Meneja mradi wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Aggreko, Shaughn Tyreman akitoka nje ya lango la kuingia eneo la mradi huo baada ya kuamriwa na Kampuni ya Udalali ya Majembe ili ifunge eneo hilo, kufuatia idhini waliyopewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inayowadai kodi ya Sh bilioni 10.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezuia kwa kuweka makufuli katika lango la kampuni ya kufua umeme ya Aggreko Dar es Salaam jana, baada ya kuwapo taarifa inahamisha kinyemela mitambo yake na kuipeleka nje ya nchi, kwa lengo la kukwepa kulipa deni la Sh bilioni 10 inalodaiwa na mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka chanzo cha habari ndani ya TRA juzi na jana, zilidai kuwa Aggreko inadaiwa Sh 10,117,558,321 ikiwa ni deni la kodi ya miaka mitatu ya uzalishaji umeme nchini. TRA ilithibitisha Aggreko kudaiwa deni ingawa hawakuwa tayari kusema ni kiasi gani, kwa kuwa ni mkataba wa siri kati yake kampuni hiyo ambayo wanaitambua kama mlipakodi wao.

“Tangu wameingia hapa nchini hawa wawekezaji ambao waliitwa kutokana na dharura iliyolikumba taifa kipindi cha nyuma, hawajawahi kulipa kodi, na tumefanya nao mikutano bila mafanikio, tumewaletea taarifa za maandishi, hawajaonyesha kujibu,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Katika eneo la tukio jana, tafrani ilizuka wakati maofisa wa TRA pamoja na wa Kampuni ya Majembe Auction Mart, walipofika wakiwa katika magari ya kawaida na kuwaamuru walinzi wafungue mlango mkuu wa kuingia ilipo mitambo hiyo.

Kutokuelewana kulianza pale walipogundua kuwa ni maofisa wa TRA na wanahitaji Mkuu wa eneo ili waamuru wafanyakazi wake watoke ndani, kwani mtambo huo unafungwa hadi deni hilo litakapolipwa; ndipo walinzi walipotaka kuwatoa kwa nguvu maofisa na wanahabari, jambo lililozua zogo bila mafanikio ya kuwaondoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Get them all! Wamezidi sana mikampuni kama hii!

    ReplyDelete
  2. Another Travesty, I have said numerous time, and I am saying again, WE ARE OPEN UP FOR EXPLOITATION, we must understand that, THE GOVERNMENT should have come hard on these so called investors!

    This is not the first time it happen, not a single person held accountable 10billion plus thats a lot of money, it has been going on for three years, no one dare to come hard on them.

    The question is, Why they keep reaping us apart, I am not economists, but it doesnot make a sense, for any companies/investors comming onto our shore, and lied to us and make a huge exploitation on our back, I dont know how long these type of companies come over and do the sequel all over again, 10 years, I dont know. But it makes us upset of whats going on. It is UBELIEVABLE.

    When we gonna learn, I just want to know! GOVERNMENT should take full responsibilities, and come one, someone should join the ranks of Mbowe and sent to jail for these mess. TRA start smelling FISHY, I would start with them. I guess, they keep the accounts, aren't they??

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  3. Na dhani inabidi tumnyonge mwekezaji mmoja ndipo watajua WaTz hawana mchezo. Hapa watapelekwa mahakamani baadae dhamana baadae tuwafidie. Dawa watanzania tuanze kujichukulia sheria mkononi. tumtie mwekezaji kibiriti halafu hao waliowaruhusu kulimbikiza kodi kubwa hivyo nao wafuate. MUNGU IBARIKI TZ

    ReplyDelete
  4. Yani miaka mitatu mtu halipi kodi, whatever company af Tiaraeii mnaenda kazini kila siku na kurudi nyumbani...for God's sake when will these things end in bongoland? halafu kifua mbele eti mmemkamata mkwepa kodi kweli? haiingii akilini...

    ReplyDelete
  5. Na kweli, Mungu ibariki Tanzania. Kama ni hivi, kwa kweli Tanzania tutajitikia kitanzi wenyewe kwa wenyewe. Tunamkaribisha mgeni nyumbani, tunamwacha anafanya vitu vyake kwa mwaka mzima na sisi tuko nae pale nyumbani, au tumeenda kwenye kiti moto, na kujisahau? Jamani, huu ni upuuzi, huwezi kumweleza mtoto wa darasa la saba kwamba, mwekezaji wangu, au aliyekuja nyumbani anahamisha nguo zake kimya kimya....LOL...Wacha, Wewe mkurugenzi wa TRA, jiuzulu...wewe waziri wa fedha jiuzulu, wewe raisi wa nchi jiuzulu. Kwa kweli nasema hivi kwa sababu ni sawa na nyumbani, unamkaribisha mgeni anakula chakula chote na kile ulichowaandalia watoto wako, utakubali? Au tuseme, mgeni anaiba nyumbani kwako, alafu anamegemea kile kile alichokuibia na unamwambia asante. WAPI NA WAPI? Sisi watanzania tuliala, tukaendelea kulala lakini ilivyokia karne ya ishirini na moja, kila mmoja wetu ameamka, tumeamka, na tunataka ukweli. Tafadhali tupewe ukweli, na ukweli kabisa. Asante. Ni mimi, mwalimu, E, hapa marekani

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na wewe ndugu yangu. Tulilala na viongozi wetu wakafikiri bado tunaendelea kulala. Waache wajinga wale ujinga wao? Ni msemo uliokuwepo na viongozi hao wanafikiri bado sisi tumelala na bado ni sisi ni wajinga. Utajiri walio nao ni wetu sote sisi watanzania. Inabidi siku moja niwe raisi wa inji hii, na niwaambie wafanya mahesabu ya jinsi walivyoupata utajiri wao wa mabilioni ya madola, ambayo hata madona, oprah winfrey, ronaldo, ronabinho, na hata wale matajiri wa marekani hawana! Je mramba, mkapa, na mama nkapa, hizo pesa mmetuibia mifukoni kwetu halafu mnataka tuwaite matajiri? Tugawane basi kwa njia ya nyie kulipia ushuru ambao itabidi muuze nyumba zenu, magari yenu na ikibidi hata watoto wenu!!! Lol...Kali hii, si ndio. Rungu kwa rungu. Watanzania hatuwezi kuendelea kuibiwa namna hii bwana. Rais uko wapi? Waziri mkuu uko wapi? Na nyie viongozi wengine tuliowachagua mko wapi? Mmelala? Au mnataka impeachment ya bunge tukufu. Mzee Sitta, tubadilishe katiba nini, tuwafanyie hawa wenzetu impeachment wangali uongonzini? Wasalaam, Mpita njia!!

    ReplyDelete
  7. SIKUAMINI MACHO YANGU NA MASIKIO THT DAY!!!!!
    ila tutafika tuu siku na izi EPALISM zitashughulikiwa tu sijui na nani bt one day yes
    yan uyo mzungu avokua afoka na yule mtangazaji wa ITV Neema alipokua ajaribu kumhoji???kidogo nivunje screen
    nilisikitika sana
    BT PANA HARUFU NZITO YA NANIHII YA VIBOSILE
    YAN HAINGII AKILINI KABISA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...