Home
Unlabelled
mtumishi wa mungu mwanza anyakua RAV4 ya zain
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Dada Celine unatuua na hiyo mipaja mtumeeeee!!!
ReplyDeleteMdau, Boston, US
Mgonja atoka Keko kwa Sh. bilioni sita
ReplyDelete2008-12-20 14:43:43
Na Hellen Mwango
Hatimaye, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuachia kwa dhamana aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.
Mgonja aliachiwa jana kutoka katika rumande ya Keko baada ya kujidhamini kwa hati sita za mali isiyohamishika zenye thamani ya Sh. bilioni 6.1.
Yeye mwenyewe ambaye anakabiliwa na mashitaka manane likiwemo la kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7, alitoa hati mbili kati ya sita zote zikiwa na thamani ya Sh. 1,024,000,000.00.
Dhamana hiyo ilitolewa mbele ya Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja anayesikiliza kesi hiyo.
Wakili anayemtetea Mgonja, Profesa Leonard Shaid, alidai kuwa, mshitakiwa amekamilisha masharti ya dhamana na kuiomba Mahakama kuwasilisha hati sita za mali isiyohamishika ambapo Mahakama iliridhia.
Profesa Shaid alidai kuwa, hati ya kwanza ni nyumba katika kiwanja namba 106 kilichopo Msasani ambayo mali ya mshitakiwa ina thamani ya Sh. milioni 903, ya pili iko katika kiwanja namba 405 pia mali ya mshitakiwa na ina thamani ya Sh. milioni 121.
Aidha, alidai kuwa hati nyingine ni kiwanja namba 21 Kinondoni, mali ya Mary Nguluma nyumba yenye thamani ya Sh. bilioni 1.7, kiwanja namba 61 Mikocheni mali ya Steven Kageni ina thamani ya Sh. milioni 793, kiwanja namba 80 Mikocheni Viwandani mali ya Hemed Salehe ina thamani ya Sh. bilioni 2.040 na kiwanja namba 208 Mikocheni mali ya Amina Abdul ina thamani ya Sh. milioni 544 ambapo hati zote ziliambatana na hati za wamiliki pamoja na taarifa ya uthibitisho kutoka kwa mthamini wa Wizara ya Ardhi.
Mbali na kujidhamini kwa hati hizo, mshitakiwa huyo ambaye alikamatwa na kufikishwa mahakamani Desemba 15, mwaka huu, alidhaminiwa na wadhamini wawili.
Hakimu Mwankenja alisema Mahakama imeridhika na hati hizo kwa hiyo mshitakiwa yuko nje kwa dhamana na Mahakama ilimtaka asitoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha chake, kuwasilisha hati ya kusafiria na kuripoti kila ijumaa ya mwisho wa mwezi mahakamani hapo na kusaini kitabu maalum.
Katika kesi hiyo, Mgonja akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, anakabaliwa na mashitaka manane.
Moja ya mashitaka hayo anatuhumiwa kuwa, kati ya mwaka 2003 na 2007, alipuuza ushauri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliomtaka kutoza kodi kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 29, mwaka huu.
Wakati huo huo, washitakiwa 20 wanaokabiliwa na kesi za wizi wa fedha katika Akaunti ya za Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jana walifurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kutimiza moja ya masharti ya dhamana ya kuripoti kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi mahakamani hapo na kusaini kitabu maalum.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwa Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu kuangukia siku ya sikukuu, hali ambayo imewalazimu kufanya hivyo jana. Ijumaa ijayo itakuwa sikukuu ya Boxing Day.
Washitakiwa hao ni Jayantkumar a.k.a Jeetu Patel, Amit Nandy, Ketan Chohan, Devendra Patel, Eddah Mwakale na Manase Mwakale. Wengine ni, Bosco Ndimbo, Sophia Joseph, Esther Komu, Imani Mwakosya, Rajabu Maranda, Farijala Hussein, Bahati Mahenge, Davies Kamungu, Godfrey Mosha,Japhet Lema.
Wengine ni Ajay Somani, Jai Somani, Jonhson Mutachukurwa Lukaza na Mwesiga Rutakyamilwa Lukaza ambao wote kwa kutumia makampuni ya kughushi walichota jumla ya Sh. bilioni 45.8 mali ya BoT.
Miongoni mwa masharti waliyopewa na mahakama hiyo ni kudhaminiwa na wadhamini wawili kila mshitakiwa, kuwasilisha hati za kusafiria, kutokutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuripoti kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi.
SOURCE: Nipashe
Celine Njuju, hiyo figure utafikiri umechorwa kwenye gazeti la Sani?
ReplyDeleteCeline tuwasiliane nahitaji urafiki wa kalamu
ReplyDeletefabhumphery@yahoo.com
Jamaa wa Dec 21 10:08pm anataka urafiki wa kalamu!!! anatufanya sisi tumezaliwa jaaaaana!!!
ReplyDeleteBIBE HESHIMA YAKO...UNAFAA SANA..UNAUMBO LA NYUMBANI.
ReplyDelete