nikiwa na skina na mai waifu wake ambao leo wamemeremeta huko mwananyamala kwa mama zakaria. bw. harusi ni mchezaji wa zamani wa asante tololo ya mtaa wa kongo na bi harusi ni mwananetiboli mahiri
muda wa pete
nivishe nikuvishe, tuonyeshe ishara ya mapenzi eeee...
wana asante tololo na kimamba fresh walijitokeza kwa wingindugu, jamaa na marafiki
ndo 'nshabeba hivyooo....;
black moses akipongeza maharusi
bw. harusi na marafiki wa karibu
majirani na mawifi
wazee wa baraza hawakosekani

bila tarumbeta harusi haijanoga

sasambu sasambu kama kawa

sherehe zilihamia temeke vetenari ambako wali mweupe kwa pilau ilikuwepo
raha ilioje kupiga mpunga harusini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Michuzi,

    I miss Bongo. Raha iliyoje kuchapa mpunga wa harusi, it doesn't taste the same, compared to the one at home. isn't it?

    I really miss Bongo.

    ReplyDelete
  2. Michuzi nimekukubali wewe uko kila sehemu mara unakula kuku na Mafisadi na siku nyingine unajichanganya uswahilini kwa walalahoi. Lakini acha kubania comments zinawapiga madongo washikaji zako MAFISADI.

    ReplyDelete
  3. hongeara maharusi,
    Aaaaaaa, Michuzi bwana umenikumbusha huo mwimbo nilikua naupenda sana... Nishike mkono,tuwaonyeshe kweli tunapendana ha... nilishe nikulishe... mbuzi ishara ya upendo o,
    Ni Kasongo Mpinda aliimba? Sasa umenikumbusha mbali zaidi, my other favorite was...Ufitina...na upelelezi ni sumu ya mapeeeenzi...tumependana wenyewe bila nyinyi kujuaaaa...sasa mwajua mwaanza kuleta matatizo...mimi kupendwa na yeyeee...nyinyi mwakerwa nanini yo yo yo yo...
    Michuuuuuu, those days, Mtafute Kasongo Bwana Balozi, yuko wapi siku hizi? Mpige interview ya nguvu humu globuni na picha nyingi, ntashukuru sana mzee ukifanya hilo. He was the best.
    Kasongo Mpinda's fan.

    ReplyDelete
  4. OMG namiss hilo pilau mweee. yaani la kupika kwa wingi hivyo, jiko la mkaa linanoga kweli....

    hongera maarusi

    ReplyDelete
  5. Duh, kachumbari kwenye bakuli la purple imetulia,

    ReplyDelete
  6. dah michuzi unanikumbusha mbali sana.. yan leo umeniwekee pic za kitaa M/NYAMALA KWA MAMA Z. vp aujapiga pic sehem nyingine like M/NYAMALA UJIJI.. M/NYAMALA KWA MANJUNJU weka hizo pic kama umepiga broo nimemiss sana mitaa yangu hiyo na masera wangu kwa sana, mdau UK

    ReplyDelete
  7. dah michuzi unanikumbusha mbali sana.. yan leo umeniwekee pic za kitaa M/NYAMALA KWA MAMA Z. vp aujapiga pic sehem nyingine like M/NYAMALA UJIJI.. M/NYAMALA KWA MANJUNJU weka hizo pic kama umepiga broo nimemiss sana mitaa yangu hiyo na masera wangu kwa sana, mdau UK

    ReplyDelete
  8. Hongera bwana na bibi harusi.Mungu awabariki.

    Very sImple wedding! I really like it.

    ReplyDelete
  9. Kweli nyumbani kuna raha zake,hasa kwa waru waliopo Ughaibuni kuna yale mazuri ya huku na mabaya yake pia.Moja ya ugumu ni social life ambayo ni tofauti kabisa na ile ya kwetu.

    Lakini mtu akisema anamiss nyumbani naona kama amejilipua kwa nani kakukataza kwenda. Mimi huwa nakwenda mara mbili kwa mwaka.Just a matter of plan and strategies only. Tuacheni kujibana kiasi hicho hata wanaolipwa Minimu pay hapa U.K ya paundi 5.80 unaweza ukajibajetia kisawasawa kabisa, kwa walio Marekani cjui kikamilifu lakini nishakutana na washikaji kibao wakitokea huko.

    Ujumbe kama unamiss nyumbani wakati huweki efforts za kuja basi humiss wewe ama ni mtumwa wa kazi ama wa talanta.Wakuchonga mchonge sasa.Walavumbi mnanisikia jiandaeni nakuja na paundi Krismass hii

    ReplyDelete
  10. Brother Michuzi nakupa KUDDOS kwa kuwa mtu dynamic. Ukiwa kwenye state business una act accordingly na ukiwa nyumbani sehem sehem una act the way wenyeji should act. Yaani una fit kuishi NY, London, Buguruni, Düsseldorf, Magomeni Mapipa, Johanesburg, Manzese...etc,. You are a true GLOBAL CITIZEN.

    ReplyDelete
  11. mmependeza jamani..

    mungu awabariki...

    mnaonekana ni watu wa furaha!na ibaki hivyo!

    ReplyDelete
  12. Naam hizo ndio harusi zetu za kiafrika, za kiswahili, hazina presha wala nini, sijui mpaka ukatafute holi, mara limo, sijui ugombane na ndugu ambao hukutaka waje harusini kwako kwa sababu wametoa mchango chini ya kiwango, yoote hayo ya nini? Cheki hiyo harusi nafikiri kila aliyekuwepo hapo mtaani alihudhuria, na chakula alikula cha kutosha! Sio kipapatio na kijiko kimoja cha wali, ndizi moja iliyopikwa, na kiazi kimoja!

    ReplyDelete
  13. WENZIO TWASEMA TWAPIGA PUNGA, ILA SIJAONA SODA KWA PEMBENI, SI WAJUA KISHUSHIO INCASE UKIKABWA NA NYAMA!!!!!

    ReplyDelete
  14. du umeshanitamanisha hiyo pilau yako na mimi naenda kuikoroga yaku sijui kama nitaipatia kama hiyo au?

    ReplyDelete
  15. hahahahha,nimefurahi kukuona mshkaji Juma wakumeta

    ReplyDelete
  16. Haki ya nani vile huyu ni balozi wa nanihii ni msanii kwelikweli. Yaani akiwa na mafisadi kama jamaa alivyodokeza hapo juu basi huwezi jua kama ni mswahili wa maeneo maeneo. Duh! we mkuu wa wilaya ya nanihii msanii kwelikweli. Ila anngalia wasije wakaondoka na kichwa babake kwani nasikia Mengi wamemu-alert wataondoka na kichwa chake. Wa-tz hawana dogo. Big up!!!

    ReplyDelete
  17. washikaji na wamisi sana hongera martini,vipi ndugu yetu kitwana amepatwa na maswahibu gani mbona anaonekana mzee kuliko hao kaka zake na anatembea na mkongojo.big up harusi poa sana.

    ReplyDelete
  18. DUUUUUH. HAPO ZIMEPUNGUA NDIZI MBIVU TUUU AU VIPI WADAU???????

    ReplyDelete
  19. Kaka Michu, Balozi wa Zein na Mkuu wa wilaya ya nanii, hilo neno Post A comment huwezi kuliweka kwa kiswahili aisee( au unamana kuliacha hivyo)

    Huyo Balck Moses ni yule alikuwa mcheza Dance enzi hizo au ni mwingine?

    ReplyDelete
  20. Shukrani kaka Michuzi kwa kutuwekea picha za harusi ya brother Skina kwa kweli nimefurahi sana kwani ni muda miaka mingi sijamuona,nakumbuka tulikuwa tunafanya naye mazoezi pale shule ya karume magomeni mwembe chai na timu yetu ya Kagera Rangers,nilikuwa nimemsahau kabisa mpaka nilivyorudia kuangalia picha na kurudisha memory ndiyo nikajua ni brother Skina.Mungu aibariki ndoa yenu.Ni mimi Niger Boy(Peter Dawo)

    ReplyDelete
  21. Hongera maharusi na nawatakieni maisha marefu pa,oja. pia hongera kwa kudumisha mila na desturi za harusi za kikwetu, wengi siku hizi wanapofunga ndoa waanaiga desturi na mila za kigeni, ushindani na kujionyesha tu!

    ReplyDelete
  22. Dah harusi ya kiswahili sana, angalia pilau ilipowekwa uchafu mtupu , ndio maana nachukia Africa ni uchafu na hakuna aliye ona hilo , najuliza uandaaji wa hicho chakula ulivyo kichafu .uchafu , uchafu , uchafu .

    ReplyDelete
  23. We mshamba wa UK 8:28am hivi unajua maana ya neno kumiss. Unaweza ukatoka jana home na still leo ukakumiss home kishenzi . Hilo lipilau nimelila summer hii na bado nimeliona hapo na ukweli ni kuwa hata mimi nalimiss.

    Sherehe kama hizi za bongo ukipanda tu ndege kuondoka unaanza kumiss it is not the matter of how many times you visit the country.

    Wewe kama ni mwanaume au mwanamke si una mwenzi wako...? why missing her/him akiwa ameenda tu japo kazini. If you don't miss her/him you have no feelings.....Na wanaosema wanamiss whatever wanafeeling na it is a huma nature.....

    Pilau linaonekana zuri na harusi yao very simple...I like that....

    ReplyDelete
  24. Hii inaitwa Harusi Dume. Vinjwaji hamna angalau wangeweka gudulia la maji watu watumie kushushia pilau. Kabila nyingine mfano Wachaga kwenye shughuli kama hii ni bora uwawekee mbege kuliko pilau

    ReplyDelete
  25. Ewe msafi wa 11:10, una uhakika hicho unachokula mahotelini ni kisafi? Eti harusi za kiswahili uchafu mtupu, unajua unaweza kumsoma mtu mara moja, ukajua tu ni mtu aliyetokea wapi. Hii harusi ni nonstalgia imekukumbusha ulikotoka, imekukumbusha maisha yako yalivyokuwa kabla hujaondoka huko uswahili kuchafu na kwenda uzunguni kusafi, lakini kumbuka mdharau kwao mtumwa! Iko siku utarudi tu huko kuchafu aidha kwa miguu yako au sandukuni, kwani kwenu ni kwenu tu!

    ReplyDelete
  26. wewe unayesema uchafu,, hebu jirekebishe umeshakuwa mkubwa sasa,kitendo cha kutoka nchini kimekupa kichwa,.

    pilau linaonekana tamu tuu,na lina mvuto.harusi nzuri imependeza bila waalikwa na maaharusi wanafuraha pia..

    kwenu maharusi nawatakila kila liliojema,, maisha mema yenye furaha tete,

    ReplyDelete
  27. Hongera sana maharusi! Mwenyezi Mungu aijalie ndoa yenu iwe na amani na furaha tele! Michu hivi kweli na uislamu wote hata kanzu huna ya kuendea kwenye shughuli kama hii!! Unatuangusha!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...