KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain imeendeleza programu yake ya kusaidia jamii kwa kufadhili kituo cha watoto yatima cha SOS Children's Village kilichopo Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe, alitangaza Zain kudhamini nyumba namba tatu ya kituo hicho kwa mwaka mzima, na kwa kuanzia ilitoa udhamini wa sh. milioni 3 katika hafla ya chakula cha mchana juzi mchana Dar es Salaam, iliyoambatana na kutoa zawadi anuwai za Krismasi kwa watoto wa kituo hicho.
Tunu alisema hatua hiyo ya kusaidia watoto wasiojiweza, ni programu inayoendelezwa na Zain katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, na hiyo inadhihirisha Zain inavyowajali wasiojiweza, na akasema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
Mbali ya Tunu, katika hafla hiyo, Zain yenye mtandao katika nchi 23 barani Afrika na Mashariki ya Kati, pia iliwakilishwa na Meneja Mradi, Doris Kibassa. Mkuu wa kituo cha SOS Children's Village, Alex Lengejo aliishukuru Zain kwa ufadhili huo aliosema utakuwa ni kichocheo cha kuwapa malezi bora watoto wa kituo hicho wanaosoma shule ya awali.
Hivi karibuni, Zain ilishinda tuzo ya kuwa Kampuni Bora Inayoheshimika Afrika Mashariki na pia Zain Tanzania ilishinda nishani ya Kampuni Bora ya Mawasiliano ya simu Afrika Mashariki mwaka 2007.
Dada anaonekana anaroho ya huruma angalieni alivyokuwa busy kumlisha mtoto,safi sana ana sifa ya mke.Kwani sio wasichana wote wenye mioyo hiyo.Mungu akuzidishie!!
ReplyDelete