JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO ITALY INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU YETU ANTHONY EMMANUEL NAMPELENGA KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO KATIKA HOSPITALI YA PINETA GRANDE CASTELVOLTUNO CASERTA, ITALY.
MAREHEMU ANTHONY AMBAYE PIA ALIJULIKANA KWA JINA MAARUFU LA MMACHINGA, ALIZALIWA TAREHE 12/07/1963 HUKO MKOANI LINDI.
SABABU YA KIFO CHA MAREHEMU INASEMEKANA ALIANGUKA NA WASAMARIA WALIOKUWA KARIBU WAKAITA GARI LA WAGONJWA NA AKAPELEKWA HOSPITALI AMBAKO ALIFANYIWA OPERESHENI YA KICHWA.
TANGU SIKU YA JUMATATU 1/12/2008 ALIYOANGUKA ALIKUWA KATIKA KITENGO CHA WAGONJWA MAHUTUTI AMA ICU, HADI JIONI YA JUMATANO WAKATI MWENYEKITI WA JUMUIYA ALIPOPATA SIMU KUTOKA HOSPITALI HAPO NA KUPEWA TAARIFA YA KIFO CHA MMACHINGA.
TUNAOMBA YEYOTE MWENYE MAELEZO YA ANUANI YA NDUGU ZAKE ATULETEE HARAKA ILI HATUA MUHIMU ZA MSIBA HUU ZICHUKULIWE.
IMETOLEWA NA:
JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY
Poleni sana, tena sana ugenini. Mani yangu, ebu jaribuni kupekuwa pekuwa kwenye makazi yake pengine mtapata barua toka nyumbani, pia passport yake nahisi ina-address yake jaribuni kuandika barua kupitia hiyo address, pia wadau wa LINDI NA MTWARA munaosoma hii blog jaribu kusambaza habari hizi. Poleni tena.
ReplyDeleteJamani mbona kama anafanana na yule mwanamziki aliyeimba..SALAMU ZA MJOMBA..Siji ni wa parapanda vile...anafuga rasta..hebu jaribuni kumuuliza huyo kaka huenda ni ndugu yake...ila poleni sana ndugu zangu wa Italy.
ReplyDeletemwenyekiti muulize minya kama ana mawasiliano na ambari mmachinga yule aliekuwa umangani ndio mtu ambae anamfahaumu marehemu vizuri,poleni sana marehemu nimeishi nae mwanzoni mwa miaka ya 80 syria,lebanoni,uturuki na italy ukalale pema.
ReplyDeletePoleni sana kwa msiba uliowafika watanzania mnaoishi Italy. Inasikitisha kupata shida hii ugenini. However, let this be a lesson/somo kwa mabeba mabox na wazamiaji, mabaharia n.k...Walau mjulishe mtu mmoja wa muhimu kwako kuhusiana na mahali ulipo-siyo lazima mueleze mnafanya nini but at least upo nchi gani. Jitahidini pia mjifunze kuacha will's. Hivi mnafanya kazi saaaaana huko nje ili nani abenefit na mapensions yenu-ni nyie wenyewe tu? Communication is key. Samahani natoa ujumbe huu sasa hivi mkiwa na majonzi lakini naona ni muhimu.
ReplyDeletePoleni sana, tena sana kwa tatizo hili.
Poleni sana wafiwa. may his soul rest in peace.
ReplyDelete