Blaza Michu, na mwenzio Kamanda Kombe
Nimekutumia hii picha niliyoipiga hivi punde, ili na wadau wengine wajionee Bongo isivyo tambarare.
Ni wiki mbili tu zimepita tangu ajali itokee huko Tanga kwa basi kuligonga nyuma lori lililokuwa limeharibika, pasi kuwa na vielelezo vyovyote kuwa limesimama kwa ubovu, na wala hapakuwa na reflectors nyuma ya lori hilo.
Hebu tazama hili gari ya takataka, hapa niliibamba ikikata kona, kutoka barabara ya M/nyamala kuingia Kawawa, indiketa zake hazifanyi kazi, taa za nyuma hata moja haiwaki, kibao cha namba hakipo, na huu wavu waliozuia nao uchafu unavujisha kidogo kidogo, thus uchafu ulikuw aunadondoka barabarani. Pia tairi zake kipara wakati limebeba mzigo mzito namna hii.
Swali; Hii inamaanisha traffic hawalioni? Au mnaliona na huwenda hawaruhusiwi kulikamata? au huwenda ndio linavyotakiwa kuwa kiuchafuuchafu?, au hili lori liue watanzania wangapi ndio mpate pa kuanzia kuchukua hatua ili tuione mnafachapa kazi?
Imagine gari kama hilo mdau linapata breakdown usiku, alafu unakuja nyuma yake itakuwaje? Natumai kama mhishimiwa fulani angekuwa na maono kuwa baada ya siku kadhaa gari yake ingejibamiza hapo nyuma ya hii lori, maamuzi yake ya leo yangekuwa tofauti.Au angekuwa na maono kuwa school bus alilopanda mtoto wake italivaa lori hili kwa nyuma, angechukua hatua flani leo. Kwakuwa haya yoote hatuwezi kuwajua ni bora kuchukua hatua leo.
Mdau MG

( Koplo wa polisi jamii)

AFANDE KOMBE NAONA KAZI INAKUSHINDA. HAUKO PRO-ACTIVE, UKO REACTIVE. NI MPAKA AJALI ITOKEE NDIO UCHUKUE HATUA? LORI KAMA HILI HALITAKIWI LIPITE BARABARA YA MJI WOWOTE SEMBUSE DAR. LAKINI LINAPITA MJINI KATIKATI TENA KWEUPE. HIVI VIJANA WAKO MZEE WANAKUSUBIRI WEWE NDIO ULIONE NA KULIKAMATA? HUWAULIZI ILIKUWAJE HILO GARI LIKAPITA KOTE HUKO? WALE WOTE WALIOKUWA BARABARANI AMBAKO LILIPITA WAWAJIBISHE ILI WAAMKE. WASIKUACHIE WEWE UFANYE KILA KITU. JUZI NIMEKUONA UNAONGOZA MAGARI KWA STAHILI YA UKAKAMAVU WA HALI YA JUU LAKINI NAHISI WAFUASI WAKO WANAKUSANIFU TU, HAWAKUIGI ILI KUBORESHA UTENDAJI WAO. MZEE KOMBE WE NEED A CHANGE, ROADS ARE FINISHING OUR PEOPLE AS IF WE ARE AT WAR. DEFINATELY IT IS POSSIBLE TO MAKE A CHANGE. START BY DEALING WITH OWNERS OF SUCH VEHICLES.
ReplyDeleteHATA MIE NASUPPORT MDAU, MALORI MABOVU BONGO MENGI TU YANAONEKANA BARABARANI....HATA MTU USIE NA UJUZI WA MAGARI UKILIONA TU UNAJUA HILI LINA DEFAULT. TRAFIKI WANATAKIWA KUWA WAKALI KURUHUSU MAGARI YA AINA HII YASITEMBEE BARABARANI..NDIO KAMA MDAU ANAVYOSEMA MPAKA ITOKEE AJALI NDIO UTASIKIA OHOOO KWA NINI AJALI ZINAZIDI WAKATI SABABU ZINAJULIKANA...MHESHIMIWA RAISI ANADAI ANAUMIA SANA NA AJALI ZA BARABARANI..LAKINI JE WATENDAJI WANACHUKUA HATUA MADHUBUTI ZA KUSITISHA MALORI YASIYOFAA KUWA BARABARANI YANATOLEWA. SASA HAPO NI BONGO AMBAPO SERIKALI NZIMA IPO..LAKINI MALORI MABOVU, YASIYO NA TAA USIKU YANATEMBEA..JE HUKO MIKOANI..SI ISSUE????!!!! JAMANI TUCHAPE KAZI KWA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYOOO..HII YA KUSIKITIKA BAADA YA TUKIO SI LOLOTE KAMA UTENDAJI UMELEGEA
ReplyDeleteUuuuwiiiiiiiiii!!! Jamani hii tambarare ya bongo itatumaliza!!! Kuachia magari kama haya kupita katika barabara zetu nao ni ufisadi! Please Act before more accidents happen.
ReplyDeleteHio ndio bongo bwana "PUNDA AFE MZIGO UFIKE"hapo utakuta gari la mnene fulani hilo linapiga kazi kuhudumia nyumba ndogo fulani sasa wee trafic lipige bao uoteshe kibarua nyasi.Cha kushangaza gari hizi hizo barabara zinazopita waheshimiwa pia wanazipita na sio kama hawayaoni hayo yote sema wako busy sana na jinsi gani ya kuzificha nchi za nje pesa za walalajoi walizoziiba
ReplyDeleteQuoting anonymous.....................(January 27, 2009 1:12 PM)" MZEE KOMBE WE NEED A CHANGE, ROADS ARE FINISHING OUR PEOPLE AS IF WE ARE AT WAR. DEFINATELY IT IS POSSIBLE TO MAKE A CHANGE. START BY DEALING WITH OWNERS OF SUCH VEHICLES".............. si ajabu yeye mwenyewe ndiyo owner, hagusiki!!
ReplyDeleteDuh Afande Komba kawaona hawa? hahahaa.
ReplyDeletekweli annon ni mradi wa "mkubwa" huu,kama ile miradi ya kinguvu-kibabe ya kufunga mnyororo magari ya raia eti no parking,na parking fees,,,,wanankera haooooo
ReplyDeleteJukumu la kwanza la kulinda maisha na mali zetu ni letu sote tusiwaachie Police na akina Afande Kombe peke yao! Ushauri; Ukiona 'wauaji' kama hao kwa Dar piga simu no.0732 928723. Trust me hao jamaa (traffic) ukiwapigia simu wana - respond ASAP!
ReplyDeleteMdau Lily
BONGO HAMNA SHERIA NA MNAFIRI KUONGOZA NCHI RAHISI MKATEGEMEA HAYO MAKUNDI YANOJAZANA SERIKALINI WAKAFANYA KAZI? NCHI HAIONGOZWI NA MARAFIKI PEKE YAO LAZIMA KUWE NA MAADUI HILI WAWEZE KUKOSOANA KATIKA KUFANYA KAZI.
ReplyDeleteWOTE NYIE MNAJUA KITU GANI KINAWEZA KUTOKEA KAMA BIASHRA WAAJILIWA WOTE NI NDUGU AU MNASEMAJE?
MDAU "cha mtu mavi"
Dahhh hii wananchi wenzangu inasikitisha kwani hilo gari nahisi siyo la mweshimiwa yoyote na kama muheshimiwa basi anamapungufu tena mengi sana, namaanisha hili gari mama yangu mzazi utakuta la jamuhuri ya muungano wa Tanzania,
ReplyDeletekwahiyo maofisa polisi wanashindwa au waoga wa kufanya kazi zao, kutokana na kuto kujua right zao za kazi pengine wakiwa na uwoga wakufukuzwa kazi,
Kinachotakiwa ni kutenda kazi basi ndugu zanguni wahusika mlichukulie hatua suala hili haraka iwezekanavyo.
(www.scis-ltd.blogspot.com)
NB Kwako bratha michuzi aka misupu katika hii blog yako chini kabisa unatakiwa ubadilishe copyright issue zako bado zinaonekana za zamani mwaka 2006, wakati huu mwaka 2009, changamka kwa hilo please.
Cheers!
MDAU LILY,
ReplyDeleteKWA NINI MTU AHANGAIKE KUPIGA SIMU LABDA MIKOANI. LAKINI DAR SIKU HIZI MIE NOANA KILA HATUA KUMI KUNA TRAFIKI...TRAFIKI WAKO WENGI SANA BARABARANI..NA MAGARI MAMBOVU YANAPITA KWENYE MACHO YAO..SASA UPIGE SIMU YA NINI...INACHOTAKIWA WAWAJIBIKE..SIO TU KUSIMAMA BARABARANI NA KUSIMAMISHA MAGARI YA WALALAHOI KUDAI CHOCHOTE
YA PILI GARI KAMA HILO KWENYE PICHA LA TAKATAKA HATA NAMBA ZA GARI HALINA, SASA UTAPIGA SIMU UKITOA REFERENCE IPI...
SIJUI NI KOMBE PLEASE HAKIKISHA WATU WANAFANYA KAZI KUNUSURU MAISHA YA WATANZANIA. BORA KINGA KULIKO AJALI...KWA DAR NI MBAYA SANA MAGARI KAMA HAYA YAKISABABISHA AJALI YATAONDOKA NA WENGI KUTOKANA NA ULE MSULULU WA MAGARI....MIMI UKWELI HUWA INANIKERA VIBAYA SANA NINAPOONA MATRUCK MABOVU BARABARANI...NA YANAENDA TU BILA HOFU NA KUPITA MBELE ZA TRAFIKI..NA USIKU NDIO BALAA, TAA HAYANA YAKO BARABARANI..JAMANIIII
HILO LORI LIMEPASI VIPI KWENYE WEEK YA NENDA KWA USALAMA,UTAKUTA LINAYO HIYO STIKA KWENYE KIOO.NDO UJUE KWELI RUSHWA IPO KWA WINGI KWA MATRAFIKI,WANAUZA STIKA BILA KUKAGUA GARI ILIMRADI APATE CHA JUU TU!
ReplyDelete