Basi la Tashriff T768ALW ambalo liliparamia lori la magogo (chini) katika eneo la Hale wilayani Muheza mkoani Tanga na kusababisha vifo vya abiria wake 27 na kujeruhi wengine 23 likiwa katika kituo cha Polisi Hale.
Lori la magogo T 594 APA ambalo liliparamiwa na basila Tashriff

Orodha ya majeruhi na majeruhi waliofariki wakiwa Hopitali Teule ya Muheza mkoani Tanga.

Salaam kaka Michu,
Napenda kuleta dukuduku langu kwa wadau wote wa blog yetu ya jamii ili tulijadili ktk kujenga kuhusu AJALI ZA BARABARANI BONGO.
Jamani, jamani kwa kweli tumechoka watu wanateketea imefikia steji sasa na tuseme ENOUGH IS ENOUGH sasa na sisi.
Yaani haijatimia hata week1 tangia basi la kampuni ya TASHRIFF liwafyeke abiria zaidi ya nusu waliokuwa wakisafiri (30)na wengine 29 kulazwa ktk hospital za muheza teule na Bombo tanga, huu ni msiba mkubwa sana UHAI NI KITU CHA THAMANI NAFUU MTU AKUIBIE HELA AU MADINI KULIKO AKUTOE ROHO YAKO.
Basi la kampuni hiihii wadau mkumbuke lilishawahi kupoteza maisha ya abiria (78) lilipofunikwa na maji meneo ya kibanda muheza tanga.
KITU GANI kifanyike wadau kuepuka vifo vya kizembe vya namna hii?dereva kaua kakimbia ni mhuni anakabidhiwa chombo kilichobeba roho za watu.
Kwa uzoefu wangu wa kuishi bongo miaka mingi naamini karibia nusu ya waendesha magari mijini hawana leseni na nusu ya waendesha vyombo wanaendesha wamelewa.
Ni kawaida kuwakuta watu wamepaki magari yao bar wanakunywa pombe kisha wanaendesha, jamani jamani tunauana jamani!!
HILI JESHI LA POLISI KITENGO CHA TRAFFIC utawakuta wote wana vitambi kwa rushwa na kutafutia watu leseni kwa njia za mazabe.
JK MAISHA BORA NI PAMOJA NA SHERIA KALI ZA BARABARANI KWANI ZINAHUSU UHAI AMBAO NI KITU CHA THAMANI KULIKO CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)....
Mungu Ibariki tanzania
Mungu Ibariki Afrika.

mdau wa kwasemgaya
safarini DENMARK mara1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Mbali ya kuwa na leseni nyingi za hewa, ambazo zinasababisha vifo vingi sana hapo nyumbani, naomba nizungumzie huo ubebaji magogo. 1m3 ya magogo ni kama 700kg!!! Yaani gogo lenye urefu wa mita 6 na diametre ya cm 42 kule juu lina tani moja nzima. Sasa jamani, mzigo huu tunaubeba juu ya platform iliyokingwa na vijitawi? Gogo hilo likianguka wakati gari liko speed, hao litakao wakuta hawatapona. Hivyo ningefurahi iwapo wahusika pamoja na kupenda rushwa zao, waweke sheria kuwa mitingo hiyo ya maroli ya magogo iwe ni ya chuma tu , na iwe either welded or screwed na sio kupachikwa tu.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. UKWELI NI KWAMBA NDUGU ZETU WANAKUFA KILA SIKU NA HII SERIKALI YETU IPO KAMA ALIVYOSEMA HAPO NDUGU YANGU KWAMBA SASA LESENI UNAIPATA UNA HAJA YA KUSOMEA WALA NINI SASA MUESHIMIWA JK TUTAFIKA KWELI,ANGALIA ASKARI WAKO WA BARABARANI JINSI WALIVYO WANENE NI RUSHWA TUU, JK BWANA TUNAKUOMBA MZEE MABADILIKO MZEE NILIKUWA NASHAURI HIVI KITU KILICHOKUWA KIBOVU BORA KIFUNGIWE TUU KULIKO KUSABABISHA MAAFA KWA NDUGU ZETU.MUESHIMIWA JK WEWE UNAPANDA NDEGE KWENYE SAFARI ZAKO LAKINI UNGEKUWA UNAPANDA MABASI HAYA KWA KIPINDI HIKI UNGEKUWA UNAFAHAMU KILA KITU JUU YA HAWA WADUDU (MADEREVA WA MABASI) KASIIII KASIIII, BANGE BANGEEE, POMBE POMBEEE, YANI NI BALAAAAAAA TUPU HAYA MIMI MWISHO WANGU HAPO.
    ROHO ZETU JAMANI MADEREVA MBONA HIVYO JAMANIIII.

    ReplyDelete
  3. AJALI VIONGOZI WANAZICHANGIA KWA MIPANGO MIBOVU,JUZI KWA BAHATI NILIPATA KUPITIA WEB MOJA INAITWA KAMA SIKOSEI DULLONET.ORG,HAPA NILIPATA BAHATI KUSIKIA TAARIFA YA HABARI KUTOKA KTK REDIO MOJA YA BONGO INAYOITWA RFA-HABARI,KWA VILE HAPA MKUU HII NDIO SITE YETU KUBWA YA WABONGO WOTE DUNIANI,TUNAKUWA HATUPATI HABARI KAMA HIZO ZINAKUWA ZINAZUNGUMZWA NA VIONGOZI, HAPA KWA BAHATI NILIPATA BAHATI YA KUMSIKIA KAMANDA WA POLISI WA DAR ANAEITWA SULEIMANI KOVU,ALIKUWEPO WAKATI HUO KTK KITU CHA MABASI YANAYOSAFIRI MIKOANI NA NJE YA NCHI, ALISEMA KUANZIA SASA WATAKUWA NA ZOEZI MAALUM LA KILA SIKU LA KUWADHIBITI MADEREVA KABLA YA KUANZA SAFARI ZAO,HAPO WATAWEZA KUGUNDUA KAMA,GARI NI MBOVU HAISTAHILI KUWAFANYA SAFARI,KAMA DEREVA NI AMELEWA,NA KADHALIKA WATAWEZA KUJUA PALE PALE HATUA ZA KUCHUKUA KABLA YA GARI KUONDOKA,NA WAMEWAPA ABIRIA NAFASI YA KUWADHIBITI MADEREVA WAKIWA SAFARINI KAMA DEREVA ANAENDESHA KWA GARI MWENDO WA KASI,AIDHA ABIRIA WAPIGE SIMU AU WATUME SMS KWA POLISI,

    HILI LA KUWA DEREVA AMELEWA,SIO KWANZA NI JIBU LA AJLI, KWANI MAGARI YANAYOONDOKA ASUBUHI VITUONI SIO LAZIMA DEREVA ALEWE WAKATI HUO WA ASUBUHI,MADEREVA WENGI HUANZA KULEWA NDANI YA SAFARI,AIDHA WANAPOANZA KUPATA MLO WAO WA MCHANA NJIANI,AU CHAI WAKIWA SAFARINI PALE WANAPOSIMAMA KWAAJILI YA MLO WAO, KWAHIO HATA KAMA DEREVA LIKUWA HAKULEA KULE KITUONI BASI ATAKWENDA KULEWA MBELE YA SAFARI,

    MBONA HUKU ULAYA MADEREVA WANAOCHUKUA ROHO NJINGI ZA WATU WAKATI MMOJA KAMA HAO MADEREVA WANAKUWA NA JUKUMU KUBWA NA KUWA HAWAFANYI UZEMBE KAMA HAO WA NYUMBANI AMBAO HUONA KAMA WAMEPAKIA VIFURUSHI TU NDANI YA GARI NA SIO BINADAMU,

    KAMA HAKUTOKUWA NA CONTROL YA KILA BAADA YA KILO MITA 75, AU 100 MBELE YA SAFARI NJIA ZOTE ZA MIKOANI YA POLISI KUKAA HAPO NA KUANZA KUWAPIMA MADEREVA WALIOLEWA WAKIWA KTK SAFARI, BASI KILA SIKU MADEREVA WATALEWA NA KUUA WATU,

    KAMA SERIKALI HAWAKUWEKA KIWANGO CHA MADEREVA KUPUNGUZA MWENDO WA KASI BASI KILA SIKU WATU WATAKUFA KWA AJALI NA HAITOPATIKA SOLUTION YOYOTE,

    UNAJUA SERIOUS HII AJALI YA MAGARI SASA IMEKUWA IKITUTISHA SISI HUKU TULIOPO NJE NA KTK UCHUNGUZI NI KUWA MAGARI YANAUWA WATU MARA 10 ZAIDI YA UKIMWI HAPO NCHINI,

    HII NI SERIOUS CASE KWA SERIKALI KUWEZA KUIFANYIA KAI KWA KINA, HII NI ZAIDI YA UFISADI,KWANI UFISADI UNAIBA SOME MONEY LAKINI HAWA JAMAA WANAUA WATUKWA MAKUSUDI KABISA,

    KAMA HAKUKUWEKWA KASI YA KUENDESHA MAGARI KILOMITA 80 KWA SAA KWA MABASI YOTE YANAYOKWENDA MIKOANI,NA KUFANYA CONTROL KWA MUDA WA KUFIKA VITUONI AMBAVYO VITAKUW NI KILA KTK MASAFA YA KILOMITA 100, AMBAPO ASKARI POLISI WATAKUWA WAKIANGALIA NA KUPOKEA KUTOKA VITUO VILIVYOTOKA MAGARI AMBAYO YATAPITA HAPO KUKAGULIWA MUDA WALIOFIKA,NA KUANGALIA KAMA HAWAKULEWA MADEREVA BASI MADEREVA WATAENDELEA KUUA TU,KWA TAMAA ZAO ZA KUKIMBIA KUFIKA HARAKA,

    NI BORA KUCHELEWA LAKINI UFIKE SALAMA,KARIBUNI TULISIKIA GARI LIMEUA FAMILIA MOJA YA WATU 15 KAMA SIKOSEI, HUU NI MSIBA MKUBWA ANA KWA FAMILIA MOJA KUONDOKEWA NA WATU KAMA HAO AMBAO WALIKUWA WAKIENDA HARUSINI,

    MAGARI YAPATE CONTROL KILA KTK KILOMITA 100, NAKAMA WAMEZIDISHA NA KUWAHI HAPO KITUONI HATA KAMA NI DAKIKA 5 BASI WANYANG'ANYWE LESENI NA WAFUNGULIWE MASHTAKA,YA KUTAKA KUUA WATU KWA MAKUSUDI,

    HUKU EUROPER KILA BASI LINAPITA KTK KITUA ILICHOPANGIWA KUPITA KUCHUKUA ABIRIA KWA MUDA WAKE MAALUMU, AMBAPO MWENDO ULIOPANGWA KUKIMBIZA GARI NA KUFIKA HAPO KITUONI UNAKUWA NI ULE ULE AMBAPO KILA ABIRIA ANAJUA GARI ANALOTAKA KUPANDA LITAFIKA HAPO MUDA GANI,HATA INAPUNGUZA USUMBUFU WA MTU KUFIKA HAPO NA KUSUBIRI GARI KWA MASAA KADHAA AMBAPO HATA HAELEWI NI GARI GANI LITAPITA NA SAA NGAPI,

    NAOMBA CHUKULIWE SERIOUS HILI SUALA LA MADEREVA, KWA IMEKUWA NI TOO MUCH WANAVYO UWA WATU KWA MAKUSUDI ETI KWA KUSINGIZIA WANAWAHI KUFIKA,AU WANATAKA KUWAHI ABIRIA MBELE YA SAFARI KABLA GARI NYINGINE HAIKUPIT KUWACHUKUA,

    HIZI NI TAMAA ZA KIJINGA, KAMA MASKINI NI MASIKINI TU HATA KAMA UKIWAHI KUCHUKUA HAO ABIRIA MBELE AU UKWAHI KUFIKA HUKO KITUO UNACHOTAKA,

    WEWE KAMA NI DEREVA SI UNAFANYA KAZI? NA UNAPATA MSHAHARA? KUWAHI, NA KUTOKUWA SIO LAZIMA, UNATAKAW UFIKE SALAMA, SIDHANI KAMA KUNA MATAJIRI WA MAGARI WANTAKA KUSIKIA KWA GARI LAO LIMEPATA AJALI,LIMEHARIBIKA LOTE NA HALIFAI TENA,PIA LIMEUA,HATA KAMA NI TAJIRI KIASI GANI HII INAKUWA NI REPORTE MBAYA KWAKE, KWANINI WASICHUKUE TARATIBU ZA KUWATAKA MADEREVA WAO KUTUMIK IPASAVYO NA KUKUBALIA NAO NAKUWATAKA WASIONE WAKIWAHI NDIO WATAPATA MSHAHARA MKUBWA,

    KAMA WEWE UNAESOMA NI DEREVA, BASI "WACHA TAMAA ZAKO ZA KIJINGA, GARI LITAKUUA, NA KUUA WATU WENGINE KWA TAMAA ZAKO, HUTOWEZA KUWA TAJIRI HATA SIKU MOJA ETI KWA AJILI UNAENDESHA MBIO, NA KAMA UNATAKA SIFA YA WATU KUSEMA ETI WEWE UNAENDESHA MBIO KULIKO DEREVA YEYETO BASI UJUE GARI LITAKUUA KWA KUTAKA SIFA ZAKO, AIDHA DINI YOYOTE ULIYONAYO, KAMA UKIUA KWA MAKUSUDI NA KAMA IKIKUWA UNAO UWEZO KUEPUKA KUUA NA HUKUFANYA HIVYO,NA UMEKUFA NA KUUA WATU WENGINE, BASI UJUE HII DUNIA SIO CHOCHOTE,MBELE YA SAFARI UTAKWENDA KUJIBU KWA NINI UMEUA NA UJUE ADHABU YAKO HUKO SIO ULE UTAJIRI ULIOTAKA HAPA DUNIANI BALI MAKAAZI YAKO YA MILELE ITAKUWA NI MOTONI, KWAAJILI YA SIFA ZAKO"

    ENOUGH IS ENOUGH,

    MDAU, kutoka
    GERMANY

    ReplyDelete
  4. barabara ndogo ,madereva speed kubwa na traffic hawafanyi kazi zao barabarani zaidi ya kula rushwa.

    ReplyDelete
  5. inasikitisha sana, uzembe wa madereva ni sababau mojawapo lakini,kuna mambo ya ushirikina pia wamiliki kutoa sadaka ya damu9za marehemu) kwa spirits/mapepo ili kupata utajiri zaidi. Maombi ni muhimu jamani. kila wakati, hasa unaposafiri! This is very true.

    ReplyDelete
  6. Hii hali inasikitisha kwa sababu serikali na idara ya traffic imenyamaza kwa sababu binadamu hawathaminiwi tena. Siajabu pia utakuta kwamba basi lenyewe lilikuwa linatembea bila bima"INSURANCE", dereva amelewa akiwa kazini "DWI", dereva kwenda mwendo wa kasi bila sababu "DRIVING FASTER THAN CONDITION ALLOWS", gari halikuwahi kukaguliwa kabla halijaanza safari "PRE-TRIP INSPECTION", dereva hajapumzika "FATIGUE". Mambo yeto hayo yanasababiha ajali jiulize hatua gani Traffic inachukua mtu akipatikana na kosa lolote hakuna. Look in America anybody who holds a CDL "COMMERCIAL DRIVERS LICENSE" any two moving violation "tickets" in 3 yrs you"re license is suspended. That stops drivers in doing anything stupid, because you will loose your job.

    ReplyDelete
  7. eeeeh bwana majina karib yote ni ya kislam,hii inamanisha waislam wengi zaid TZ kuliko wa kristo?

    ReplyDelete
  8. Tatizo letu watanzania tunaweka dharau hata kwenye mambo ya hatari.Hakuna hata mmoja anayejali uhakika wa maisha yetu wenyewe.
    Mabasi haya yakikiuka sheria za usalama barabarani na kwenda mwendo wa kasi, sisi tunashangilia na kumsifia dereva kuwa anaweza kuendesha sana. Hakuna ushujaa kwenye hivi vyombo vya moto. Inabidi watu kama hao watambuliwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Polisi wa usalama barabara nao wanaweka maslahi binafsi mbele badala ya kufanya kazi inayowapatia kipato halali,ingawa ni kidogo.Mtindo huu umetuganda kama ugonjwa wa ukimwi! Hao viongozi wetu nao ndiyo kabisa, hakuna kitu, hamna hata mmoja mwenye mmtazamo wa mbele wa nini kifanyike ili kukomesha hali hii.Ni kama vile wote hawjaenda shule vile.Tunaweza kumchukua mtoto wa darasa la sabab na kumuweka awe kiongozi wetu kwenye hzi kazi na hakuna kitakachokuwa tofauti,kweli nawaambieni.
    Tutamalizika sana tukifikiria kuwa siku moja tutaamka asubuhi na kuona hizo ajali hazitokei tena bila kuchukua hatua sasa hivi.
    Viongozi wakishakaa kwenye mashangingi yenye viyoyozi,kwa hisani ya pesa zetu za kodi,hawana tena habari na jinsi gani sisi tunasafiri na kuumia au kufariki humo njiani,wao wameshapata.
    Wanashindwa kabisa kufikiria.Kwa nini ajali nyingi zinatokea maoneo hayohayo tu ? Ngoja niwasaidie kidogo.
    Sababu ni kuwa, sehemu hizo msongomano wa magari karibu yaendeyo sehemu kubwa ya Tanzania hupitia ! Inabidi sehemu hizo barabara zipanuliwe, ziwe double road, ajali zitapungua. Sasa hivi njia hizo ni nyembamba sana kwa idadi ya magari yanayopita hapo ?
    Those machines are human operated,and humans do make mistakes sometimes.They tend to act and react imetionally most of the time. If we don`t accomodate ourselves in a organised and controlled manner, are still going to perish like chicken or kuku in a chicken farm !! Tome to get these readers, either back to school, or out of their offices,NOW !
    Barabara ngapi zingeboreshwa kwa fedha zetu wenyewe badala ya kuagiza VX 100 na zaidi ? Au tunataka wazungu waje ndiyo watuambie hayo yote ? Hatuwezi kufikiria sisi wenyewe ? Au ni ubinafsi umetujaa ?
    Inaumiza na kutia uchungu kupita kiasi. Hasa pale inapokuwakuta watu ambao hawana uwezo wa kufanya chochote kile, zaidi ya kulia na kusikitika. Sina uhakika kama wanalipwa na makampuni ya bima au na serikali.
    Ni mengi ya kuandika,lakini muda umeniishia, got to GO !!

    ReplyDelete
  9. Bw Michuzi,
    Katika post yangu hii:http://drfaustine.blogspot.com/2009/01/motor-traffic-accidents-possible.html#links, nimejaribu kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kupunguza ajali nchini Tanzania.
    Nawasilisha
    Mdau
    Faustine

    ReplyDelete
  10. Michuzi asant kwa kututembelea BLOGG zetu

    ReplyDelete
  11. HABARI YA WAISLAMU WENGI SANA KULIKO WAKRISTU INAKUJAJE HAPA KWENYE HABARI YA VIFO VYA NDUGU ZETU HAWA!!! KWANI WAKIWA WENGI NDI NINI? NI DNI KAMA DINI ZINGINE TU WALA HAINA TIJA. NASHANGAA SANA, HUO NI UDINI AMBAO TULIUPIGA VITA NA BADO TUNAUPIGA VITA, HUO NI MKOA WA TANGA WENYEJI WENGI NI WAISLAMU, NI MKOA ULIOKO PWANI AMBAKO WAARABU AMBAO WENGI WAO NI WAISLAMU WALIFIKIA KUFANYA BISHARA IKIWEMO YA WATUMWA. HIYO AJALI INGETOKEA MBEYA MAJINA MENGI YANGEKUWA YA WATU WANAMUABUDU YESU. ACHANENI NA UDINI HAUNA FAIDA YOYOTE. TUWAPE POLE HAWA NDUGU ZETU WALIOUMIA NA KUFIWA, MUNGU AWAPATIE NGUVU ZA KUPONA HARAKA NA WALIOFIWA KUVUMULIA, HIYO YOTE NI KAZI YA MUNGU YEYE NDIE MTOWA NA MTWAA

    ReplyDelete
  12. Wapinzani nao ebu waache kupigania mafisadi kwa muda mchache tu wajaribu nao kuzigeukia SHERIA ZA BARABARANI zifanyiwe marekebisho au zitungwe sheria nyingine zitakazosaidia sio hizi za sasa DON`T DRINK AND DRIVE" labda zitasaidia maana hizi naona hazifatwi.JK SIJAMSIKIA AKITOA TATHMINI WAMEDHIBITIJE AJALI AU NI ROHO NGAPI ZISHAPOTEA NA MAJERUHI KIBAO KTK HOSPITAL ZENYE UHABA WA DAWA NA WAHUDUMU WASIOPATIWA MALIPO YAO SAWASA.Ni mwendo wa shida juu ya shida maumivu juu ya maumivu bongo.JE NI WANGAPI WAMEPATA KUFUNGWA KWA SABABISHA AJALI??KAMA SIO WOTE KUISHILIA KUWADAKISHA KITU KIDOGO MAHAKIMU TU NA KUENDELEA KUTEKETEZA ROHO MAENEO MENGINE KWA LESENI NYINGINE FAKE.MWISHO..naamini kwa jinsi JK anavyozurura zurura ovyo nje ya nchi kama angekuwa ndio anasafiri kwa haya mabasi ya mikoani simuombei mabaya rais wangu ILA TUNGESHAMZIKA ZAMANI TU.NI BAHATI KUBWA MNO BONGO KUSAFIRI MARA 20 ZOTE SALAMA

    ReplyDelete
  13. we unaeanziasha udini ni mjinga kabisa,hujui kwamba wakristo wengi hawana shida wanamagari yao,na wanapanda ndege kwa sana tu .michuzi usinibanie ili huyu jamaa mdini akome umbeya wake hapa,eti oooh waislamu wengi akome.

    ReplyDelete
  14. Inasikitisha sana kuwa hizi ajali za kizembe zinazidi kutokea pasi na wahusika kuchukua hatua za kupunguza ajali.kwanza inakuwaje ni baadhi ya police(traffic) ndio wanamamlaka ya kuangalia usalama wa magari?nadhani ni kazi ya police wote kuwa wanaangalia usalama wa raia na magari.kama hilo lori hapo pichani linatakiwa kufungiwa na dereva kushitakiwa maana pia sio salama, but no body care.

    ReplyDelete
  15. Waige mfano wa rubani alieokoa maisha ya watu 154 kwa kutua kwenye mto Newyork. Mbali na hayo alikuwa wa mwisho kutoka kwenye ndege baada ya kuhakikisha abiria wote wametoka salama. Angekuwa mwingine angekuwa wa kwanza kujiokoa. Ukiwa rubani, dereva fikiria abiria wako kwanza. Kama huna roho hiyo basi utakuwa unafanya kazi kwa kizembe. Hao unaowaendesha siyo magogo ni watu wenye roho zao. Maisha yao yako mikononi mwako. Dereva jaribu kuendesha kwa uangalifu,acha kunywa bia kabla ya kuendesha, acha kuongea na simu unapokuwa kwenye usukani, acha kuongea na abiria ukiwa unaendesha,serikali iunde kamati ya kuchunguza hizi ajali. Watu wasipewe leseni ovyo. siyo kila mwenye gari yuko barabarani. Faini ya milioni moja itolewe kwa wanaoendesha bila leseni, bima, walevi . Serikali itengeneze barabara ziwe commuter friendly. Ndiyo hayo tu. Poleni ndugu wafiwa.

    ReplyDelete
  16. Hicho ki taarifa chenyewe cha vifo na majeruhi, sijui ndio ki press release hicho kimetoka hapa hospitali kuu Tanga au kimekuwa put together na konda wa basi???

    Kile kitaarifa tu kinakuonyesha nchi ni ya watu illiterate jamani.

    Hawawezi ku spell hata jina la basi, achilia mbali neno "discharge."

    Lakini waliponimaliza ni jinsi walim describe majeruhi namba 18!

    ReplyDelete
  17. sio udini au ubaguzi au waislam wengi ni masikini hawapandi ndege umekosea ndugu yangu waislamu ndo matajari zaidi TZ raisi wako mwenyewe ni muislamu,

    NI KWELI DINI YA KISLAMU INAKUWA KWA KASI MNOOOOO.NA NINADHANI KWA HIVI SASA WAISLAMU NI WENGI ZAIDI TZ.
    shukran

    ReplyDelete
  18. Swala kubwa ni sisi sote kubadilika na kuheshimu taratibu na sheria mbali mbali zilizopo. Madereva wengi wamekuwa hawajali maisha ya watu na taratibu zilizopo. Jamani hata traffic polisi wangekuwa wangapi, bado swala ni watu kuwa wastaarabu. Nchi za wenzetu wanaheshimu taratibu, kama taa nyekundu imewaka manake ni kusimama na sio kuangalia kushoto na kulia kama kuna gari kama wafanyavyo ndugu zangu madereva wa Bongo.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  19. Kaka michuzi nipatie mda na mimi nitoe dukuduku langu kuhusu haya mauaji ambayo asilimia 100 serikali inachangia.

    Kuna baadhi ya watu huuliza kwa nini kila kitu tulalamikie serikali??? Jibu ni simple, mtoto akikosa mashitaka hupelekewa jirani??? Jibu hapana. Mashitaka yanaenda kwa wazazi. Sasa sisi kama wananchi tuna haki yakila kibaya tulalamikie serikali. Na ni wajibu wao kurekibisha hili. Mbaya kila sheria inayotungwa kwa ajili ya kurekebisha inakua chanzo kipya cha kuongeza rushwa je tufanye nini???

    hata sijui tuseme sisi waafrika tuna lana ama?? hata sijui. Ajali za namna hizo kwenye nchi za wenzetu nje ya bara la afrika ni nadra na maajabu. Kwetu hususan tanzania kwa mwaka mara hata kumi mpaka imekua jambo la kawaida. Swali TUFANYE NINI??? na kila tunachoshauri ni ongezeko la rushwa??

    Kazi ya Udereva wa mabasi kwa nchi zilizoendelea ni profeshion kama kazi ya upolisi ama ya uwakili.Hapa tanzania hata mvuta bangi na mlevi pia ni dereva wa mabasi. MATRAFIKI wanawajua vyema hawa wahuni liakini wameweka rushwa mbele.

    Nimesafiri sana na mabasi haya mwendo wanaokwendanao ni hatari na utashangaa abiria wenyewe wanashadidia. Sasa ajali za namna hii alaumiwe nani???

    Lawama langu kwa serikali ni kwamba hakuna elimu za kutosha hasa kwenye vipindi vya televisheni kwa wananchi kuelewa madhara ya dereva aliolewa na mvuta bangi na madawa mengine yanaweza sababisha nini. Hili wanachi wangelielewa vizuri nahisi wangewasaidia hata hao matrafiki kuwaumbua. Lakini hilo pia gumu utakuta ofisi ya raisi iko tayari kumlipia Maximo mahela kibao kuelemisha wananchi utasikia hiyo nigharama. SASA tufanye nini.Tukubali tu.Muuaji si dereva ila ni serikali hili tulielewe.

    ReplyDelete
  20. annon apo juu hahaaaaaa
    ni kweli ni ki-press release cha nurse attendant wa Tnaga hospital
    discharg,namba 18-chaga,tashirif ata plate number ya basi hakuna kwani yako mengi tuuu,
    ki-inglish bwana???unapokilazimisha
    AFU WADINI WOTE JEHOVAH AWAREHEMU KUWA MATAJIRI,WENGI,WACHACHE nk sii tiketi ya kufika Mbinguni,waweza kukomaa kiivo na bado tukakuacha,dini yako wewe ni za kijadi walizokuwanazo wazee wetu sio dini za kudhungu na kiarabu khaaaaaaa simple brai tu can help yu,tunaomboleza apa
    grow up yu hypocrit people

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...