Mtoto wa Rais Khalfan Kikwete akimpokea Baba yake Dr. JK kwa maua ya pongezi muda mfupi baada ya kurejea nyumbani akitokea Nairobi Kenya ambapo alitunukiwa Degree ya Doctor of Humane Letters(Honoris Causa) ya chuo kikuu cha Kenyatta kwa kutambua mchango wake uliopelekea kufikiwa makubaliano ya amani nchini Kenya na sehemu mbalimbali barani Afrika kwa jumla.
Makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Dk. JK muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Nairobi ,Kenya. Kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar Mh. Abbas Kandoro


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. acheni kumkuza mtoto. mambo ya makubaliano ya ... nchi za afrika ... umri huu anayajulia wapi?

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi,
    Naomba tu niseme kuwa Rais wetu siyo Dr. Kama ulivyosema, ametunikiwa hiyo Doctoral ya heshima, huwezi kumwita Dr. Kikwete yet, yeye anayo BA tu, hiyo Doctoral ni ya heshima tu. Asante,
    John,
    Indonesia

    ReplyDelete
  3. Mkapa: 40 yake yatimia

    2008-12-20 23:06:50
    Na Emmanuel Lengwa, Jijini


    Baada ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kutuhumiwa sana kuwa yeye na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini Bw. Daniel Yona walijiuzia kwa bei poa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, hatimaye suala hilo limefikia arobaini yake kwani sasa litaanikwa hadharani na kujadiliwa kipengele kimoja baada ya kingine.

    Aidha, wabunge kibao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanadaiwa kuwa wameshajipanga katika kulijadili kwa undani suala hilo, ambalo linadaiwa kuwa limejaa utata na kuna wakati lilizusha mjadala wa aina yake bungeni.

    Kufikia kwa arobaini ya sakata hilo linalodaiwa kumhusisha zaidi Mkapa na Yona, kunatokana na taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, aliyesema kuwa ripoti kamili juu ya suala la Kiwira iko tayari na kilichobaki ni kuiwasilisha bungeni.

    Lakini, baada ya Waziri Ngeleja kusema hayo na kisha Spika wa Bunge kukaririwa vilevile akisema kuwa Bunge linaisubiri kwa hamu ripoti hiyo na nyingine kadhaa, baadhi ya wabunge wamedaiwa kuwa tayari wamejipanga vilivyo katika kumlipua Mkapa na wengine wanaodaiwa kushiriki katika kuuza kwa bei poa mgodi huo wa Kiwira.

    Chanzo chetu kimoja kimedai kuwa bila woga wala kumuonea haya mtu yeyote, baadhi ya wabunge wamepania kulijadili kwa kina suala hilo na hatimaye kutetea raslimali za taifa.

    ``Kuna mambo mengi yanayotia shaka juu ya uuzwaji wa raslimali za taifa... sasa kuna wabunge kibao waliojipanga katika kuhakikisha kuwa suala hili linajadiliwa bila kufunikwafunikwa,`` kikadai chanzo hicho.

    Hatahivyo, akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mbunge aliyeliibua sakata hilo bungeni na kuwatuhumu wazi Mkapa na Yona, Mhe. Aloyce Kimaro wa Jimbo la Vunjo (CCM), amedai kuwa taarifa hiyo ya Mgodi wa Kiwira anaisubiri kwa hamu bungeni na kwa sababu kila kitu kiko wazi, anaamini kuwa Serikali haitaficha kitu.

    Mheshimiwa Kimaro amesema kuwa suala hilo litakapotua bungeni, yeye binafsi atahakikisha kuwa, kama walivyo wabunge wengine, atapigania kwa kila namna kuona kuwa sasa mgodi huo unamilikiwa kihalali.

    Akasema hivi sasa, suala sio mmiliki wa mgodi ni nani, bali ni kuona mgodi huo unamilikiwa kihalali na unafanya kazi iliyokusudiwa ili kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.

    Akaongeza kuwa kipindi hiki ni cha kusafisha uchafu wote wa ufisadi ili baada ya hapo, nchi ianze kuzungumzia namna ya kujiletea maendeleo.

    ``Hiki ni kipindi cha kusafisha uchafu. Tuweke mambo yote kwenye mstari, uchafu ufike mwisho na kisha tuanze kupigania zaidi maendeleo yetu,`` akasema Bw. Kimaro.

    Akasema lengo ni mgodi huo ufanye kazi ya uzalishaji kama ilivyokusudiwa na kuwa wale wote waliokuwa wakiuchezea kwa madai ya kujiuzia kwa bei poa, sasa wavune walichopanda.

    Naye Mbunge wa Viti maalum kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Halima Mdee, amedai kuwa ikiwa taarifa hiyo ya Mgodi wa Kiwira itakuwa na maudhui kama watu wengi wanavyolifahamu sakata la mgodi wa Kiwira, inabidi wahusika wake wachukuliwe hatua kama walivyoanza kuchukuliwa watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akauti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA.

    ``Tunaisubiri kwa hamu taarifa hiyo. Na kama kweli itafanana na taarifa tuliyonayo kuhusu mgodi huo, sioni kama `treatment` yao itatofautiana na ile ya watuhumiwa wa EPA,`` akasema Mheshimiwa Halima.

    Akadai kuwa ikiwa sheria za nchi zitafuatwa, ni dhahiri kuwa wahusika kwa kujimilikisha mgodi kinyume cha taratibu ni kosa la jinai na kuwa hawafai kuendelea kuumiliki.

    ``Kama walinunua kinyume cha utaratibu, hawana uhalali wa kumiliki mgodi huo,`` akasema.

    Akaongeza Mheshimiwa Halima kuwa yeye anatarajia kuona wabunge wote wakipitisha maazimio ya kuwanyang`anya wahusika mgodi huo na kuurejesha Serikalini, ili taratibu na sheria zifuatwe.

    Kwa taarifa zilizowahi kutolewa na Mheshimiwa Kimaro Bungeni, ni kwamba Mgodi huo uliuzwa kwa bei poa ya shilingi milioni 700 kwa kampuni ambayo wamiliki wake ni pamoja na Mkapa na Yona.

    Cha kusikitisha zaidi, ilidaiwa kuwa licha ya kampuni husika kuuziwa kwa bei hiyo poa, bado ililipa Sh. Bilioni 70 pekee.

    Hata hivyo, madai hayo yatakuja kubainika kuwa ni ya kweli au la baada ya ripoti kamili kuhusu Mgodi wa Kiwira kutolewa bungeni kama alivyoahidi Waziri Ngeleja.


    SOURCE: Alasiri

    ReplyDelete
  4. We John acha wivu. Honoris Causa ni academic 'Doctorate' degree kamili kabisa. ''A doctorate is an academic degree that in most countries represents the highest level of formal study or research in a given field'' Chuo kinaweza kumpa mtu kutokana na mchango wake kwenye jambo au taaluma fulani kwa kumpa 'waiver' ya matriculation, mitihani nk, lakini ni 'Doctorate' Kamili hata kama hupendi!

    ReplyDelete
  5. Hongera JK kwa hiyo PhD ya kupewa kwa kuitambua kazi yako. Lakini ukweli unabaki palepale kuwa PhD ni ngoma nzito si mchezo kuipata kwa maana ya kuisoma. Ina shughuli nene ndio maana wengi wa wanaopewa PhD za heshima huwa hawajiiti madaktari kwani wanajua ugumu wa Uzamivu.

    ReplyDelete
  6. JK ana mshauri wa mavazi au? naona siku hizi amezidisha mchuzi mix au x-mass tree.

    ReplyDelete
  7. Jamani acheni longolongo, PhD ni PhD tu hata kama ni ya heshima, ya kusomea, ya mtihani wa matriculation au vinginevyo recognized university itakavyoiita. Kikwete kuanzia hapo alipotunukiwa Shahada ya heshima "Doctor of humane Letters(Honoris Causa)" kutoka Kinyatta University tayari ni Dr. JK. Wadau tuungane kumpongeza na kumtakia uchapa kazi uliotukuka. Mfano, kwa sasa hivi anapambana na MAFISADI akimaliza kazi ya kusafisha mafisadi TZ, chuo kikuu cha DSM nacho tutakiomba kimtuku PhD nyingine ya heshima. Maana fupa la ufisadi Nyerere aliliacha, Mwinyi akaliacha, Mkapa akaliimariimarisha zaidi lakini JK ameamua kulitafuna na kulimaliza kabisa. Mara tu akishalimeza lote na vipande vyake, basi atastahili PhD nyingine.
    Hongera sana JK.
    Mdau

    ReplyDelete
  8. Ni nyinyi tu wa-AfrICA MNAPENDA SANA KUJIITA Madoctor mkipata PhD, wezungu wengi huwa katikamaisha ya kawaida mtaani ni mara chache sana ukamsikia akiji-address kwa doctor eti kwa vile ana PhD unless ni doctor wa professional ya medicine, otherwise wanajiita majina yao ya kawaida tena first name, PhD ni degree kama degree zingine sasa haina haja ya mtu kuji-address kama doctor. Wazungu wengi wenye ngazi ya uprofessor ndo wanaji-address kama professors kwa vile professor si degree na upatikanaji wake process yake si kama ya degree.

    ReplyDelete
  9. Ni nyinyi tu wa-AfrICA MNAPENDA SANA KUJIITA Madoctor mkipata PhD, wezungu wengi huwa katikamaisha ya kawaida mtaani ni mara chache sana ukamsikia akiji-address kwa doctor eti kwa vile ana PhD unless ni doctor wa professional ya medicine, otherwise wanajiita majina yao ya kawaida tena first name, PhD ni degree kama degree zingine sasa haina haja ya mtu kuji-address kama doctor. Wazungu wengi wenye ngazi ya uprofessor ndo wanaji-address kama professors kwa vile professor si degree na upatikanaji wake process yake si kama ya degree.

    ReplyDelete
  10. MICHUZI UNAONA NAMBA YA WATU WANAOTEMBELEA BLOG YAKO INAVYOKWENDA KWA KASI SASA IMESHAFIKIA 5,004,339 HIYO NI MIMI KWA LEO. MAMBO HAYO. FANYA BIASHARA YA MATANGAZO UTAPATA MIPESA, google, yahoo hupata pesa kupitia matangazo, ungekuwa huku majuu ungetengeneza pesa kibao kama ungeanzisha website yako na kuuza nafasi za matangazo. nilishaona mtoto wa secondary kaanzisha web kufumba na kufumbuwa aliamka milionea na kuacha shule, ebu lifikirie hilo kwa makini bro.

    ReplyDelete
  11. Muheshimiwa Mkuu wa Wilay,mi sitajadili kuhusu uDR wa JK lakini ni swala la Rais kupokelewa na ujumbe mzito kama huu.mi nilidhani kuwa inafaa Rais akapokelewa na ujumbe mzito pale tu anapotoka katika shughuli nzito za kiserikali na sio vinginevyo.unajua vitu vidogodogo kama hivi vina ghalama zake sababu ujumbe wote huo inabidi upewe huduma za ulinzi,usafirishaji wa misafara ya magari,bila kusahau kufungwa kwa barabara WANAPOPITA WAHESHIMIWA.
    NAOMBA KUWAKILISHA.
    MDAU uGIRIKI

    ReplyDelete
  12. MICHUZI NA WEWE UWE UNATULETEA HABARI ZA WATU WA KAWAIDA MITAANI HUKO MANZESE, BUGURUNI NA KWINGINEKO SI ZA AKINA JK WANAOISHI MAISHA YALIYOTUKUKA TU, TUNATAKA TUONE NA MAISHA YA KIMASIKINI MITAANI ILI NA WATU WA SERIKALI WANAOPITIA HI BLOG WAPATA SOMO JUU YA MAENDELEO KWA WOTE SI KWA WAO TU

    ReplyDelete
  13. Hongera Mh Rais Dr J.Kikwete, endelea kufanya maajabu ulimwenguni na mungu akujalie uzima, na hakika mungu atapokea sara zangu juu yako uishi maisha marefu zaidi.Na haters wazidi kudidimia.
    Michuzi Nicheki kwenye site yangu bruv,am asking for your comments please?

    ReplyDelete
  14. ano wa 7:39 am. PhD si degree kama nyingine, ina uzito wake mkubwa na hadhi kubwa. ni kutokana na hilo ndio maana inatolewa hata kwa heshima kwa watu waliofanyakazi za kutukuka kama JK. Kwa kutambulika kwa uzito, hadhi na heshima ya PhD ndio maana JK hajapewa BA au BSc au MA au MSc ya heshima. Ndugu usidanganye watu. Pili acha utumwa wa akili, Wazungu wanajiita DR na bila shaka huu mfumo wa elimu tunaofuata ni wa hao hao wazungu sasa una maana gani kusema wazungu hawajiiti DR. Uko katika walewale wapondaji wa mila na tamaduni za zetu na kuiga za kigeni.

    ReplyDelete
  15. ano wa 7:39 am. PhD si degree kama nyingine, ina uzito wake mkubwa na hadhi kubwa. ni kutokana na hilo ndio maana inatolewa hata kwa heshima kwa watu waliofanyakazi za kutukuka kama JK. Kwa kutambulika kwa uzito, hadhi na heshima ya PhD ndio maana JK hajapewa BA au BSc au MA au MSc ya heshima. Ndugu usidanganye watu. Pili acha utumwa wa akili, Wazungu wanajiita DR na bila shaka huu mfumo wa elimu tunaofuata ni wa hao hao wazungu sasa una maana gani kusema wazungu hawajiiti DR. Uko katika walewale wapondaji wa mila na tamaduni za zetu na kuiga za kigeni.

    ReplyDelete
  16. Wakenya wajanja sana ...hapa naona wanamroga Rais wetu kwa kizungu ili akubaliane na dili lao la EAC awe mlaini kupitisha mkataba tata wa EAC

    JK anabidi ashtuke mapema

    ReplyDelete
  17. watu kwa kupenda u-Dr??sijui dili?
    poa tu,,,aya maisha bongo ni mteremko kwa kwenda mbele
    afu kaenda pokelewa na misafara mireeeeefu gharama kodi ya m-Tz

    ReplyDelete
  18. Watanzania kwa UBISHI! sijapata kuona mwanawane. Sasa hapo mnabishaniana nini hata sikielewi, kama ni rahisi kupata hiyo Honorary PhD na haina thamani yoyote mbona nyie HAMJAPEWA? Eeh hebu siku nyingine punguzeni stress kuweni na roho nyeupe stress zitaondoka, jaribuni kuwa positive na kufurahia mafaninikio ya wenzenu na ya kwenu yatakuja, once you have positive thinking hayo mastress yote yataondoka na mambo yenu yatakuwa positive as well.

    Sijaona TANGAZO lolote la REDIO au TV ambalo JK amewatangazia watu wamuite Dr. Wala hajamlazimisha mtu Mweee! Mnakuwa kama wale walimu wa UDSM ambao wanataka ma Dr na Maprofesa wawe wao tu maana hicho kibano wanachowapa wanafunzi wao ili kuhakikisha idadi ya madr haiongezeki ni tafrani. Na pia usipowaita hao walimu wa UDSM na kwingineko Bongo kwa title zao basi jua lazima utafeli, umeacha kumwita Dr? Prof? Unamwita kwa jina lake utakiona cha moto!

    Nyie ambao mnaona kuwa hapaswi kupongezwa KAMA MNAWEZA PANDENI JUU MKAZIBE!

    ReplyDelete
  19. ushuzi mtupu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...