Hesabuchini kuelekea ndoani (Countdown to the wedding)

Kwa wadau wa old good times of Azania na Tambaza as well as Deutchland, this is to officially announce and inform you that William Kaijage aka "Coco Madimba Camarade Pamba" anatarajiwa kufunga ndoa Jumamosi ya tar 27-Dec-2008 katika kanisa la RC Mwenge na kufuatiwa na Le Grand Ceremony katika ukumbi wa Landmark Ubungo.
One and all are cordially invited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera sana Kaijage aka "Coco Madimba Camarade Pamba" kwa mipango yenu ya kumeremeta. It is great pleasure to hear such good news particularly ex-Azania. However I have a small reservation, your couple (fiance) seems older than you. Anyway ng'ombe hazeeki maini???. Hongereni sana na tunaahidi kufika kwa wingi na kuwashangilia kwa nguvu. Bravo Kaijage!!
    Mdauzzzz

    ReplyDelete
  2. 1.) ndoa siyo shela.
    2.) mnatukaribisha wanablogu wote lakini tutakaoruhusiwa kuingia, kama sio ruta..., koku..., nk basi utasikia, "mupe fwanta".

    ReplyDelete
  3. Babu Jage, mzee wa "Coco Madimba Camarade Pamba".. hii inapendeza sana. Naona wawili mmependeza, naamini harusi yenu, maisha baada ya harusi, vyote vitapendeza this way for the rest of your lives.

    Merry x-mass and happy new year with full of blessing from his Almighty.

    Nas!

    ReplyDelete
  4. Hongera ndugu yangu. Wish you all the best on your big day

    Lakini wabongo tuna maneno huyo hapo juu anyesema mwanamke anaonekana ni mkubwa kuliko mwanamme...Una tatizo lingine au? What is wrong if a bride is older than a groom? Duh bongo ukiwa unasikilia ya watu utakufa na Heart attack?

    Mapenzi ni kokote na hayana umri.

    ReplyDelete
  5. Sitta: Ngeleja lete hoja ya Kiwira

    2008-12-19 11:31:05
    Na Joseph Mwendapole


    Spika wa Bunge la Muungano, Samwel Sitta, amesema suala la mgodi Kiwira linaweza kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge endapo Wizara ya Nishati na Madini itasema iko tayari kutoa taarifa hiyo.

    Akizungumza na Nipashe jana, Sitta alisema endapo wizara hiyo italiarifu Bunge kuwa imekamilisha taarifa yake ni wazi Kamati ya Uongozi ya Bunge itaipa nafasi ya kuwasilisha bungeni ripoti yake.

    ``Kwa utaratibu Bunge linapoipa kazi serikali, yenyewe inatakiwa kusema tuko tayari na hapo ndipo wanapopangiwa muda wa kuwasilisha wanachotaka kusema,`` alisema Sitta.

    Alisema kuna masuala mengi yanayosubiri kujadiliwa kwenye vikao vya Bunge hivyo lazima wizara husika iseme kama imekamilisha kazi iliyotumwa na Bunge.

    ``Unajua kuna mambo mengi ya kujadiliwa bungeni kama mkataba wa TICTS, TRL, Nyumba za Serikali na utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba tata wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond, hivyo kila kitu kikiwa tayari lazima kipangiwe siku,`` alisema Sitta.

    Juzi Wiraza ya Nishati na Madini, iliahidi kupasua jipu hivi karibuni kuhusu nani mmiliki wa mgodi wa Kiwira, ambao unahusishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

    Akizungumza na Nipashe, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kwa kuwa suala hilo liliibuliwa bungeni basi jibu hilo watalitoa huko huko bungeni.

    Alipoulizwa wizara yake inatarajia kutoa jibu hilo katika mkutano upi wa Bunge, Ngeleja alisema hilo linategemea zaidi ratiba itakayopangwa na Bunge.

    Alisema tayari wizara ina taarifa ya kutoa kuhusu mgodi huo na anachosubiri ni muda wa kusoma taarifa hiyo watakaopewa.

    Mgodi huo ambao umekuwa ukihusishwa na Mkapa na Yona, kwa pamoja wanadaiwa kujimilikisha kwa Sh. milioni 700 wakati thamani yake halisi ni Sh. b
    Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), nayo ilikaririwa hivi karibuni ikisema kuwa itatoa taarifa ya uchunguzi wa mgodi wa Kiwira hivi karibuni.

    Mkurugenzi wa Mashitaka, Elieza Feleshi, alisema ofisi yake bado inalifanyia uchunguzi suala hilo.

    Alipoulizwa kwanini uchunguzi huo unachukua muda mrefu, Feleshi alisema wanafanya uchunguzi huo kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zinazohusika.

    ``Bado tunalifanyia kazi ila halitakaa sana kila kitu kitawekwa hadharani hivi karibuni msiwe na haraka tuacheni tufanye kazi kwanza,`` alisema Feleshi.

    Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alikuwa wa kwanza kuibua tuhuma katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu, alipowataja bungeni Mkapa na Yona kuwa wanamiliki mgodi huo na walijiuzia kwa bei ya kutupa, hivyo wanastahili kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.

    Kimaro alisema mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakamilikishwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

    Hata hivyo, Kimaro alisema cha kushangaza ni kwamba, kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh. milioni 70 tu.

    ``Wakauziwa kwa Sh. milioni 700 bila kutangazwa na wao wakalipa down payment (malipo ya awali) ya Sh. milioni 70,`` alisema Kimaro.

    Kimaro alisema mwaka 2006, Mkapa na Yona, waliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kufua umeme kwa makubaliano ya kulipwa `capacity charge` (gharama za uwekezaji bila kujali kwamba wamefua umeme au la) ya Sh. milioni 146 kila siku (dola 3.6 milioni kwa mwezi) pasipo kufuata utaratibu.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  6. Old skul wamwaka gani unaedhani kila mtu anakufahamu

    ReplyDelete
  7. Mfumo dume bana! Unatangaza harusi yako jina lako unataja la mwanamke hutaji! Yani dem ni kama sio kitu worth mentioning vile. Ndoa ni ya Wile, huyu dem ni kama afterthought tu.

    Wile, mzee wa ma differential equations, you know better, achana na mfumo dume!

    ReplyDelete
  8. hapo walipo pigia picha ni wapi?

    ReplyDelete
  9. Acha uhaya wewe mbona China hujasema au hakuna ujiko?

    ReplyDelete
  10. Dume la nyani linaoa...du mikona kama ya nyani...lol
    Mdau William hongera sana!
    mimi dau wa Azania form 1G.
    Mdau wa USA....E...hahhah

    ReplyDelete
  11. Some of the comments are just too funny. Ebwana mzee umesoma mwaka gani, tukumbushane kidogo. Hongera sana.

    ReplyDelete
  12. I hope hapa wamepiga picha bongo, kama ni nje ya nchi, sidhani kama mzee mzima amevaa kufaa kuwa maeneo hayo, hata kama alikuwa anapita tu.

    ReplyDelete
  13. Hapo ni kunduchi beach hotel, bongo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...