Hi Kaka Michuzi,Katika gazeti la the Guardian la tarehe 4/12/2008 ilichapishwa habariyenye kichwa cha habari"Mengi: Minister wants me declared bankrupt".
KamaMtanzania mwenye uchungu na nchi na wananchi wenzangu, naomba upublish hiikwenye blog yako ikiwa ni support kwa ndugu yetu Reginald Mengi dhidi yamafisadi wanaoingia madarakani na kusahau walikotoka.
Ahsate.
Mdau

Mengi: Minister wants me declared bankrupt

I absolutely concur to Mr Mengi's reaction that even if they are able tosilence him, they will never stop the movement against corruption. No onehas the right to threaten others, let the Law decides your innocence orguiltiness. This is time to liberate the country from our own colonies. Iurge Mr Mengi to continue encouraging the media to fight corruption.History indicates that in fighting for true democracy, transparency andaccountability the media suffers a lot from torture and persecution ofjournalists.

For sure, president Kikwete has marked a history in this country andWananchi should join him. Watch dogs and whistle blowers have a uniquerole in fighting against corruption. Our country has enough resources togive Wananchi the acceptable living standards.
Most of the scarceresources available end up being misused by egoist bureaucrats. Thecountry will never move forward unless corruption and public embezzlementdo perish.

The new Institutional Economics Theories have shown evidence thatcountries with weak institutions will never develop. In fact, corruptionand public embezzlement have crowding out effect on both economic growthand economic development.
Can't we be tired of being backbitten by Donorcountries? A lot of Aid and grants supplied but still pervasive povertyfor the majority just because of few egoist people.
This is time to say NO, it is enough.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. "Mengi: Minister wants me declared bankrupt" Mdau una uhakika hiki ndicho kilichokuwa kichwa cha habari?? kama ni hivyo basi Editor lazima afukuzwe maana ni kichekesho.

    Uncle Misupu naona na wewe unahitaji Blog EDITOR.

    Kingemake sense kama kingeandikwa hivi:
    "Mengi: Minister wants me to declare bankruptcy"

    Mchango wangu,
    B.Mbakiaji

    ReplyDelete
  2. Ingawa kama binadamu ana matatizo yake sawa na mimi, kati ya wajasiliamali wetu nchini ninaowaheshimu, ndg. Mengi ni mmoja wapo.

    Ujasiri alionao wa kuumbua madudu ya wakuu wazi wazi ni hulka yake kama vile alivyotoka na kusema kuwa kulikuwa na 'mchezo mchafu' wakati wa kutafuta tenda ya uuzwaji wa 'Kilimanjaro Hotel'.
    Penye ukweli uongo ulijitenga!

    Mtakumbuka tena kuwa wakati huo aliletewa vitisho vya nyau kama sasa Waziri anayempa siku saba (chata ya Mrema) eti atoe ushahidi.

    Sasa na sisi nguvu ya umma tuliomwajiri Waziri kama Mbunge wetu tunatoa siku tatu (mtu huyu mkubwa sana) aondoe kauli yake ili (wadogo wanaohusika) OCD au RPC tu ndie amwandikie Mengi agizo hilo. Maana katika utawala wa sheria Waziri hawezi kuingilia kazi za polisi na mahakama.

    Swali ni kuwa je Mengi akitoa maelezo yake, Waziri huyo ana uwezo na mamlaka ya kusema ni kweli au si kweli? kwa kutumia nyenzo na mamlaka yapi?

    Nchi ni lazima iendelee kuwa na vyombo mbalimbali (vinavyomilikiwa na Serikali na pia vingi vya sekta binafsi) kutuhabarisha yanayojili kwa uwazi, ukweli na ukamilifu.

    Move ya aina yeyote ya kunyamazisha the Media run by the Private Sector haikubaliki hasilani.

    IPP Media naombeni kazi nishughulike kuanzisha KITENGO na KIPINDI kipya kiitwacho:-
    'MIZANI YA HADAA NI CHUKIZO KWA MOLA'

    Hiki kitakuwa kipindi kinachopiga hatua moja mbele ya kipindi kilichoitwa 'Kiti Moto' ambapo sasa tutakuwa tunatoa alama za wazi na kueleza hali ya ufisadi (corruption Index) baada ya kufanya utafiti wa kisayansi kila baada ya miezi sita katika ngazi za Wizara, Mikoa na Halmashauri na pia Asasi na Taasisi za umma na kutoa mapendekezo yetu baada ya kuwahusisha wataalamu mbalimbali wa maeneo ambayo ufisadi au kutoajibika kumefanyika.

    Katika karne ya 21 Media haiwezi kuendelea kuwa wahabarishaji tu wao pia ni vyombo vya kuleta mabadiliko chanya ( Positive Change Agent)

    Namalizia kwa kuwarushia swali,

    'Bila CNN - Obama asingekuwa rais Mteule wa Marekani'- Jadili

    ReplyDelete
  3. It is true that freedom of speech through uncensored media such as INTERNET is the only weapon we ordinary people can use to fight for our rights.

    ReplyDelete
  4. Mtu anayekuwa declared bankrupt ni yule ambaye hawezi tena kulipa madeni yake wakati wadai wanataka chao, sasa kama MENGI wanaomdai wanataka chao na hawezi kulipa basi ni sawa kuwa declared bankrupt, hatuhitaji cheap politics and and simple popularity hapa, vitu vya ukweli visemwe wazi kama ni vya ukweli kwa maslahi ya watanzania wote si mtu mmoja mmoja. To be declared bankrupt is just a normal thing in life, here in Europe even an individual could be declared bankrupt, and I have seen many people be declred bankrupt here by court of laws and the good thing about that is you gonna be free and you won't be required to pay you debts anymore.

    ReplyDelete
  5. we usijifanye mwalimu wa grammar si umeelewa au unataka kuleta masheuzi,hebu tutokee hapaa muone kwanza!!

    ReplyDelete
  6. Anon wa kwanza kabisa hapo juu nimeshtushwa sana na uelewa wako finyu wa lugha ya Kiingereza uliotuonesha.

    Hiyo title ya Minister wants me declared bankrupt iko sahihi kabisa.

    Kama huelewi maana yake ni "Waziri anataka nifilisiwe"

    Iko katika passive form. Kwa maana ya kwamba Mengi anafanyiwa... anaonewa.

    Hiyo title uliyotoa wewe grammatically iko sahihi lakini haina mvuto maana iko katika active form. Yaani Mengi mwenyewe ajifilisi... Kwa ufupi haina mvuto wa kihabari.

    Bila shaka itakuwa ngumu kwako kuelewa somo hili hivyo nakushauri ukipata muda na vijisenti kidogo pitia kozi ya uandishi wa habari.

    Nina wasiwasi pia na performance yake katika English Grammar toka primary hadi form four.

    ReplyDelete
  7. LAZIMA MUELEWE KUWA MENGI ANATUMIA VYOMBO VYA HABARI KUONYESHA KUWA ANAONEWA HATA KAMA PANA UKWELI?
    LAZIMA MFIKIRIE SAANA KWA NINI?
    NA ANATUMIA NGUVU ZA WANANCHI KUJILINDA CHUNGUZENI SAANA MANENO YAKE.

    MWISHO NASEMA TAARIFA YA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UFISADI NI SAWA KABISA LAKINI VISITUMIKE KUCHOCHEA CHUKI KWA FAIDA YA MTU MMOJA NA FAIDA BINAFSI NA SIO KWA WATANZANIA
    KUMBUKA KILIMANJARO HOTEL NA MENGINE MENGI!

    ReplyDelete
  8. Kweli Mengi alikuwa na hela zamani lakini sio sasa kwani matumizi yanazidi mapato, na kosa lingine alilolifanya kwenye biashara zake hakuangalia uwezo na utaalamu wa mtu katika kuajiri, ataacha kweli kufilisika? Na kama kakopa mapesa ya watu ayalipe sio alete ule mchezo wake wa kujikosha na vyombo vyake. Nakumbuka siku za nyuma alikuwa na deni kubwa la nbc kama sikosei na akatumia njia hiyo2. Ndio maana wakenya wanatucheka maana tunafanya mzaha na pesa, maana hata Freeman Mbowe kachukua mapesa kibao ya nssf akidaiwa na yeye ataanza kupiga mayowe kachezewa faulo! Warudishe tu hayo mabilioni sio kukimbilia magazetini maana hilo nalo halina tofauti na ufisadi.

    ReplyDelete
  9. Mengi:minister wants me to be declared bankrupt...anon wa kwanza kaiona error kama mm pia

    ReplyDelete
  10. Mengi asifikirie watanzania tumelala usingizi mzito kwa kuanza kujihami mapema kwa staili ya kuonewa. Hiyo ni staili ya kitoto kuangua kilio kabla hata kesi haijafika mezani. Hana haja ya kuwa na wasiwasi kama mahesabu yake yako sawa ulipaji kodi, mikopo na kila kitu, he should be ok. Ni mtu ambaye amekuwa karibu na ccm kwa muda mrefu. Waziri, auditors au wahusika wengine wana kila sababu kuangalia katika makampuni tofauti kuhakikisha sheria zinafuatwa. Hata katika nchi za Ulaya tumesikia CEO wanavyofuja mali and needs to take responsibility na siyo kulalama

    ReplyDelete
  11. KAZI LAZIMA IFANYIKE HATA MKILALAMIKA KAZI INAFANYIKA. IKIENDA VIBAYA AU VIZURI KAZI INAFANYIKA NA ITAENDELEA KUFANYIKA...............BONGO OYEEEE

    ReplyDelete
  12. Mimi langu ni kwahuyo aliyesema 'Bila CNN - Obama asingekuwa rais Mteule wa Marekani'- Jadili

    Kama ni hivyo basi fox news channel ingechangia kikubwa kumwondoa. Kwanza CNN ni neutral (independent) channel....at least ungesema MSNBS imeachangia

    Lakini ukweli ni kuwa none of those played a major role. Hivi unajua ni watu wangapi wana cable TV in the USA? Tafuta jawabu la hili kwanza ndio utajua.

    Obama iwe TV au internet....sio sana....It is about time. Ujue culture zimeshift sana wazee wengi bado ni rasist lakini watoto wao hawana ukabila tena, immigrants wengi siku hizi wana makaratazi na ni smarter people wanaona mbali and awareness of what is going on.


    Back to the topic kama anadaiwa alipe asitumie vyombo vya habari kuwanyamazisha watu. Kama hana hela basi kampuni yake ifilisiwe.....I hope ni LLC kwa hiyo personal haitamuaffect yeye. Na huyo anayesema hiring process yake ilikua mbovu hakukosea. Wakati kampuni yake ilivyokua juu waliokuwa wameajiriwa pale wengi walikua ni ndugu za fulani na fulani au Waziri akimpiga simu tu kazi unapata haijali elimu yako. Walikua wengi pale hawana hata elimu ya form four

    ReplyDelete
  13. 1. Mengi unadaiwa Lipa. Dawa ya deni ni kulipa maneno maneno hayasaidii.

    2. Waandishi wa habari wanaokufanyia kazi hawawezi kuacha kukufagilia na kuandika habari nzuri kukuhusu hivyo usifanye watu wajinga kwa kuwatumia kufutia Historia ya madeni yako tunayoyafahamu.

    3. Mengi anapowasema wengine ni mafisadi na yeye anapaswa achunguzwe kwa historia yake ya Sexual Abuse and Exploitation. Kutumia cheo chake kuajiri wanawake warembo na kulala nao hata wengine wakiwa wake wa watu kwa kuwa tu ana hela na ana uwezo wa kuwapa kazi tabia ambayo media owners wengi kama Diallo Anthony naye anayo.
    Inasikitisha lakini lipa deni Mengi.

    ReplyDelete
  14. "Minister wants me declared bankrupt" was very right! Please ignore some of these small editorials. Contribute to the debate, if you cant just shut your mouth, please. Mpita njia. Obama camp. USA

    ReplyDelete
  15. if u scare go to church.....drive very fast no drive slow money money money till the end....bongo tambarare kwa wajanja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...