MREMBO wa Burundi Claudio Noyimana jana alijinyakulia gari aina ya Lexus lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 40 lililotolewa na kampuni ya Sozmyya Dar es Salaam, baada ya kushinda taji la Miss East Africa.
Katika shindano lililofanyika kwenye hoteli ya Club Di Luc Tanganyika ya mjini hapa, nafasi ya pili ilichukuliwa na Mtanzania, Annete John Mwakaguo wakati nafasi ya tatu ilikwenda Mauritius kwake Anais Veerapraten.
Annete amejinyakulia dola za kimarekani 5000 wakati Anais amejinyakuliadola 3000 huku wote wakipata mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya RenaEvents ya Dar es Salaam ambayo ndiyo iliandaa shindano hilo.
Burundi wanapiga kona wenyewe wanafunga wenyewe.
ReplyDeleteHuyo mshiriki wetu katika vazi lake chini ya bendera kumeandikwa TANZANIE ndiyo lugha gani hiyo hadi kwenye majina!?Kwanini wasiandike TANZANIA.
Mengi-Wanaotetea mafisadi nao pia mafisadi
ReplyDelete2008-12-20 14:35:04
Na Joseph Mwendapole
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT), Reginald Mengi, amesema viongozi wanaokumbatia mafisadi ni sehemu ya mafisadi hao.
Amewashangaa watu wanaopinga vita dhidi ya ufisadi na kusema watu hao ndio wanaoweza kuifanya nchi isitawalike.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mengi alisema lazima watu wamuunge mkono Rais Kikwete katika vita dhidi ya ufisadi aliyoianzisha kwa maslahi ya Taifa.
``Watu hao wajue kuwa ufisadi ndio unaweza kuifanya nchi isitawalike na sio wanaoandika kuhusu ufisadi, hawa wanaosema uongo na kutumia fedha za ufisadi kuchafua amani ya nchi yetu,`` alisema Mengi na kuongeza kuwa watu wanaosema hivyo wanahusika na ufisadi kwa namna moja ama nyingine.
Aidha, alisema katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya nne, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele na vimepata ujasiri mkubwa wa kufichua na kupinga ufisadi.
Alisema ujasiri huo umetokana na dhamira kubwa na ya dhati ya Rais Kikwete katika kutokomeza rushwa na ufisadi na kwamba alishatamka kwamba anaunga mkono juhudi za vyombo vya habari katika vita hiyo.
``Hatuwezi kuvipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri vinavyofanya kupiga vita ufisadi bila kumpongeza Rais Kikwete kwanza....lazima jamii ijue kwamba kama Rais asingeunga mkono vyombo vya habari wananchi wasingeweza kujulishwa matukio ya ufisadi ili wachangie katika vita hivi kwa kuwa wangekuwa kwenye giza nene,`` alisema Mengi.
Mengi alisema ufisadi mkubwa uliofichuliwa sasa haukufanyika katika serikali ya awamu ya nne.
Alisema ufisadi huo ulitokea kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005, lakini kabla ya hapo waandishi wa habari waliogopa kufichua na kuandika kutokana na mazingira ya vitisho yaliyokuwepo wakati huo.
Aidha, alisema wako watu wanaosema ni unafiki mtupu kuwapiga vita viongozi wanaohusishwa na ufisadi kwa njia moja ama nyingine na hapo hapo kumsifu Rais Kikwete kwa jitihada zake za kutokomeza ufisadi.
Alisema watu hao wamekuwa wakijitahidi kuchonganisha vyombo vya habari na Rais Kikwete.
Alitahadharisha kuwa juhudi zao hizo zenye nia mbaya kamwe hazitaweza kuvunja nguvu na dhamira ya Rais, vyombo vya habari na umma ya kutokomeza ufisadi.
Alisema jitihada zinazofanywa na Rais Kikwete na serikali ya awamu ya nne katika kupambana na ufisadi wa kila aina nchini zinastahili pongezi za watu wote wenye kuitakia mema Tanzania.
Alisema pongeza kubwa ya vita hivi lazima apewe Rais Kikwete kwani yeye ndiye aliyefungua mlango wa uhuru wa vyombo vya habari.
Aliwataka waandishi wa habari kukumbuka kuandika mambo mengi yanayofanywa na Rais Kikwete ili jamii isije ikadhani kuwa hakuna mambo mazuri yanayofanyika.
Alisisitiza kuwa bila jitihada za Rais Kikwete nchi ilikuwa inaelekea pabaya kwani rushwa ilishaonekana kama sehemu ya maisha.
``Lazima tujue kuwa Rais Kikwete amefungulia milango vyombo vya habari na ndipo vikapata ujasiri wa kuandika masuala ya ufisadi...vingetishiwa tishiwa kama ilivyokuwa zamani visingethubutu kuandika,`` alisema Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP.
SOURCE: Nipashe
Phine, TANZANIE ni Lugha ya Kifaransa!
ReplyDeletehuyu mengi nakumbuka alipewa seven days awe ameshapeleka madai yake kwa waziri masha la sivyo waziri masha angemchukulia hatua kali kwa niaba ya serikali je alishapeleka wadau????
ReplyDeleteBrother Michuzi, mbona sijasikia taarifa ya lynette lwakatare ameshika namba ya ngapi kwenye hayo mashindano ya Miss East Africa? Maana hata kwenye top five simuoni. Alikuwa kwenye top 20 nini? Hongera zake kama ndiyo nafasi aliyoshika. Next time waandaji wajitahidi kumwandaa vema mwakilishi wa Tanzania.
ReplyDeleteMdau
WAACHIENI WACHUKUE "WALICHINJANA" SANA HAWA
ReplyDelete