JK akisalimiana na Bibi Rahma Chahbal, mmoja wa wajumbe kutoka Gulf African Bank, uliofika Ikulu kwa mazungumzo, katikati ni mwenyekiti wa benki hiyo bwana Suleiman Chahbal.

Kampuni ya Gulf-Africa Group yenye makao yake makuu katika Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) itaanzisha benki nchini itakayojulikana kama Gulf-Africa Bank (Tanzania) Limited.
Kampuni hiyo ya Gulf-Africa Group inaundwa kwa pamoja na kampuni mbili ambazo ni Gulf Capital yenye makao yake Dubai, na Noor Capital yenye makao yake Abu Dhabi.
Mtendaji Mkuu wa Noor Capital, Suleiman Bin Shahbal amemwambia JK siku ya Jumatano, Januari 14, 2009, kuwa tayari kampuni yake imewasilisha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) maombi yake ya kufungua benki hiyo katika Tanzania.
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, mtendaji huyo mkuu amemwambia JK kuwa kuanzishwa kwa benki hiyo katika Tanzania ni kupanua shughuli za kampuni ya Gulf-Africa Group katika Afrika Mashariki.
Amesema kuwa tayari kampuni hiyo inayo benki kama hiyo yenye matawi tisa katika Kenya. Amesema kuwa kampuni hiyo pia inajishughulisha na uwekezaji katika maeneo ya mafuta na gesi, mawasiliano ya simu, elimu na ujenzi wa nyumba za biashara.
JK ameikaribisha kampuni hiyo kuwekeza katika Tanzania, akisisitiza kuwa sera ya Serikali yake ni kukaribisha wawekezaji wote kutoka ndani na nje ya nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. haya mabenki wahuni wankuja kutuibia pesa zetu na kutambaa. hawana lolote

    ReplyDelete
  2. A:Wanakaribishwa sana watupunguzie misongamano kwenye mabenki mengine,lakini wasikae Dar tu,wasambae na mikoani.
    B:Tunaomba Ajira ziwe zaidi kwa watanzania(walau 80% wawe vijana wetu wanaotembea na diploma/degree zao mifukoni).Tafadhali.

    ReplyDelete
  3. tutawapa na grace period....teh teh tanzania tanzania...nakupenda kwa moyo woteeeee

    ReplyDelete
  4. hivi tanzania ina baraza la mawaziri?

    ReplyDelete
  5. Hivi nikitaka kuanzisha benki shurti nitinge kwanza Ikulu nikutane na mkulu? Hayo ndiyo mambo ya 3rd world?

    ReplyDelete
  6. Ndio tunabaraza la mawaziri kizungu linaitwa Cabinet, sina uhakika saana lakini najua linundwa na mawaziri woote. Kazi yao kuchapa usingizi na kusema ndio kwa kila kitu.

    ReplyDelete
  7. TUNASHUKURU MABENKI YA NGUVU TOKA GULF YANAKUJA MAANA UK NA MAREKANI WANALINA NA CREDIT CRUNCH.WENZETU HAWA HAWANA RIBA WANAPETA TU.ASANTE JK.

    ReplyDelete
  8. HAHAHAHAHAHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAHA
    ninacheka kwa hasira na kutetemeka kwa hali hizi,
    mawaziri wapo ila laba-stempu,yes-people,marupurupu kibao na kulala,safari za nje ndo acha nk nk
    hii benki ya ar******ni???ok lets see kama wataenda mikoani,ajira zao sasa wataishia kuajiri watu 2maarufu" a.k.a vigogo,sie tunaosugua viatu na sory zetu ndo ivo,SIKU IPO
    JAMANI TUSIUZANE TUUUUUU PATAKUA HAPATOSHI BONGO

    ReplyDelete
  9. Tunataka benki zitakazo wajali walalahoi kama kuwakopesha mitaji na kadhalika Tumechoka kuona msongamano wa mabenki yasio na faida kwa mtanzania wa kawaida

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...