TIMU YA TAIFA YA BARA KILIMANJARO STARS IMEIFUNGA KARUME HEROES YA ZENJI BAO 2-1 KATIKA MCHEZO WAO WA KOMBE LA CHALENJI HUKO KAMPALA, NA MPIRA UMEKWISHA DAKIKA 3 ZILIZOPITA
Home
Unlabelled
BARA YAIFUNGA ZENJI 2-1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
asalam alaikum bwana michuzi,
ReplyDeletebwana michuzi wanapo pata taifa stars unatoa habari mbio mbio lakiini wanapo fungwa mbona hutoi jeee huo ndio uwana michezo uliokua nao
karume heroes? majina yote ya kuipa timu yetu ya taifa tumeita karume heroes!?
ReplyDeleteMbona matokea ya wasomali kutuburuza bila aibu hayakuwekwa hapo?ati tunakwenda Ivory Coast, sijui kufanya nini...wabongo tusikubali 'foreign currency' yetu itumike ovyo kwani ukweli ni kwamba sisi ni wasindikizaji tuu!!
ReplyDeleteHAKUNA KOCHA STARS TUNA TEKNISHENI BWANA MAXIMO BAHATI MBAYA KATULISHA LIMBWATA.HATA ZENJI 2-1?
ReplyDeleteMDAU KISIJU.
walipiga kilele sana, oh tumefungwa na Somali timu isiyo na serikali, sasa wanasemaji hao
ReplyDeletewa-Pemba?
kisiju naingia.
ReplyDeletenaanza kwa kuipongeza timu yetu kwa kubahatisha tena.je ile homa ama uchovu waliokua nao kabla ya mechi na somalia gafla imekwisha? yaani FATIGUE.wachezaji hupata FATIGUE wakicheza mechi nyingi kubwa kwa mfulilizo. mechi hizi zote kulikua na gapu. halafu wachezaji wakaachiwa kwa mda waende majumabani kupumzika.. alafu naweka sawa kiporo nilichobakiza.tuna msifia nini MAXIMO.? kucheza mechi 20 kushinda 13 kufungwa 7 ni maendeleo? maximo an hasira zisizoeleweka. kwanza kwa kaseja eti alimcheka IVO kufungwa magoli ya kijinga. kunaubaya gani? mbona lehman na almunia walikua wakichekana na WENGER aliona ni part tu ya kuhamasishana?? ama anelka kufunga goli benchi zima la Chelsea walishangilia kasoro DROGBA mbona si ishu?? halafu kumuacha IVO kwenye kampeni hii eti hajui maendeleo yake je ya Dani Mrwanda alijuaje progress yake??? kuna mdau ana ndoto ya wachezaji wetu kuchezea soka ulaya!!kaka ndoto bila MIKAKATI ni ziro.hata kocha wa zenji kamshinda MAXIMO timu yake ina wachezaji wengi wako kwenye age avarage ya miaka23. Jamani tusifagilie ujinga. tuangalie ukweli wa mambo. watanzania tumeaidiwa na uongozi mpya wa TFF timu yetu itapelekwa ulaya kujiuza i hope hatutaenda cheza na timu za mitaani kama tulivyoenda denmark na Uswiss.tusisahau tulienda BRAZIL kwa miezi mitatu tukabakia kuogelea tu. kama ishu bahari hata KISIJU iko.tulienda brazil kujifunza nini??
Waosha vinjwa midomo yenu itafungwa tu nyie subirini. Na wewe ambaye unasema hayakuwekwa matokea na somalia sijaelewa kama wewe ni mgonjwa au unahitaji msaada wa kuwekewa links.
ReplyDeleteBonyeza hapa.
http://issamichuzi.blogspot.com/2009/01/taifa-stars-yalala-kwa-somalia-0-1.html#comments
Watu mnaanza kujifunza mpira ukubwani. Wewe unayeshangaa 2-1 hebu niambie mara ya mwisho tuliwafunga Zenji lini. Kila tukikutana nao huwa wanatufunga.
ReplyDeleteKina Kisiju wanapokuwa wengi kwenye soka letu tusitegemee maendeleo yoyote yale zaidi ya kuendekeza historia.
ReplyDeleteKila siku Kisiju unaambiwa kuwa kuandaa timu imara ya taifa inahitajika miaka mingi sio hii mitatu ambayo Maximo amekuwepo hapa nchini, kila siku unaambiwa kitu kile kile lakini sijui tatizo ni upeo wako au asili yako ya kuendekeza ubishi wa kwenye vijiwe vya kahawa.
Wenzetu walikuwa very serious na soka la vijana ndio maana leo timu zao za taifa ziko juu sana, sisi tulikuwa na tunaendelea kuwaendekeza watu kama wewe Kisiju ndio maana bado soka letu liko chini.
Kisiju jitahidi sana kuzifuatilia historia za timu za taifa za mataifa kama Tunisia, Misri, Afrika ya Kusini na utagundua kuwa misingi ya yao ni timu imara za vijana, Kisiju narudi kukueleza kitu ambacho watu wamejitahidi kukueleza , haiwezekani uunde timu imara ya taifa ya wakubwa bila kuwa na timu imara za vijana, isingewezekana eti Maximo aje halafu eti ndani ya miezi sita awe ametengeneza timu imara ya taifa, kwa kuwatumia wachezaji gani? hawa akina Kaseja , Costa na Mwaikimba?, timu ya taifa ya Angola ya sasa hivi ilianza kuandaliwa miaka zaidi ya kumi iliyopita, timu ya Cameroon tuliyocheza nayo mwaka jana ina wachezaji ambao wameshakaa pamoja kwa miaka kumi, mfano ni Eto`o na Rigobert Song ambao walicheza pamoja world cup ya 1998, jiulize miaka kumi iliyopita hawa akina Said Maulidi,Juma Kaseja ,Abdi Kassim na Mecky Mexime walikuwa wapi na walikuwa kweli wanafanana na wachezaji wa timu ya taifa?.
Kisiju unaendekeza chuki za kijinga kwa Maximo lakini Maximo ni mtu wa kupita tu, anytime anaweza akatuachia huu mzigo wa kuifundisha timu ya taifa , kumbuka kuwa heshima hainunuliwi , wewe usiyeujua mpira unaweza usielewe kabisa kitu gani anachokifanya lakini sisi ambao hatuongozwi na siasa za akina Kaseja na Mapunda hatutaacha kumpa heshima yake.
Kisiju unaona wachezaji wetu kwenda ulaya ni kitu cha ajabu!. mbona wakenya na hata wanyarwanda wanacheza kwenye ligi bora za ulaya!, timu zetu zimejaa watu kama wewe sasa zitaweza vipi kutimiza mipango ya kimaendeleo?
Kucheza mechi 20 na kushinda 13 ni maendeleo makubwa sana , umeshasahau kwamba tulikuwa tunafungwa na kenya goli 5-0 tena hapa hapa Tanzania, tulishawahi kucheza mechi zaidi ya saba za kimataifa na tukafungwa mechi zote hizo bila hata kufunga goli la offside!, Kisiju hukuwahi hata siku moja kuwaponda makocha wa wakati huo, kama wewe sio mnafiki ni nani? tukuiteje?, leo hii timu yetu imecheza mechi tano na ikashinda zote lakini kufungwa na Somalia tayari imeshakuwa nongwa!!, badilika , unavyozidi kutoa maoni ya kitoto ndivyo watu wanavyozidi kukushusha thamani.
Kisiju unaendekeza ubishi wa mitaani lakini unapaswa kufahamu kuwa timu imara ya taifa haifanani kabisa na kitendo cha kununua maembe njiani, inahitajika miaka mingi kuweza kutengeneza timu imara ya taifa,tukiyaendekeza mawazo na fikra za watu kama Kisiju basi kila siku tutakuwa tunaajiri makocha wapya na matokeo yatakuwa mabovu , mfano ni simba sports club , inaajiri makocha kila siku kumbe tatizo sio makocha bali ni watu wenye fikra na upeo mdogo kama Kisiju.
kisiju nae bwana,uwanjani kwenyewe hata sijui kama unalipa ticket wewe kihalali,na mpira huujui ongelea ndoma minanda na mnichiriku huko
ReplyDeleteFA CUP ya Uingereza inashindanisha timu mchanganyiko toka premier league hadi daraja la nne.
ReplyDeleteNdio hutokea timu kama Barnsley ya daraja la chini kuitoa Chelsea ktk FA CUP, na timu nyingi zilizo juu ktk premier league hutolewa kamasi au hata kufungwa na timu za madaraja ya chini.
Ni Tanzania ambako timu kama Yanga na Simba ambazo hazijashiriki ktk mashindano rasmi yanayoshirikisha timu za daraja la pili, tatu au nne. Mfano Simba/Yanga waombe mechi na Mbagala Market(African Lyon)tuone kama watashinda kirahisi.
TFF ianzishe mashindano ya timu za madaraja mchanganyiko zilizo juu ktk madaraja yao ili tutumie mashindano hayo kuona wachezaji ambao ni bora lakini kwa bahati mbaya hawajapenya kati ligi kuu.
kisiju naingia kwa mara nyingine tena.
ReplyDeletemwanzo naanza na mdau anaesema nimejifunza mpira ukubwani kwa kusema hakumbuki lini tuliwafunga wa zenji. swali kama tunahangaika kuwafunga wa zenji kwa nini inpokuja selection ya timu ya taifa tuna chukua wawili tu? je ina maana katika timu nzima ni wapemba wawili tu ndio wanaojua mpira na kutuhangaish??? ni ubaguzi huo. kama tuna kocha wa kigeni matabaka ya aina hii anatakiwa ayafungie macho likini sio MAXIMO!!Ali Bushri hana usemi anaburuzwa tu. Tunaelewa hilo.
kuna mdau mwingine ameshikilia kua mimi ni mtu nisietaka maendekeo na sijui historia.!! inaelekea historia haijui yeye alikua wapi kabla raisi kuingia uwanjani na kuonyesha ushabiki na vibupa kujipendekeza kwa kuisapoti timu?? kama historia na kujenga timu tunajua leo baada ya MAXIMO kuja? 1980 timu ilivyoqualify kwenye African Cup ya kweli chini ya Bendera hatukulijua hilo? baada ya kurudi alisisitizia umuhimu wa kuendeleza vijana. Nani alijali?Ama kwa sababu alikua Mzawa? Tuacheni akili za kitumwa hizo..
kama unajua historia usiongee Akina Kaseja, mwaikimba na ivo. Haya ni magarasa tu kama yale yaliokua kwenye timu sasa ivi. huwezi linganisha na talents kama zile za akina Method Mogela,Masha,Masatu,Nteze,Lunyamila,Ali Bushiri, Idi pazi,Mohamed SAlum TALL,amour aziz, inocent haule, zamoyoni mogela,China,Gagarino,
mwanamtwa kiwelo mchunga bakari,,ally maumba, yasini napili..listi inaweza kuendelea.Je serikali na FAT yao walikua wapi? walijua kula viingilio vya Simba na Yanga tu.Tukubalini hii timu ya sasa ni magarasa tu. Ila shinikizo la wafadhili na ahadi za mamilioni hata mimi nawezajiua ndugu.
Kua na wachezaji ULAYA ni ishu ndugu. mbona upeo wako mdogo. hujui kama kua na mchezaji mmoja tu ana weza litangaza taifa kuliko mahela yanayotoka wizara ya utalii??ina muacha raisi atuambie ukitaka kula lazima uliwe bungeni. si fezea hii ndugu??Si unaona upeo wenu huo, alipita Nonda hapa akawa hafai yanga sasa yuko mamtoni anapokea kuliko mshahara wa meneja wa benki mia hapa nchini. Usitoe mifano ya klabu hapa, si mahala pake. ushaona mwili unaenda bila ya kichwa? na kama ukienda basi itakua majabu.kama TFF haina mwelekeo usitegemee vilabu vitakua na mwelekeo.Tujiulize TFF ina mwelekeo gani wa kuendeleza soka hapa nchini? subiria utaona maana nahisi upeo wako ni mdogo sana. Swali ndugu 1994 si tulipeleka wachezaji Ureno matokeo unayajua?? tamaa za viongozi si wa vilabu bali wa TFF ya wakati huo yaani FAT. Najua hulijui maana ushabiki wako ulianza raisi alipoingia uwanjani na kuja kwa MAXIMO.
Unashangaa timu ya taifa ya wakati huo ilikua inafungwa 5-0 na kenya sababu ulikua unaijua? Wachezaji walikua na njaa, wafazili wawili. uchungu wangu ningejieleza wapi na kaka michuzi alikua hajatuokoa??
MDAU WA BWENI NAMUUNGA MKONO MDAU WA KISIJU KWA VISHINDO.
ReplyDeleteNILIKUA NAKUZARAU KUMBE UPEO NA UCHUNGU WAKO NI MKUBWA. HONGERA SANA KWA HILO. ILA KUNA MAMBO LAZIMA UKUBALANE NAYO KAMA YALE YA NYUMBA BILA MSINGI IMARA HAIWEZI KUSIMAMA VIZURI.
TIMU YETU CHANGA JAPO IMEJAA VIBABU. ILITAKIWA NUSU YA MABINGWA WA COCOA COLA WAWEMO KWENYE TIMU HII ILI WAWEZE KUPATA UZOEFU.
TINOKO ANAITAJI MSAADA KWENYE KUIBUA VIJANA. NAHISI TFF ITAFUTE KOCHA WA BEI RAHISI TOKA ULAYA ILI VIJANA WAKIKUA WAWE NA AKILI YA KIBRAZILI NA NGUVU ZA ULAYA.KOMBINESHENI HII ITAKUA NOMA. AMA SIVYO KAKA MICHUZI?
Kisiju naona unajikanyagakanyaga tu..unasema hakuna mwili bila kichwa!!..bado unaendekeza desturi zile zile za kibongo, desturi za kupenda kulaumu ovyo.
ReplyDeleteTimu zetu tunazoziita kubwa hazina hata viwanja vya kufanyia mazoezi, unataka TFF wawajengee viwanja vya kufanyia mazoezi!!?..timu zetu mpaka sasa hivi bado zinaendeshwa kwa kutegemea pesa za wafanyabiashara wachache lakini zina mamilioni ya mashabiki nchi nzima..unataka TFF wawasaidie kupata mbinu za kuweza kupata mtaji?.
Mpaka leo hii bado timu zetu zinaendeshwa kihuni..unataka TFF waingilie na kusimamia shughuli za uongozi wa kila siku ndani ya vilabu? halafu shughuli za TFF atazifanya nani?.
Unajaribu kuiponda TFF lakini jiulize huyu Maximo ambaye wewe unamponda , kama angekuwa anafundisha vilabu vyenu angekuwepo mpaka leo hii..ikiwa kila shabiki wa timu zetu za kibongo anajiona yeye ndio kocha, yeye ndio katibu mkuu wa timu, yeye ndio namba tisa bora!!.
Hata akija Ferguson lazima atakatishwa tamaa ya kuendelea kufundisha ikiwa ataona kila mtu hata makomandoo wanaoingia bure uwanjani eti wakitaka kumfundisha kazi ya ukocha!
Kuingia uwanja wa taifa kabla Maximo hajaja nchini sio ujanja..Mwanakatwe alikuwa kiongozi wa Yanga mwanzoni mwa miaka ya 1980 lakini katika uchaguzi wa juzi wa TFF alipata kura moja tu!!
Unasema eti mchezaji mmoja tu wa kitanzania anatosha kuliuza jina la taifa!!..wewe ndio mwenye upeo mdogo..mchezaji nyota atapatikanaje ikiwa timu zetu zimejaa makocha wa majukwaani ambao fikra zao ni kama zako..kocha Bezinski alisema Obinna na Emeh ni wazembe na akawaweka benchi..Obinna alipokasirika na kumpiga Bezinski , akajitokeza jamaa mmoja wa friends of simba na akaunga mkono kitendo kilichofanywa na Obinna!! , yaani mtu wa karibu kabisa na uongozi wa timu anaunga mkono kitendo cha kumdhalilisha kocha!!..katika mazingira ya kishenzi kama hayo ,hata akiwa Fabio Capello hawezi kuvumilia, ataamua kuondoka...na katika mazingira kama hayo huwezi ukamuandaa mchezaji wa kuja kuichezea Arsenal, Liverpool au Barcelona.
Simba na Yanga ziwe za kisasa , ziendeshwe kisayansi ..na ziachane kabisa na haya mambo yanayoitwa "utoto wa mjini" ambayo kwa kiasi kikubwa yanakusumbua hata wewe Kisiju..TFF ambao wewe unawalaumu wameingiza viongozi vijana wenye damu changa ili walete mabadiliko..wameachana na fikra pamoja na desturi za kupenda kulaumu ovyo..Simba na Yanga na zenyewe zibadilike..haingii akilini timu kama Enyimba iliyoanzishwa mwaka 1976 iwe tajiri kuliko Yanga au Simba zilizoanzishwa mwaka 1936!!..halafu bado kwa upeo wako mdogo bwana Kisiju unataka kuilaumu TFF?.