidhaa Nje cha Uganda, George Walusimbi, alionya kwamba Waganda wawe waangalifu na hili wazo la soko la pamoja la Afrika Mashariki.

Tatizo la Walusimbi pengine lilikuwa kuitilia mashaka sekta binafsi ya Tanzania, na kutolea mfano wa makao makuu kuwekwa Arusha. Sikumuelewa. Nadhani ingawa alijitahidi kuwaonya Waganda lakini alipotea kwenye kutoa sababu. Hata hivyo inaonesha kwamba Waganda wanaanza kujihoji.

Hivi karibuni wakati wa kikao kilichofanyika Kampala, Mkurugenzi mmoja kwenye Wizara inayoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki ya Uganda, Edith Katende, alisema: “Kwetu sisi, Waganda, Wanyarwanda na Warundi, tunachotaka ni kuwa na urahisi wa kuzifikia bandari ili watu wafanye biashara kirahisi, wapate fedha.” Haya ni maneno ya ubinafsi wa waziwazi.

Ofisa mwingine wa Kenya, Barrack Ndengwa, alisema kwamba kufikia mwaka 2010 lazima soko la pamoja lililo huru liwe limesimikwa Afrika Mashariki huku waziri wa Uganda, Gaggawala Wambuzi, akisema mwaka 2009 tu mambo yatakamilika.
Naye Naibu Waziri wa Burundi akiwa Kampala pia, Nduwimana Deogratius, alisema kuhusu soko hili: “Mambo yanakwenda vizuri.”

Wakati viongozi wa Uganda, Rwanda na Burundi wakiendelea kutoa matamko yenye matumaini kwao na hata ya kulazimisha, Wakenya wao wanaendelea na lugha yao ile ile ya kijeuri. Lugha chafu, ujeuri na kiburi ni ugonjwa kwa wenzetu hawa. Hivi nani asiyejua kuwa tatizo kubwa la Kenya ni ardhi?

Lakini turejee kwenye mada, hivi kuna sababu gani ya Wakenya kutulaumu hivi? Kwani ni lazima tuungane? Hebu tujikumbushe kidogo. Miaka ya 1960 wakati Waafrika tukipigania uhuru, Mwalimu Julius Nyerere aliwaambia Wakenya na Waganda kwamba ataichelewesha Tanganyika kupata uhuru hadi wao watakapokuwa tayari, kisha tuungane na kuwa nchi moja.
Nadhani ambao hata hatukuwepo tunajua majibu yalikuwaje. Mwaka 1967 Nyerere tena akawaweka pamoja wenzetu hawa na ikaundwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Miaka kumi baadaye Uganda ikiwa na mwendawazimu Idi Amin na Kenya ikiwa na Mzee Jomo Kenyatta, wakaivunja Jumuiya. Mabwana wakubwa hawa hawakujali umoja.

Jumuiya ilipovunjika mwaka 1977, Wakenya walisherehekea kwa mvinyo na Waganda hawakujua kinatokea nini kwani Dikteta Amin alikuwa anawamaliza kwa risasi. Chuki na dharau ya Wakenya kwa Tanzania ikafikia kilele, wakatucheka sana na Ujamaa wetu na wakajivuna na viwanda vyao wa Wazungu na Wahindi. Safi!

Kwenye miaka hiyo pia, Tanzania tulikuwa tukitumia kila senti yetu, ardhi na damu yetu kuwapigania wenzetu wa kusini mwa Afrika ili wapate uhuru. Tanzania ilikuwa makao ya kila wapigania uhuru, achilia mbali Kamati ya Ukombozi wa Afrika. Wakenya wajipendekeza kwa makaburu na nchi za magharibi, wakadharau harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Hawakujali umoja.

Wakati Watanzania tunajenga Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, Wakenya walikuwa wanajenga ukabila. Leo hii ni wavunaji wazuri wa ukabila. Mabwana wakubwa hawa. Nasikia wanatuonea wivu sana, na hata Rais wao wa zamani, Daniel Arap Moi alikuwa akiwasihi waige Tanzania. Safi sana!

Hata hivyo baada ya kuvunjikia kwa Jumuiya mwaka 1977, Watanzania hatukujali sana pamoja na hasara kubwa tuliyopata ilihali wenzetu Wakenya wakifaidika. Marehemu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Sokoine, alianzisha mkakati wa uhusiano na Kenya.

Mzee Ali Hassan Mwinyi alipokuwa Rais aliwakalisha Moi na Museveni na kuzungumzia mali na madeni. Hatimaye wazo la Jumuiya likarejea tena. Mambo yakaanza vema lakini kumbe wenzetu walibaini mwanya ambao sasa unaonekana wazi.

Wakati wa Rais Benjamin Mkapa wazo la Jumuiya lilizaa Shirikisho na sasa umekuwa mzigo. Kimsingi, nionavyo mimi, hii mijadala inayoendelea ni unyang’anyi. Inasikitisha sana kwamba Watanzania tumefikishwa hapa huku tukitukanwa. Hivi tangu lini Wakenya wakajua umoja kuliko sisi? Hii hata mtoto mdogo hadanganywi.

Mambo kama kuruhusu eti mtalii akija Afrika Mashariki atumie viza ya nchi moja kuzunguka kwenye nchi zote, ni wizi wa mchana. Tanzania hivi sasa tunajenga utalii wetu kwa nguvu, na serikali inatumia mamilioni ya dola kuitangaza nchi. Inawezekanaje mwisho wa siku tuchangie faida ya watalii.

Upo ukweli kwamba Kenya ilijitangaza zaidi kuliko sisi huko nyuma, ikiwa ni pamoja na kutumia Mlima Kilimanjaro, na imejenga miundo mbinu bora ya utalii. Kwa mazoea tu, watalii wote watakuwa wakifikia Kenya, na kuingia Tanzania bila kulipa viza kwetu. Tatizo la ulaghai lililokithiri Kenya kwa watalii tunalijua; hivi tuna sababu gani ya kuongeza shida hii ya viza? Hii ni dhambi.
Wakati mwingine huwa najiuliza, hivi kama si busara na ushujaa wa Rais Kikwete hivi karibuni kukataa maoni bandia yaliyowasilishwa na Tume ya Amos Wako, Mwanasheria Mkuu wa Kenya, tungekuwa wapi? Akina Wako walidai eti watu wa Afrika Mashariki wanataka shirikisho haraka.
Itakumbukwa kuwa Rais Kikwete baada ya kukataa ujanja ujanja huu, aliunda Tumeya Rais iliyoongozwa na Profesa Samuel Wangwe. Tume hii ilizunguka nchi nzima na asilimia 76 ya Watanzania wakasema hawataki kusikia Shirikisho mpaka hapo baadaye.

Nchi yetu siku hiyo ilikombolewa na kama kuna sifa anazostahili Rais Kikwete, basi ni hii ya kuiokoa Tanzania. Watanzania tuna tatizo la viongozi wetu kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu wengine wa nje, lakini hapa tuliamka.

Na huu ni mfano mmojawapo unaoonesha kwamba tunahitaji mfumo wa kuangalia maamuzi yanayofanywa na kila upande kabla ya utekelezaji, yaani urari wa madaraka. Hebu fikiria kama tungekuwa na Rais asiye makini katika kulinda maslahi ya nchi, kingetokea nini?

Kimsingi Tanzania imepona kwa huruma ya Rais Kikwete, hebu fikiria kama angekubali mawazo ya akina Wako? Leo hii Watanzania tungekuwa tunapelekwa machinjioni. Na kama kuna mtu mwingine anayestahili sifa ni Waziri wa Afrika Mashariki, Dkt. Diodorus Kamala, na Naibu wake, Mohamed Aboud. Hawa watu wanastahili sifa kwa kuitetea Tanzania.

Naomba mniwe radhi wasomaji, najisikia kuwasifu mno viongozi hawa kwa sababu Watanzania tumezoea kuumizwa na viongozi wasiofanya maamuzi kwa maslahi yetu. Mifano ya mashirika ya umma yaliyouzwa, migodi yetu inayochimbwa na masuala ya umeme na gesi inajulikana na kila Mtanzania. Kwa taarifa tu, tunachekwa duniani kwa haya mambo!

Inapotokea viongozi wakafanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa ni lazima tuwapongeze kwa vyovyote vile. Narejea tena pongezi zangu kwa serikali ya awamu ya nne, na kama tungekuwa hivi siku zote, mali zetu zisingepotea kijinga kama inavyotokea sasa.

Kutokana na mjadala huu kuwa nyeti, natarajia kupiga kambi kwenye suala hili kwa takriban mwezi mzima hivi. Wiki ijayo nitapekua zaidi sababu zinazowafanya majirani zetu watung’ang’anie.

Barua pepe:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Mkuu hapa nimekupata vilivyo, hawa jamaa zetu naona wanataka kutudharau na kuona hatujui na nchi ambayo haina wachambuzi wa mambo. Umenipatia Morari wa kupekua nami niwatungue ili wapunguze kidomodomo. Hapa ni lazima tusimamie ukweli hatutaki dhuluma iliyozoeleka,ilikwishatendeka na sasa muda umekwisha.
    Michuzi midahalo kama hii ukiisikia na kuiona tuletee wadau tupo tayari kukuunga kwa kutoa michango yetu kwa dhati kabisa.

    ReplyDelete
  2. Wananchi wenzangu, bila shaka tumeshaona wale wote wanaotaka umoja huo kwa haraka ili tu wapate faid bila kuangalia madhara yake.
    Kwa undani zaidi,tunaona kuwa hapa Tanzania ndiyo itapoteza zaidi kuliko kupata. Kama wama tumeshawafanyia sana hawa watu,na wala hutukusubiri kupewa shukurani. Viongozi wetu waangalie hayo yote kwa makini kama hawajatuingiza huko. Wala wasiwe watu wa kujali tu umaarufu wao wa kisiasa badala ya kuweka nchi mbele.
    Watanzania tutakuwa sawa kabisa bila hiyo jumuiya. Kati ya nchi zote hizo,hakuna ambayao ipo imara kisiasa kama sisi,ingawa tuna matatizo yetu.
    Wakenya wanaweza kujisifia kuwa wako mbele kiuchumi. Wasije wakajidanganya, kama kisiasa hawako imara,ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga ufukweni mwa bahari.Nadhani hilo wanalijua vizuri sana kutokana na uchaguzi wao mkuu uliopita. Uchumi wao ulisaidia nini wakati wakiuana kama nyani ? Au ndiyo uliwasaidia wamalizane zaidi ? Si viongozi wao ndiyo walisema wanataka kuja TZ kujifunza jinsi ya kuishi kwa ustaarabu ? Uimara wetu kisiasa hatujapewa na Mungu kama zawadi.Tumejitolea sana ili kufikia hapa, na hata ndugu zetu wengine wamepoteza maisha yao sababu ya hali hiyo. Leo hii hawa wehu wanataka kutuvuruga, not on our watch !!
    Tuna kila sababu ya kuchambua kila kitu kabla hatujachukua uamuzi wowote.Kama lengo lao ni kuungana mbona wasiungane na wasomali na wasudani ?
    Hayo ni maoni yangu binafsi .

    ReplyDelete
  3. Ni jambo la kumshukuru Muumba wetu kwamba hili suala limekua heated up sasa baada ya Our former BELOVED Prez,Ben(Tanzania is for sale)Mkapa!The guy wd have no problem signing us in! Baadae ingesikika tungejaribu kulalamika angetupa speech moja kali na chafu sana, (si tunamjua asivo jeuri)na tunge shut the hell up, as always!(maskini siye,,,)Tungeambiwa this is 4 our own benefit na matunda yake tuta yaona baadae na tutamshukuru!(as wv always bn told in such circumstances!)
    Therefore kujua kwamba JK alipause kwanza na kuamua kuuliza wananchi kuhusu hii sensitive issue, I have a whole new respect for my President Kikwete. Najua he is not perfect i havent always supported him, but im giving credit where credit is due, alicheza hapa kama Pele.
    Yani ajabu kwamba sie ambao sheria zetu za ardhi ziko perfect na tuko poa nazo ndo tunashinikizwa kuzibadili na watu ambao hawana hata land kwa watu wao?! Puleeease!
    Kenya,CRY ME A FREAKING RIVER!
    Upole si ujinga, just bcze sie wapole don mistake that for ujinga!
    grace.

    ReplyDelete
  4. Mwandishi shukrani kwa kuweza kuwaelimisha watu nini kiko mbele yetu kuhusiana na suala hili,ni kweli the same muungano wanaoouongelea ni ule ele uliovunjwa 1977 TZ hatukuambulia kitu wanasema mtu alieumwa na nyoka hata ujani ukitisika anapapalika ndivyo TZ sasa nchi imejijenga kwa jasho la watu wake na bado inazidi kukua tutayamuda wenyewe kwani macho yetu yamefunguka

    ReplyDelete
  5. Wakenya wanajifanya kusema kwamba muungao uendelee bila Tanzania... kwakwakwakwakwa, hehehe, teh teh teh, sina mbavu, mnakumbuka ile movie ya Will Smith, sijui ni Enemy of the state? yule babu wa kizungu anamwambia Will,"Son, you got what they want", something like that. Hakuna hiyo muungano hapa bila Tanzania, cause we got what they want,(more vicheko). Kama Tz ikishajitoa sijui kimaandishi officialy, then tutaona kama wataungana! hii kitu yote ni geresha tu ishu ni moja tu, Ardhi yetu.Plse jitoe tuendelee na maisha bila bugudha na nakuhakikishieni mtasikia hii ishu imedisapia.

    ReplyDelete
  6. Hili liwe fundisho kwetu wabongo now that we know our neba to the north and north west wanakodolea macho ardhi yetu!
    Tungepitisha sheria kabisa zenye kulinda ardhi yetu kwenye katiba yetu kabisaa. Kwa sababu hawa watu hawataacha, wataendelea kutumia ujanjaujanja wee, all it takes is a few greedy politicians and this thing can be signed whether we like it or not!Au tuandike sheria ambazo zinaweza ku overturn ikitokea wanasiasa wetu mafisadi wanatusainisha kwenye ujinga kwa faida zao binafsi.Tunashukuru viongozi Kiongozi wetu wameweza kuliona hili, lakini kuna awamu zijazo, tena wakati huo wenzetu tatizo lao la ardhi litakua limefikia pabaya hasa, natabiri watakatana mapanga tena, hivo ikitokea tuna viongozi mafisadi we should be able to turn into our constitution and rescue ourselves and our number one asset, udongo wetu.
    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  7. Kabla ya kujiunga kwanza waTanzania wote watafakari ni nini maana ya huu muungano mpya na utakuwa wa aina gani na tutapata faida gani na pengine kama kuna hasara je hizo hasara ukilinganisha na faida kipi ni kingi kuliko kingine. Kwa kuanzia tu inatubidi turejee kwenye muungano wa zamani, EAC, EAST AFRICA COMMUNITY, watu wafanye reference huko, kwa wengi walio na umri wa chini ya miaka 30 hawajuwi huu muungano ulikuwaje na kwa nini ulikufa, so lazima tuelezwe wazi kwa nini ulikufa, na kwa sababu hizo hizo huu wa sasa hauwqezi ukafa tena?. Kwa kifupi tu ulikuwa muungano wa kiuchumi kati ya nchi hizi tatu, KENYA, UGANDA na TANZANIA, Kenya ikiwa makao makuu karibu ya mbao yote, hata hayo maendeleo mengine waliyofikia ni kwa sababu ya muungano huo na wala si juhudi za Kenya pekee, kwa mfano uwanja wao wa ndege, bandari ya Mombasa,baadhi ya Barabara za lami, na majumba makubwa yalikuwa ya EAC na hata profit kubwa ya EAC ilikuwa inatumika sana Kenya kuliko nchi zingine, hayo yote ni matunda ya EAC. Wakenya wadai wao wameendelea na uchumi wao ni mkubwa kuliko sisi wengine, ukweli ni kwamba vitega uchumi karibu vyote vya Kenya ni vya watu wa nchi za nje, hata hizo mbuga za wanyame zote ni za waingereza, mashamba makubwa yote ni ya waingereza, viwanda ni vya waingereza, wanachofaidika wao ni ajira tu na si vinginevyo. Kwa nini huu muungano uwe hadi kwa ardhi, hii ni hatari kwani tukianza kunyang'anyana ardhi ni mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe(civil wars). Wakenya wanataka muungano kwa ajili ya ardhi,ajira na opportunity zingine ambazo ni rahisi kupata Tanzania na si KENYA, hawa watu ni wabinafsi na wachoyo, wamekuwa wakija huku kwetu kwa wingi katika miaka hii ya karibuni kwa sana tu kwa ajira ambazo wala si za kiufundi na kielimu kama wanavyodai, kuna madereva, ma-house girls, shamba boys, shop assistants, makarani wa benki na kazi nyingi za ovyoovyo ndogo ndogo tu hapa nchini zinafanywa na wakenya, lakini kazi hizo hizo mtanzania ukienda Kenya hutaajiriwa na ni vigumu kwa mtanzania kupata ajira ya aina yoyote Kenya kwa kisingizio cha English , sasa huu ni muungano gani? wa upande mmoja tu! sana sana watakuambia watanzania hawajuwi English, jamani kuwa house girl unahitaji english, mbona hata huko Kenya asilimia kubwa ya watu pia hawajuwi english, ni lugha inayotumika maofisini tu kama ilvyo Tanzania, wengi wa watu ama wanaongea kiswahili au lugha zao za jadi, cha msingi kabisa ni kwamba kabla ya yote ni lazima watu tuwe wakweli na wawazi, tuondewe tofauti zetu za nyuma na tuanzie hapo kujenga huu muungano mpya wanaoutaka, pia swala la EAC litazamwe upya na mahesabu yafanye kila nchi ipate chake kulingana na mahesabu ndipo tuannze mazungumzo mapya, kwa hali ilivyo hadi sasa Kenya ndio walichukua mali kubwa kuliko nchi zingine, hivyo ni lazima tugawane sawa na tuanza sote toka zero pamoja. KWA KIFUPI HATUHITAJI HUU MUUNGANO, WAENDELEE NA MUUNGANO WAO NA WAJENGE UCHUMI WAO, SASA TU WAMESHAANZA KUTOZA WANAFUNZI WA NJE YA KENYA HATA KAMA UNATOKA TANZANIA FEES KUBWA WANAYOITA INTERNATIONAL STUDENT FEES FROM PRIMARY SCHOOL TO UNIVERSITY WAKATI WAO WAKISOMA TANZANIA WANALIPA KAMA WATANZANIA WENGINE WANAVYOLIPA, KWELI HUU NDO MUUNGANO TUNAOTAKA? TUACHE UBINAFSI SISI NI NDUGU MOJA. TUWE WAKWELI WA NFSI ZETU. MICHUZI HUU MJADALA MPELEKE KIWETE NAJUWA WEWE NI SWAHIBA WAKO UNAWEZA HATA KUPELEKE MWENYEWE OFISINI KWAKE.

    ReplyDelete
  8. KULE RWANDA, BURUNDI NA UGANDA, KENYA KUNAWALE JAMMAA WALIOPIGANA VITA NA KUWAWEKA MADARAKANI VIONGOZI WA SASA, HAO JAMAA HAWANA PA KWENDA NA WANAOGOPWA KWA UCHINJAJI WAO KAKA. GESS WHATTTT !!! TUSILOGWE AFADHALI KUHUDUMIA WAKIMBIZI.....TUKIJIUNGA SISI TUTAKUWA WAKIMBIZI WA NANI ???

    ReplyDelete
  9. Poa Matinyi, ninyi waandishi washambulieni Wakenya hao. Wamejifanya kutaka kutuibia nchi yetu, inabidi tujitutumue.

    ReplyDelete
  10. Article nzuri nainaonyesha Watanzania tuko macho na hatuko tayari/hatutaki hio shirikisho.

    Lakini, siku zote nina wasiwasi na waandishi wanaomsifia rais wete na mawaziri wake. Hujakaa sawa unasikia mtu kwa mbunge wa kiti maalum, mkuu wa wilaya au waziri!

    Ukweli ni kwamba Kikwete alilazimishwa na wananchi na wasomi waliodai kupewa nafasi ya kutoa maoni yao baada ya kuona tayari JK na wenziwe wanaelekea kwenye shirikisho. Naamini hata JK alitumaini mwenyekiti wa tume yake ya kutafuta maoni ya wananchi angetoa taarifa ya kukidhi nia yake na marafiki zake. Ukikumbuka majibu ya maoni ya wananchi yalivyotolea na mwenyekiti wa tume ilionekana wazi aliyatoa katika mazingira yanayoonyesha kuna hali yeye amekuwa 'shujaa' wa kutoa report isiyomfurahisha rais. Kwa ufupi wananchi wa Tanzania ndio tuliokataa na sio rais.
    Ukitaka ujue JK hana ushujaa au uzalendo wowote angalia issue za EPA, Kagoda,Richmond, Bunzwagi etc. Bado unaamini JK ni safi w chini yake (aliowateua yeye)ndio wana matatizo?

    NO EAC! No JK! NO CCM! Let's take our country back!

    ReplyDelete
  11. Angekuwa Mkapa hii tungepigwa bao! Hivi kwanza tulifikaje hapo?

    Mobhare mwambie Michuzi aiweke nyingine hapo ikitoka tu.

    ReplyDelete
  12. wakenya wanataka mlima kilimanjaro, tanzanite na mbuga za wanyama za serengeti, manyara, na ngorongoro.......hivi hamjawastukia tu!Wakishindwa wataanzisha vita kama Amini.
    Si umesikia shehena ya masilaha kutoka ukrania iliotekwa na majangiri baharini wakati inaelekea Kenya! Kaa chonjo bajameni

    ReplyDelete
  13. Woa, mchangiaji hapo juu umenitisha kuhusu yale machinjachinja ambayo hayana pa kwenda! Mungu tuepushe. Nasikia wako kwenye mapori ya CONGO.Kwa hiyo Kagame anasubiri bongo tujiunge aje ayabwage machinjachinja Kigoma, na kusema Finally i got rid of them! Uuuuwiiiii, mwili unanisisimka!

    ReplyDelete
  14. MIMI NI MTANZANIA NAISHI HAPA UGANDA NAUNGANA NA WATANZANIA WANAOCHANGIA KUWA HILI SHIRIKISHO HALINA MANUFAA KWA TANZANIA YA SASA UGANDA HAINA ARDHI NA HAPA KUNA UGOMVI MKUBWA SANA WA ARDHI HUWEZI KUSAFIRI DAKIKA 10 BILA KUONA KIJIJI UKABILA UNATISHA NI NCHI YENYE UKOSEFU MKUBWA WA AJIRA,SASA NAKUBALIANA NA MCHANGIAJI MMOJA MKAPA ALIKUWA ANATUBURUA KWENYE HILI,MUNGU WABARIKI WATANZANIA HATUTAKI HILI SHIRIKISHO KWA NINI TUSIBAKI MAJIRANI WEMA TU,TANZANIA NI MWANACHAMA WA SADC NINA UHAKIKA IKIPIGWA KURA MAONI YA WATANZANIA WOTE NAKUHAKIKISHIA 80%-90% HAWATAKUBALI WATAKATAA,TANZANIA INAKWENDA SASA JUU WAACHE WAUNGANE WENYEWE,BADO TUNA MATATIZO YA MUUNGANO WETU NA ZANZIBAR .SASA TUNAINGIZWA KWENYE MATATIZO MENGINE KENYA WAACHENI WAUNGANE NA WASOMALI KWANI LAZIMA SISI,VIONGOZI WATANZANIA WATU WA AJABU SANA KUIINGIZA NCHI KWENYE MIKATABA YA AJABU AJABU HATA HUWEZI KUAMINI TUAMKE SASA NCHI INAKWENDA AGENDA YA HAWA JAMAA NI ARDHI YA TANZANIA NDIYO MAZUNGUMZO YALIYOPO HAPA KAMPALA,NAOMBA MICHUZI HIZI ARTICLES WAANDISHI WAMAGAZETI WAZIANDIKE NASISI TUTAJITAHIDI KUPOST KILA WANCHOTUSEMA WAPO VIBAYA SANA JUU YETU TUKATAE MSIMAMO NI HUO HUO
    ASANTE.....ismakabengo@yahoo.com

    ReplyDelete
  15. Du mkuu hapo kweli umenifumbua macho kwani hata mimi sikuwa nikifikiria sana kuhusu side effects za huo muungano, especially suala la Ardhi. Kwa kweli umesaidia kufumbua macho ya Wazalendo wengi wa kitanzania ambao walikuwa hawajui tunakoelekea. Basi mimi nakupa support katika hilo kwani unajitahidi sana kuelimisha jamii kama Mwanahabari.

    ReplyDelete
  16. naona wanatuuzia chai tu hakuna haja ya kuharakisha.WIZI MTUPUUU....Enzi za Mwaaalim walikuwa hawana ubavu wa kutuharakisha hivyo

    ReplyDelete
  17. Fungua Macho,

    Sikiliza, mimi ndugu yangu yumo kwenye timu ya Tanzania. Kila hatua ya kuundwa Shirikisho inajadiliwa na viongozi wakuu wa nchi, kisha inakwenda kwa wataalam na halafu wanasaini mkataba (protocol). Watanzania hakuna aliyekuwa anajua kuwa Tume ya Wako ilisema kila kitu tayari. Ni Kikwete ndiye aliyekataa. Baada ya kukataa huku media ya Tanzania ikiwa haina habari, akasena zoezi lirudiwe, na ndipo yeyeb akaja kuunda Tume ya Wangwe. Wakati anaunda Tume ya Wangwe tayari alishaiokoa Tanzania na alitaka tu ridhaa ya wananchi. Kumbuka Tume ya Wangwe iliundwa bila ombi la wananchi, kimsingi wananchi wala hatukujua kuwa tuko hatarini.

    Ngoja nikuulize unafahamu kuwa mkataba wa umoja wa ushuru wa forodha ulishasainiwa? Wewe unaujua unasema nini?

    Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Jamaa ameandika na ameweka wazi kwamba anawasifia viongozi kwa jambo hili moja, siyo yote. Soma vizuri utamuelewa, hakusema Kikwete kapatia kila kitu, la hasha. Hili la Shirikisho, ndiyo kasema: kwenye hili tuliamka.

    Asante, acha ubabaishaji.

    ReplyDelete
  18. We are totally missing the point. Yes kuingia hii kitu kwa pupa ina madhara makubwa.

    Sioni hoja za watu kuongelea jinsi ambavyo Tanzania inataka kuingia kwenye Shirikisho kwa kutumia mkakati gani. Labda yameandikwa sijasoma, ila mawaidha mengi ni kuongelea historia ambazo kila mtu anazijua na kukuza uwoga na hofu ambazo hazima misingi ila ni rahisi kwa kuwagawa watu. Mbona tuna ndugu zetu humu humu ambao ni wasaliti wakubwa wa watu kwa Ufisadi - Uncles wetu and Sisters and Brothers au hata Fathers?? Haimaanishi eti kwa ajili hiyo ndio kujengana hofu. Kuna process za kuaddress kila jambo, basi tuzijenge hizo process and tujue lengo ni nini haswa. Kuingia shirikisho au la? Na kwa njia gani?

    Ndio maana nadhani huu mjadala ungefaa umove on kuonyesha ni njia gani inafaa kuweka mkakati sema baada ya miaka X or Y, Tanzania iingie Shirikisho tena with values : A, B, C and D etc ambazo zote hizo ziwe ni zile tulizojengea umoja wa watu with proven example ya Tanzania. On top of that, kila nchi ipewe hivyo vigezo vya shirikisho kama internal conflicts zitolewe na pia kulipa jeshi la shirikisho meno to move in and resolve matters ikibdi etc. Pia mikakati kuhamasisha na kutayarisha watanzania kugamala kwenye soko huria kwa standards za kimataifa hata kama ni za kikweti ila ziwe zinatupa edge kwenye ulingo wa kimataifa kama ilivyo kwenye sifa zetu za umoja na ukarimu. Na akina other members waje na yao kuhusu what is good and how it can be done or how' they have done it etc

    Umoja na Ukubwa ni Muhimu sana huku tuendako - tupende tusipende.

    ReplyDelete
  19. Mimi nadhani hoja zinazoandikwa kitaalam na kutoka kwenye magazeti zitatusaidia zaidi kuelewa haya mambo.

    Tunaomba mnaofahamu masuala kama hiyo customs union ambayo nasikia tulishaingia, basi mtueleze.

    Kelele za Mashaka zinatosha.

    ReplyDelete
  20. Hivi kuna haja ya kujibizana na Wakenya kweli?

    Mimi nadhani tujadili faida kama zipo tujipange, vinginevyo, tuachane na huu upuuzi kama hakuna faida. Mbona tulitoka COMESA, kwani EAC haiwezekani kutoka? Au kwa sababu makao makuu yako Arusha.

    Tunaomba viongozi wetu waliangalie hili.

    Mzalendo.

    ReplyDelete
  21. Michuzi tunaomba hizi atiko za mashambulizi uwe unazikusanya kwenye magazeti Bongo huko halafu unatuwekea tunasoma.

    Haitoshi kujibizana wenyewe tu, tunataka vitu vinavyoandikwa huko nyumbani pia ili tujue kila hatua inavyokwenda.

    Hata kama huwezi kila siku, jaribu mara moja moja.

    Mdau, Japan.

    ReplyDelete
  22. Bwana Mobhare ingawa makala yako ndefu, lakini nashukuru ni ya kwenye gazeti. Hii itasaidia hata akina pwagu na pwaguzi wasio na intaneti kusoma wajue tunakwenda wapi.

    ReplyDelete
  23. Kinachonikera mimi ni watu kushambuliana. Wakenya watatudharau. Tusishambulie wanaoandika, kama akina Mashaka. Ni mchangiaji mzuri tu, sijui kwa nini watu wanamshambulia. Ni kweli wapo wengi wazuri wenye uwezo, lakini si lazima wote waandike kwenye blogu hii. Mimi nadhani tunamisi pointi, tuungane Watanzania wote, tuwashinde Wakenya. Uandishi uliotulia na kujibu kwa ufasaha ni vema zaidi.

    Mdau Mzalendo, Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  24. Inakuwaje safu ikitoka MAJIRA halafu inatoka na hapa? Naomba zingine za kwenye UHURU, DAILY NEWS, na magazeti mengine yaliyozaliwa zitoke pia.

    Sijui magazeti ya nyumbani, niko nje muda mrefu, tangu 1982, nisameheni jamani.

    Mchizi, Spain.

    ReplyDelete
  25. Ingekuwa enzi za Nyerere huu upuuzi wa Wakenya kutupigia kelele usingetokea. Ni aibu kwamba viongozi wetu wa leo wanashindwa kutetea nchi kwa uwezo wao wote.

    Mkapa katufikisha hapa, kwa nini alikubali kila kitu?

    Wewe Matinyi ulikuwa Tanzania, hebu tueleze.

    ReplyDelete
  26. Hii analysis imetulia. Naomba hiyo ya Desemba 14 iwekwe pia.

    ReplyDelete
  27. Jamani andikeni kwa Kimombo ili Wakenya wakome. Mashaka kajitahidi ingawa kachapia kwenye sentensi chache, wajibuni hawa wahuni kwa Ung'eng'e. Michuzi waambie jamaa Daily News washuke vitu vya nguvu.

    ReplyDelete
  28. Jamani someni East Africa la leo, Warwanda wanakunya mavi huko. Wamewaachia Wakenya sasa kibano kimeanza, wananyang'anywa ajira, biashara zinafungwa, halafu Wakenya wanacheka eti ni ubatizo wa kutumia moto!

    ReplyDelete
  29. Mimi hili shirikisho likizaliwa najiua.

    ReplyDelete
  30. Wadanganyika mpo? Haya Wazenji hatusemi, Yahe yetu macho. Makenya yanakuja hayo, yazuieni kama nyie madume!

    ReplyDelete
  31. We anony hapo juu acha uhuni. Kiswahili ni chetu, siyo ng'eng'e.

    ReplyDelete
  32. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
    ila viongozi tuliowachagua Tz hili na liwakae kichwani wal'hahi taondoka mtu,,,
    mdau ulietoa hii atiko endeleza mwanangu nenda chimbo njoo na newz za uhakika tutete apa
    MICHU IZI NEWZ ZIINGIZENI KATIKA MAGAZETI YOOOTE YANAYOSOMEKA NA WATU KWA LUGHA ZOTE,,(kiinglishi cha wakenya,,,hahahaaaaa)
    ila its really inantia kichaa yan.
    yan ukiona mtu anakuganda ujue ana HILA ZA KWAPA UYO yan walakini
    HATUTAKI TUBURUZWE YAAN TWAENDA TARATIIIIBU ADI TUONE MIKUCHA IKO WAPI

    ReplyDelete
  33. na wanatung'ang'ania aswaaa,,,jaman what the heck!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...